Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Jibu la Swali

Hali ya Kisiasa Nchini Gambia

(Imetafsiriwa)

Swali:

Tunataraji Hizb inatia maanani kadhia za Waislamu katika Afrika kama inavyotia maanani kadhia nyengine za Waislamu ambazo likizuka jambo tu hutoa toleo baada ya siku moja au mbili…Lakini, kwa mfano, Gambia, haijatoa toleo lolote kuhusu (nchi hiyo) hadi leo, pamoja na kwamba yaliyotokea yameendelea kwa karibu miezi miwili. Basi tunaomba ufafanuzi wa kilichotokea. Kisha kwanini nchi za Afrika ya magharibi zinamuunga mkono rais mpya Adama Baro? Na kwanini shinikizo lao kubwa kwa rais alyetangulia kuwa ang’oke madarakani? Na je kujitoa kwake ICC au kuita Gambia kuwa Jamhuri ya Gambia ya Kiislamu yote haya kuna mahusiano? Na hasa kwa kuwa rais mpya katika mkutano na waandishi wa habari 28/01/2017 katika mji mkuu Banjul alisema: “kuwa yeye atatekeleza ahadi yake kubadilisha uamuzi wa kuitoa nchi yake katika ICC ambao aliuchukua rais aliepita Yahya Jammeh” Na akaweka wazi azma yake ya “kubadili jina la nchi kutoka Jamhuri ya Kiislamu ya Gambia na kuwa Jamhuri ya Gambia katika utaratibu wa marekebisho ya katiba…” (Aljazeera, 29/01/2017)?

Jawabu:

Hakika Hizb ut-Tahrir ni chama cha kisiasa na mfumo wake ni Uislamu, basi kadhia zote za Waislamu ni kadhia zake. Na namna inavyochunga ya kupewa kipaumbele, basi hutoa matoleo yanayohusu mambo fulani na kuyachelewesha yanayohusu mambo mengine haimaanishi kutoyapa umuhimu. Na nataraji hili litakuwa wazi (limefahamika) bila mazonge. Na mwendo wa Hizb (katika kubeba da’awa) katika fikra yake na njia yake hunena hivyo. Wallahulmusta’an. Baada ya hayo najibu swali. Wabillahittaufiq:

Hakika jawabu linalazimisha kuchunguza hali halisi ya kisiasa ya Gambia tangu ulipoingia Uislamu kisha mpambano wa madola juu yake…kwa namna ifuatayo:

1- Gambia ni ardhi ya Kiislamu, kwa kuwa watu wake wameingia katika Uislamu wakawa Waislamu wapatao 95% katika wakaazi wa nchi inayofikia idadi ya wakaazi kiasi cha milioni mbili. Gambia iliendelea kutawaliwa na Muingereza na akaipa uhuru mwaka 1965 na akaiunganisha na jumuiya ya Common Wealth ya Muingereza… Ikamteua Dawda Jawara kuwa Waziri Mkuu chini ya nidhamu ya Kifalme inayofata utawala wa Kifalme wa Uingereza. Na baadae ikamfanya mwaka 1970 atangaze Jamhuri ili awe Rais wa mwanzo wa Jamhuri. Na yametokea hayo katika wakati wa mashambulizi ya Marekani dhidi ya nchi za Afrika ambazo zinafata ukoloni wa Ulaya na hasa nchi ambazo nidhamu zake ni za Kifalme. Na mfano wa hayo kama ilivyofanya Uingereza nchi ya Libya wakati yalipozidi mashambulizi ya Marekani katika kipindi cha Ufalme, ilipomfanya ofisa aliyechanganyikiwa kama Gaddafi wakati huo umri wake ni miaka 26 afanye mapinduzi baridi mwaka 1969 dhidi ya kibaraka wake Mfalme na atangaze Jamhuri ili akate njia ya majaribio kadhaa ya Marekani kutaka kuipindua nidhamu ya Kifalme nchini Libya. Hivi ndivyo ilivyo Uingereza haitilii umuhimu kufanya mabadiliko katika muundo wa utawala lakini la muhimu (kwake) ni kubakia mwenye kudhamini ushawishi wake na ukoloni wake.

2- Na wakati shinikizo na mashambulizi ya Marekani dhidi ya Gambia yalipozidi mwisho wa karne iliopita, Uingereza ilimleta Jenerali wa Kijeshi aliyehadaiwa, ambaye ni Yahya Jammeh na umri wake ulikuwa hauzidi miaka 29 ikamtaka afanye mapinduzi baridi siku ya tarehe 22//07/1994 dhidi ya Rais wa mwanzo kibaraka wake Dawda Jawara aliyekaa madarakani kiasi cha miaka 30, hayo yalifanyika ili kuhifadhi ushawishi wa Uingereza nchini. Na Libya katika kipindi cha Gaddafi ilikuwa ikitoa mafunzo kwa majeshi ya Gambia kwa sababu Uingereza ilikua inamtumia kibaraka wake Gaddafi kuwalinda vibaraka wake Afrika.

Na kama alivyoanza Gaddafi kauli zake za uhuru huku akizichanganya na baadhi ya misemo ya Kiislamu na maneno ya Uarabu dhidi ya ukoloni katika wakati ambao alikuwa akitekeleza mipango ya Muingereza na kuwa mbali na kuutekeleza Uislamu. Na hivyo ndivyo zilivyokuwa hatua za Yahya Jammeh wakati alipotangaza mwaka 2013 Gambia kujitoa katika jumuiya ya Common Wealth ya Muingereza, na akaielezea jumuiya hiyo kuwa “Utumwa wa ukoloni mpya” na kwamba ipo “Ili kulazimisha mipango ya kudhalilisha ya magharibi juu ya nchi zote ulimwenguni zinazoendelea”. Na akaifuta lugha ya kiengereza kama lugha rasmi ya nchi na kuifanya lugha ya kiarabu kuwa lugha rasmi. Akasema: “Kwa zaidi ya miaka 300 ya ukoloni, Uingereza haikutufundisha isipokuwa nyimbo “Mungu muhifadhi Malkia”. Na mwaka 2015 akatangaza Jamhuri ya Gambia kuwa ni nchi ya Kiislamu.

Akasema katika TV rasmi ya nchi yake siku ya tarehe 11/12/2015 kwamba “Kwa mujibu wa utambulisho na thamani ya kidini natangaza kuwa “Gambia ni nchi ya Kiislamu”…na kwa kuzingatia kuwa Waislamu ndio wengi zaidi ya wakaazi wa nchi basi nchi haiwezi kuendelea na urithi wa kikoloni”, kwa sababu katiba yake ilikuwa inaeleza serikali ya kisekula iliyowekwa na mkoloni Muingereza kwa nchi ambayo aliyoitenza nguvu na kuikoloni kwa mamia ya miaka. Kwa hivyo basi, jina lake litakuwa Jamhuri ya Gambia ya Kiislamu. Kwahiyo mabadiliko yamepita kwa (jina la) Uislamu na sio chenye kudhaminiwa wala kuutabikisha kivitendo Uislamu, mfano wake ni kama jirani yake, Mauritania, ambayo inaitwa Jamhuri ya Kiislamu ya Mauritania ambayo haitabikishi Uislamu bali inafuata ukoloni wa Ulaya.

Na hatua ya Yahya Jammeh ni jaribio la kuuthibitisha utawala wake na kupata kuungwa mkono na raia wengi katika kipindi cha ukosoaji dhidi ya utawala wake na majaribio ya Marekani kumuangusha na kumpindua. Na kama ni dalili ya mapenzi ya Uislamu walinayo watu, basi wengi wa wakaazi wamepinga kupeleka watoto wao katika shule za kiingereza kwa kuzichukulia kuwa ni shule zenye kufundisha ugeni ambazo hutoa vizazi vyenye utambulisho hasi wenye kufata ukoloni. Wakashurutisha usomeshaji uwe kwa lugha ya kiarabu na kuingizwa somo la malezi ya kiislamu katika mitaala. Pamoja na yote haya na yale, ushawishi wa Uingereza umeendelea bila kuguswa, na imebakia ndio yenye kushika hatamu za mambo moja kwa moja au nyuma ya pazia kupitia vibaraka nchini. Na wala Uingereza kwa kuongezwa jina la Uislamu kwenye Jamhuri haikupata athari muda wa kwamba imebakia lafudhi bila maana, yaani bila kuutabikisha Uislamu. Na muda wa kwamba inahifadhi umaarufu wa kibaraka wake mbele ya shinikizo la Marekani.

3- Siku ya tarehe 30/12/2014 lilitokezea jaribio la mapinduzi dhidi ya Yahya Jammeh waliposhambulia kasri lake la uraisi kwa matarajio ya kumuangusha wakati yuko nje ya nchi. Marekani ilikua nyuma ya jaribio hili kwasababu ilibainika mpangaji alikua mfanyabiashara anayeitwa “Cherno Njie” anaeishi jimbo la Texas, Marekani na wenzake watatu waishio Marekani. Na baada ya kufeli mapinduzi haya, hawa watu wanne walihukumiwa nchini Marekani kwa kupewa adhabu nyepesi. “Cherno Njie” alihukumiwa mwaka mmoja jela, kwa sababu kama alivyosema waziri wa haki wa Marekani Andrew Luger: “Hawa watu wanne walivunja sheria zilizopo za kulinda siasa ya nje ya nchi yetu, Wamarekani wote ni sawa sawa ndani na nje ya Marekani” (Reuters, 13/05/2016). Kwahiyo Marekani imewahukumu raia wake wenye asili ya Gambia ili kufunika ukweli, kana kwamba haijui jambo hilo, na lau mapinduzi yangefaulu ingeliyaunga mkono. Lakini kwasababu yamefeli ndio imefanya mchezo huu wa kuigiza kwa kuwahukumu watu hawa adhabu nyepesi.

4- Ndio namna hii, mashambulizi ya Marekani dhidi ya ushawishi wa Ulaya ikiwemo Uingereza imezidi katika eneo la Afrika ya magharibi kama ilivyo katika maeneo mengine. Na imekua kisingizio chake ni rekodi mbaya ya haki za kibinadamu ya nchi hii au ile, na wao kwa kweli hawathamini haki za kibinadamu! Na Marekani wakatilia nguvu kisingizio hichi kwa Yahya Jammeh nchini Gambia ili kumbadilisha na kuingiza ushawishi wake eneo la ushawishi wa Muingereza. Mashambulizi yalikuwa makali kwa kiasi kwamba Ulaya ilikwenda sambamba na mashambulizi ili kukata njia kwa Marekani… Umoja wa Ulaya ukasimama kidete ukasimamisha misaada yake kwa muda kwa Gambia kwa kisingizio kilekile “rekodi zake mbaya za haki za kibinadamu”.

Na Uingereza ikataka kubadilisha kibaraka wake kwa sura ambayo Marekani haitaweza kusimama mbele yake kwasababu ya jina la demokrasia, na ndio mbinu zinazoitumia nchi za magharibi kuondoa ushawishi baina yao hutumia kisingizio cha kuingilia kati, kwa kujua kuwa katiba ya Gambia inataka kufanyike kila baada ya miaka mitano. Na Dawda Jawara alikua daima anashinda katika chaguzi, na vilevile chama chake cha Chama cha Watu Maendeleo ambacho kilikua kinatawala siasa za Gambia, yaani maisha ya kisiasa ya Gambia ni ya Muingereza. Na pia kipindi cha Yahya Jammeh kilikua miaka 22 ambacho alkuwa daima akijitangazia ushindi. Na hivi ndivyo ulivyofanyika uchaguzi wa urais mwaka uliopita tarehe 02/12/2016. Akatangaza kushinda kwa mpinzani wake Adama Barrow ambae alikua akifanya kazi London, Uingereza kama mlinzi wa usalama wa duka kubwa, akarejea nchini kwake Gambia mwaka 2006 akaanzisha kampuni ya ujenzi na umiliki wa majumba ambayo bado anaiendesha. Kwahiyo yeye amejifunga na Muingereza mwanzo hadi mwisho.

5- Yahya Jmmeh alikubali kushindwa, akitangaza katika runinga rasmi kwamba “Wagambia wameamua ning’oke na wamemchagua mtu mwengine kuongoza nchi “, na akawasiliana na mpinzani wake kwa njia ya simu akisema: “Wewe ndie rais mteule wa Gambia, nakutakia kheri na fanaka”. Lakini akakataa hayo pale chombo cha kuchunguza matokeo ya mwisho kilipopunguza tofauti baina ya washindani wawili kutoka elfu 60 hadi chini ya elfu 20, na akazungumza kuwa “baadhi ya watu kutoweza kupiga kura wakati wengine walizuiliwa kupiga kura na elimu isiyo sahihi”, akasema pia: “Tutarudi kwenye masanduku ya kura kwasababu nataka kuhakikisha kuwa kila Mgambia anapiga kura chini ya mamalaka ya Tume huru, isiyo na upendeleo, na isiyoegemea upande wowote, na wala hainyenyekei ushawishi wowote wa nje”. Yaonesha kana kwamba kulikuwa na makubaliano ya kuwa ang’oke na aache madaraka ya urais kwa ajili ya kibaraka mpya, lakini alidhani kuwa ataweza kuikinaisha Uingereza kuendelea kubakia miaka mingine kadhaa!

Ila Ulaya na hasa Uingereza iliona kwamba hajajitayarisha kuweza kubakia kwa hofu Marekani isitawale nchi hii kwa kuichukua kutoka kwa Muingereza. Na hasa kwa kuwa Marekani imelaani kupitia msemaji wa wizara ya mambo ya nje Mark Toner tarehe 10/12/2016 kukataa rais wa Gambia matokeo ya uchaguzi, akasema msemaji huyu wa Marekani: “Hakika msimamo wa Jammeh ni hujuma ya kuvunja uaminifu wa Wagambia nchini kwake, ni jaribio la fedheha la kudhoofisha imani ya watu wa Gambia katika mchakato wa uchaguzi wa haki. Na kuwa lengo la Jammeh ni kubakia madarakani kwa njia isiyo ya kisheria”.

Na hii ni hoja yenye nguvu kwa uingiaji wa Marekani, kwahivyo Uingereza ikakataa abakie, ikatatua (kwa kukabidhi) suala hili kwa maamuzi ya nchi za Afrika ya magharibi(ECOWAS) kwa uingiliaji, na ni kitendo cha Ulaya na hasa Muingereza na Ufaransa ambazo ndizo zenye ushawishi katika eneo hilo. Basi Senegal ambayo si mwanachama wa kudumu katika Baraza la Usalama ikapeleka mswada wa azimio katika Baraza ili kuruhusu uingiliaji kwa msaada wa Uingereza na Ufaransa ambazo ni wanachama wa kudumu wa Baraza la Usalama. Na Marekani katu haiwezi kukataa, na ndio inayoongoza upinzani dhidi ya Yahyha Jammeh na intafuta mbinu tu ya kuingilia. Kwahivyo basi, kwa pamoja, Braza la Usalama lilipitisha mswada wa azimio siku ya Alkhamis 19/01/2017 na likaeleza:

“Kuunga mkono kikamilifu Jumuiya ya nchi za Afrika ya magharibi katika kujifunga kuhifadhi heshima ya matakwa ya watu wa Gambia kupitia njia za kisiasa kwanza”. Yaani inafaa kutumia njia zisizokuwa za kisiasa ikiwa hizi zitafeli, italazimika kutumia nji za kijeshi.

6- Namna hii ndivyo jambo hili lilivyotatuliwa… Akaapishwa Adama Barrow anaeishi Senegal tangu tarehe 15/12/2016, aliapishwa katika ubalozi wa nchi yake nchini Snegal siku ya tarehe 19/01/2017… Na Senegal, Naigeria na Ghana zikatuma majeshi ya ardhini karibu na mipaka ya Gambia pamoja na kusimamia upatanishi ili kumlazimisha Jammeh ang’oke na ahame nchi. Nchi za Afrika ya magharibi zikampa Jammeh fursa hadi mchana siku ya tarehe 20/01/2017 kung’oka na kuhama nchi. Na viongozi wa nchi hizi waliwasili mji mkuu wa Gambia ili kumpa Yahya Jammeh fursa ya mwisho ili kukabidhi madaraka kwa amani kabla hajang’olewa na wanajeshi wa eneo ambao wameshafika nchini hasa…

Siku ileile ya tarehe 20/01/2017 kiongozi wa kijeshi wa Gambia akatangaza kwamba anamtambua rais mpya Adama Barrow kuwa ni amiri jeshi mkuu na hatopambana na majeshi ya eneo ambayo yamejiandaa kumng’oa Yahya Jammeh, rais uliemaliza utawala wake…”

Yahya Jammeh tarehe 21/01/2017 akalazimika kufanya maamuzi ya kung’oka na kuhama nchi kwasababu hakua na jeshi la kumlinda yeye nchini wala nje ya nchi…Na hapo tena Umoja wa Mataifa, Umoja wa Afrika, na Jumuiya ya Uchumi ya Nchi za Magharibi ya Afrika zikatangaza kusimamisha hatua kijeshi nchini Gambia pamoja na kuhakikisha haki ya Yahya Jammeh kurudi nchini kwake baada ya kutangaza kung’oka kwake madarakani na kuhama nchi. Na msemaji wa serikali ya Equatorial Guinea Augustine Nze tarehe 24/01/2017 alithibitisha kuwa nchi yake imempa rais wa Gambia Yahya Jammeh haki ya ukimbizi wa kisiasa, hayo ni kwa ajili ya kuepusha makabiliano yoyote ya kisilaha nchini Gambia (AFP, 25/01/2017).

Na hapo tena mzozo wa kisiasa wa Gambia umemalizika ambao uliendelea kwa muda wa wiki saba. Na hivi ndivyo pazia lilivyokunjuka dhidi ya utawala wa Yahya Jammeh ambao uliendelea kwa miaka 22, kwa kubadilisha kibaraka kwa kibaraka ili ahifadhi ushawishi wa Ulaya.

7- Kwa ufupi mabadiliko yaliyotokea Gambia hayakuwa kwasababu Yahya Jammeh alijitoa ICC, kwani kuna nchi nyingi ambazo hazimo ICC ikiwemo Marekani… Na wala si kwasababu Yahya Jammeh ameweka katika jina la nchi neno “Ya Kiislamu”, kuna nchi kadhaa zina jina hili kwasababu kinachowahofisha wamagharibi ni utabikishaji wa Uislamu katika nchi ya Uislamu. Ama lafudhi tu bila maana haiwahofishi…

Hakika mabadiliko yaliyotokea ni katika mada ya mpambano wa kimataifa. Marekani inamnyemelea Ulaya katika makoloni yake ya Afrika ili iyavute upande wake wakati wowote ipatapo fursa. Kana kwamba imeipata nchini Gambia katika utawala wa Yahya Jammeh kwa kisingizio cha uvunjifu wa haki za kibinadamu. Basi Ulaya “Uingereza” ikaona yenyewe iyapande mawimbi na kumbadili kibaraka kwa kibaraka ili kukata njia ya Marekani na ikahifadhi kuendelea kwa ushawishi wa Uingereza nchini Gambia ijapokuwa kwa muda mfupi…

Hakika watu wa Gambia ni kama wengine katika Waislamu wanatraji utawala wa Kiislamu na wanamsubiri atakae wafungua pingu za mkoloni na utawala wa ukafiri. Na ni jukumu la kila Muislamu anayeweza afanye bidii katika kubeba da’awa kama alivyobeba Mjumbe wa Allah (SAW) na wakapita njia yake Masahaba zake (ra), hapo tena isimame Khilafah Rashidah, aishi kwayo mwenye kuishi kwa ubainifu na aangamie mwenye kuangamia kwa ubainifu pia.

وَيَوْمَئِذٍ يَفْرَحُ الْمُؤْمِنُونَ * بِنَصْرِ اللَّهِ يَنْصُرُ مَنْ يَشَاءُ وَهُوَ الْعَزِيزُ الرَّحِيمُ ﴿

(Na siku hiyo Waumini watafurahi. Kwa nusura ya Allah humnusuru amtakaye. Naye ndiye mwenye Nguvu, Mwenye kurehemu) [AR-Rum: 4-5]

3 Jumada 1 1438H                                                                                                                            

Jumanne, 31/01/2017

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoAlhamisi, 02 Aprili 2020 20:42

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu