Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Jibu la Swali:

Je, Hizb ut Tahrir Yazingatiwa kuwa ni Ash'ariya?

Kwa: Riyadh Abu Malik

(Imetafsiriwa)

Swali:

Mwenyezi Mungu akubariki Ewe Shekh na akufungulie, nina swali tafadhali: Je, Hizb ut Tahrir huzingatiwa kuwa ni Ash'ariya katika maudhui ya Aqeeda ama Hizb ina ufahamu wake maalum katika maudhui ya Aqida? Shukran

Jibu:

Assalam Alaykum Wa Rahmatullahi Wa Barakaatuhu,

Kabla ya kujibu moja kwa moja swali lako napenda kusititiza yafuatayo:

Kwanza: Uhalisia wa Hizb ut-tahrir:

1- Hizb ut Tahrir imejitambulisha nafsi yake kama ifuatavyo: (Ni chama cha kisiasa mfumo wake ni Uislamu. Siasa ni kazi yake, Na Uislamu ni mfumo wake, Chama kinafanya kazi baina ya Umma na pamoja na Umma ili kuufanya Uislamu ndio kadhia yake. Na kuongoza Umma katika kuirudisha Khilafah na kuhukumu kwa yale yote aliyoteremsha Mwenyezi Mungu. Na Hizb ut Tahrir ni kundi la kisiasa, na sio kundi la kiroho, wala kundi la kielimu, wala kundi la kufundisha, wala sio kundi la kimsaada, na fikra ya Kiislamu ndio roho ya mwili wake, na kukua kwake na siri ya uhai wake.) Hivyo basi Hizb ut Tahrir kwa mujibu wa utambulisho huu sio Madrasa ya kifikra wala sio kipote cha ufafanuzi wa maswala ya kiimani (firqa al-kalamiyah) wala dhehebu la kifiqhi. Bali ni chama cha kisiasa kinachotabanni kadhia za Umma na kuzitetea na kufanya kazi ya kusimamisha Uislamu katika uhalisia wa maisha na kuuhifadhi baada ya kusimamisha… Hizb inaamini Aqida ya Kiislamu na inamuhisabu kila anayeamini aqida ya Kiislamu kuwa ni ndugu yake. ﴿إِنَّمَا الْمُؤْمِنُونَ إِخْوَةٌ﴾ "Hakika waumini ni ndugu" [Al-Hujuraat: 10] Na inajadiliana naye kwa uzuri katika kila nukta yenye tofauti ya rai...

2- Hizb imetabanni Fikra, Hukmu na Rai inayojifunga nazo kwa ajili ya kusimama na kazi yake, na miongoni mwake ni vitabu vyake na Machapisho yake (Isdaaraat)… Lakini Hizb haikufanya utafiti wa kila suala na kila fikra, na haikutabanni katika masuala mengi haswa katika masuala ya Itikadi na Ibada, kwa kuwa hayo sio lazima kwake katika kazi yake kwa sifa yake kama chama cha kisasa kinachoenda mbio kwa ajili ya kuamsha Umma na kusimamisha Dola ya Khilafah na kusimama juu ya fikra ya Umma na hisia zake... Kwa mfano Hizb imetabanni katika maudhui ya kutofanya madhambi manabii na mitume (I'smah), na kutabanni katika maudhui ya Ijtihad ya Mtume (saw), kwa kuwa hayo yana athari juu ya kufahamu mambo ya sheria... lakini haikutabanni katika masuala mengi mengine ambayo wameyajadili wanazuoni wa Al-Kalaam...

3- Hizb imejifunga na Dalili zenye nguvu, Na ikadhihiri pupa yake daima ya kurudia thaqafa yake na tabanni zake kwa kutegemea dalili zenye nguvu... Ikaweza kusahihisha vitabu vyake na kuvirekebisha kwa sura ya hali ya juu. Haikushikamana na rai yoyote ambayo imethibiti udhaifu wa dalili yake na kuwa na uzito dalili nyengine, bali iliwacha Rai ambayo imethibiti udhaifu wa dalili yake na kuchukua rai ambayo imethibti kuwa dalili yake ni ya nguvu. Na hili liko wazi katika jumla ya usahihishaji na urekebishaji wa vitabu vya Hizb, na kadhalika katika kurudia kwake vitabu vyake (Murajaa'h) kila baada ya muda...

Pili: Baadhi ya Waislamu wamezipa majina maalum baadhi ya madaris na madhehebu ambayo yamekhtalifiana katika chambuzi zinazoambatana na matagaa ya aqida (Furu'ul Aqidah) na masuala ya maelezo ya Aqida (Kalamiya) kama vile Ash'ariyah ikinasibishwa na Al Imam Al-asha'riy Mwenyezi Mungu amrehemu na Maaturidiyah ikinasibishwa na Al-imam Maaturidiy Mwenyezi Mungu amrehemu, Na salafiyah na majina mengineo... Walizipa rai zao tamshi la aqidah wakasema: Aqida ya kiash'ariya, Aqida ya kimaturidiya, Aqida ya salafiya na mfano wake, bali wakataja na maandishi ya wanachuoni maalum na vitabu vyao kuwa ni Aqida wakasema: Aqida Twahawiya wakinasibisha kwa Imam Twahawiy Mwenyezi Mungu amrehemu, Wakasema Aqida wasitiya wakinasibisha kwa Risala aliyoiandika Imam Ibn Taymiyya Mwenyezi Mungu amrehemu kwa watu wa Waasit...Na kihakika kulipa neno Aqida juu ya hayo sio sahihi na sio mahala pake, huleta sintofahamu na kuwatenganisha Waislamu, kwa kuwa msimamo wa madhehebu juu ya masuala yanayoambatana na chambuzi za kiaqida sio Aqida yenyewe. Bali Aqida ya Kiislamu imethibitishwa katika sheria kupitia dalili zilizokatikiwa na hili halijuzu kukhtalifiana kwalo... Kwa hiyo hakuna kitu kinachoitwa Aqida ya kiash'ariya au Aqida ya kisalafiya au Aqida Twahawiya, bali kuna Aqida ya Kiislamu inayowakusanya Waislamu wote katika kila zama pamoja na utofauti wa madhehebu yao na rai zao. Kuna tofauti ya rai baina ya madhehebu na madrasa za kifikra kama Ash'ariya, Maturidiya, Salafiya na wengineo katika chambuzi za kadhia ya kimitagaa isiokuwa Aqida ya Kiislamu na kila upande una rai yake ambayo haimtoi katika Aqida ya Kiislamu.

Tatu: Hakika njia (manhaj) ambayo Hizb imepita katika kutabanni fikra, hukmu na rai ni kuchukua rai kwa mujibu wa dalili zenye nguvu sawa iwe dalili ya kiakili au ya kunukuu pasi na kumtizama aliyesema, Hizb ut Tahrir imetabanni katika baadhi ya masuala ya matagaa ya Aqida (Furuu'l Aqida) mambo ambayo wameyasema Ash'ariya na kutabanni mambo mengine waliyoyasema wengineo… Na katika masuala ya kisheria Hizb imechukua rai kutoka kwa madhehebu ya kifiqhi mashuhuri na rai zenginezo bila ya kujifunga na dhehebu maalum… Kwa hiyo haisemwi kuhusu hizb ut tahrir kuwa ni mashafi au Hanafi, wala haisemwi kuwa Hizb ni Ash'ariy au Salafiy, wala Maturidiy au Muu'taziliy, wala haisemwi kuwa Hizb ni katika madrasa ya rai au Madrasa ya Hadith… Hizb sio katika hayo yote, bali ni chama cha kisiasa mfumo wake ni Uislamu. Inachukua rai kwa mujibu wa dalili zake za nguvu kwa manhaj madhubuti iliotabanni katika vitabu vyake pasi na kuangalia aliyesema. Katika rai zake baadhi ni walizozisema Ash'ariya na baadhi wamezisema masalafiya na baadhi zimesemwa na madrasa zengine. Na yote hayo ni kwa kujengea uzito wa dalili, na sio kujifunga na rai mojawapo ya hizo madrasa na kuifuata manhaj yake au fikra zake au rai zake, Hizb haitambui tofauti zilizotokea baina ya Waislamu katika zama zilizopita, bali inawahisabu Waislamu kama Umma mmoja pamoja na tofauti ya madhehebu yao au mapito yao na inawalingania kuitikia mwito na kufanya kazi pamoja nao katika kusimamisha Uislamu na kubeba Daawah na kuunganisha Umma chini ya bendera ya Khilafah ya Kiislamu.

Nataraji iwe Jibu limetosheleza

Wallahu Aa'lamu wa ahkamu.

Ndugu Yenu

Ata Bin Khalil Abu Rashtah

 17 Dhu al-Hijjah 1442 H

27/07/2021 M

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu