Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Tahrir al-Sham Iliamiliana Vipi na Hizb ut Tahrir eneo la Kaskazini mwa Syria?
(Imetafsiriwa)

Mwanachama wa Hayat Tahrir al-Sham, Usalama wa Umma, na bendera ya Rayah ya Hizb ut Tahrir (imehaririwa na Enab Baladi)

23/05/2023 Enab Baldi

Mivutano na vikwazo vya usalama bado viko katika miji na vijiji kadhaa kaskazini mwa Syria. Hii ni tangu uvamizi na kampeni ya ukamataji iliyoanzishwa na Vyombo vya Usalama vya Umma vinavyofanya kazi Idlib, dhidi ya wanafamilia wa Hizb ut Tahrir.

Tangu tarehe 7 Mei, kuna maandamano, usiku na mchana, na matakwa ya watu, huko Deir Hassan, Killi, Al-Sahara, Babka na Al-Atareb, wakisisitiza kuachiliwa huru kwa wafungwa katika magereza ya Hay'at Tahrir al- Sham (HTS), ambayo inadhibiti eneo hilo, huku wakikataa sera ya kukamata watu kiholela ambayo wanaitekeleza.

Wanachama wa Hizb ut-Tahrir, chama cha kisiasa cha Kiislamu ambacho hakitambui mipaka ya dola za kitaifa, huku wakitoa wito wa kuregeshwa kwa Khilafah ya Kiislamu, wanaituhumu Tahrir al-Sham kwa “kuziba midomo, ikiiga mbinu ya utawala kandamizi na kufunga mipaka.” Hii ni huku Tahrir al-Sham ikiituhumu Hizb kwa "kugawanya safu, kuwasaliti wale wanaolinda mipaka na kueneza uvumi."

"Uvamizi, Kukamata na Kushambulia"

Mnamo asubuhi ya tarehe 7 Mei, Usalama wa Umma ulizindua kampeni ya kukamata na kuvamia nyumba za wanachama wa Hizb ut-Tahrir, bila vibali rasmi au vya kisheria, kulingana na ushuhuda wa watu katika eneo hilo.

Kanda za video zilionyesha uvamizi wa vikosi vya Usalama wa Umma katika majira ya mapema wa nyumba katika kijiji cha Deir Hassan. Waliingia ndani yazo kupitia kuta. Ilisababisha wimbi la ukosoaji mkubwa, kama vitendo vya kutia woga, sambamba na sera ya serikali ya Syria.

Enab Baladi alipata ushuhuda kutoka kwa vyanzo vitatu vya shirikishi katika kijiji cha Deir Hassan. Walisema kwamba wanachama wa Usalama wa Umma walivamia nyumba hizo, “bila taarifa yoyote rasmi, na bila kujali utukufu wa nyumba na heshima.” Walitumia vifaa kuvunja ukuta unaozunguka mojawapo ya milango ya nyumba hizo.

"Wakati wa ubomoaji huo na majaribio ya kuwazuia askari, mkono wa mwanamke mmoja ulijeruhiwa, na mwanamke mwengine alipoteza mimba, pamoja na hali ya kuogofya na hofu iliyotokea katika kijiji," vyanzo viliongeza.

Ukamataji ulilenga watu 18 katika kijiji hicho. Wengi wao ni wanachama wa Hizb ut Tahrir. Usalama wa Umma uliwakamata watoto wawili walio chini ya umri wa miaka 18 (miongoni mwa walioorodheshwa).

Ufyatuaji Risasi

Hali iliendelea kuwa ya wasiwasi hadi saa 12:00 jioni siku hiyo, wakati wakazi wapatao 150 walikusanyika kutoa taarifa, kupitia kanda ya video, kulaani kukamatwa kwa watu hao.

Vyanzo hivyo vilieleza kuwa mkusanyiko huo ulitawanyika. Takriban watu 15 walikusanyika katika nyumba ya mkuu wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Syria, Ahmed Abdel-Wahhab, ili kuzifariji familia za waliokamatwa. Watu wa kijiji hicho walishangaa pindi magari hayo ya Usalama wa Umma yalipoingia yakiwa na askari 30 hadi 40.

Askari hao walianza kufyatua risasi nyingi hewani huku kukiwa na hofu kubwa ambayo watu walijikuta ndani yake. Kijana mmoja kijijini hapo alijeruhiwa mguuni. Watu wakatoka kuelekea uwanja wa kijiji. Kulikuwa na mkanyagano na kurushiana mawe, kati yao na askari hao.

Vyanzo vilieleza kuwa watu hawakubeba silaha yoyote. Walikanusha kile kilichosemwa kuhusu Usalama wa Umma kufanya shambulizi. Walakini, kutoka kwa kikundi cha watu 15 kutoka kwa nyumba hiyo kuliashiria hilo.

Vyanzo vilisema kuwa watu walishiriki katika kuwahamisha askari wawili wa Usalama waliojeruhiwa kwa risasi na kuwapeleka hospitali. Hii ni huku kukiwa na uvumi kutoka kwa vyanzo hivyo kwamba ufyatuaji risasi wa askari ulikuwa wa kirafiki.

Wanaharakati na kurasa za mitandao ya kijamii zilisambaza video ya gari la Usalama wa Umma likiwa na mwanachama aliyejeruhiwa, ambaye inasemekana aliuawa. Usalama wa Umma ulisema kuwa mwanachama mmoja aliuawa na wawili walijeruhiwa.

12 Walikamatwa

Vyanzo hivyo vilieleza kuwa baada ya majeruhi hao kuhamishwa wananchi walishangazwa na askari wa Usalama wa Umma kuingia kijijini hapo, kwani “walikamata watu kadhaa bila kutofautisha umri kati ya vijana, watoto, wazee na watu ambao hata hawakuwako wakati wa mapigano."

Siku iliyofuata, watu kadhaa walikamatwa, akiwemo fundi wa magari na mmiliki wa duka la kahawa, miongoni mwa wengine wanaofanya kazi nje ya kijiji hicho. Walikamatwa waliporudi. Makumi ya watu waliondoka kijijini kwa hofu ya kukamatwa, kulingana na vyanzo hivyo.

Kuna zaidi ya watu 40 hadi 50 ambao wanatafutwa na wako mafichoni, kwa sababu tu wao ni “jamaa za watu wanaozuiliwa.” Baada ya hapo, Usalama wa Umma uliwaachilia huru baadhi ya watu, huku watu 12 wakizuiliwa kwa sasa, nao ni:

Ahmed Mohamed Mansour.

Ahmed Mohamed Abdel Wahab.

Jihad Ahmed Mansour.

Ibrahim Ahmed Abdel-Wahhab.

Ahmed Zakaria Al-Dhalea.

Fares Zakaria Al-Dhalea.

Mtoto wa Ahmed Omar Al-Dhalea (umri wa miaka 14).

Mtoto wa Youssef Muhammad Al-Dhalea (umri wa miaka 14).

Mostafa Mohamed Al-Dhalea.

Muhammad Abdul Karim Al-Dhalea.

Hossam Mohamed Al-Zayyat.

Shady Fawzy Abdel Raouf.

Uvamizi na Ukandamizi wa Nyumba

Vyanzo hivyo vilimueleza Enab Baladi kwamba Usalama wa Umma walikamata nyumba saba, na kuzigeuza kuwa makao makuu ya kijeshi. Nyumba hizo ni za:

Ahmed Mohamed Omar Mansour.

Mustafa Najjar.

Muhammad Mustafa Al-Dhalea.

Omar Mohammed Mansour.

Mostafa Mohamed Al-Dhalea.

Ahmed Abdel Wahhab, almaarufu “al-Mukhtaar.”

Jihad Mansour.

Mawakala wa Usalama wa Umma walikamata mtambo wa kuchuja maji na kiwanda cha Tasnim, kinachomilikiwa na Jihad Mansour. Kiwanda hicho kiligeuzwa kuwa makao makuu. Kiwanda hicho kilivunjwa na vichungio vilichukuliwa, kulingana na ushuhuda wa vyanzo.

Enab Baladi alipata ushuhuda wa ndani kutoka kwa watu watano huko Deir Hassan, ambao walisema kuwa Usalama wa Umma umeweka vituo kadhaa vya ukaguzi katika barabara za kijiji na nje yake kidogo. Hii huku kukiwa na hali ya mateso katika kijiji hicho, ikidhihirika kama uvamizi wa majumba, kwa kisingizio cha kuwasaka watu wanaotafutwa.

“Tunaishi katika hali ya hofu. Unahisi kuwa nyuma ya kila jiwe kuna mtu wa usalama. Kila baada ya saa tano hadi sita, kunakuwa na kampeni ya uvamizi wa nyumba maalum,” alisema mmoja wa wakaazi wa eneo hilo.

Familia za watu waliokamatwa, na wale ambao nyumba zao zilitekwa, wamehamia nyumba za jamaa zao tangu Mei 7.

Matakwa ya mkaazi yanaendelea kuwawajibisha wavamizi kwa kukiuka heshima na utukufu wa majumba.

Enab Baladi aliwasiliana na afisi ya habari ya Vyombo vya Usalama wa Umma. Aliomba ufafanuzi kuhusu kuchukuliwa kwa majumba na kubadilishwa kwao kuwa makao makuu ya jeshi, na hali ya vizuizi vilivyowekwa na Vyombo hivyo kwenye kijiji hicho. Hata hivyo, hakupokea majibu, hadi wakati wa kuandaa ripoti hii.

Upingaji Ushawishi

Mjumbe wa Baraza la Shura la Deir Hassan (Enab Baladi anakataa kutaja jina lake kwa sababu za kiusalama) alisema katika kijiji hicho kuna baraza la Shura. Linajumuisha watu wenye ushawishi na mashuhuri tangu 2016. Walijitenga, bila kujali chama au kikundi chochote, kutoka kwa kila mtu. Walikataa mapigano yoyote ya ndani na hawakumdhuru mujahid yeyote.

Aliongeza kuwa kupaza sauti katika kijiji hicho miaka iliyopita kuliifanya Tahrir al-Sham kuwachukia watu wake na kuwavamia, bila kujali mafungamano ya chama yoyote. Alitaja kwamba wanachama wa Hizb ut Tahrir hapo awali walitoa wito kwa Hayat at-Tahrir kutaja watu, au hata kutoka Hizb, ambao wamewadhuru au kuwasaliti mujahidina au walitoa wito wa mapigano ya kindani. Hata hivyo, hawakuweza.

Aliongeza kuwa suala la mujahidina na kujitolea mhanga limekuwa "gingi" linalotumiwa na Tahrir al-Sham kukihangaisha chama chochote, kikundi au ushawishi. Alibainisha kwamba Hizb ut Tahrir haijazaliwa leo, wala haitokani na Mapinduzi. Hata hivyo, “tuhuma zimetayarishwa.”

Aliashiria kwamba wanachama wa Hizb ut Tahrir na watu wenye ushawishi wamekamatwa hapo awali, na makundi kadhaa, ima kutoka katika vuguvugu la Nour al-Din Zinki, kwa kisingizio cha kuwa "al-Nusra" na kinyume chake. Vyama hivi vinavitupia tuhma kwa sababu haviendani na mradi na sera za kikundi chochote.

Hizb ut Tahrir inajieleza kuwa ni “chama cha kisiasa kilichoasisiwa mwaka 1953. Mfumo wake ni Uislamu na kazi yake ni ya kisiasa. Inafanya kazi kurudisha mfumo kamili wa maisha wa Kiislamu na kuibeba Dawah duniani.” Shughuli yake haijajikita katika nchi maalum. Haitambui dola ya kitaifa. Hizb inauchukulia ulimwengu mzima kama mahali pafaapo kwa Dawah ya Kiislamu. Hizb haina mrengo wenye silaha.

Chanzo: https://www.enabbaladi.net/archives/642913

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu