Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake
H. 8 Jumada I 1444 | Na: 1444 H / 019 |
M. Ijumaa, 02 Disemba 2022 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
China Yawalazimisha Wanawake wa Kiislamu wa Uyghur kuolewa na Makafiri ili Kuufuta Uislamu kutoka Turkestan Mashariki
(Imetafsiriwa)
Mnamo tarehe 16 Novemba 2022, gazeti la Telegraph iliripoti juu ya dhurufu za ndoa ya kulazimishwa ambayo inawasibu wanawake wa Kiislamu huko Turkestan Mashariki. Makala hayo yana kichwa "Wachina walipwa kuwaoa Waislamu katika mpango wa kuwaangamiza Wauyghur". Shirika moja la kutetea haki za binadamu limegundua kuwa maafisa wa Xinjiang wanawahonga na kuwatishia wanawake wa Uyghur ili wafunge ndoa za kulazimishwa. Mradi wa Haki za Kibinadamu wa Uyghur (UHRP), shirika lisilo la faida lenye makao yake makuu jijini Washington, limeandika usaliti na hongo kwa Wayghur wa kike katika mikataba ya ndoa mchanganyiko na wanaume wanati wa Han wasio Waislamu. Ripoti hiyo inathibitishwa na nyaraka rasmi za sera, machapisho ya mitandao ya kijamii na mahojiano na Wayghur nje ya nchi. Mwandishi wa habari Samina Mistream ananukuu yafuatayo katika ripoti yake: "Maafisa wa Xinjiang wamekuwa wakitoa zawadi za pesa taslimu pamoja na ruzuku ya nyumba na elimu, kazi na bima ya matibabu kwa wanawake wa Uyghur ambao wako tayari kuolewa na wanaume wa Han - na vile vile wanaripotiwa kuwatishia wanawake kwamba wao au familia zao zinaweza kuishia katika kambi za uzuizi ikiwa watakataa. Katika tukio moja, maafisa kutoka kijiji cha Kalasa katika Mkoa wa Aksu walitoa yuan 40,000 (£4,750) kwa wanandoa wawili mchanganyiko wa Uyghur-Han kama sehemu ya kampeni ya kijiji hicho ya "Umoja wa Kitaifa, Familia Moja". Pia kulikuwa na nyaraka kuhusu "tuzo za ndoa za kikabila" za kila mwaka katika jiji la Kashgar ambazo zilifadhiliwa kwa yuan 20,000 (£2,380).
Toleo la Kichina la TikTok, Douyin linaonyesha wanawake wa Kiislamu waliofazaika katika dhurufu za ndoa ya kulazimishwa. Hatua hizo zinafafanuliwa na mamlaka ya China kama moja muhimu kuzuia ugaidi na kuhakikisha uwiano wa kijamii. Ukweli wa mambo ni kwamba huo ni mfano mwingine unaoendelea wa hofu ya kupindukia ambayo utawala wa China unao dhidi ya Uislamu na nguvu zake zinazoongezeka katika eneo hilo. Wanawake wa Kiislamu ndio ufunguo wa fikra za baadaye za Ummah; kufifisha uwezo wao wa kupata watoto waliolelewa kwa maadili safi ya Kiislamu yenye nguvu ni njama ya kimkakati ya kuhujumu uwepo wa muda mrefu wa fikra na mawazo ya Kiislamu katika eneo hilo. Hili ni shambulizi tasa la kisiasa ambalo litatumika tu kuwatia moyo Waislamu katika kuilinda Dini yao. Ukandamizaji wa haki na dhulma dhidi ya Waislamu haujawahi kufanya kazi kihistoria kwa sababu nusra ya Mwenyezi Mungu (swt) imekuwa nao daima. Wanawake wa Kiislamu wa Turkestan Mashariki mateso yao hayatapita patupu bila malipo kwa Mola wao Mlezi (swt). Mwenyezi Mungu (swt) asema:
[إِنَّمَا يُوَفَّى الصَّابِرُونَ أَجْرَهُم بِغَيْرِ حِسَابٍ]
“Hakika wenye subira watapewa ujira wao bila ya hisabu.” [Az-Zumar: 10].
Kwa hakika kimya cha watawala wa Kiislamu juu ya unyama wa dada zetu wa Kiislamu ni jinai inayostahiki kupinduliwa kwao, na kusimamisha Khilafah kwa njia ya Utume ili kulinda heshima ya dada zetu dhidi ya maadui wa Uislamu.
Kitengo cha Wanawake
katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Kitengo cha Wanawake |
Address & Website Al-Mazraa Sanduku la Posta. 14-5010 Beirut- Lebanon Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43 www.domainnomeaning.com |
Fax: Telefax E-Mail: ws-cmo@domainnomeaning.com |