Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Bangladesh

H.  18 Safar 1446 Na: H 1446 / 05
M.  Ijumaa, 23 Agosti 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Uchokozi wa Maji Usio na Kifani wa India Kutia Shinikizo la Kisiasa kwa Bangladesh;
Hakuna Njia Mbadala ya kuitambua India kama Dola Adui

(Imetafsiriwa)

Leo, Ijumaa (23/08/2024), baada ya swala ya Ijumaa katika Msikiti wa Taifa wa Baitul Mukarram, Hizb ut Tahrir / Wilayah Bangladesh iliandaa maandamano na msafara kupinga uchokozi wa maji wa India dhidi ya Bangladesh. Wanachama wa Hizb ut Tahrir walitoa hotuba katika maandamano hayo. Msafara huo uliandamana kuelekea Bijayanagar Mor, kisha Dainik Bangla Mor na kurudi tena hadi Baitul Mukarram Lango la Kaskazini na kumalizia kwa kufanya Du`a. Wazungumzaji katika maandamano hayo waliangazia nukta zifuatazo:

India ilianzisha uchokozi wa maji ambao haujawahi kutokea juu ya Bangladesh ili kuunda shinikizo la kisiasa kwa Bangladesh. Walifungua milango ya Bwawa la Dumbur bila onyo lolote, jambo ambalo lilisababisha nyumba za mamilioni ya watu katika wilaya kumi za Bangladesh kuzama haraka chini ya mafuriko. Watu achilia mbali kulinda nyumba na mali zao, wanajitahidi kuokoa maisha yao. Huku umeme na mawasiliano ya simu yakikatika, familia ziko katika hali ya wasiwasi mkubwa na hazijui hali ya sasa ya watoto wao, wazazi wakongwe walioathiriwa na mafuriko, na hata hawajui ikiwa wanafamilia wao walinusurika au la. Sera ya India ya kuendelea ya uchokozi si chochote ila uadui na watu wa nchi yetu hii iliyo na idadi kubwa ya Waislamu. Mwenyezi Mungu (swt) asema,

[لَتَجِدَنَّ أَشَدَّ النَّاسِ عَدَاوَةً لِلَّذِينَ آمَنُوا الْيَهُودَ وَالَّذِينَ أَشْرَكُوا]

“Hakika utawakuta walio shadidi kuliko watu wote katika uadui kwa walio amini ni Mayahudi na washirikina.” [Surah Al-Ma'ida: 82].

Katika kipindi hiki cha janga nchini humo, Hizb ut Tahrir/Wilayah Bangladesh imetoa wito kwa utawala wa nchi hii, jeshi la wanamaji, jeshi la anga na ngazi zote za watu kutumia nguvu na uwezo wao wote kulinda maisha na mali ya watu walioathirika na mafuriko hayo, na kuwataka watu kuitisha yafuatayo:

1. Kwa kuzingatia matarajio ya watu wa nchi hii, ubalozi wa India unapaswa kufungwa mara moja kwa kutangaza India kama nchi adui. Mikataba yote dhidi ya Uislamu na serikali na Makubaliano yaliyotiwa saini na India inapaswa kufutiliwa mbali mara moja.

2. Vikosi vya jeshi na walinzi wa mpaka wa nchi hiyo, BGB, viwe tayari kukabiliana na uvamizi wowote kutoka India na jeshi la nchi hii na BGB zifanywe kuwa kikosi chenye nguvu kukabiliana na nchi adui.

3. Hasina na majambazi wake waliotekeleza njama ya India ya kudhoofisha jeshi la nchi kupitia mauaji ya Pilkhana wafikishwe mahakamani na kupewa adhabu ya mfano.

4. India imeendeleza uchokozi wake kwa nchi hiI kwa miongo mitano iliyopita kutokana na sera ya kujipendekeza ya India kwa tawala vibaraka za nchi za kisekula. Zinapinga India kwa maneno, lakini kwa kweli hawazichukua hatua zozote za kukabiliana na uchokozi wa India. Hivyo vibaraka hawa lazima wakataliwe.

5. Zaidi ya yote, mpango wa kuona mbali na wa muda mrefu lazima uchukuliwe ili kuiregesha India chini ya utawala wa Kiislamu ili kukomesha kabisa uchokozi wake wote; kwa sababu ni wakati tu wa kipindi cha utawala wa Waislamu, ndipo watu wa eneo hili waliishi maisha ya furaha na mafanikio kwa umoja bila kujali dini, rangi, na tabaka.

Hatimaye wazungumzaji walimalizia kwa kuwataka watu wajitokeze kuanzisha taifa linaloongoza - Khilafah kwa njia ya Utume.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Bangladesh

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Bangladesh
Address & Website
Tel: ‎+88 01798 367 640‎
www.ht-bangladesh.info
E-Mail: contact@ht-bangladesh.info, htmedia.bd@outlook.com Skype: htmedia.bd

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu