Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Jibu la Swali
Maandamano Makali Nchini Algeria

(Imetafsiriwa)

Swali

Habari za Sky News zilichapisha mnamo 17/3/2019 chini ya anwani (Ndani ya masiku … Maandamano ya Algeria Yamegonga “Mshipa wa Uchungu” wa Utawala Huo) yafuatayo: (Kinara wa muungano huru mkubwa zaidi nchini Algeria alisema kuwa alichukua hatua za kisheria ili kutekeleza mgomo mkubwa katika sekta za Kawi, ikiwemo mafuta na gesi, katika siku chache zijazo …) Bouteflika mnamo 11/3/2019 aliondoa ugombezi wake, bali kufutilia mbali tarehe ya uchaguzi uliopangwa kufanyika Aprili 18, na kutangaza mradi wa kongamano ili kuamua tarehe ya uchaguzi huo. Lakini watu wakakataa hili na kuliona kama urefushaji wa muhula wake wa nne wa sasa, na kujitokeza kwa mamilioni mnamo Ijumaa 15/3/2019, mkutano mkubwa zaidi tangu maandamano hayo yaanze mnamo 22/2/2019. Swali au maswali ni: Je, maandamano haya makali, hususan ikiwa mgomo wa mafuta utatokea, yameundwa kindani au kuna vidole vya kimataifa nyuma yake? Je, yataleta mabadiliko katika mandhari ya kisiasa nchini Algeria? Je, Bouteflika, licha ya maandamano haya, ataendelea kutawala mwaka mwengine tena kama yalivyo maamuzi yake ya hivi karibuni? 

Jibu

Mkondo wa matukio, vidole vya kimataifa na mengineyo yaweza kutathminiwa ili kufikia majibu ya maswali haya kama ifuatavyo:

1- Inaonekana kana kwamba maandamano haya yalikuwa ya kawaida na ya ghafla kwa watu kwa sababu ya dhulma walizofanyiwa na ufisadi wa utawala huo, serikali na wale wanaoiendesha, na ufujaji wa mali ya umma, huku ikiwaacha watu kuteseka kutokana na umasikini na ufukara. Hali zao za kimaisha zimekuwa mbaya zaidi na matatizo yao kuongezeka katika viwango tofauti tofauti. Bouteflika alikiuka mipaka katika utawala wake hadi alipo badilisha Katiba mnamo 2008 na kuliondoa sharti la kudhibiti vipindi vya raisi kuwa viwili pekee, ambapo ilimwezesha kuchukua mamlaka mara nne mfululizo, na alikuwa anatazamia kipindi cha tano licha ya kudhoofika afya yake baada ya kupata kiharusi cha ubongo mnamo 2013 kilichomfanya kulemaa, ikimwathiri kutembea na kuzungumza, lakini licha ya hili, alitangaza siku ya tatu ya mwezi huu kuwa amewasilisha rasmi ugombezi wake kwa ajili ya uchaguzi. Watu walighadhabika na maandamano yakapamba moto katika sekta mbali mbali lakini yakawa ya amani.     

2- Kwa uhadaifu, Bouteflika akatuma ujumbe kwa watu mnamo 11/3/2019 akitangaza maamuzi yafuatayo: “Kwanza, hakuna nafasi ya muhula wa tano, bali kamwe sijawahi kuulizia, kwa kuwa afya yangu na umri wangu zaniruhusu pekee kutekeleza jukumu langu la mwisho kwa watu wa Algeria, ambalo ni kufanya kazi kusimamisha jamhuri mpya ambayo itakuwa ni kingo za serikali ya Algeria tunayo tamani iwe. Pili, hakutakuwa na uchaguzi wa uraisi mnamo 18/4/2019, na lengo lake ni kujibu ombi la haraka ambalo mumenifikishia kwangu. Tatu, nimeamua kufanya mabadiliko makubwa katika muundo wa serikali haraka iwezekanavyo. Nne, Muungano wa Kongamano Huru la Kitaifa utakuwa ni chombo kitakacho furahia mamlaka yote muhimu ili kutafiti na kutayarisha na kutabanni aina zote za mabadiliko ambayo yataunda misingi ya serikali mpya na uteuzi wa mwili wa uraisi unaohusisha kila mtu… na yuko makini kumaliza kipindi chake kabla ya kumalizika 2019. Tano, uchaguzi wa uraisi utaandaliwa baada ya kongamano la Umoja wa Mataifa …” (Radio Algeria, 11/3/2019). Ujumbe huu uliwakasirisha watu zaidi, huku akijaribu kuwasihi watu na kudai kuwa kamwe hakudhamiria kugombea ingawa aligombea uchaguzi huo! Watu wanaelewa kuwa Bouteflika anataka kuongeza muhula wake wa nne kupitia uhadaifu! Na kwamba aliufutilia mbali uchaguzi huo ili kuangazia ushawishi wa genge lake la wafisadi.

3- Bouteflika, chini ya shinikizo la barabarani, alitangaza kuwa angeifutilia mbali serikali ya Ahmed Ouyahia katika maamuzi yake mnamo11/3/2019 ili kuonyesha kuwa angefanya mabadiliko nchini humo na kupambana na ufisadi, kana kwamba watu wangemuidhinisha endapo ataondoa kwa uhadaifu moja ya ala zake katika ufisadi kwa ala nyengine sawa na hizo! Lakini yaonekana kama ambaye wanaujua uhadaifu huu, hivyo maandamano yao yalipamba moto mnamo Ijumaa, 15/3/2019, kufuatia maamuzi yake. Hivyo basi, maamuzi yake ya kumteua Nouruddin Badawi kama waziri mkuu, na uteuzi wa Ramtan Lamamra kama naibu waziri mkuu huku akiendelea kuishikilia Wizara ya Kigeni, hayakufua dafu. Wawili hao walijaribu kuwahadaa watu kwa maamuzi ya Rais Bouteflika. Katika mkutano wa pamoja wa waandishi habari pamoja na naibu wake mnamo 14/3/2019, Noureddine Badawi alisema kuwa “kipindi cha mpito hakitazidi mwaka mmoja, na kuwa uakhirishaji wa uchaguzi wa urais ni kuitikia matakwa ya watu, na mashauriano yanaendelea ili kuunda serikali ambayo itakuwa ni serikali ya ujuzi. Alitoa wito wa kuasisiwa dola mpya ya kisheria, na kutoa wito kwa upinzani kushiriki” (Algerian TV 14/3/2019). Ramtan Lamamra siku moja kabla aliiambia radio ya serikali ya Algeria mnamo 13/3/2019: “Kuna haja ya mazungumzo, kipaumbele chetu ni kuwaunganisha Waalgeria. Serikali mpya itafuata matakwa ya watu,” lakini watu walikuwa na utambuzi na hawakudanganyika na hili. Iligeuka kuwa watu nchini Algeria wanatambua mno nukta hii. Walikataa yote haya na kusisitiza kung’atuka kwa rais. Waliwakataa Badawi na Lamamra na kuwataka wajiuzulu. Walikataa wito wa mazungumzo na kuakhirisha kujiuzulu kwa raisi na ubadilishaji sura. Kukataa huku kulikuwa wazi pindi mamilioni walipojitokeza mabarabarani na viwanjani mnamo Ijumaa, 15/3/2019. Serikali ilikuwa matatani, na ukamataji ukaanza!

4- Jeshi lilionekana kumuunga mkono Bouteflika na utawala wake. Ahmad Qaid Salih, naibu waziri wa ulinzi wa Algeria na mkuu wa majeshi anayejulikana kwa utiifu wake mkubwa kwa Bouteflika, aliwatishia waandamanaji kwa kusema (“kuna mtu anataka kuiregesha nchi hii katika miaka ya machungu na (uhasama).” Na akaahidi: “kuwa jeshi litachukua udhibiti ili kuhakikisha usalama na ustawi”, alisema: “Kuna watu ambao wanakereka kuiona Algeria kuwa salama na yenye ustawi, wanataka kuiregesha katika miaka ya machungu na (uhasama)” (Mashariki ya Kati, BBC, 5/3/2019) Mnamo Februari 26, alitishia kutumia nguvu dhidi ya waandamanaji, ambao aliwataja kuwa waliopotoka. Aliwashtumu watu wasiojulikana wanaoitisha maandamano mabarabarani, lakini Wizara ya Ulinzi ilikataa na kuviomba vyombo vyote vya habari kutochapisha vitisho vyake.

Kisha akaanza kuonyesha upole kwa watu, akasema: “Kamwe sikomi kuwa na fahari kwa utukufu wa uhusiano na uaminifu unaowafunga watu kwa jeshi lake, na kutokana na mahusiano haya mazuri, watu ni wakweli, wenye ikhlasi na wanatambua athari za yale ninayo sema.” (Sky News 13/3/2019). Inajulikana kuwa jeshi ndilo lililo na udhibiti nchini humo. Bouteflika alifaulu kuwapindua waliokuwa viongozi vibaraka wa Ufaransa na kuwaleta watiifu kwake, hivyo inaoneka kuwa jeshi na viongozi wa usalama wamekuwa watiifu kwa mrengo wa Uingereza wa Bouteflika. Tumeiona BBC mnamo 8/3/2019 ikimsifu na kumtambulisha vizuri kamanda wa Jeshi hilo, Ahmad Qaid Salih: “Wengi wanamchukulia Jenerali Ahmad Qaid Salih, ambaye tangu Septemba 2013 amekuwa naibu waziri wa ulinzi huku akibakia na wadhifa wa mkuu wa majeshi ya Algeria, kama mtu mkuu kuliani mwa Bouteflika. Imekaririwa kuwa uliokuwa uongozi wa ujasusi ukiongozwa na Madeen Jenerali Tawfeeq ulitaka kumpindua rais alipokuwa yuko Ufaransa kwa matibabu … lakini baada ya kupandishwa cheo Qaid, aliweza kuwapindua maafisa wengi wakuu wa ujasusi). Bouteflika alimuondoa Jenerali Tawfeeq kutoka katika uongozi wa chombo cha ujasusi mnamo 13/9/2015.    

5- Hivyo, maandamano yalianza ghafla lakini baada ya kuzuka kwake, vidole vya kimataifa vilijaribu kuyapatiliza na kuingilia kati kwa njia inayo tumikia maslahi yao. Kabla ya kufafanua hili, nataka kutaja baadhi ya yale tuliyochapisha mnamo 23/9/2015, ambapo tuliwasilisha uhalisia wa mzozo wa kimataifa nchini Algeria, tulisema: (“ni dola yenye nguvu iliyopinga mipango ya Amerika kwa nguvu zaidi kuliko majirani zake. Tangu mapinduzi ya Boumediene juu ya Ben Bella, aliyekuwa mfuasi wa mrengo wa Amerika pamoja na Abdul Nasir, na tangu siku hiyo, ushawishi wa Uingereza una nguvu nchini Algeria pamoja na baadhi ya athari za Kifaransa, ambazo wakati mwengine zilikuwa kali, hususan katika enzi za maraisi dhaifu… Boumediene aliendelea kutawala kuanzia 19/6/1965 hadi kifo chake mnamo 27/12/1978 … Kisha Bouteflika akawa rais tangu 1999 hadi leo, na Bouteflika angali na uhusiano wa karibu na Uingereza, na thibitisho ya hili ni ziara yake ya Uingereza mnamo 2006 kama ziara ya kwanza kwa rais wa Algeria kuwahi kuzuru Uingereza.  

Ingawa kundi la Ufaransa katika jeshi la Algeria kwa kiasi fulani lina ushawishi, wanatambua uhusiano wa Bouteflika pamoja na Uingereza. Pia wanatambua kuwa Bouteflika hakuwa na amani na sera ya Ufaransa … Huku watiifu kwa Ufaransa wakishindwa kuzuia ugombezi wake wa uraisi hadi leo! Ingawa Uingereza haikuhofia Ufaransa kwa ushawishi wake nchini Algeria kama ilivyoihofia Amerika, bali iliona kuwa kumaliza athari zao ingetilia nguvu ushawishi wake. Lakini ilifanya hili kidogo kidogo kwa sababu haiko katika mzozo na Ufaransa bali na Amerika,

Kwa hivyo mabadiliko ya hao maafisa watiifu kwa Ufaransa yalifanyika kimya kimya bila ya kutia joto mazingira kana kwamba kuna mzozo. Hata wakati Bouteflika mnamo 13/9/2015 alipo mwachisha kazi afisa mkuu aliye mtiifu kwa Ufaransa, aliyekuwa mkurugenzi wa Huduma Kuu ya Ujasusi, Mohammad Lamin, anaye julikana kama Jenerali Tawfeeq, ilifanyika pasi na athari au ushawishi wowote katika muundo wa serikali hiyo. Yaweza kusemwa kuwa Bouteflika kwa kiasi fulani alifaulu katika ufutaji kazi huu kwa usaidizi wa Uingereza kwake, ingawa jeshi lingali na nafasi kwa Ufaransa, kwa kuwa thaqafa na mafunzo ya jeshi hilo sana huwa yanatoka Ufaransa … Lakini kama tulivyosema, mzozo wa Bouteflika pamoja na jeshi ulikuwa kimya, karibu zaidi katika kukamilisha wanariadha na hauathiri kadhia msingi za serikali hiyo) Mwisho wa nukuu.  

6- Tumetaja pia katika toleo hilo: [(“Hii ni tofauti na mzozo halisi kwa Amerika na mipango yake nchini Algeria juu ya umilikaji wa siasa … Kwa mfano:

a- Baada ya Uhispania kuondoka Sahara mnamo 1976 baada ya miaka 91 ya ukoloni, Amerika ilipata fursa katika harakati ya uhuru wa Sahara ya Polisario, na kuitumia kama kisingizio cha kuingia eneo la Afrika Kaskazini, hususan Algeria … Lakini utawala nchini Algeria, “Uingereza”, ulitambua kadhia hiyo. Hivyo uliidhibiti Polisario mpakani na kuifuatilia kwa sababu ilitambua kuwa Amerika imepenya ndani yake … Licha ya Amerika kutawala juu ya misheni za Umoja wa Mataifa na wajumbe wake kwa Sahara, haikuweza kupata ushawishi nchini Algeria …  

b- Amerika imejaribu kutafuta kambi nchini Algeria kwa majeshi iliyo ya asisi chini ya kisingizio cha kupigana na ‘ugaidi’, majeshi hayo yaliitwa AFRICOM, lakini Algeria ilitakaa kwa sababu Algeria, na nyuma yake Uingereza, inafahamu kuwa kambi hii ya Kiamerika ni kwa lengo la kuingilia mambo ya Algeria. Hivyo basi, Wizara ya Kigeni ya Algeria ilisema mnamo 3/3/2007: (Kuwa Algeria haina hamu ya kuwa mwenyeji wa makao makuu ya Majeshi Maalumu ya Amerika kwa ajili ya Afrika (AFRICOM).

c- Amerika ilijaribu kuchochea vita dhidi ya ‘ugaidi’, ikipatiliza fursa ya matukio ya Mali mnamo 22/3/2012, na kulikuweko na ziara baina yake na Algeria ili kuihusisha Algeria katika ushirikiano pamoja na Amerika katika vita dhidi ya ‘ugaidi’ kwa kisingizio kuwa huenda vikafika Algeria. Lakini, Algeria ilikataa, “Uingereza ikiwa nyuma yake,” na kupinga mpango wa Amerika. Ziara ya Hillary Clinton na mkutano wake pamoja na Bouteflika mnamo 29/10/2012 ni mojawapo ya ziara kuu …)] Mwisho wa nukuu

7- Ni wazi kutoka na hilo, kuwa mahusiano ya kimataifa kati ya Uingereza na Ufaransa katika dhurufu za sasa yakaribia kuwa ya kimashindano kwa sura ya michezo mizuri. Lakini kati ya Amerika na Uingereza, yakaribia kuwa mzozo mkali wa kimataifa. Hali hii bado ingalipo. Amerika na Ufaransa zinajaribu kupatiliza fursa ya maandamano kwa matarajio kuwa kila mmoja wa vibaraka wao atapiga hatua na kuwaongoza watu na kisha kupenya ndani ya serikali na kupiku vibaraka wa Uingereza kwa mbinu zao tofauti tofauti:

- Ama kwa Amerika, imetangaza kupitia msemaji wa Wizara ya Kigeni ya Amerika Robert Palladino, mnamo 5/3/2019: (“Tunafuatilia maandamano haya yanayojiri nchini Algeria na tutaendelea kufanya hivyo,” “Tuna heshimu haki za Waalgeria za kujumuika na kutoa maoni yao kwa amani …” (BBC 6/3/2019) Haya ndio majibu ya kwanza kutoka Amerika kwa matukio ya Algeria. Hii yaonyesha kuwa Amerika inataka kuyatumia maandamano haya kwa maslahi yake.

Baada ya maamuzi ya Bouteflika ya kufutilia mbali uchaguzi, Amerika ilitangaza kupitia msemaji wa Wizara ya Kigeni ya Amerika Robert Palladino “Tunaunga mkono juhudi nchini Algeria za kuidhinisha njia mpya kwa msingi wa mazungumzo yanayo mulika matakwa ya Waalgeria wote na matarajio yao ya mustakbali wenye amani na ufanisi,” “Tuna heshimu haki za Waalgeria za kujumuika na kutoa maoni yao kwa amani,” “Tunafuatilia kwa karibu ripoti kuwa uchaguzi wa Algeria umeakhirishwa.” “Tunaunga mkono haki za Watu wa Algeria za kupiga kura katika uchaguzi huru na wa haki,” (Reuters, Al-Shorouk, Algeria 12/3/2019) Lakini msemaji huyo wa Amerika hakugusia juu ya maamuzi ya Bouteflika. Amerika imeyapuuzia; hii inatoa sura kuwa msimamo wake hauungi mkono maamuzi haya, na inapinga kufutiliwa mbali kwa uchaguzi huo.


Magazeti ya Kiamerika yanayo fuatilia maamuzi ya Bouteflika yameonekana kuwa dhidi yake na maamuzi yake. Gazeti la ‘New York Times’ liliripoti msimamo wa upinzani na kutilia shaka nia za Rais Bouteflika na kuutaja ujumbe wake kwa waandamanaji kama njama. Huku gazeti la ‘Washington Post’ likionya juu ya jaribio fiche la Rais Bouteflika la kuongeza muhula wake na kukwepa kukabidhi mamlaka na kutoa nafasi kwa mrithi wake. Hivyo, msimamo wa Amerika waonyesha kuwa haiko pamoja na Bouteflika na kwamba inayatumia maandamano haya ili kupenya na kupanua ushawishi wake nchini Algeria, kama ilivyo fanya nyuma kama ilivyo elezwa juu, na ingali inafanya juhudi kupatiliza tukio lolote linalojiri kama inavyo fanya katika kila nchi. Haifanyi hivyo kwa kuwa inawajali watu, kwa sababu imewasagasaga watu hao hao nchini Misri, Iraq, Syria, Somalia, Afghanistan na kwengineko, ima kupitia uingiliaji wa moja kwa moja au kupitia mapinduzi au kwa kuzifanya nchi washirika au vibaraka wake kuingilia kwa njia ya wakala. 

- Ama kuhusu msimamo wa Ufaransa, umekuwa ukiyumba; wakati mwengine iko pamoja na Bouteflika na wakati mwengine dhidi yake. Inajaribu kutafuta fursa ili kupenya pasi na kupambana na Uingereza. Ufaransa imefuatilia matukio nchini Algeria kwa maslahi kana kwamba ni tukio la kindani. Inajikadiria kibinafsi kama mlinzi wa zilizokuwa koloni! Wizara ya Kigeni ya Ufaransa ilitangaza mnamo 4/3/2019: “Paris imepata habari ya uamuzi wa Rais wa Algeria Abdelaziz Bouteflika kugombea katika uchaguzi wa urais uliopangiwa Aprili na inataraji kuwa upigaji kura utafanyika katika dhurufu nzuri zaidi ziwezekanavyo.” alisema pia: “uamuzi huo, lakini, umo mikononi mwa watu wa Algeria ambao ndio watakao mchagua kiongozi … na uamuzi ni wa watu wa Algeria kuhusiana na mustakbali wao.” (Reuters 4/3/2019) … Waziri wa Kigeni wa Ufaransa, Jean-Baptiste Lemoyne, aliiambia redio ya kimataifa ya Ufaransa mnamo 5/3/2019 kuwa “mamlaka za Algeria zinakaribishwa kuwaruhusu vijana kuandamana. Ufaransa imeona kuwa vijana wanajieleza kwa utulivu, waache wajieleze.” Lakini pindi Bouteflika alipotoa maamuzi yake, Raisi wa Ufaransa Macron aliwakaribisha na kusema: “Uamuzi wa Raisi wa Algeria Abdelaziz Bouteflika kujiondoa kutoka kwa ugombezi kwa muhula wa tano unafungua ukurasa mpya katika historia ya Algeria” na kutoa wito wa “kipindi cha mpito kwa muda maalum” na akasema “tutafanya kila tuwezalo kuwa pamoja na Algeria katika kipindi hiki cha mpito, kwa urafiki na heshima”. Waziri wa Kigeni wa Ufaransa, Le Drian, aliikaribisha hatua iliyo chukuliwa na Bouteflika na hatua zilizo chukuliwa kuboresha nidhamu ya kisiasa ya Algeria” (Radio Algeria 12/3/2019).

Hapa, inaonekana kuwa Ufaransa inaunga mkono vuguvugu la maandamano na wakati huo huo haitaki kumkasirisha Bouteflika na kuyakaribisha maamuzi yake! Kwa sababu imetegemeza hili kwa vitu viwili: inataka kuingilia kati kwa njia rahisi ambayo haitaukasirisha utawala huo, na pili ni kuwa haitaki ionekane kana kwamba iko upande wa Amerika dhidi ya Bouteflika. Ufaransa ni sehemu ya Ulaya; inapo hitajika endapo haitaweza kuipiku Uingereza nchini Algeria, inapendelea kuendelea kwa ushawishi wa Uingereza nchini Algeria kuliko ushawishi wa Amerika.

Ama kuhusu vyombo vya habari vya Ufaransa: runinga ya France 24 ili nukuu maoni ya magazeti ya Ufaransa: (gazeti la Ukombozi la Ufaransa lilisema: “Vijana wa Algeria wana njaa ya uadilifu wa kijamii na wanataka mabadiliko, hususan wale ambao wamemjua Rais Bouteflika pekee katika maisha yao.” na likaongeza kusema: “Vijana wa Algeria hawafahamu ni kwa nini wavumilie matokeo ya nyuma ambayo hawana uelewa nayo. Vijana hawa waliojaa nguvu na harakati wanastahiki zaidi kuliko uongozi wa kisiasa ulio lazimishiwa juu yao na serikali inayo jificha nyuma ya rais bandia. “Gazeti la kila siku la ‘Le Figaro’, liliweka kichwa kikuu cha habari cha gazeti moja kikiunga mkono maandamano hayo nchini Algeria: “Wimbi kuu dhidi ya serikali ya Algeria.” Gazeti hili lilitaja “kushiriki kwa baadhi ya viongozi wa kisiasa na vyama vya kisiasa katika maandamano hayo, kama vile Ali bin Flis, kiongozi wa Chama cha haki kuu na Rashid Nikaz mgombezi wa uchaguzi ujao, Ahmed Ben-Bitur, aliyekuwa waziri mkuu na Abdel Aziz Rahabi, Waziri wa Utamaduni, aliye jiuzulu wakati wa muhula wa kwanza wa Abdelaziz Bouteflika … (imenukuliwa kutoka kwa runinga ya France 24 mnamo 2/3/2019).

8- Ama kuhusu Uingereza, haikutoa taarifa rasmi yoyote. Shirika la habari la BBC haliyaangazii maandamano hayo, bali linayataja kwa kupita tu. Magazeti ya Uingereza hayavikashifu vitendo vya Bouteflika na hayawaungi mkono waandamanaji, jambo linaloonyesha kuwa Uingereza iko pamoja na Bouteflika.

Inamuunga mkono na haitaki aanguke. Hivyo basi, haikuwakasirisha watu kupitia vyombo vya habari na kuyatia chumvi matukio na kuyaangazia, kama ilivyo fanya katika maandamano ya Misri, Uturuki na Sudan na kuangazia harakati za upinzani na taarifa zao na viongozi wake, na haikukashifu vitendo na ukatili wa serikali ili kuzima maandamano hayo. Hili halikujitokeza nchini Algeria. Hii yathibitisha kuwa ushawishi wa kisiasa wa Uingereza nchini Algeria umetosheka na vitendo vya Bouteflika na genge lake. Uingereza kwa mujibu wa sera yake chafu inajifanya kuwa maandamano hayo hayana maana sana kwake; haionekani kuwa mstari wa mbele kutokana na sera yake chafu ya kuwamakinisha vibaraka wake!   

9- Tamati ya kutarajiwa ya maswali yaliyo ulizwa:

a- Maandamano hayo ni ya ghafla na ni ya kimaumbile na ni ya kujibu dhulma za kisiasa na kiuchumi. Bouteflika na genge lake walichukua utawala na pesa, na wakageuza Katiba kwa mujibu wa matakwa yao. Licha ya hali yake mbaya ya kiafya na kukosa uwezo wa kutembea na kuzungumza, alirefusha muhula wake wa nne, badala ya watano! Yeye na genge lake wanatuhumiwa kwa ufisadi na ufujaji wa mali, huku watu wakiteseka kutokana na ugumu wa maisha unao sababishwa na umasikini, bei za juu na ukosefu wa ajira na ukosefu wa uwezo wa kununua mahitaji msingi na muhimu. Kile wanachokiita nguvu duni ya ununuzi wa bidhaa ya watu ingawa nchi hiyo imejaa utajiri, hususan mafuta na gesi. Lakini makampuni ya kigeni yanaufuja zikishirikiana na serikali hiyo na wale waliomo ndani ya duara la Bouteflika. Na watu wanateseka na ugumu wa maisha.

b- Bouteflika anasisitiza kutoondoka kutoka katika mandhari, isipokuwa alazimishwe na kifo na jeshi linamuunga mkono na tabaka la wanasiasa wa Kiingereza vile vile. Uingereza ina ushawishi wa kisiasa na inataka kuidumisha serikali hiyo na watawala wake. Kwa kuwa serikali hiyo ni kibaraka wa Uingereza, ni muhimu sana kwake eneo la Afrika Kaskazini usoni mwa Amerika. Algeria inasimama dhidi ya Haftar kibaraka wa Amerika nchini Libya. Inafanya kazi kulidhibiti vuguvugu la Polisario linalo saidiwa na Amerika.

c- Ufaransa ina maslahi ya kikoloni nchini Algeria: kisiasa, kithaqafa na kiuchumi; hisia za ukoloni mkongwe kwa Algeria zinaendelea ili kuchochea hisia zake. Imekubaliana na Uingereza ambayo imepanua ushawishi wake wa kisiasa huko tangu mapinduzi mjini Boumediene mnamo 1965 ili kusimama dhidi ya Amerika, ambayo inashindana nao katika ukoloni na upanuzi wa ushawishi. Pia walikubaliana kusimama dhidi ya Waislamu wa nchi hiyo wanaotafuta ukombozi kutokana na udhalimu wa ukoloni wa Kimagharibi katika nchi na aina zake zote, na ambao wanahamu na Uislamu na kusimamisha dola yake na utekelezaji wake. Wengi wa watu nchini humo wanajua kuwa uadilifu, ukweli na kheri ziko katika Uislamu pekee, na hakuna uadilifu au kheri katika kitu chengine chochote. Watiifu wa Ufaransa walipanga mapinduzi mnamo 1992, wakaleta uovu na ufisadi, na kuuwa maelfu ya watu, mithili ya bwana wao Ufaransa, iliyo uwa Waalgeria milioni 1.5 katika vita vya ukombozi. Vibaraka wa Ufaransa walishiriki katika maandamano hayo na kuendesha wimbi hilo, lakini kama tulivyosema; kwa uangalifu.   

d- Amerika inafanya kazi kuingia nchini Algeria, ikitumia dhurufu za Algeria na maandamano, ikidai kuwa inasimama dhidi ya dhulma na udikteta na kuunga mkono haki ya watu, ingawa haijali dhulma, ukandamizaji wala udikteta, bali ina yafadhili haya kote ulimwenguni, na inaziunga mkono serikali za kidhalimu na za uk andamizaji, hususan katika biladi za Kiislamu na za Kiarabu. Inaiunga mkono serikali ya Salman na mwanawe nchini Saudi Arabia na serikali ya Sisi nchini Misri na serikali ya Iraq moja kwa moja, na serikali ya Syria kwa njia isiyo ya moja kwa moja kupitia washirika na vibaraka wake. Haijali kuwasaidia watu wa Algeria; badala yake, Amerika inataka kuasisi kambi nchini Algeria ya majeshi yake, US AFRICOM, ili kupanua ushawishi wake eneo la Afrika Kaskazini na hususan kuelekea kutoka huko hadi Jangwa la Sahara la Afrika Kusini na Afrika Magharibi ambako kuna ushawishi wa Ufaransa ili kuubadilisha. Amerika inakerwa na majibu ya Algeria kwa kibaraka wake, Haftar, anayetaka kuidhibiti Libya magharibi, ikiongezewa na matarajio yake ya kuudhibiti utajiri wa Algeria.   

e- Watu wa Algeria wana utambuzi wa yale yanayojiri, kutokana na nyimbo zake: “Sio Washington, wala Paris, sisi ndio tunaochagua rais”, zinazo onyesha kuwa watu wanatambua uingiliaji kati wa kigeni na malengo yao, na wana utambuzi wa hayo. Watu wana ujuzi na vibaraka na uhalifu wao na wanafahamu dori ya nchi za kikoloni na usaidizi wao kwa serikali na vibaraka wafisadi. Watu wanatafuta mabadiliko kwa umakinifu mkubwa na wanasubiri kwa hamu kurudi kwa Uislamu. Wale waliosema tutaurudisha Uislamu mamlakani mnamo 1991 walichaguliwa kwa asilimia 84 ya kura. Kuibuka kwa hisia za Kiislamu kulikuwa wazi kupitia kuanzisha maandamano kuanzia misikitini baada ya swala za Ijumaa. Masekula wanaoshiriki maandamano hayo walitambua hili pindi walipoona kufurika kwa Waislamu misikitini kuswali.

f- Ama kuhusu yale yanayo tarajiwa kama natija ya vuguvugu hili, tabaka kaimu la kisiasa nchini Algeria linalo dhibiti vituo vya uchukuaji maamuzi ni tiifu kwa Uingereza. Vibaraka wa Ufaransa wamedhoofika na kupungua kiidadi. Bouteflika, wakati wa utawala wake uliozidi miaka ishirini, aliweza kuwaondoa wengi wao kutoka katika nyadhifa muhimu na vituo vya uchukuaji maamuzi. Lengo lao kuu wanalolitafuta kwa sasa sio kumbadilisha kibaraka wa Uingereza aliye mamlakani, bali kushiriki nao katika baadhi ya vituo visivyokuwa vikuu, na hata hilo lina tegemea jinsi gani wanavyo yatumia vizuri maandamano yaliyoko kwa sasa ili kudandia wimbi lao kupata baadhi ya uzani.

Amerika haina tabaka la kisiasa itakalo lielekea, na kama ilivyo tabia yake katika nyakati kama hizi, hufuata chaguo la jeshi ambalo sasa ni mfuasi mkubwa wa serikali.

Kwa maana nyengine, maandamano ya sasa hayatarajiwi kubadilisha utiifu wa kisiasa wa serikali hiyo kutoka kwa Uingereza hadi kwa Ufaransa au Amerika.

g- Ama kuhusu swali: Je, Bouteflika ataendelea au la, kiuhalisia kwa sasa hatawali, lakini serikali inaendeshwa na duara lake linalomzunguka ambao kama yeye ni watiifu kwa Uingereza. Haitarajiwi kuwa endapo maandamano hayo yataongezeka, hususan kwa kutarajiwa mgomo wa mafuta na gesi, kuwa Uingereza itachagua mbinu yake ya kawaida ya uovu na ujanja na uhadaifu na kumuondoa Bouteflika, ambaye rangi yake imebadilika na kuchakaa, na kuja na Bouteflika mwengine na sura mpya inayo nga’aa zaidi na aliye na ulimi mkali zaidi.   

j- Lakini yote haya hayatakhafifisha janga hili na hayataondoa ugumu wa maisha maadamu serikali hiyo iko mbali na Mwenyezi Mungu na Mtume Wake (saw) na kujisalimisha kwa nidhamu za Kimagharibi za kirasilimali, chanzo cha uovu na ufisadi. Bali suluhisho la tatizo linalo ondoa janga hili ni kuchagua sheria ya Mwenyezi Mungu (swt). Jukumu juu ya waandamanaji, na wengi wao ni Waislamu, ni kuifanya njia yao kuwa ni Uislamu na Dola ya Uislamu "الخلافة على منهاج النبوة"... “Khilafah kwa njia ya Utume”. Katika hili ndio izza ya ulimwengu huu na kesho Akhera. Itapeana maisha stahiki na kueneza uadilifu na kheri nchini. Hakutakuwepo na mateso wala shida, bali izza hapa ulimwenguni na mafanikio kesho Akhera.

(فَمَنِ اتَّبَعَ هُدَايَ فَلَا يَضِلُّ وَلَا يَشْقَى * وَمَنْ أَعْرَضَ عَنْ ذِكْرِي فَإِنَّ لَهُ مَعِيشَةً ضَنْكاً)

“... basi atakaye ufuata uongofu wangu, hatapotea wala hatataabika. Na atakaye jiepusha na mawaidha yangu, basi kwa yakini atapata maisha yenye dhiki” [TA-HA: 123-124]

 14 Rajab 1440 H
Alhamisi, 21/3/2019 M

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoAlhamisi, 02 Aprili 2020 20:56

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu