Alhamisi, 26 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/28
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Silsila ya Maswali Yaliyowasilishwa kwa

Amiri wa Hizb ut Tahrir

Sheikh Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah katika Ukurasa Wake wa Facebook

Jibu la Swali
Uhalisia wa Hizb ut Tahrir Baada ya Kusimamishwa Khilafah
Kwa: Munthir Abu Ubaida
(Imetafsiriwa)

Swali:

Assalam Alaikum Wa Rahmatullah Wa Barakatuh

Inaelezwa katika Utangulizi wa Rasimu ya Katiba, Kifungu cha 21: Waislamu wana haki ya kuanzisha vyama vya kisiasa ili kuwahisabu watawala, au kufikia madaraka kupitia Ummah.

Swali ni: Ikiwa chama kilicho chukua utawala kilikuwa na mpango wake wa kisiasa, itautabikisha kama ilivyo kwa vyama katika nchi za sasa?

Pia, je ni sahihi kwa Amiri wa chama - kama chama chetu - kushikilia wadhifa wa uongozi wa chama na ule wa khalifa wakati huo huo?

Ikiwa ni sahihi, je chama kinawezaje kumhisabu Khalifa, huku kikiwa chini ya uongozi wa Amiri wake, ambaye ni Khalifa?

Baraka za Mwenyezi Mungu ziwe kwako Amiri wetu, na Mwenyezi Mungu akuruzuku matendo mema.

Jibu:

Wa Alaikum Assalam Wa Rahmatullah Wa Barakatuh

Tumetoa swali zaidi ya Jibu la Swali moja juu ya mada hii: mnamo 14/8/1967 na mnamo 26/12/2014, na yana maelezo ya kutosha, kwa hivyo yaregelee.

Lakini kwa kifupi ni kama ifuatavyo:

1- Kuchukua utawala wa Hizb ut Tahrir sio kama uchukuaji utawala wa vyama vilivyopo sasa ulimwenguni. Kinachofikia madaraka ni fikra ambayo juu yake chama kimeasisiwa, katika umbo lake la kina, kama ilivyoitabanni, na sio wanachama wa chama. Chama kinafanya kazi kuzileta fikra zake madarakani, sio kuwaleta wanachama wake madarakani.

2- Lakini, kwa kuwa fahamu za hizb haziwezi kutekelezwa vizuri isipokuwa na wale wanaozitabanni na kuishi nazo na kwa ajili yake, hapana budi khalifa awe kutoka kwa hizb, hapana budi wasaidizi wawe kutoka kwa hizb, na hapana budi Amiri wa Jihad awe kutoka kwa hizb. Pande hizi tatu za vyombo vya utawala hapana budi ziwe kutoka kwa hizb ili fikra itekelezwe na kuhakikisha utekelezaji wake sahihi. Ama kuhusu viungo vyengine vya utawala, vinaweza kuwa kutoka kwa hizb, au vinaweza kuwa kutoka nje ya hizb kwa mujibu wa nguvu na uwezo.

3- Mbali na ukweli kwamba fikra ya hizb kuja madarakani, ni kuwasili kwa hizb madarakani, hizb ni mwangalifu kutowalazimisha wanachama wa hizb kutawala watu na kuchukua tahadhari kubwa dhidi ya hilo. (imesimuliwa kutoka kwa Umar bin Al-Khattab kwamba alipowachagua wanachama wa Baraza la Shura, yaani, wagombea sita wa uongozi wa Khilafah, alikuja kwa Ali na kumwambia: ewe Abu al-Hassan, ikiwa watakupa wewe, usiruhusu Bani Hashim waendelee kutawala watu. Akaja kwa Uthman na kumwambia: Ewe Uthman, ikiwa watakupa (Khilafah), jihadharini na kuwafanya Bani Umayyad waendelea kutawala watu), na ikiwa Khalifa ni kutoka Hizb ut Tahrir, basi wanachama wa hizb watakuwa kwake kama Bani Hashim kwa Ali na Bani Umayyad kwa Uthman, kwa hivyo sio sawa kwake kupitisha uamuzi kwao juu ya watu wengine.

4- Ama kuhusu hizb kumhisabu mtawala pindi chama kinapoingia madarakani, jibu la hilo ni:

Hizb hufanya amali nne: utoaji thaqafa (ya umakinifu na ya jumla), na mvutano wa kifikra katika suala la kufafanua fikra sahihi kutokana na fikra ya batili na fisadi. Amali hizi mbili sio mada ya kuhisabu uwajibikaji, lakini badala yake ni kazi ya kithaqafa na kifikra ya hizb. Kazi ya hizb kufanya yote haya inaendelea, kabla na baada ya utawala, kwani haziathiriwi na kuchukua madaraka ya hizb.

Ama kazi ya tatu (kufichua mipango), sio kazi ya hizb tena kwa sababu uwepo wa hizb madarakani umeondoa suala la chama kinachoonyesha mipango ya kikoloni. Badala yake, inafanywa na vyombo vya serikali, na kuwahisabu watawala kuwajibika kwa kutabanni maslahi, kama ilivyokuwa kabla ya utawala, inabaki na inafanywa na kamati za Wilayah.

Kamati za Wilayah, kama ilivyokuwa kabla ya utawala, zina mamlaka ya kuuhisabu uongozi wa chama kuwajibika (Amiri na afisi yake), kwa hivyo wanaendelea kuwa na mamlaka haya ya kuuhisabu uongozi wa chama wakati kiko madarakani, na katika kutabanni maslahi ya Ummah kwa mujibu wa hukmu za Sharia na kuwaangalia kwa wema na ustadi.

Natumai, haya yametosheleza, na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi zaidi na Mwingi wa hekima.

Ndugu Yenu,

Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah

4 Rabi ul Awal 1445 H

19/9/2023 M

Link ya jibu hili kutoka ukurasa wa Amiri wa Facebook.

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu