Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Mamlaka ya Palestina Iliyofungamana na Maadui wa Mwenyezi Mungu Yakamilisha Dori ya Ghadhabu katika Kuwatesa Watu wa Palestina na Kuwakamata Watetezi wa Haki

Siku chache zilizopita, vikosi vya usalama vya Mamlaka ya Ndani ya Palestina (PA) viliwakamata Sheikh Aws Abu Arqoub na Sheikh Muhammad Manasrah, wanachama wa Hizb ut Tahrir. Kwa kuwakamata wale wanaosema ukweli, PA na vikosi vyake vinasisitiza kuwa kiongozi wa Mayahudi, wakidunga visu watu wote wa Palestina.

Soma zaidi...

Mgogoro wa Nishati nchini Jordan na Suala la Ufisadi wa Kiuchumi wa Mradi wa Al-Attarat, Utiifu wa Kisiasa, na Kuongezeka kwa Deni

Ripoti ya habari ya Shirika la Habari la Jordan, Petra, ya tarehe 6 Agosti 2024, ilisema kwamba “Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi iliamua kwamba serikali wala Kampuni ya Kitaifa ya Umeme hazihitajiki kulipa sehemu yoyote ya gharama kwa Kampuni ya Umeme ya Al-Attarat.” Habari hizi za upotoshaji zinakusudiwa kuficha hasara inayotarajiwa ambayo serikali ya Jordan itaipata kutokana na ukweli wa hukumu hiyo, inayosema: “Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi inaamuru kwamba mkataba huo ni halali na hauhusishi ukosefu mkubwa wa haki.”

Soma zaidi...

Mlima Geneva Umefanya Kazi Na Kuzaa Panya Aliyekufa!!

Jana, Ijumaa, Agosti 23, 2024, mkutano wa Geneva, ulioanza Agosti 14 kujadili mgogoro wa Sudan, ulihitimishwa kwa kuunda “Muungano wa Umoja wa Kimataifa” ili kumaliza vita nchini Sudan. Kwa mujibu wa Mjumbe Maalum wa Marekani nchini Sudan, Tom Prillo, muungano huo unajumuisha, pamoja na Marekani, Umoja wa Mataifa, Muungano wa Afrika, IGAD, pamoja na Uswizi, Saudi Arabia, UAE na Misri. Hata hivyo, pamoja na urefu wa majadiliano ya Geneva, matokeo hayana thamani ya halisi katika kusimamisha vita vya kikatili vinavyoendelea nchini Sudan.

Soma zaidi...

Ardhi Iliyobarikiwa - Palestina Sio Karata ya Uchaguzi kwa Ruwabidha Mzembe

Mnamo siku ya Jumatatu, tarehe 19/8/2024, Rais wa Algeria Abdelmadjid Tebboune alitoa wito kwa Misri kufungua mipaka na Ukanda wa Gaza kwa jeshi la Algeria, ili kuwanusuru wakaazi wa Ukanda wa Gaza, na kusema: “Naapa kwamba haraka iwezekanavyo tutapeleka vitengo huko na kujenga upya kile kilichoharibiwa,” na akasema: “Jeshi la Algeria liko tayari kwenda Gaza na sisi tuko tayari, tunasubiri tu Misri itufungulie mipaka yake.”

Soma zaidi...

Damu za Waislamu zinamwagika huku watawala wao wakishuhudia na hakuna suluhu!

Umbile la Kiyahudi linaendeleza uvamizi wake dhidi ya watu wa Palestina na linaendelea na jinai zake mbele ya masikio na macho ya walimwengu, bila kuzuiwa na azimio au hukumu yoyote ya Umoja wa Mataifa kutoka Mahakama ya Kimataifa. Idadi ya mashahidi waliohesabiwa imezidi 40,000, na pengine idadi sawia bado wamenaswa chini ya vifusi. Idadi ya waliojeruhiwa inakaribia 100,000, huku wale waliosalia wakiwa hai wanateseka sana kutokana na njaa.

Soma zaidi...

Marekani Yarefusha Vita ili Kufikia Ajenda yake, Kuteketeza Watu, Miti, na Mawe - Hakuna Njia ya Kutoweka Isipokuwa Kupitia Khilafah!

Mnamo Jumapili, Agosti 11, 2024, mikutano ya Jeddah ilikamilika kati ya wajumbe kutoka serikali ya Sudan na Mjumbe Maalum wa Marekani nchini Sudan, Tom Periello, bila kufikia maelewano yoyote kuhusu ajenda ya mazungumzo na waangalizi. Baada ya kuregea kwa wajumbe wa mazungumzo, serikali ilitoa taarifa ikibainisha kushindwa kwa ujumbe wa Marekani kuwasukuma wanamgambo wa waasi kujitolea kutekeleza Azimio la Jeddah.

Soma zaidi...

Mwanachama Mwengine wa Hizb ut Tahrir Atiwa hatiani kwa Kutoa Wito wa Ukombozi wa Palestina: Historia Itakumbuka Neno la Kweli na Wahalifu wa Kweli

Siku 303 baada ya mauaji ya halaiki ya Wazayuni yanayoungwa mkono na Denmark dhidi ya raia wa Gaza, hukumu nyengine imetolewa katika Mahakama ya Wilaya ya Copenhagen dhidi ya mwanachama wa Hizb ut Tahrir kwa kutoa wito wa ukombozi wa kijeshi wa Palestina.

Soma zaidi...

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu