Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Kenya

H.  23 Safar 1437 Na: 1437/03 H
M.  Jumamosi, 05 Disemba 2015

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Usalama wa Raia ni Kadhia Muhimu Mno na Haipaswi Kuchukuliwa kwa Usahali

Kifo cha mwanafunzi mmoja na kujeruhiwa vibaya kwa wanafunzi thelathini wa Chuo Kikuu cha Strathmore katika jiji kuu la Nairobi katika Zoezi lililo kwenda mrama la Kupambana na Ugaidi ni jambo la kuvunja moyo na ambalo lastahili kukemewa na kila muekaji amani. Ripoti kutoka kwa vyombo vya habari nchini zimesema kuwa tukio hilo lilipangwa na uongozi mkuu wa Chuo hicho kwa ushauriano na maafisa wakuu wa polisi bila ya kuwaarifu wanafunzi hao.   

Ruhusa iliyotolewa kwa kitendo hicho kiovu cha kigaidi imethibitisha namna vyombo vya usalama vinavyo vuruga na kuhatarisha usalama wa raia. Kwa nini vitendo kama hivyo vyenye kupelekea kupoteza maisha na majeraha kwa watu vivumiliwe kufanyika kwa kisingizio cha matayarisho dhidi ya mashambulizi ya kigaidi! Ni vipi inaingia akilini kwa upande mmoja kudai kupigana na ugaidi huku upande mwingine ukitekeleza vitendo vya kigaidi vinavyo pelekea majeraha na kupoteza maisha? Hili haliwezi kushabikiwa ikizingatiwa kuwa kadhia ya usalama ni maslahi muhimu mno kwa watu na ambayo serikali na taasisi zake ina jukumu la kulinda raia wake. Tumeshtushwa na wanaodaiwa kuwa wasomi na ambao pia ni wasimamizi wa chuo hicho kuwaona wakichukua maisha ya watu kwa urahisi ambapo hata wajinga wa mwisho kabisa huyatukuza na kuchukua tahadhari kuyalinda.   

Bado tungali tunaiona Kenya ikiendelea kupalilia njama ya dola za Kimagharibi hususan Amerika kuuhusisha Uislamu kimakusudi na vitendo vya kigaidi. Dola hizo zimekuwa zikiwatoa sadaka raia wake ili kuwalazimisha waziunge mkono katika mauaji yao ya kinyama ya Waislamu. Tunahisi kitendo hiki kililengwa kulazimisha fikra kwa wasiokuwa Waislamu za kuendelea kuwachukia Waislamu na kuwaona kama tishio kwa usalama wa watu wote wakiwemo wanafunzi.  

Uislamu unatambua kuwa kadhia ya usalama sio kadhia inayopaswa kuchukuliwa kwa usahali na ndio sababu ukailazimisha Dola ya Kiislamu, Khilafah, kudhamini usalama kwa wanadamu. Kulinda maisha ya mwanadamu ni moja ya mafunzo ya Uislamu. Sheria imeeleza ndani ya Qur'an:

مِنْ أَجْلِ ذَلِكَ كَتَبْنَا عَلَى بَنِي إِسْرَائِيلَ أَنَّهُ مَن قَتَلَ نَفْسًا بِغَيْرِ نَفْسٍ أَوْ فَسَادٍ فِي الأَرْضِ فَكَأَنَّمَا قَتَلَ النَّاسَ جَمِيعًا وَمَنْ أَحْيَاهَا فَكَأَنَّمَا أَحْيَا النَّاسَ جَمِيعًا

“Kwa sababu ya hayo tuliwaandikia Wana wa Israili ya kwamba aliye muua mtu bila ya yeye kuua, au kufanya uchafuzi katika nchi, basi ni kama amewaua watu wote. Na mwenye kumuokoa mtu na mauti ni kama amewaokoa watu wote.” [TMQ Al-Maidah: 32]

Shabani Mwalimu
Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir Afrika Mashariki

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Kenya
Address & Website
Tel:  +254 707458907
E-Mail: mediarep@hizb.or.ke

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu