Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Kenya

H.  13 Safar 1437 Na: 1437/04 H
M.  Alhamisi, 24 Disemba 2015

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Mazazi ya Mtume Muhammad (saw) Yanatoa Wito wa Uokozi kwa Wanadamu Wote
(Imetafsiriwa)

Katika mwezi wa Rabi ul-Awwal, sherehe na shamra shamra nyingi hushuhudiwa miongoni mwa Waislamu wengi, kama kumbukumbu ya mazazi ya Mtume Muhammad (saw). Matukio haya ni thibitisho la kutosha linalo ashiria kuwa Ummah huu ungali umejifunga na hamasa za kutukuza ibada zao. Kuhusiana na kumbukumbu ya mazazi ya Mtume (saw), Chama cha Kisiasa cha Kiislamu Hizb ut Tahrir Afrika Mashariki kingependa kutoa maoni yafuatayo:

Kadhia ya kumpenda Mtume (saw) haipaswi kuwa kadhia ya kihamasa pekee; mbali na hayo, ni wajibu ichukuliwe kama sehemu ya pendekezo la imani ya Kiislamu kwa Waislamu kumpenda Mtume (saw) zaidi ya kitu chochote chengine ulimwenguni. Imeripotiwa kutoka kwa Anas (ra) kuwa Mtume (saw) amesema:

«لَا يُؤْمِنُ أَحَدُكُمْ حَتَّى أَكُونَ أَحَبَّ إِلَيْهِ مِنْ مَالِهِ وَأَهْلِهِ وَالنَّاسِ أَجْمَعِينَ»

“Hatoamini mmoja wenu mpaka niwe napendwa zaidi naye kushinda mali yake, na jamaa zake, na watu wote”.

Waislamu wamewajibishwa kuihami na kuilinda heshima ya Mtume (saw) kuliko mtu mwengine yeyote. Mwenyezi Mungu (swt) asema:

لِّتُؤْمِنُوا بِاللَّـهِ وَرَسُولِهِ وَتُعَزِّرُوهُ وَتُوَقِّرُوهُ وَتُسَبِّحُوهُ بُكْرَةً وَأَصِيلًا﴿

“Ili mumuamini Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na mumsaidie, na mumheshimu, na mumtakase asubuhi na jioni” [TMQ 48:9].

Lakini, ni huzuni kubwa kuona heshima hii ikitwezwa na kudunishwa na makafiri waliojaa chuki dhidi ya ujumbe wake na kumchukia yeye mwenyewe. Leo Wamagharibi na serikali zao za kitwaghut, bila ya aibu wanatohifadhi na kuwapa ulinzi wahuni wote wanaomtusi (saw) chini ya kisingizio cha "uhuru wa rai na kujieleza".

Katika mwezi huu wa mazazi ya Mtume (saw), ni muhimu Waislamu wakumbuke na pia watambue thamani kubwa aliyoleta (saw) nayo si nyingine ila ni Uislamu. Lengo lake msingi likiwa ni kuwakomboa wanadamu wote kutoka katika giza la ujinga hadi katika nuru ya Uislamu. Hili ni lazima liwakumbushe zaidi Waislamu uhalisia na dhati ya Uislamu, kuwa sio dini ya kiroho pekee, kama inavyo dhihirishwa kirongo na kilazima na Wamagharibi. Ni muhimu mno kudiriki kuwa Uislamu ni mfumo kamili wa maisha ulio na nidhamu yake ya kipekee ya kisiasa/utawala, nidhamu ya kiuchumi na hata nidhamu ya kijamii iliyoteremshwa kwa lengo moja pekee la kutawala juu ya mifumo mengine yote iliyotungwa na wanadamu, hata kama makafiri watachukia hilo.

هُوَ الَّذِي أَرْسَلَ رَسُولَهُ بِالْهُدَىٰ وَدِينِ الْحَقِّ لِيُظْهِرَهُ عَلَى الدِّينِ كُلِّهِ وَلَوْ كَرِهَ الْمُشْرِكُونَ﴿

“Yeye ndiye aliye mtuma Mtume wake kwa uwongofu na Dini ya haki ili ipate kuzishinda dini zote, ijapo kuwa washirikina watachukia” [TMQ 61:9].

Mwisho, tungependa kumkumbusha kila Muislamu umuhimu wa kumuiga Mtume Muhammad (saw) kama kiigizo cha kisiasa kuwahi kutokea ulimwengu mzima, ambaye alifaulu kusimamisha dola ya kwanza ya Kiislamu mjini Madina Munawwara na kufaulu kutawalalisha Uislamu. Dola hiyo iliwafanya Waislamu kuwa taifa lenye nguvu zaidi na kuwadhamini amani na usalama katika utekelezaji dini yao anayoiridhia Mwenyezi Mungu (swt). Vilevile tunawajibishwa kuiga siasa ya Mtume (saw) aliyoifuata ili kurejesha maisha kamili ya Kiislamu, kupitia kusimamisha tena Dola ya Kiislamu ya Khilafah kwa njia ya Utume ambayo itaangamiza na kuondoa kila aina ya dhulma na unyanyasaji ulioanzishwa na Wamagharibi dhidi ya Waislamu. 

Shabani Mwalimu

Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir Afrika Mashariki

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Kenya
Address & Website
Tel:  +254 707458907
E-Mail: mediarep@hizb.or.ke

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu