Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Enyi Majeshi ya Waislamu, Je Hakuna Muongofu Miongoni Mwenu?
Gaza, Al-Quds na Palestina Nzima Zinateketea kwa Moto wa Mayahudi Ilhali Mumekaa Kimya!
(Imetafsiriwa)

Mayahudi makatili wanaeneza mashambulizi yao ya kinyama katika maeneo yote ya Palestina, haswa Masra (eneo la Isra') ya Mtume (saw) na Gaza ya kishujaa, na kuchoma moto mawe na miti, na kumwaga damu, na waliojeruhiwa miongoni mwa watu wa Palestina wanazidi kuongezeka.  Na watawala katika nchi za Kiislamu na mfano wao wanahesabu tu mashahidi na waliojeruhiwa! Na wanalaani na kupinga kwa matamshi wanayoyatoa kwa uoga ili wasiondoke kwenye duara la kero isiyowezekana la umbile la Kiyahudi ... na haya yote yanatokea wakati majeshi yapo kimya kwa kutii viongozi wao na wamesahau au wanajifanya kusahau maneno ya Mwenyezi Mungu (swt):

]وَقَالُوا رَبَّنَا إِنَّا أَطَعْنَا سَادَتَنَا وَكُبَرَاءَنَا فَأَضَلُّونَا السَّبِيلَا]

“Na watasema: Mola wetu Mlezi! Hakika sisi tuliwat'ii bwana zetu na wakubwa wetu; nao ndio walio tupoteza njia.” [Al-Ahzab: 67]. Na maneno ya Mwenyezi Mungu:

[إِذْ تَبَرَّأَ الَّذِينَ اتُّبِعُوا مِنَ الَّذِينَ اتَّبَعُوا وَرَأَوُا الْعَذَابَ وَتَقَطَّعَتْ بِهِمُ الْأَسْبَابُ]

“Walio fuatwa watakapo wakataa wale walio wafuata, na hali ya kuwa wamekwisha iona adhabu; na yatakatika mafungamano yao.” [Al-Baqara: 166].

Enyi Majeshi ya Waislamu: Je! Hakuna muongofu miongoni mwenu? Je! Damu haichemki ndani ya mishipa yenu mnapotazama na kusikia unyanyasaji wa kinyama wa Mayahudi kwenye Ardhi Iliyobarikiwa? Je! Vipi mko upande wa watawala waovu madhalimu? Je, hamtachangamka? Je! Hamuisomi Qur'ani Tukufu na mkagundua kuwa kuwa upande wa dhulma ni jambo kubwa, lenye adhabu kubwa?

]وَلَا تَرْكَنُوا إِلَى الَّذِينَ ظَلَمُوا فَتَمَسَّكُمُ النَّارُ وَمَا لَكُمْ مِنْ دُونِ اللَّهِ مِنْ أَوْلِيَاءَ ثُمَّ لَا تُنْصَرُونَ]

“Wala msiwategemee wanao dhulumu, usije ukakuguseni Moto. Wala nyinyi hamna walinzi badala ya Mwenyezi Mungu, wala tena hamtasaidiwa.” [Hud: 113].

Enyi Majeshi ya Waislamu: Je! Nyinyi mko wapi kutoka kwa ndugu zenu huko Palestina ambao wanakabiliwa na uvamizi wa Mayahudi asubuhi na jioni? mko wapi?! Kwa nini msiongoze mapigano huko Palestina na mkazanishe mikono yenu na ya watu wa Palestina ili kuliondoa umbile lililoinyakua Palestina, mzizi wa ugonjwa na chanzo cha msiba? Je! Umbile hili linawezaje kusimama kwa miguu yake mbele yenu, ilhali wao sio watu wa vita

[لَنْ يَضُرُّوكُمْ إِلَّا أَذًى وَإِنْ يُقَاتِلُوكُمْ يُوَلُّوكُمُ الْأَدْبَارَ ثُمَّ لَا يُنْصَرُونَ]

“Maadui hawatakudhuruni ila ni maudhi tu. Na wakipigana nanyi watakupeni mgongo, na tena hawatanusuriwa.” [Aal-i-Imran: 111].

Hakika mko na mafunzo kutoka kwa wale waumini waliokutangulieni ambao hawakuwathamini Mayahudi waliogawanyika vipande vipande, endapo wanaishambulia ardhi ya Uislamu na matakatifu yake,  wao ni duni zaidi kwa Mwenyezi Mungu na kwa waja wa Mwenyezi Mungu kukaa kwenye kibla cha kwanza kati ya viwili ... Wao ni duni zaidi kwa Mwenyezi Mungu na waja wa Mwenyezi Mungu kudumisha dola yao katika Ardhi Iliyobarikiwa na huku nyinyi mkiweka kambi zenu pambizoni mwa Palestina, mkitazama pasi na kuchangamka!

Enyi majeshi ya Waislamu, je! Hakuna muongofu miongoni mwenu ambaye anajua kuwa kuliondoa umbile la Kiyahudi ambalo limeinyakua Palestina kunaweza kutokea tu kupitia vita ambavyo nyinyi mtakuwa ndio mashujaa wake, na sio kuridhika na watawala wenu wakishutumu kwa uoga uadui wa Mayahudi na hali nyinyi mumekaa pasi na kuchangamka kwa kutii watawala ambao wanachunga kubakia kwa umbile la Kiyahudi hata kuliko Mayahudi wenyewe! Zisikizeni kauli zao kuhusiana na hilo, na ndege za Kiyahudi na mabomu yake yanayoipiga Gaza kushoto na kulia, vikosi vyake na wanajeshi wakizingira nyumba za Waislamu huko Sheikh Jarrah, na magenge yake yakivamia Al-Aqsa iliyolindwa na askari hao ... Sikilizeni kauli zao ili muwajue wao ni  nani na wanataka nini: rais wa Uturuki na mfalme wa Jordan wanasisitiza umuhimu wa ushirikiano ili kukomesha mashambulizi ya (Israeli) ... Rais wa Uturuki alifanya harakati kali za kidiplomasia kuishinikiza (Israeli) ... Saudi Arabia inalaani kwa maneno makali uvamizi dhidi ya Msikiti wa Al-Aqsa ... Mfalme Mtarajiwa wa Abu Dhabi anathibitisha kulaani kwake aina zote za vurugu na chuki huko Al-Qudsi ... Misri Inalaani kwa nguvu zote kushambuliwa Al-Aqsa kwa kukiuka sheria za kimataifa ... Misri yawasiliana na Hamas na Mayahudi kusitisha mapigano ... Pakistan inalaani mashambulizi (ya Israeli) ... Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu anasifu uimara wa wale waliokaa Al-Aqsa na Al-Qudsi ... Javad Zarif, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, atangaza Suluhisho pekee la haki kwa suala la Palestina ni kuipeleka kwa mapenzi ya watu wa ardhi hii na kukimbilia kura maarufu ya maoni ... Amiri wa Kuwait aelezea kulaani kwake ... Waziri wa Mambo ya nje wa Jordan ametoa wito kimataifa, pamoja na Washington, wa kutowahamisha wakaazi wa Sheikh Jarrah ... Jordan inalaani tangazo la 'Israeli' la operesheni ya kijeshi huko Gaza na tunashirikiana na ndugu zetu kuimarisha hatua ya kimataifa ... Mkutano wa dharura wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu ... Mkutano wa dharura wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu ... nk.

Hii ndio misimamo yao. Je! Kuna mtu mwenye akili timamu ambaye hatambui kuwa jibu la uhalifu wa Mayahudi ni kwa kupitia kuhamasisha tu majeshi kuliondoa umbile la Kiyahudi na kuirudisha Palestina yote katika nyumba ya Uislamu? Je! Kuna yeyote aliye na macho na ufahamu asiyetambua kwamba kumaliza uadui wa Mayahudi sio kupitia kulaani tupu au kwa kukata rufaa kwa jamii ya kimataifa, ambayo ilikuwa nyuma ya kuanzishwa kwa dola hiyo ya vamizi? Je! Suala la Palestina halijulikani mpaka suluhisho lake lihitaji kupelekwa kwa kura ya maoni maarufu? Je! Huu sio udhalilishaji na fedheha na kushindwa kwa wanajeshi kuchangamka kutoka kwenye kambi zao ndio chanzo cha fedheha duniani huu na adhabu kali kesho Akhera?

Enyi Waislamu: Wanajeshi hawa ni watoto wenu, kaka zenu, majirani zenu na marafiki zenu, na wanaishi kati yenu, na mna ushawishi juu yao ... Vipi basi wataacha kuinusuru Ardhi Iliyobarikiwa? Wanashindwaje kuinusuru Masra ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw)? Ni kupitia mikono ya wanajeshi hawa ndio huondoa fedheha ya ulimwengu huu na adhabu ya Akhera kutoka kwenu na kwao, na huo ndio ushindi mkubwa ... Kwa hivyo waamrisheni wafanye haraka kuwanusuru ndugu zao huko Palestina, na hivyo basi wamridhishe Mola wao na wawaregeshee izza yao ... Na wauvishe taji ushindi wao kwa kuwaondoa watawala waovu na kusimamisha utawala wa Uislamu, Khilafah Rashida ambao utarudisha kwa Umma kheri zake, kama Mwenyezi Mungu (swt) alivyosema:

]كُنْتُمْ خَيْرَ أُمَّةٍ أُخْرِجَتْ لِلنَّاسِ تَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَتَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنْكَرِ وَتُؤْمِنُونَ بِاللَّهِ]

“Nyinyi mmekuwa bora ya umma walio tolewa watu, kwa kuwa mnaamrisha mema na mnakataza maovu, na mnamuamini Mwenyezi Mungu.” [Aal-i-Imran: 110].

Kwa hivyo, maadui wa Mwenyezi Mungu watakuwa madhalili na wanyonge mbele yetu, sio Wayahudi pekee, watakaopatwa na idhlali na shida, lakini pia watawala wote waovu wa dunia ambao wanafanya ufisadi katika ardhi, kwa hivyo Uislamu na Waislamu wanatapata izza na wema kuenea katika sehemu zote za dunia, na hakika hili litakuwa kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Ahmad amepokea katika Musnad yake kutoka kwa Salim bin Amir ambaye alisema: Nilimsikia Al-Miqdad bin Al-Aswad akisema: Nilimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) akisema:

«لَا يَبْقَى عَلَى ظَهْرِ الْأَرْضِ بَيْتُ مَدَرٍ وَلَا وَبَرٍ إِلَّا أَدْخَلَهُ اللَّهُ كَلِمَةَ الْإِسْلَامِ بِعِزِّ عَزِيزٍ أَوْ ذُلِّ ذَلِيلٍ إِمَّا يُعِزُّهُمْ اللَّهُ عَزَّ وَجَلَّ فَيَجْعَلُهُمْ مِنْ أَهْلِهَا أَوْ يُذِلُّهُمْ فَيَدِينُونَ لَهَا»

“Katika mgongo wa ardhi hakutabakia nyumba ya udongo wala ya manyoa isipokuwa Mwenyezi Mungu atauingiza Uislamu kwa izza na nguvu au kwa udhalilifu, ima Mwenyezi Mungu 'Azza wa Jalla atawapa izza na kuwajaalia kuwa Waislamu au atawadhalilisha kwa ajili yake.”

 #الأقصى_يستصرخ_الجيوش

#Aqsa_calls_armies

#AqsaCallsArmies

H. 29 Ramadan 1442
M. : Jumanne, 11 Mei 2021

Hizb-ut-Tahrir

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu