Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari

H.  26 Rabi' I 1446 Na: H 1446 / 031
M.  Jumapili, 29 Septemba 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Kuinusuru Gaza si kupitia Hotuba na Sherehe, Enyi Wanazuoni!
(Imetafsiriwa)

Mnamo siku ya Alhamisi, tarehe 26 Septemba, shughuli za Wanazuoni wa Mpango wa Umma wa Kukinusuru Kimbunga zilizinduliwa kwa mnasaba wa mwaka wa kwanza wa Hijri tangu kutekelezwa kwa Kimbunga cha Al-Aqsa katika tamasha kubwa la umma katika mji wa Istanbul. Tamasha hilo lilishuhudia ushiriki wa idadi kubwa ya wanazuoni wa Kiislamu ana kwa ana au kupitia hotuba zilizorekodiwa, pamoja na mamia ya Waturuki na wanachama wa jumuiya za Kiarabu wanaoishi Istanbul. Wahudhuriaji waliswali rakaa mbili na kuomba dua ya Qunut, huku wakiinua mikono juu kumuomba Mwenyezi Mungu, wakiomba nusra kwa watu wa Gaza na kuondolewa mzingiro juu yao.

Tuna hakika kwamba msiba wa watu wetu huko Gaza umechochea hisia za wana na mabinti wote wa Ummah katika ngazi zote, na hakuna hata mmoja miongoni mwao ambaye hajaonyesha hisia zake za mshikamano, maonyesho ya masikitiko na mihemko ya huzuni juu ya hali ya watu wetu wanaokandamizwa huko Gaza, ambayo yanayeyusha nyoyo kwa huzuni na maumivu. Yeyote anayefuatilia harakati za watu wengi katika sehemu zote za nchi za Kiislamu atagundua na kutambua ukubwa wa mafungamano, mawasiliano na mshikamano wa Ummah na uungaji mkono wa wana na mabinti zake kwa njia yoyote inayopatikana ya kuonyesha hasira zao na kuwafariji watu wetu huko Gaza, Ukingo wa Magharibi, na sasa nchini Lebanon.

Kadhalika, maandamano yaliyoshuhudiwa katika barabara za Ulaya na Marekani kupinga mauaji ya halaiki na vitendo vya kutisha vya mauaji na ukatili vinavyofanywa na umbile la Kiyahudi kwa dhulma na kiburi, ambavyo havizuiliwi na hata mahakama ya kimataifa au azimio la Baraza la Usalama, wala kuathiriwa na ususiaji, wala kuzuiwa na tishio au shutuma.

Imedhihirika wazi kwamba Umma, pamoja na maandamano, mikusanyiko, sherehe na hotuba zake zote, haujainusuru Gaza hata kidogo, na haujamzuia dhalimu kusitisha uvamizi wake na kurudi nyuma kutoka kwa nia yake ya kuharibu, kuhamisha, kuua na kufukuza. Mwaka mzima sasa umepita, na hakuna hata siku moja imepita bila maandamano au sherehe. Ajabu ni kwamba ushahidi wote huu haujawazuia wanazuoni wa Kiislamu duniani kufanya kongamano la aina hiyo na kuchukua hatua hiyo kwa uratibu na Jumuiya ya Wanazuoni wa Kipalestina, yenye lengo angavu na linalong'aa, bali ni lengo lisilo wazi na lisilokuwa na njia ya kufikia, ambayo ni “kuunganisha juhudi za Kiislamu kuinusuru kadhia ya Palestina”! Kinachofanya mambo kuwa mabaya zaidi ni kwamba bado wanaswali na kuomba nusra ya kimada na kimaadili kwa wananchi wa Palestina. Hotuba zao hazijakosa aina za kukashifu mateso ambayo watu wa Palestina huko Gaza wamekuwa wakiyapata kwa takriban mwaka mmoja. Baadhi yao wamesubutu katika hotuba zao kuangazia haja ya kuendeleza mapambano dhidi ya uvamizi huo, na baadhi yao wamesisitiza umuhimu wa kupanua duara la uungaji mkono na upinzani!

Enyi Wanazuoni Watukufu: Ikiwa udhaifu uliowasibu watu umetokana na ujinga wao na umewatupa katika dimbwi la mapenzi kwa Dunia hii na chuki ya kifo, pamoja na hayo, baadhi yao wamejitokeza na kudhihirisha, kupinga, kunyanyua sauti zao na kuonyesha mshikamano wao. Labda hili ndilo kubwa zaidi ambalo watu wengine wanaweza kufanya kutoka kwa wafanyikazi, waajiriwa, wahandisi, madaktari, kina mama wa nyumbani na kina mama. Hali hii waliyofikia ni matokeo ya sera ya kuziba midomo iliyotanguliwa na sera ya kuwaweka watu kwenye ujinga, ikiambatana na sera ya kuwaweka gizani na sintofahamu. Matokeo yake, hofu na udhaifu umetanda miongoni mwa watu, hivyo huwaoni wakichukua hatua zinazohitajika na zenye ushawishi katika jamii na katika ngazi ya kimataifa.

Hapana shaka kwamba kazi hii yenye taathira imekabidhiwa kwa wanachuoni na mafaqihi. Ni wajibu wa kuongeza ufahamu juu ya jinsi ya kuchukua hatua yenye ushawishi inayoleta matokeo yanayotarajiwa, ambayo ni kubadilisha hali, kusaidia wanyonge, na kuondoa dhuluma kutoka kwa wanyonge. Imeshangaza kwamba tamasha lenu la kejeli halikwenda zaidi ya kile kinachojulikana kuhusu umuhimu wa kuinusuru na kuisaidia Gaza. Ilistaajabisha kuwa tamasha hilo lilijikita katika shughuli za kimaadili zisizo na manufaa yoyote na matakwa yasiyo na umuhimu, na kauli za kukashifu na kulaaniwa zimekataliwa kwani watu wameshazoea kuzisikia kutoka kwa tawala za kifisadi!

Enyi Wanazuoni watukufu: Nyinyi ndio warithi wa Mitume. Umma unawategemea nyinyi na unatarajia vitendo kutoka kwenu, sio maneno tu, na kwamba muuongoze kwenye haki na muuhuishe kwa yale aliyokupeni Mwenyezi Mungu katika elimu na ufahamu, na hofu na ucha Mungu. Ni juu yenu kusema ukweli, bila kuogopa lawama ya mwenye kulaumu au dhulma ya dhalimu. Mnajua kwamba faradhi kutoka kwa Mwenyezi Mungu ya jihad si faradhi kwa watu wa Gaza, Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan, au Lebanon pekee; bali ni faradhi juu ya Ummah mzima wa Kiislamu mpaka faradhi hii ya kutoshelezana itimizwe, na kwamba Ummah ni wenye dhambi kwa ukamilifu wake - isipokuwa kwa wale wanaofanya kazi nzito – na nyinyi mnabeba mzigo mkubwa na jukumu. Basi, msiwe kama yule ambaye Mwenyezi Mungu alimpa Aya zake kisha akazitelekeza, wala msiwe kama wale waliokabidhiwa Taurat lakini hawakuibeba! Msisahau kuwa Mwenyezi Mungu atakuulizeni juu ya elimu aliyokupeni huku mukisoma maneno ya Mwenyezi Mungu (swt):

[وَقِفُوهُمْ إِنَّهُم مَّسْئُولُونَ]

“Na wasimamisheni. Hakika hao watasailiwa.” [As-Saffat: 24]

Enyi, Wanazuoni, mlipaswa:

- Kueleza ni nani alikuwa sababu ya kukaliwa kwa mabavu Palestina na kuhamishwa watu wake, na kufichua ushirikiano wa mashirika ya kimataifa na Umoja wa Mataifa katika kuendeleza uvamizi huo, na kwamba hakuna manufaa yanayotarajiwa kutokana na kushughulikia suala hilo ili kuondoa dhulma kutoka kwa watu wa Gaza.

- Kuwafichua watawala wa Waislamu na walaji njama na washirika wengine, na kuwadhihirishia Ummah khiyana na njama zao, na hata furaha yao kwa ushindi wa Mayahudi na kuangamiza kwao Mujahidina.

- Mueleze Ummah kwamba harakati yenye ufanisi ndiyo inayopelekea kubadili hali ya kisiasa, kuwang'oa watawala, na kuuunganisha Ummah katika umoja wa kisiasa wenye kurejesha izza yake, sio tu umoja wa juhudi za kunusuru kadhia ya Palestina.

- Kuwa viongozi wa Ummah katika kukabiliana na madhalimu wanaounga mkono umbile la Kiyahudi na wale walioufunga pingu Ummah, wakauziba midomo yake, na kulazimisha juu yake udhalilifu na kujisalimisha, ili Ummah uinuke pamoja nanyi na umuonyeshe Mwenyezi Mungu yale yanayomridhisha, na una hamu na unatamani hilo.

- Kutangaza Jihad, na wala msiridhike na tamko hilo mpaka muianze na majeshi mashujaa ya Waislamu, na wala msiridhike kuwaita vijana kwa ajili ya Jihad kama mnavyofanya, kwani vijana wamejitayarisha lakini hawana vifaa, na majeshi yaliyowekwa katika kambi yanastahili zaidi hotuba yenu kwa sababu yamefunzwa na yako tayari, na hapana shaka kwamba wengi wao wako tayari kimwili, kiroho, kimada na kimaadili kwa ajili ya muhanga na ukombozi. Lakini kikwazo ni utawala mbovu wanaoutii, ambao unawazuia kusonga, hivyo ilikuwa ni wajibu juu yenu kuwatanguliza mbele ya majukumu yao na kuwataka nusrah (msaada wa kimada) yao.

- Mnalo funzo, enyi wanazuoni, katika mwanachuoni mtukufu Al-Izz bin Abdul Salam na Imam mwema Ahmad bin Hanbal, na wanazuoni wengine wa Mujahidina Waislamu ambao hawakunyamazia dhulma na ufisadi, na wakapambana katika njia ya Mwenyezi Mungu kwa mapambano ya haki, na mnasoma wasifu zao na kujua fadhila zao katika kuunusuru Uislamu na kuwa mshindi kwa Waislamu.

Na tunakukumbusheni yale asemayo Mola Mlezi Mtukufu katika Surat Al-Saf:

[إِنَّ اللهَ يُحِبُّ الَّذِينَ يُقَاتِلُونَ فِي سَبِيلِهِ صَفّاً كَأَنَّهُم بُنْيَانٌ مَّرْصُوصٌ]

“Kwa hakika Mwenyezi Mungu anawapenda wanao pigana katika Njia yake kwa safu kama jengo lilio kamatana.” [As-Saf: 4].

Afisi Kuu ya Habari
ya Hizb ut Tahrir

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari
Address & Website
Al-Mazraa P.O. Box. 14-5010 Beirut- Lebanon
Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43
www.domainnomeaning.com
Fax: Telefax
E-Mail: media (at) domainnomeaning.com

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu