Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Silsila ya Maswali Yaliyowasilishwa kwa

Amiri wa Hizb ut Tahrir

Sheikh Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah katika Ukurasa Wake wa Kifikra wa Facebook
Jibu la Swali

Dua kwa ajili ya Kuangamizwa Umbile la Kiyahudi
Kwa: Agus Trisa
(Imetafsiriwa)

Swali:

Assalamu Alaikum Wa Rahmatullahi Wa Barakatuhu

Mwenyezi Mungu akulinde popote ulipo.

Nataka kukuuliza kuhusu ayah hii tukufu Mwenyezi Mungu Subhanahu Wa Ta'ala asema:

[وَإِذَا سَأَلَكَ عِبَادِي عَنِّي فَإِنِّي قَرِيبٌ أُجِيبُ دَعْوَةَ الدَّاعِي إِذَا دَعَانِي فَلْيَسْتَجِيبُوا لِي وَلْيُؤْمِنُوا بِي لَعَلَّهُمْ يَرْشُدُونَ]

“Na waja wangu watakapo kuuliza khabari zangu, waambie kuwa Mimi nipo karibu. Naitikia maombi ya mwombaji anapo niomba. Basi na waniitikie Mimi, na waniamini Mimi, ili wapate kuongoka.” [Al-Baqara: 186].

Je, ni kweli kwamba Mwenyezi Mungu hujibu dua zote za mwanadamu? Je, kuna dua ambayo Mwenyezi Mungu haijibu? Baadhi ya watu wanauliza, tumeombea Israel iangamizwe na Mwenyezi Mungu, lakini kwa nini umbile lao bado lina nguvu na linaendelea kuishambulia Gaza?

Shukran kwa jibu lako, Mwenyezi Mungu akulipe kheri kwa jibu lako zuri

Wassalamu Alaikum Wa Rahmatullahi Wa Barakatuhu

Jibu:

Assalam Alaikum Wa Rahmatullah Wa Barakatuh

Kuna mambo ambayo ni lazima yafahamike kuhusu Dua:

1- Iwapo Muumini atamuomba Mwenyezi Mungu kwa moyo wa ikhlasi, dua isiyokata kizazi, basi Mwenyezi Mungu (swt) atamjibu kwa njia moja kati ya tatu, kama ilivyo katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu (swt) na Sunnah za Mtume wake (saw):

Mwenyezi Mungu (swt) hujibu Dua ya muombaji anapomwomba, na humjibu mwenye haja anapomwomba; [وَقَالَ رَبُّكُمُ ادْعُونِي أَسْتَجِبْ لَكُمْ] “Na Mola wenu Mlezi anasema: Niombeni nitakuitikieni.” [Ghafir: 60]

[وَإِذَا سَأَلَكَ عِبَادِي عَنِّي فَإِنِّي قَرِيبٌ أُجِيبُ دَعْوَةَ الدَّاعِ إِذَا دَعَانِ] “Na waja wangu watakapo kuuliza khabari zangu, waambie kuwa Mimi nipo karibu. Naitikia maombi ya mwombaji anapo niomba.” [Al-Baqara: 186] [أَمَّنْ يُجِيبُ الْمُضْطَرَّ إِذَا دَعَاهُ وَيَكْشِفُ السُّوءَ“Au nani yule anaye mjibu mwenye shida pale anapo mwomba, na akaiondoa dhiki” [An-Naml: 62].

Hata hivyo, jibu lina uhalisia wa Shariah ambao ulielezwa na Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw):

«مَا مِنْ مُسْلِمٍ يَدْعُو اللهَ عَزَّ وَجَلَّ بِدَعْوَةٍ لَيْسَ فِيهَا إِثْمٌ وَلَا قَطِيعَةُ رَحِمٍ، إِلَّا أَعْطَاهُ اللَّهُ بِهَا إِحْدَى ثَلَاثِ خِصَالٍ: إِمَّا أَنْ يُعَجِّلَ لَهُ دَعْوَتَهُ، وَإِمَّا أَنْ يَدَّخِرَهَا لَهُ فِي الْآخِرَةِ، وَإِمَّا أَنْ يَصْرِفَ عَنْهُ مِنَ السُّوءِ مِثْلَهَا». قَالُوا: إِذًا نُكْثِرُ. قَالَ: «اللهُ أَكْثَرُ»

“Hakuna Muislamu yeyote atakayeomba dua isiyokuwa na uovu ndani yake wala isiyokata kizazi isipokuwa Mwenyezi Mungu atampa moja katika mambo matatu: Atamjibu haraka dua yake, au atamwekea kesho Akhera, au amuepushie kiasi sawa cha uovu.”

Wale waliosikia wakasema wataomba dua nyingi na akajibu kuwa Mwenyezi Mungu yuko tayari zaidi kujibu kuliko wanavyoweza kuomba.” (Imepokewa na Ahmad 3/18).

Pia,

«لَا يَزَالُ يُسْتَجَابُ لِلْعَبْدِ مَا لَمْ يَدْعُ بِإِثْمٍ أَوْ قَطِيعَةِ رَحِمٍ مَا لَمْ يَسْتَعْجِلْ». قِيلَ: يَا رَسُولَ اللهِ، مَا الِاسْتِعْجَالُ؟ قَالَ: «يَقُولُ قَدْ دَعَوْتُ وَقَدْ دَعَوْتُ فَلَمْ أَرَ يَسْتَجِيبُ لِي فَيَسْتَحْسِرُ عِنْدَ ذَلِكَ وَيَدَعُ الدُّعَاءَ»

“Mja hataacha kujibiwa kwa sharti kwamba haombi chochote cha dhambi au kukata kizazi, na maadamu hana pupa. Alipoulizwa ni nini maana ya kuwa na pupa, Mtume wa Mwenyezi Mungu alijibu: “Ni pale anaposema kwamba ameomba na kuomba laikini sijibiwi, basi basi akachoka katika hali hiyo na kuacha dua.” (Imesimuliwa na Muslim 4918).

Tunamuomba Mwenyezi Mungu (swt) na tukiwa wakweli, waaminifu, na watiifu, basi tuna yakini na jawabu kwa namna alivyoeleza Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw).

2- Dua sio njia ya Shariah ya kufikia lengo katika hali zote... Inapendekezwa, lakini sio njia ya kupata ushindi katika vita au kusimamisha dola nk. Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) alitayarisha jeshi huko Badr na kuwapanga askari, kila mmoja kwa nafasi yake, na akawatayarisha vyema kwa ajili ya vita, kisha Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) akaingia kwenye hema, na akamuomba Mwenyezi Mungu apate ushindi, na akazidisha dua mpaka Abu Bakr, Mwenyezi Mungu amuwiye radhi, akamwambia: “Baadhi ya haya yanakutosha ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu.” (Sirat Ibn Hisham 2/626). Dua haimaanishi kuacha kuchukua njia zinazohitajika, bali ni sehemu muhimu yake.

Pia anayetaka Khilafah isimamishwe tena, asitosheke na kumuomba Mola wake ili kufanikisha hilo, bali ashirikiane na watenda kazi ili kuisimamisha na kumuomba Mwenyezi Mungu msaada katika hilo, na kuliharakisha kufanikiwa, na dumu katika kumuomba Mwenyezi Mungu kwa ikhlasi huku ukichukua njia zinazohitajika. Hivyo, katika matendo yote, mtu anatakiwa kuwa na ikhlasi katika kitendo kwa Mwenyezi Mungu na awe mkweli kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) na aombe dua na kudumu katika kuomba, na Mwenyezi Mungu ni Samiy’ Mujeeb (Mwenye kusikia na Mwenye kujibu).

3- Siku za nyuma tulijibu swali kama hili mnamo tarehe 4 Dhul-Qi'dah 1432 H - 1/10/2011 M, na linasema:

[...Ama dua huku ukichukua njia zinazohitajika, ina athari katika matokeo, na hivi ndivyo alivyofanya Mtume (saw) na walivyofanya maswahaba zake. Mtume (saw) alilitayarisha jeshi na akaingia kwenye hema kuomba dua. Waislamu katika Al-Qadisiyah walijitayarisha kuuvamia mto. Sa'd, Mwenyezi Mungu amuwiye radhi, alielekea kwa Mwenyezi Mungu kwa dua...Na hivyo waumini wenye ikhlasi hujitayarisha kimada na kuomba dua. Mwenye kutafuta riziki hujitahidi huku akiomba dua, na mwanafunzi husoma na kujitahidi huku akimuomba Mwenyezi Mungu ili afanikiwe. Hili lina athari katika matokeo, Mwenyezi Mungu akipenda.

Imeelezwa katika “Mafahim” (Fahamu za Hizb ut Tahrir) mwishoni mwa ukurasa wa 50: “Lazima ifahamike kwamba ingawa kitendo kilichoashiriwa na Tariqah ni kitendo cha kimada (maadiyyah), ambacho kinapata matokeo ya kuhisika (mahsuusa), kitendo hiki lazima kiende kwa kufuata maamrisho (awaamir) na makatazo (nawaahi) ya Mwenyezi Mungu (swt). Kufuata maamrisho na makatazo ni kwa ajili ya radhi (riDwaan) ya Mwenyezi Mungu (swt). Muislamu pia lazima atawaliwe na utambuzi wake wa uhusiano wake na Mwenyezi Mungu (swt), ili atafute ukaribu (qurbah) na Mwenyezi Mungu (swt) kupitia Swalah, Dua, kisomo (tilawah) cha Quran na kadhalika. Ni lazima pia aamini kwamba Nasr (ushindi) unatoka kwa Mwenyezi Mungu (swt). Ni lazima taqwa (uchamungu) iwekwe katika nyoyo ili kutekeleza hukmu za Mwenyezi Mungu (swt). Pia ni muhimu kuomba Dua na kumdhukuru Mwenyezi Mungu (swt), huku tukidumisha uhusiano na Mwenyezi Mungu (swt), wakati wa kufanya vitendo vyote.”

Ni wazi kutokana na hili kwamba umuhimu wa dua kuambatanishwa na kuchukua njia zinazohitajika katika matendo yote ya muumini. Umuhimu huu unaongezeka kwa kurudiwa kwa neno “ni lazima” kuashiria umuhimu mkubwa kwamba vitendo vyote viambatanishwe na dua na mwendelezo wa kushikamana na Mwenyezi Mungu ...

- Utumiaji wa dua pamoja na kuchukua njia za lazima ni kama tulivyosema, aliyoyasema Mtume (saw) na Maswahaba zake, na Waumini walikuwa juu yake, na ikiwa yataunganishwa basi yanakuwa na athari juu ya matokeo, Mwenyezi Mungu akipenda. Utumiaji wao kwa pamoja haugongani na njia ya Uislamu, bali kinachogongana nayo ni kujifunga na dua peke yake bila ya njia ambayo nususi zimeonyesha katika utekelezaji fikra ya Kiislamu...]

Kwa hivyo, yaliliyotajwa katika swali lako kuhusu dua ya kuondolewa kwa umbile la Kiyahudi... dua haitoshi kwa hili, bali kitendo cha jeshi la dola linalopigana na Mayahudi lazima kiambatane na dua, kama ilivyokuwa kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) na Maswahaba zake, Mwenyezi Mungu awe radhi nao. Na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye msaada.

Ndugu Yenu,

Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah

4 Rabi’ Al-Akhir 1446 H

7/10/2024 M

Link ya jibu hili katika ukurasa wa Amiri wa Facebook

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu