Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Jibu la Swali
Majadiliano Kati ya Amerika na Taliban
(Imetafsiriwa)

Swali:

Duru za Taliban kutoka Afghanistan zimeripoti maendeleo makubwa katika majadiliano yao ya siku sita pamoja na mjumbe wa Amerika Zalmay Khalilzad jijini Doha, na kuwa Amerika itaondoa vikosi vyake ndani ya miezi 18 baada ya makubaliano hayo kukamilishwa. Ingawa makubaliano hayo ya Doha yamebakia kuwa kielelezo tu kilicho tajwa katika taarifa huku na kule, na hayajakalifisha bado, na kwamba mzunguko mwingine wa majadiliano utafanywa mnamo 25 mwezi huu 2/2019 kama ilivyo ripotiwa na wanahabari wa Reuters mnamo 27/1/2019 … Lakini swali msingi lingali linabakia: Je, Taliban ilianguka ndani ya mtego wa Amerika baada ya miaka hii mingi ya Jihad? Je, hilo lilitokea vipi? Na je, mambo yanaelekea wapi? Jazak Allah Khair.

Jibu:

Mwanzo nataka kukukumbusha jibu la swali lililotangulia kwa anwani “Mkakati wa Amerika nchini Afghanistan” la mnamo 16/8/2017 ambalo tulionyesha kuwa Amerika na washirika wake wa Atlantiki wameshindwa kufikia ushindi wa kijeshi nchini Afghanistan, na kwamba mengi ya maeneo ya Afghan tayari yameingia chini ya udhibiti wa Taliban. Pia tulifichua kutokuwa na uwezo kwa serikali ya Afghan kupigana vita hivi vya Amerika, na kwamba inadhibiti kwa uchache mno mji mkuu na maeneo mengine. Pia tulitaja katika jibu hilo la swali kuwa Amerika – Trump anafanya marekebisho sera zake nchini Afghanistan, “Marekebisho haya yanalenga kupunga moto uwanja kivita wa Afghan, kudhibiti uwepo wa Amerika katika kambi za kijeshi na kuzitumia kunapotokea hatari, na kuonyesha misheni yake kana kwamba iko dhidi ya ISIS” … na tukaongeza: “Ili kuharakisha kuivutia Taliban ili ikubali, Amerika itarudi kutilia nguvu upya dori ya Pakistan ili kuonyesha kuwa uongozi mpya wa kijeshi nchi Pakistan uko laini zaidi na wenye huruma kwa Taliban ili kuwasukuma kuketi na kujadiliana na serikali kibaraka jijini Kabul na kugawanya mamlaka pamoja na nidhamu ya kisiasa ya Amerika nchini Afghanistan … Baada ya Amerika kutambua uchache wa machaguo yake na kufilisika kwa chaguo la India, ilichagua kujadiliana na Taliban kwa matarajio ya kuwiana kwao na serikali ya Amerika nchini Afghanistan, na imetumia vibaraka wake katika serikali ya Pakistan kuwaburuta vinara wa Taliban katika majadiliano. Licha ya hayo, majaribio yote hayo yamefeli; Amerika haikufaulu kijeshi wala kisiasa juu ya kadhia ya Afghanistan.” Mwisho wa nukuu. Lakini Amerika haikukata tamaa kufikia hili kwa kuwategemea vibaraka wake katika eneo hilo, hususan kwa kuwa Amerika inateseka nchini Afghanistan, kijeshi na kifedha, na kuikosesha usingizi … Tathmini ya mgogoro wa Amerika nchini Afghanistan unaonyesha yafuatayo: 

Kwanza: Amerika inateseka kutokana na madeni makubwa yanayotishia uchumi wake, ambao ulianikwa hadharani na mgogoro huo mnamo 2008 na unaendelea kuwa na matokeo, na kuamini kuwa imetumia rasilimali kwa vita katika Mashariki ya Kati, yaani katika biladi za Kiislamu, sawia na dolari trilioni saba na haikupata chochote kama badala, kama alivyo sema Raisi Trump katika akaunti yake ya Twitter mnamo 22/1/2017: “Baada ya kutumia kijinga trilioni $7 eneo la Mashariki ya Kati, ni wakati sasa wa kuanza kujenga upya nchi yetu!” shirika la habari la BBC lilinukuu Jarida la Amerika la Forbes likisema mnamo 9/1/2016: “Vita nchini Afghanistan vimeigharimu Amerika hadi $ 1 trilioni na $ 70 bilioni, ikiongezewa na mauwaji ya zaidi ya vikosi 2,400 vya Amerika, majeraha kwa maelfu ya watu walioa na ulemavu wa kudumu, na licha ya hasara hizi za kibinadamu na kifedha, Amerika imeshindwa kuimaliza harakati hii.”    

Pili: Baada ya Amerika kushindwa kuimaliza harakati hii kijeshi, iliona kuwa hakuna njia nyengine isipokuwa kuiburuta Taliban katika majadiliano kama chaguo la pekee la Amerika ili kuondoka katika vita vya Afghan pasi na kuonyesha kushindwa … Chaguo hili likawa ndio mkakati wa Amerika unaoshinikizwa nchini Afghanistan, linalothibitisha hili ni uteuzi wa Wizara ya Kigeni ya Amerika wa Zalmay Khalilzad mnamo 5/9/2018 kama mjumbe wake nchini Afghanistan aliye na misheni maalumu: “Wizara ya Kigeni ya Amerika imeeleza kwa mukhtasari katika taarifa ya awali kazi ya Khalilzad, ya kupangilia na kuelekeza juhudi za Amerika zinazolenga kuhakikisha uwepo wa Taliban katika meza ya majadiliano.” (Turkish Anatolia Agency, 12/1/2019) Hivyo basi, Amerika ilifuata chaguo hili la kipekee, ili kuisukuma Taliban na kuwatia shinikizo kukaa katika meza ya majadiliano. Maono haya ya Amerika ya kuondoka katika vita vya Afghan sio mageni, Amerika imejaribu kwanza kuanzisha mkondo wa majadiliano kati ya Taliban na serikali, lakini ikashindwa. Hivyo basi, majadiliano yakabadilika kuwa pamoja na Amerika, licha ya hayo ilitaka yawe baina ya Taliban na serikali ya Afghan, lakini Taliban ikakataa, kwa sababu inaitazama serikali hiyo kama kibaraka wa Amerika na baadaye kukubali kujadiliana pamoja na Amerika, ingawa ndiye muasisi wa serikali hiyo.

Tatu: Ni muhimu kuzingatia kuwa Amerika, ili kuibembeleza Taliban kuingia katika majadiliano ya amani, imeunda mazingira ya hili kwa njia yao ovu. Imetekeleza oparesheni za kindani nchini Afghanistan na katika eneo kupitia vibaraka wake na wengine wasio kuwa vibaraka pambizoni mwa Afghanistan:

1- Kuelekeza mashambulizi ya Amerika kwa viongozi wa Taliban, hususan wale waliokataa majadiliano hayo: “Maafisa wa Amerika walisema kuwa Amerika ilianzisha mashambulizi ya droni mnamo Jumamosi dhidi ya kiongozi wa Taliban kutoka Afghan Akhtar Mansour … Pentagon ilimtaja kuwa kizingiti cha amani na maridhiano kati ya serikali ya Afghan na Taliban” (Dunya Al-Watan, 22/5/2016). Hii ni kusema alikuwa amelengwa kwa kukataa majadiliano hayo, hili lilikuwa wakati wa utawala wa Obama. Amerika imeendelea na sera hiyo hiyo wakati wa utawala wa Trump. “Misheni ya usaidizi ya NATO, ilisema katika taarifa kwa vyombo vya habari mnamo Jumatano jioni: “Makamanda wawili wa Taliban waliuwawa katika mkoa wa Kapisa katika shambulizi la Amerika la kuyasaidia Majeshi Maalumu ya Usalama wa Afghan katika wilaya ya Tajab mnamo Julai 22.” (Russian Sputnik News Agency, 25/7/2018). Kulikuweko na tukio jengine ambapo kamanda mwengine wa Taliban aliuwawa: “Kanali Dave Butler, msemaji wa majeshi ya Amerika nchini Afghanistan, alisema: “Tunaweza kuthibitisha shambulizi la angani la Amerika lililotekelezwa jana, limepelekea kuuwawa kwa kiongozi wa Taliban, Mullah Manan,” akiongeza kusema: “Tunakwenda katika suluhisho la kisiasa” (CNN Arabic, 2/12/2018)

2- Iran imenyosha mkono wake kwa Taliban. Taliban inaamini kuwa Iran ilikuwa “dola hasimu kwa Amerika.” Baadhi ya viongozi wake walichagua kwenda kwake. Haikutambua kuwa kuuwawa kwa kamanda wake, Mullah Akhtar Mansour, kulitokea punde tu alipokuwa anarudi kutoka Iran, na katika mipakani mwake, pengine ilikuwa ni kwa ushirikiano kati ya Amerika na Iran, Taliban imeendelea kuiamini Iran … huku Iran ikiwa tu inaisukuma kuelekea katika suluhisho la kisiasa pamoja na Amerika: “Iran imesema kuwa wawakilishi wa Taliban wa Afghan walifanya majadiliano na maafisa wa Iran jijini Tehran mnamo Jumapili, huku Jamhuri hiyo ya Kiislamu ikitafuta kusukuma mazungumzo ya amani katika nchi hiyo jirani ili kuzuia ushawishi wa makundi mengine ya wanamgambo wa Kiislamu.” Bahram Qasimi, msemaji wa Wizara ya Kigeni alisema mnamo Jumatatu kuwa mazungumzo hayo yalifanyika kwa utambuzi wa Raisi wa Afghanistan Ashraf Ghani na yalilenga kuchora mipaka ya majadiliano hayo kati ya Taliban na serikali ya Afghan. (Euro News, 31/12/2018)

3- Qatar imefungua afisi kwa ajili ya Taliban jijini Doha, kwa hivyo Taliban ikadhani kuwa utambuzi wa Qatar kwa harakati hiyo unaipa nguvu, lakini Qatar imesema hadharani kuwa afisi hii iko wazi kwa ushirikiano na Amerika kwa ajili ya majadiliano pamoja na Taliban. Wakati wa mgogoro wake na nchi zilizoitenga, Qatar ilisema: “Taarifa za aliyekuwa mkurugenzi wa CIA David Petraus zinatosha kusema kuwa mkutano wa Taliban na Hamas jijini Doha ulikuwa kwa matakwa ya serikali ya Amerika, ambayo yenyewe inathibitisha kuwa Qatar haikufanya lolote kuficha hili, na hilo lilikuwa kwa utambuzi wa kila mmoja na wala sio nyuma ya migongo … Kuwepo kwa Hamas na Taliban jijini Doha ilikuwa ni kwa matakwa ya Amerika ili kutafuta njia kutatua kadhia ya Palestina na Taliban.” (Gazeti la Qatar la Al-Sharq, 04/07/2017) Qatar imeidanganya Taliban kuwa iko upande wake na inaiunga mkono, hivyo basi Taliban ikaanguka ndani ya mtego. Huku mgogoro ukipamba moto juu ya Qatar kutoka kwa nchi zilizoitenga, iliuomba utawala wa Trump kulipa pesa zake ili kuilinda serikali hiyo, Qatar, kibaraka wa Uingereza, iliongeza kuikabili kwake Amerika na kuisukuma Taliban katika majadiliano, kwa matarajio kuwa utawala wa Trump huenda ukakhafifisha hatari ya Saudia kutokana kwake … Hivyo basi Amerika iliifanya kadhia ya huduma yake kupitia kuisukuma Taliban katika majadiliano ya amani, na kuleta ushindani kati dola mahasimu katika Ghuba. Imarati inashindana pamoja na Qatar ili kuyaburuta majadiliano hadi jiji la Abu Dhabi na Saudi Arabia hadi Jeddah. Waandishi wa habari wa Reuters wakimnukuu kamanda wa kijeshi wa Taliban anayeshiriki katika majadiliano, aliyeomba kutotajwa jina lake lake: “Ukweli ni, tofauti kati ya Saudi Arabia na Qatar zimeharibu kikamilifu mchakato huo wa amani,” alisema, “Wasaudi wanatufinyilia pasi na haja ili tutangaze kusitisha vita …” (Gazeti la Urusi la Sputnik, 14/1/2019), na kwa taharuki hii, pamoja na mgongano wazi, pamoja na mwelekeo mmoja, majadiliano na Amerika. Vibaraka wa Amerika nchini Saudi Arabia wanashindana na vibaraka wa Uingereza nchini Imarati na Qatar ili kuitumikia Amerika na kupata ridhaa yake, lakini wakati wa mashindano haya ya batili yaliyoinasa Taliban na kuunganisha hisia zake kwa majadiliano ya Amerika na suluhisho la kisiasa ndio lengo. Uingereza haipingi Qatar kuikabili Amerika kama himaya kwa serikali ya Qatar, na Imarati imewekwa na Uingereza katika safu za mbele pamoja na vibaraka wa Amerika kwa malengo mengine.

4- Ama kuhusu Pakistan, kwa Taliban ni bawaba tu, baada ya kuitelekeza harakati hiyo na vita vikali kuanzishwa na jeshi lake dhidi ya Taliban kutoka Pakistan, Pakistan ilianza kulainisha mazingira kwa harakati hiyo na kuongeza mawasiliano nayo, kwa kuwasili kwa Imran Khan kama waziri mkuu wa Pakistan mnamo 25/7/2018, na taarifa zake zinazo onyesha ukaribu kwa Taliban, dhurufu zaidi zinaundwa ili kuongeza uaminifu wa Taliban kwake, bila ya kutambua kwamba ni mtego uliotegwa kwa ajili ya kuifanya iingie katika majadiliano ya Amerika. Hivyo basi Taliban imetumbukia kwenye mtego huo, au “imejifanya kutumbukia kwenye mtego huo” na imeng’atwa mara mbili katika shimo hilo hilo moja, shimo la serikali ambayo inatekeleza sera ya Amerika pekee: iliisaidia mnamo 1996 kwa ajili ya utawala wa Taliban kutoka Afghan, na kisha kuitelekeza mbele ya shambulizi la Bush mwana mnamo 2001 na zaidi. Hata pia ilishiriki katika shambulizi la Amerika kwa kuiandama Taliban ndani ya Pakistan … Sasa ambapo Amerika imeshindwa kuimaliza Taliban na kuamua kurudi katika majadiliano kama chaguo pekee lililopo, ili kutatua na kudumisha ushawishi wake nchini Pakistan, Islamabad ilirudi na kujenga daraja zake za zamani pamoja na Taliban, lakini ikiwa na lengo pekee la kutabikisha mkakati mpya wa Amerika na kumakinisha ushawishi wa Amerika nchini Afghanistan. Hivyo basi Taliban ilitumbukia tena katika shimo! Ingawa mambo yako wazi na hayakufichika: Waziri Mkuu wa Pakistan, Imran Khan alisema mnamo Jumatatu kuwa Raisi wa Amerika Donald Trump ameomba usaidizi wake katika mchakato wa amani ndani ya Afghanistan, habari za Geo News zilimnukuu Khan akisema kuwa yeye “amepokea barua kutoka kwa Raisi wa Amerika mapema siku hiyo, ambapo aliiomba Pakistan kucheza dori katika mazungumzo ya amani ya Afghan, na kusaidia kuileta Taliban katika meza ya majadiliano” (Shirika la habari la Urusi la Sputnik, 3/12/2018)

Na kisha Waziri Mkuu wa Pakistan atakutana katika muda wa siku mbili na mjumbe maalumu wa Amerika Khalilzad jijini Islamabad, kusisitiza maendeleo ya Pakistan katika mpango wa Amerika nchini Afghanistan, “kwa upande wake, Imran alisema kuwa “Pakistan inataka suluhisho la kisiasa kwa ajili ya amani na maridhiano nchini Afghanistan” (Masrawi 5/12/2018). Waziri Mkuu Imran Khan alisema mnamo Jumanne kuwa nchi yake itafanya iwezavyo kushajiisha mchakato wa amani ndani ya Afghan, akiongeza kuwa hivi majuzi nchi yake ilichangia katika mazungumzo kati ya Taliban na Amerika jijini Abu Dhabi. (AlYoum7 18/12/2018). Imran yeye mwenyewe alifichua katika ukurasa wake wa Twitter mnamo 19/11/2018 kuhami kwake huduma yake kwa Amerika, alisema: “Pakistan imechagua kushiriki katika vita vya Amerika juu ya ugaidi, Pakistan ilipata majeruhi elfu 75 katika vita hivi, na kupoteza zaidi ya $ 123 bilioni za uchumi wake, huku msaada wa Amerika ukiwa $ 20 bilioni pekee.” Aliyekuwa waziri wa ulinzi wa Pakistan, Khawaja Asif, pia alithibitisha khiyana ya watawala wa Pakistan, na yeye ni mmoja wao, aliandika mnamo 19/11/2018 katika akaunti yake ya Twitter: “Pakistan ingali inajitolea mhanga kwa damu kwa ajili ya Amerika, kwa sababu tunapigana vita ambavyo si vyetu, tumepoteza vima vya dini yetu ili kuioanisha na maslahi ya Amerika na kuangamiza maumbile ya amani na kuyabadilisha kwa mgawanyiko na ukosefu wa uvumilivu.” Hakuna uwazi zaidi ya hivi: Pakistan ilipigana vita ambavyo si vyake na kumwaga damu ya watoto wake Waislamu kwa ajili ya Amerika … na kupoteza vima vya dini yake ya Kiislamu ili kutumikia maslahi ya Amerika … Dori ya Pakistan nchini Afghanistan ni sawa na dori ya Uturuki na mtawala wake Erdogan nchini Syria, na huduma zake kwa Amerika ni kutia shinikizo juu ya makundi ya kijeshi na kuyalazimisha katika suluhisho la Kiamerika, licha ya Amerika kumfedhehesha mara kwa mara!

5- Hizi ni hali za ndani ya Afghanistan na harakati za kieneo za vibaraka wa Amerika na wasiokuwa vibaraka wake ambao Amerika inawatumia kuisukuma Taliban kwa nguvu katika majadiliano na suluhisho la kisiasa. Licha ya hayo, Taliban, ikiwa wanaelewa wameuwezesha ufuatiliziaji wa Amerika ili kujadiliana nayo na kiwango cha shinikizo juu ya vibaraka wake kufanya wawezavyo kwa kutumia mbinu ovu ili kuibembeleza Taliban kukubali majadiliano … ikiwa wanafahamu kina cha mateso ya Amerika kijeshi na kifedha kwa miaka 17 ya jihad yao ya kishujaa. Ikiwa wanatambua msisitizo wa Amerika juu ya majadiliano pamoja na Taliban, ingawa inawabandika majina ya magaidi, kama kawaida, kupitia kumtuhumu kila anayekataa ugaidi wao na kiburi chao kama gaidi … ikiwa wanafahamu yote haya, watajua kuwa ni tangazo la kushindwa kwa Amerika nchini Afghanistan kwa njia isiyo rasmi. Amerika inataka kutoka kabla ya kushindwa huku kuivunja vunja, kuifichua kama dola kuu inayo poromoka chini. Walipaswa kutumia hili na kutia shinikizo juu ya Amerika ili kuifurusha kwa fedheha, kuliko kuipa mapumziko ya kishujaa kupitia kwenda katika majadiliano, hakuna anaye weza kuiamini Amerika:      

[لَا يَرْقُبُونَ فِي مُؤْمِنٍ إِلّاً وَلَا ذِمَّةً وَأُولَئِكَ هُمُ الْمُعْتَدُونَ]

“Hawatazami kwa Muumini udugu wala ahadi, basi wao ndio warukao mipaka”

[At-Tawba:10]

Amerika haikubali maslahi ya Taliban, namna yatakavyo kuwa kupitia majadiliano hayo isipokuwa ikiwa ushawishi wa Amerika utabakia nchini Afghanistan, hata kama wawakilishi wa Amerika watatabasamu usoni mwa Taliban, yaliyofichika nyoyoni mwao ni makubwa zaidi! 

6- Kwa yote haya, inatia uchungu kuwa majadiliano ya Doha, yaliyo chukua siku sita, ndio mwanzo wa maendeleo katika majadiliano hayo kwa ushahidi wa Taliban yenyewe:

a- Katika majadiliano na Anatolia, kiongozi wa Taliban, Wahid Mugdeh, alisema kuwa pande mbili hizo zilikubaliana mkataba mkubwa kuhusu kuyaondoa majeshi ya kigeni na kwamba Afghanistan sio tishio kwa sehemu yoyote ulimwenguni. Alifafanua kuwa harakati hiyo inatafuta dhamana kwa mchakato wa amani uliopendekezwa pamoja na hifadhi ya kimataifa. Aliongeza: “Makubaliano hayo hayakukamilishwa jijini Doha kwa sababu ya baadhi ya kadhia za kiufundi na kuandikwa kwa makubalino hayo.” (Shirika la Anatolia 26/1/2019)

b- Shirika la habari la Reuters mnamo 26/1/2019, liliripoti kutoka kwa maafisa wa Taliban: “Wamekubaliana juu ya baadhi ya vipengee pamoja na Washington ili kujumuisha makubaliano ya mwisho, na moja ya vipengee hivi cha thibitisha umuhimu wa kuyaondoa majeshi ya kigeni kutoka Afghanistan ndani ya miezi 18 ya kutia saini makubaliano hayo kwa badala ya dhamana  kutoka Taliban; kutoiruhusu al-Qaeda au ISIS kulitumia eneo la Afghan dhidi ya Amerika …” Ni wazi kutokana na ibara hii “kutoiruhusu al-Qaeda au ISIS” … kuwa Amerika inataka kuipa Taliban sehemu katika nidhamu yake kwa sababu ilihitaji dhamana kutoka kwake ili kusimama usoni mwa harakati nyenginezo, kwa hivyo inataka kuitumia kwa ajili ya lengo hili vile vile.

7- Vile vile taarifa za maafisa wa Amerika zathibitisha yale yaliyo elezwa katika taarifa za maafisa wa Taliban:

a- Mwakilishi maalumu wa Amerika, Zalmay Khalilzad, aliandika katika Twitter: “baada ya siku sita za mazungumzo pamoja na Taliban nchini Qatar, mikutano hiyo iliyofanyika hapa ilikuwa na matunda zaidi kuliko zamani. Tumepiga hatua kubwa juu ya kadhia nyeti.” (Deutsche Welle Arabic, 26/1/2019)

b- Kaimu Waziri wa Ulinzi wa Amerika Patrick Shanahan alisema mnamo 28/1/2019, juu ya mazungumzo ya amani pamoja na Taliban, “Ningependa kusema kuwa maamuzi yaliyofanywa ni ya kutia moyo.” (US Al-Hura 28/1/2019)

8- Hivyo basi, kielelezo cha makubaliano ya Doha ni uhalifu mkuu kwa ukuta wa Taliban, ambao ulikuwa imara. Serikali kibaraka ilifanya kazi kuudhoofisha zaidi, na licha ya baadhi ya taarifa za kawaida kutoka Taliban kuwa haitajadiliana na serikali ya Kabul, na taarifa kama hizo za Amerika kuwa makubaliano hayo ni lazima yawe juu ya kila kitu au hakuna makubaliano. Lakini, haraka ya pande mbili hizo kwa raundi nyenginezo za majadiliano zimejengwa juu ya kasi iliyo wekwa na majadiliano ya Doha na msukumo mzito wa vibaraka hao. Hivyo basi, yaweza kusemwa kuwa hatimaye Amerika baada ya miaka 17 ya vita imeona mwangaza mwisho wa pango ili kujitoa katika janga lake nchi Afghanistan. Isipokuwa waumini walioko sasa ndani ya Taliban wasimame, waangamize mkataba huu, na kuufanya upotee, na kuizima nuru ambayo Amerika aliona njia salama ya kutoka katika vita vya Afghanistan.   

9- Hivyo basi, Taliban na Mujahidina wote wanaompiga Kruseda Amerika na uvamizi wa Atlantiki hawapaswi kusalimu amri kwa Amerika na serikali yake, na hawapaswi kushiriki ndani yake, na wanapaswa kubakia ngangari kuwapinga hadi Amerika ilazimishwe kutoka ikiwa imevunjika na kufedheheka kwani vita si chochote ila subra ya saa moja. Amerika haikukubali majadiliano hayo mpaka iliposhindwa kuvunja ukakamavu wa Mujahidina. Ni lazima watahadharishwe na kutumbukia katika dimbwi la majadiliano, ambayo kwa Waamerika na Wamagharibi yamaanisha kulegeza msimamo kwa upande wa pili, na kushinda kupitia majadiliano yale ambayo haingeshinda kupitia vita, yaani kumshinda mpinzani mezani pasi na kumwaga tone la damu au kutumia senti yoyote! Hii ni kwa mujibu wa fahamu za kisiasa za kivitendo … Amerika ni mvamizi muhalifu ambaye anapaswa kuhesabiwa kwa uvamizi na uhalifu wake.  Imeuwa, imejeruhi, imelemaza, imekosesha mamilioni ya Waafghani makao na kuangamiza nchi hiyo. Uhalifu wake hauna kipimo na mkubwa kuliko uhalifu wa uliokuwa Muungano wa Kisovieti nchini Afghanistan. Kama ambavyo Muungano wa Kisovieti ulivyo furushwa kwa fedheha na kuvunjwa, hii pia yaweza kuwa hali kwa Amerika endapo Taliban itakuwa ngangari juu ya lile walilojitolea kwalo, kupigana na Amerika na kuwa na subra. Allah (swt) ameahidi ushindi kwa wale watakao kuwa na subra na kuwa na msimamo hata kama watakuwa ni wachache kuliko maadui.

Allah (swt) asema:   

[الَّذِينَ يَظُنُّونَ أَنَّهُمْ مُلَاقُو اللَّهِ كَمْ مِنْ فِئَةٍ قَلِيلَةٍ غَلَبَتْ فِئَةً كَثِيرَةً بِإِذْنِ اللَّهِ وَاللَّهُ مَعَ الصَّابِرِينَ]

“Wakasema wale wenye yakini ya kukutana na Mwenyezi Mungu: Makundi mangapi madogo yameshinda makundi makubwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu yu pamoja na wenye kusubiri.” [Al-Baqara: 249]

Na ni lazima wasikubali kushiriki katika serikali hiyo kibaraka nchini Afghanistan, bali waibomoe, na wasimamishe utawala wa Kiislamu, Khilafah Rashidah kwa njia ya Utume, ambayo Mtume wetu (saw) alitoa bishara ya kuwasili kwake «ثُمَّ تَكُونُ خِلَافَةٌ عَلَى مِنْهَاجِ النُّبُوَّةِ» “Kisha kutakuwa na Khilafah kwa njia ya Utume”

[ لِمِثْلِ هَذَا فَلْيَعْمَلِ الْعَامِلُونَ]

“Kwa mfano wa haya nawatende watendao” [As- Saffat: 61]

01 Jumada II 1440 H

Jumamosi, 06/02/2019 M

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoAlhamisi, 02 Aprili 2020 21:00

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu