Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari
H. 18 Rabi' I 1446 | Na: H 1446 / 027 |
M. Jumamosi, 21 Septemba 2024 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Sura Mpya katika Kampeni ya Marekani ya Kulazimisha Utawala wa Umbile la Kiyahudi juu ya Ardhi za Waislamu
(Imetafsiriwa)
Katika mfululizo wa operesheni za siri za hali ya juu wiki hii, maelfu ya wanachama wa Hezbollah nchini Lebanon walilengwa katika kile kinachoaminika kuwa shambulizi la kijasusi linaoongozwa na Mossad, kuashiria awamu mpya katika vita vya Kiyahudi. Jumanne iliyopita, milipuko ilitikisa eneo hilo wakati maelfu ya vifaa vya pagers vya wanachama wa Hezbollah vililipuka, ikifuatiwa na wimbi la pili la milipuko ambayo ilisambaratisha mamia ya wabebaji wa vifaa vya walkie-talkie mnamo siku ya Jumatano. Mashambulizi hayo yalisababisha vifo vya watu 12 na wengine zaidi ya 2,000 kujeruhiwa na milipuko ya pager, wakati milipuko ya walkie-talkie iliua watu 20 na kujeruhi takriban 450.
Umbile la Kiyahudi limekaa kimya kuhusu mashambulizi haya, na halijatoa maoni rasmi juu yake, lakini tangazo la Waziri wake wa Ulinzi Yoav Galant la “awamu mpya katika vita” mnamo Jumatano linaonyesha mabadiliko ya kimkakati katika msimamo wake wa kijeshi, mabadiliko ambayo yanalenga kulemaza uwezo wa kijeshi wa chama cha Iran na kulinda mpaka wa kaskazini wa mpaka wake na Lebanon.
Baada ya umbile la Kiyahudi kukaribia kumaliza operesheni zake za kinyama huko Gaza na Ukingo wa Magharibi, kwa ushirikiano wa mamlaka na nchi mbalimbali za ndani, kikanda na kimataifa, sasa ni zamu ya Lebanon na upinzani. Chama cha Lebanon cha Iran daima kimekuwa tishio kwa usalama wa umbile la Kiyahudi huko kaskazini. Kwa kulenga vifaa vya mawasiliano vinavyotumiwa na wanachama wake, inaonekana kwamba umbile la Kiyahudi kinalenga katika kufilisi na kubomoa miundombinu ya uongozi wake na kuchukua udhibiti juu yake. Mtazamo huu wa kistratejia katika mfumo wake wa mawasiliano unaweza kuwa utangulizi wa operesheni za kina zaidi zinazolenga kudhoofisha uwezo wake wa kuanzisha mashambulizi au kuratibu pamoja na mawakala wa Iran katika eneo, ili umbile la Kiyahudi liwe mamlaka pekee katika eneo hilo bila upinzani au matatizo yoyote.
Lengo la umbile la Kiyahudi liko wazi: kudhoofisha uwezo wa chama cha Iran katika kuendesha vita na kuweka mazingira salama ili kuwezesha kuregea kwa Mayahudi zaidi ya milioni moja waliokimbia kutoka kaskazini na wale waliokimbia kutoka kwa umbile hilo, kutokana na mzozo unaoendelea. Usahihi na ukubwa wa mashambulizi haya unaonyesha kuwa umbile la Kiyahudi kuna uwezekano linajiandaa kwa ajili ya kampeni iliyopanuliwa ya kijeshi inayolenga kupunguza vitisho kwenye mpaka wake wa kaskazini.
Kutokana na njama na ushirikiano wa kijasusi wa nchi za Magharibi, ukubwa na utata wa kiufundi wa operesheni hii unaonyesha kuwa umbile la Kiyahudi halikuitekeleza peke yake, ingawa Mossad ina historia ndefu ya operesheni chafu za kijasusi ambazo imezifanya. Ulipuaji huo mkubwa wa vifaa vya mawasiliano unaashiria kuhusika kwa mashirika ya kijasusi ya nchi za Magharibi, hasa katika kutoa ujuzi wa kiteknolojia unaohitajika kutekeleza operesheni hiyo. Kuunganishwa kwa teknolojia hiyo tata katika mifumo ya mawasiliano ya chama hicho cha Iran pia kunaonyesha kuwa vifaa vinavyotolewa au kuuzwa na nchi za Magharibi ama vimechakachuliwa au kudukuliwa. Kutokana na upuuzi wa majibu ambayo umbile la Kiyahudi limezoea kupata kutoka kwa Iran na chama chake baada ya kila uhalifu linaowafanyia, imesubutu kufanya zaidi ya uhalifu huo.
Ama kuhusu mkuu wa nyoka huyo, Marekani, imehusika katika udukuzi kama huo wa teknolojia ya kijeshi katika nchi za Kiislamu. Mnamo mwaka wa 2010, virusi vya Stuxnet, vilivyotengenezwa nayo na umbile la Kiyahudi, vililenga vituo vya nyuklia vya Iran. Wakati wa uvamizi wa Iraq wa 2003, ilibadilisha mfumo wa ulinzi wa anga wa Iraq uliotengenezwa na Ufaransa. Nchini Misri, ndege za F-16 ilizotoa zilishukiwa kuwa zilidukuliwa wakati wa mapinduzi mwaka wa 2013. Saudi Arabia pia ilishindwa kutegemea mfumo wa ulinzi wa makombora wa Patriot iliutoa, ili kuzuia mashambulizi kwenye vituo vyake vya mafuta mwaka 2019, na kuzua maswali kuhusu kiwango cha uaminifu katika teknolojia ya Magharibi.
Tukio hili ni ukumbusho mkubwa kwa kila mtu, hususan Umma wa Kiislamu na wanajeshi wake, kwamba kutegemea teknolojia ya Magharibi kunaweza kuwa upanga wenye makali pande mbili. Nchi zinazotegemea zana zinazotolewa na nchi za Magharibi kwa ajili ya miundombinu muhimu, mawasiliano, au malengo ya kijeshi zinazidi kukabiliwa na hatari ya kudukuliwa au kutumiwa dhidi yao, kama milipuko ya hivi karibuni iliyolenga chama cha Iran imeonyesha, na kwamba hujuma za hali ya juu zinaweza kutekelezwa kwa mbali, zenye athari kubwa. Funzo hapa liko wazi: Dola zinazotafuta kulinda ubwana wao haziwezi tena kuamini au kutegemea teknolojia ya Magharibi, hata ikiwa imeendelea kadiri gani. Nchi za Kiislamu, haswa, zinapaswa kuwa na wasiwasi wa kuendelea kutegemea vifaa vilivyotengenezwa na Magharibi ambavyo vinaweza kutumiwa na mashirika ya kijasusi ya kigeni. Hatari ya kupenya au udanganyifu ni ya hakika na ya kutisha.
Iwapo dola za Waislamu zingekuwa huru, zingetafuta kuunda vikundi vya teknolojia mbadala au kuwekeza katika kujenga uwezo wao wa ndani. Ikiwa zinataka kulinda mawasiliano yao ya kijeshi, miundombinu ya kijasusi, na mitandao ya kiraia, zingelazimika kuangalia zaidi ya wasambazaji bidhaa wa Magharibi ili kujilinda dhidi ya vitisho vya nje, kama vile vitisho vya mtandaoni na kijasusi. Kukuza teknolojia za ndani kunaweza kuhitaji rasilimali nyingi zaidi, lakini hutoa manufaa muhimu na yanayotarajiwa ya usalama na kujitegemea katika enzi ya kisasa, ambapo vita vya habari vimekuwa vita vinavyotegemewa zaidi kuamua matokeo ya mapigano na vita. Kwa hiyo, majeshi ya nchi za Waislamu lazima yajikomboe kutoka katika utegemezi wa Magharibi. Majeshi haya hayawezi kuvumilia kulegeza uwezo wao wa kijeshi. Shambulizi la Lebanon sio tu kuhusu chama cha Iran, bali ni kudhoofisha kwa utaratibu aina yoyote ya nguvu za kijeshi ambazo nchi za Waislamu zinaweza kuwa nazo kwa kutumia udhaifu katika teknolojia yao. Ndiyo, umefika wakati kwa majeshi ya Waislamu kujikomboa kutoka katika vikwazo vya kuitegemea Magharibi kwa namna zote.
Ili kuhakikisha uhuru na usalama wake, lazima yakatae utegemezi wa teknolojia ya kigeni na kuendeleza mifumo yake ya kijeshi na mawasiliano, yakijilinda kutokana na udanganyifu na udhibiti wa kigeni katika siku zijazo. Uchumi, jeshi na teknolojia vinavyojitegemea vinaweza tu kustawi katika hali isiyo na utegemezi kwa Amerika na washirika wake katika eneo hilo. Hili haliwezi kutokea katika kivuli cha dola zenye madhara zilizopo katika ardhi za Waislamu. Ni dola vibaraka zilizo chini ya nchi za Magharibi, na zinatawaliwa na wajinga wasio na maana (Ruwaibidha) ambao kazi yao kubwa ni kuwachunguza na kuwashambulia Waislamu. Kwa hiyo, ukombozi kutoka Magharibi na tasnia yake hauwezi kufikiriwa isipokuwa katika kivuli cha Khilafah kwa njia ya Utume. Kwa hiyo, tunatoa wito kwa wenye ikhlasi katika majeshi ya Waislamu kurekebisha hali zao, kuwapindua watawala vibaraka na kutoa Nusra (msaada wa kimada) kwa Hizb ut Tahrir ili kusimamisha Khilafah ambayo itaunda nguvu huru ya kisiasa, kiuchumi, kijeshi na kiteknolojia ili mbali na utawala wa Magharibi au uwezo wa kuipenya.
[لِمِثْلِ هَذَا فَلْيَعْمَلِ الْعَامِلُونَ]
“Kwa mfano wa haya nawatende watendao.” [As-Saffat: 61]
Afisi Kuu ya Habari
ya Hizb ut Tahrir
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Afisi Kuu ya Habari |
Address & Website Al-Mazraa P.O. Box. 14-5010 Beirut- Lebanon Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43 www.domainnomeaning.com |
Fax: Telefax E-Mail: media (at) domainnomeaning.com |