Ijumaa, 27 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/29
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari

H.  5 Safar 1443 Na: 005 / 1443 H
M.  Jumapili, 12 Septemba 2021

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Je! Kuna Nini Baada ya Miaka 20 ya Vita dhidi ya (Ugaidi)?

(Imetafsiriwa)

Miaka ishirini imepita tangu Amerika itangaze kile ilichokiita "Vita dhidi ya Ugaidi" kufuatia mashambulizi ya Septemba 11 kwenye minara ya jumba la Kituo cha Biashara cha Ulimwengu jijini New York mnamo 2001, baada ya hapo Amerika iliivamia Afghanistan na Iraq. Na hii hapa Amerika leo, ikijiondoa kutoka Afghanistan, ikiburuta mikia ya kushindwa, ikiwaacha nyuma yake wale walioiamini, wakilalamika katika uwanja wa uwanja wa ndege wa Kabul.

Miaka ishirini imepita, ulimwengu unashuhudia kwa macho yake jinsi "Vita dhidi ya Ugaidi" haikuwa chochote isipokuwa kisingizio cha uwongo cha Amerika, kusudi lake ni kuzindua kampeni ya kihistoria ya kijeshi na kisiasa kuzipiga vita nchi za Kiislamu, kuwadhalilisha watu wake, kupora rasilimali zake na kuzitawala; Au, kama vile Rais wa Amerika George W. Bush alivyoisifia pindi alipotangaza, "Kampeni ya Msalaba."

Kwa upande wa kijeshi, Amerika imezikalia moja kwa moja Afghanistan na Iraq, na kwa kisingizio cha uvamizi huu, imepeleka kambi kubwa za kijeshi katika nchi za Mashariki ya Kati na katika nchi za Kusini na Asia ya Kati. Kisha ikatumia kasi ya uwepo huu wa kijeshi, pamoja na kupenya kwake kwa mashirika mengi ya kisilaha, kwa kujilazimisha kwa kila mzozo wa kivita au mvutano unaotokea katika nchi yoyote ya eneo hili, hii ni ikiwa Amerika yenyewe haikuwa ndiyo iliyosababisha mgogoro huu kuhalalisha uingiliaji wake.

Ama kisiasa, Amerika imelazimisha serikali zote za nchi za Kiislamu kutungwa kwa sheria na marekebisho ya sera za nchi zinazokataza moja kwa moja na kuyatia hatiani mambo msingi ya sheria ya Kiislamu. Badala yake, ilishinikiza kuletwa kwa maadili zaidi ya Magharibi ndani ya nchi za Kiislamu, kwa hivyo lafdhi na fahamu za jihadi zilifutwa, na elimu ya kijinsia iliingizwa katika mitaala ya shule. Sheria za familia zilibadilishwa, na vyama vya liwati vilihalalishwa. Kwa kisingizio cha kupambana na takfir na msimamo mkali, dori ya fatwa na vikundi vya wasomi viliwekwa chini ya shinikizo kila wakati kusema kwamba Waislamu na wasiokuwa Waislamu ni sawa katika imani ...

Kisha, ili Amerika iweze kuhakikisha kuwa Waislamu hawatainuka usoni mwake na kulinda kampeni yake ya msalaba kutokana na athari ya Umma wa Kiislamu katika nchi zengine za Waislamu, na ili kufunga mlango wa huruma ya watu wengine kwa Umma wa Kiislamu, Amerika ilizishinikiza serikali za ulimwengu chini ya anwani "ima uko pamoja na sisi au uko pamoja na magaidi" ili zishiriki katika kampeni ya kuupotosha Uislamu. Ilianzisha gereza la Guantanamo, na kutoka kwake, kanda za video zilipeperushwa ili kuwadhalilisha Waislamu waliowekwa kizuizini humo, ili njia hii ya muamala iwe mfano kwa serikali zote za ulimwengu kufuata katika kuamiliana na Waislamu. Kwa hivyo iliwapiga kwayo Waislamu kote ulimwenguni kimaadili na kuwaweka kwenye kona ya tuhma, na ikawa kwa kila Muislamu authibitishie ulimwengu kuwa yeye sio gaidi mwenye msimamo mkali na sio adui wa wanadamu! Kampeni hii iliwapatia watawala wasaliti wa Waislamu idhini ya kuwanyanyasa na kuwatesa Waislamu, kwa hivyo waliwatilia mkazo makhatibu, kuvifunga vyama, na kumtia nguvuni kila kijana au msichana waliyemshuku kuunga mkono jihad dhidi ya majeshi vamizi ya Amerika, au kutaka kuhukumu kwa sheria ya Mwenyezi Mungu katika maisha yao. Wakati Amerika ilipopambana na ukali wa upinzani nchini Afghanistan na Iraq, iliwageukia wanasiasa wake, kama vile John Negroponte, ambaye aliunda sera ya "chaguo la Salvador", ambayo inategemea kuwapiganisha watu wa nchi wenyewe kwa wenyewe, na kuwaleta watu kama  Pervez Musharraf nchini Pakistan, Hamid Karzai nchini Afghanistan na Nuri al-Maliki nchini Iraq ili kutekeleza kwa niaba yake sera hizi za kishetani.

Hali ilibaki hivi mpaka mapinduzi ya Kiarabu yalipokuja, yakileta msukosuko wa matumaini ya dhati ya ukombozi kutoka kwa watawala vibaraka. Uhai wa Umma ulionekana pamoja nayo, na kila mtu aliyeyaomboleza au kutamani yafe alikuwa mrongo. Na kama ilivyo kadhia yoyote kubwa ya Umma huu, Uislamu ulijitokeza mbele, na Umma ukaanza kufikiria juu ya kutabikisha tena sheria ya Kiislamu, na ukaanza kuimba katika viwanja, "Kiongozi wetu wa milele, bwana wetu Muhammad," mpaka Khilafah ikawa ndio rai jumla miongoni mwa Waislamu, na Mapinduzi ya Kiarabu yakakaribia kugeuka kuwa mapinduzi ya Kiislamu; Magharibi ilifanya wazimu, na kiongozi wake akiwa Amerika. Mapinduzi haya, ambayo hayajawahi kushuhudiwa katika historia, yalikuwa yakitangaza kugeuzwa kwa meza kwa kila kitu ambacho Magharibi ilikijenga katika kipindi cha miongo kadhaa ya ukoloni. Amerika ilikaribia kuyafanya mapinduzi ya Kiarabu kuwa ni njama uovu, na mwanzoni ilidai kwa uwongo kuwa ilikuwa pamoja na mapinduzi hayo, kisha ikatafuta kuyabadilisha kuwa vita dhidi ya ugaidi ili kuyaua, hadi wakati Rais wa Amerika Obama aliposema kuwa nyingi ya mvi kichwa ni kwa sababu ya mikutano ya Pentagon ya mapinduzi nchini Syria! Amerika na vibaraka wake waliangamiza miji ya Umma wa Kiislam, na kuua mamilioni, na kuwaondoa mamilioni ya mamilioni, mauaji hayo yalikuwa ni habari ya kila siku, na magereza yalijaa mateso na ubakaji. Wanamapinduzi waliletewa vikosi vya kuua kutoka kote ulimwenguni, na serikali za eneo hilo zilitumiwa kufanya mapinduzi katika rubaa za kisiasa na maridhiano.

Mtazamo wa Magharibi kwa Umma wa Kiislamu ni wa kikoloni tu, na Umma huu hautaweza kukabiliana na Magharibi isipokuwa utakapoamua kuamiliana nayo kama nguvu ya kikoloni ambayo lazima ing'olewe kutoka katika nchi zetu. Pia, watawala wa Waislamu leo, ambao wanashikilia funguo za nchi mikononi mwa na kufungua milango yake kwa ukoloni; ikiwa funguo hizi za nchi hazitachukuliwa kutoka kwao, wataendelea kutudungwa kisu nyuma ya mgongo na tutalipia gharama yake kwa roho na ardhi.

Kwa hivyo tunafanya nini sasa? Jibu ni kugeuza meza juu ya ukoloni na kuondoa ushawishi wake kutoka nchi za Waislamu, na kutambua kuwa suluhisho jengine lolote ni uamuzi kwa Umma wa Kiislamu kubaki, bakuli ambalo Magharibi inalipigania! Mwenyezi Mungu (swt) asema:

﴿يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُواْ لاَ تَتَّخِذُواْ الْكَافِرِينَ أَوْلِيَاء مِن دُونِ الْمُؤْمِنِينَ أَتُرِيدُونَ أَن تَجْعَلُواْ لِلَّهِ عَلَيْكُمْ سُلْطَاناً مُّبِيناً﴾.

"Enyi mlio amini! Msiwafanye makafiri kuwa ndio marafiki badala ya Waumini. Je, mnataka Mwenyezi Mungu awe na hoja iliyo wazi juu yenu?" [Al-Nisaa: 144]

Ama kwa wale wenye uwezo wa kufanya hivyo, ni watu wenye nguvu na ulinzi ambao wana uwezo wa kuregesha utawala halisi katika nchi za Waislamu. Mwenyezi Mungu (swt) asema:

﴿وَحَرِّضِ الْمُؤْمِنِينَ عَسَى اللَّهُ أَن يَكُفَّ بَأْسَ الَّذِينَ كَفَرُواْ وَاللَّهُ أَشَدُّ بَأْساً وَأَشَدُّ تَنكِيلاً﴾

"Na wahimize Waumini. Huenda Mwenyezi Mungu akayazuia mashambulio ya walio kufuru. Na Mwenyezi Mungu ndiye Mkali zaidi wa kushambulia na Mkali zaidi wa kuadhibu." [Al-Nisaa: 84]

Ama kuhusu vipi hilo linaweza kufanywa, ni kwa kupatikana rai jumla ambayo Umma wa Kiislamu utaishinikiza kwayo watu wenye nguvu na ulinzi, kumcha Mwenyezi Mungu na kuchukua upande wa kambi ya Umma wa Kiislamu. Mwenyezi Mungu (swt) asema:

﴿وَقِفُوهُمْ إِنَّهُم مَّسْئُولُونَ﴾

"Na wasimamisheni. Hakika hao watasailiwa" [Al-Saaffat: 84]

Na hakika Hizb ut Tahrir iko pamoja nanyi na miongoni mwenu, na imejitayarisha binafsi na mashababu wake kwa ajili ya kusimamisha Khilafah Rashida ya pili kwa ya njia ya Utume, na imeweka mikononi mwenu thaqafa ya Kiislamu katika utawala na usimamiz, ambayo itaifanya Khilafah mara tu baada ya kusimamishwa kwake kuwa nambari moja inayoshindania uongozi wa ulimwengu, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu.

#أفغانستان                  Afganistan             #Afghanistan#

Mhandisi Salah Eddine Adada

Mkurugenzi wa Afisi Kuu ya Habari

ya Hizb ut Tahrir

 

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari
Address & Website
Al-Mazraa P.O. Box. 14-5010 Beirut- Lebanon
Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43
www.domainnomeaning.com
Fax: Telefax
E-Mail: media (at) domainnomeaning.com

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu