Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake
H. 28 Rabi' II 1444 | Na: 1444 H / 018 |
M. Jumanne, 22 Novemba 2022 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Mkutano wa 5 wa Kimataifa wa Wanawake na Haki Unatumikia CEDAW
(Imetafsiriwa)
Mnamo Novemba 4-5, 2022 jijini Istanbul, “Mkutano wa 5 wa Kimataifa wa Wanawake na Haki” ulifanyika, kwa hotuba ya ufunguzi ya Rais Recep Tayyip Erdogan. Uliandaliwa na kikundi cha utetezi wa wanawake, Chama cha Wanawake na Demokrasia (KADEM) pamoja na Wizara ya Huduma za Familia na Jamii. Tamko la mwisho la mkutano huo lilisisitiza umuhimu wa familia yenye nguvu kwa jamii yenye nguvu. Mkutano wa mwaka huu, ambao mada yake kuu ni “Kanuni za Utamaduni na Wanawake”, una udanganyifu ambao upo katika kila sentensi kuanzia mwanzo hadi tamko la mwisho. Kichwa hiki kwa hakika kimo ndani ya wigo wa mojawapo ya vifungu vikuu vya CEDAW (Mkataba wa Kutokomeza Aina Zote za Ubaguzi Dhidi ya Wanawake), “Kutokomeza Ubaguzi na Desturi”, na ni dhahiri kwamba unatumikia thaqafa ya kiulimwengu ya kikoloni. Tamko hilo lilisema kwamba pamoja na uboreshaji wa kisasa “utekelezaji wa kanuni moja ya kitamaduni kwa wanawake wote wa ulimwengu ni agizo ambalo linapaswa kupingwa na kugombwa” likieleza kuwa “Kupinga uwekaji huu haimaanishi kuzembea kwa kipengele cha umoja na ujumuishi cha utamaduni, lakini badala yake kutilia shaka ada na kanuni zinazosababisha dhulma, ukosefu wa usawa na ubaguzi.”
Ni muhimu kutathmini mambo machache ambayo yameelezwa katika hafla yote hiyo:
1. “Wanawake, haswa wale wanaoishi katika nchi zilizo na historia ya ukoloni na tamaduni kuu iliyowekwa kwa watu, wanakabiliwa na shinikizo la kanuni za kitamaduni”
Kabla ya wakoloni kuingia katika ardhi zetu, thaqafa ya Kiislamu iliwapa wanawake Waislamu na wasiokuwa Waislamu ladha ya uhuru ambao wanawake wa nchi za Magharibi hawawezi kuufurahia hata leo. Katika thaqafa ya Kiislamu, idadi na mafanikio waliyoyapata wanawake katika elimu, sayansi na siasa hayatoshei hata kidogo ndani ya vitabu vya encyclopaedia. Zaidi ya hayo, hatuwezi kuzungumza juu ya “ukoloni uliopita”, kwa maana ukoloni katika nchi za Kiislamu haujakwisha, umebadilika tu sura pekee. Sasa wanawake wa Kiislamu wanakandamizwa chini ya “uvamizi wa kithaqafa”, ambao ni wa siri zaidi na hatari zaidi kuliko uvamizi wa kijeshi, na chini ya kulazimishwa kwa akili zilizochafuliwa na uvamizi huu wa “kithaqafa”!
2. “Katika nchi nyingi, wanawake wanakabiliwa na ubaguzi kutokana na imani yao.”
Sentensi hii ni jinsi akili zilizotiwa sumu na uvamizi wa kithaqafa zinavyowabagua dada zao wenyewe katika dini. Kwa sababu wanawake wa Kiislamu hawapati ubaguzi huu chini ya utawala wa Kiislamu, bali chini ya ukandamizaji wa kidini na kitamaduni katika nchi za Magharibi na tawala za vikaragosi na vibaraka za Magharibi! Ni wao, ndio wanaowapora wanawake wa Kiislamu nchi zao, nyumba zao, mali zao, maisha, maadili ya kithaqafa na imani zao!
3. “Wanawake hawapaswi kujiepusha na kufanya kazi zinazotazamwa zaidi kuwa za wanaume.”
Wakati hata wanaume wenyewe wanakabiliwa na unyonyaji katika ajira, ni kipi chengine munaweza kukitoa isipokuwa kuwakandamiza wanawake ndani ya magurudumu ya kazi za kibepari za kinyonyaji kwa gharama ya kuwanyima wanawake umama wao na kuwanyima watoto mama zao? Hata hivyo, chini ya utawala wa thaqafa ya Kiislamu na mfumo wa kiuchumi wa Kiislamu, mwanamke anaweza kufanya kazi yoyote na kufanya taaluma yoyote anayoitaka kama inavyoruhusiwa na Shariah.
4. Mumesema pia, “Miundombinu ya kisheria inatoa ulinzi mkubwa kwa wanawake bila kujali dola inayotawala; hivyo basi, katiba isiyokengeuka kutoka katika mhimili wa haki ndiyo dhamana ya haki za wanawake.”
O KADEMU na washirika wake wenye mawazo sawa! Bila shaka, kama jina lenu linavyopendekeza, munatafuta suluhu ndani ya demokrasia na thaqafa ya Kimagharibi. Kwa hiyo, munafanya kazi tu kwa maslahi ya mfumo wa sasa. Mulisema waziwazi kwamba “Uislamu hautoi suluhu kwa matatizo ya ulimwengu wa kisasa” na mukatangaza kupendelea Mkataba wa Istanbul wa kikoloni na uliobuniwa na mwanadamu, CEDAW, Azimio la Beijing, na sheria zilizojengwa juu ya haya. Mulikataa wakati Uturuki ilipoamua kuzindua Kongamano la Istanbul mnamo 2021 kwa kutangaza “Kongamano la Ankara badala yake”. Munatetea Sheria Nambari 6284, inayo angamiza familia, na Kanuni ya Kiraia inayo hufungua njia ya unyanyasaji wa kinyumbani na kuhalalisha uzinzi. Mulileta hatua dhidi ya Waislamu, wanaozungumza dhidi ya batili ya mawazo yenu. Kwa hivyo munawezaje kuzungumza juu ya haki?
Mitazamo ya kisiasa na msimamo wa wanawake wa Kiislamu kutaka maisha ya Kiislamu unagongana na fahamu wenu wa uwezeshaji, hivyo munakaa kimya dhidi ya mateso yanayowakabili. Mumethibitisha mara kwa mara kwamba munapendelea kanuni za demokrasia na ufeministi. Kwa nini hamtetei haki za wanawake nchini Uturuki, wanapokamatwa kwa kulingania “Simamisheni Khilafah, Enyi Waislamu”, mithili ya wanawake wengine wanavyofanya kote ulimwenguni, au wale wanaokabiliwa na mashtaka ya kisheria kwa kufundisha wakiwa na jilbab, au kufanyiwa upekuzi wa kiholela wakiwa uchi gerezani, au wale ambao waume zao wamefungwa hadi miaka 8 kwa sababu ya ndoa za mapema?
Sisi wanawake wa Kiislamu hatuwahitaji nyinyi, wala mashirika yenu wala mikutano yenu. Simameni tu kutoka kwa jua letu! Pindi Khilafah Rashida ya Pili kwa Njia ya Utume itakaposimamishwa hivi karibuni, kama ilivyoahidiwa na Mwenyezi Mungu Subhanahu na Ta'ala, wanawake wa Kiislamu pamoja na wasiokuwa wa Kiislamu watafurahia haki zao kamili; wataishi kwa utulivu na usalama katika familia na jamii. Na watakuwa na athari ya kweli katika siasa tofauti na wengine, ambao ni vumbi tu chini ya miguu ya mtu. Wakati huo, sisi wanawake wa Kiislamu, tutauunda upya ulimwengu uliowezeshwa kwa utu na heshima ya thaqafa ya mashuhuri - Uislamu.
Kitengo cha Wanawake
katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Kitengo cha Wanawake |
Address & Website Al-Mazraa Sanduku la Posta. 14-5010 Beirut- Lebanon Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43 www.domainnomeaning.com |
Fax: Telefax E-Mail: ws-cmo@domainnomeaning.com |