Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Jibu la Swali
Dalalat Al-Iqtidha
Kwa: Zahid Talib Na’eem
(Imetafsiriwa)

Swali

As-salam Alaikum Wa Rahmatullah Wa Barakatuh

Mada: Dalalat Al-Iqtidha

Sheikh wetu Mashuhuri, Mwenyezi Mungu azibariki juhudi zako na aziongoze hatua zako na akusaidie kwa lile linalomfurahisha na kumridhisha Yeye (swt) 

Katika kitabu Shakhsiya ya Kiislamu Juzuu 3 juu ya mada (Chochote kinacho pelekea Wajib hicho nacho ni Wajib) katika ukurasa wa 44 (nakala ya Kiarabu) kinaeleza kuwa: "na ima iwe sababu ni ya kisheria kama jinsi ya kuacha huru (watumwa) kwa lazima" kana kwamba anakusudia aya ya dhwihar, katika maneno ya Mwenyezi Mungu:

  وَالَّذِينَ يُظَاهِرُونَ مِن نِّسَائِهِمْ ثُمَّ يَعُودُونَ لِمَا قَالُوا فَتَحْرِيرُ رَقَبَةٍ مِّن قَبْلِ أَن يَتَمَاسَّا ذَٰلِكُمْ تُوعَظُونَ بِهِ وَاللَّـهُ بِمَا تَعْمَلُونَ خَبِيرٌ * فَمَن لَّمْ يَجِدْ فَصِيَامُ شَهْرَيْنِ مُتَتَابِعَيْنِ مِن قَبْلِ أَن يَتَمَاسَّا فَمَن لَّمْ يَسْتَطِعْ فَإِطْعَامُ سِتِّينَ مِسْكِينًا ذَٰلِكَ لِتُؤْمِنُوا بِاللَّـهِ وَرَسُولِهِ وَتِلْكَ حُدُودُ اللَّـهِ وَلِلْكَافِرِينَ عَذَابٌ أَلِيمٌ

“Na wale wanao jitenga na wake zao, kisha wakarudia katika yale waliyo yasema, basi wamkomboe mtumwa kabla hawajagusana. Mnapewa maonyo kwa hayo. na Mwenyezi Mungu anayajua yote mnayo yatenda. Na asiye pata mtumwa kumkumboa, basi na afunge miezi miwili mfululizo kabla hawajagusana. Na asiye weza hayo basi awalishe masikini sitini. Hayo ni hivyo ili mumuamini Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Na hiyo ndiyo mipaka ya Mwenyezi Mungu. Na kwa makafiri iko adhabu chungu.” [Al-Mujadala: 3-4].

Au aya ya kafara kwa kuuwa kimakosa katika maneno ya Mwenyezi Mungu:

 وَمَا كَانَ لِمُؤْمِنٍ أَن يَقْتُلَ مُؤْمِنًا إِلَّا خَطَأً وَمَن قَتَلَ مُؤْمِنًا خَطَأً فَتَحْرِيرُ رَقَبَةٍ مُّؤْمِنَةٍ وَدِيَةٌ مُّسَلَّمَةٌ إِلَىٰ أَهْلِهِ إِلَّا أَن يَصَّدَّقُوا فَإِن كَانَ مِن قَوْمٍ عَدُوٍّ لَّكُمْ وَهُوَ مُؤْمِنٌ فَتَحْرِيرُ رَقَبَةٍ مُّؤْمِنَةٍ وَإِن كَانَ مِن قَوْمٍ بَيْنَكُمْ وَبَيْنَهُم مِّيثَاقٌ فَدِيَةٌ مُّسَلَّمَةٌ إِلَىٰ أَهْلِهِ وَتَحْرِيرُ رَقَبَةٍ مُّؤْمِنَةٍ فَمَن لَّمْ يَجِدْ فَصِيَامُ شَهْرَيْنِ مُتَتَابِعَيْنِ تَوْبَةً مِّنَ اللَّهِ وَكَانَ اللَّهُ عَلِيمًا حَكِيمًا

“Na haiwi Muumini kumuuwa Muumini ila kwa kukosea. Na mwenye kumuuwa Muumini kwa kukosea basi amkomboe mtumwa aliye Muumini, na atoe diya kuwapa jamaa za maiti, isipokuwa waache wenyewe kuwa ni sadaka. Na ikiwa ni jamaa wa maadui zenu, hali yeye ni Muumini, basi ni kumkomboa mtumwa aliye Muumini. Na ikiwa ni miongoni mwa watu ambao pana ahadi baina yenu na wao basi wapewe diya watu wake na akombolewe mtumwa aliye Muumini. Na asiye pata, basi afunge miezi miwili mfululizo, kuwa ni toba kwa Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi na Mwenye hekima” [An-Nisa: 92].

Katika kitabu hicho hicho, nakala ya Kiarabu uk. 182, kinasomeka: (Dalalat Al-Iqtidha ni maana inayo hitajika na dalili, ili iwe ni sharti la maana inayo ashiriwa kupitia kulingana kwake.)

Nimechanganyikiwa kuhusiana na kadhia mbili:

Kwanza: Kwa nini alitaja sharti bila ya sababu wakati muundo ni wa sababu kuhusiana na uachaji huru wa lazima (wa watumwa), na kwangu mimi unaonekana kuwa ni muundo wa lazima kutokana na maana inayo hitajika inayo ashiriwa kupitia dalili (Dalalat Al-Iqtida)?

Pili: Kwa nini alitaja kulingana (Mutabaqa) na sio sehemu tu (tadhamun)?

Nataraji sijakulimbikizia mzigo kwa maswali haya, Mwenyezi Mungu akubariki.

Jibu

Wa Alaikum Assalam Wa Rahmatullah Wa Barakatuh

Swali la kwanza: unauliza ni kwa nini sharti limetajwa katika maana inayo hitajika inayo ashiriwa kupitia dalili (Dalalat Al-Iqtida), na sababu haikutajwa, kana kwamba umefahamu kutoka katika Shakhsiya ya Kiislamu katika mfano (mwache mtumwa huru kutoka kwangu) kuwa  inahitaji sharti la umiliki, na hivyo sharti hilo lilitabanniwa katika ufafanuzi, na ukafahamu  kutoka katika (chochote kinacho pelekea wajib nacho pia ni wajib) katika mfano (mithili ya jinsi ya kuacha huru (watumwa) kwa lazima ambapo alieleza kuwa muundo huo ni wa sababu na kudhani kuwa hii kupitia iqtida ni sababu na hivyo kushangaa, kisha, ni kwa nini sababu haikutajwa katika ufafanuzi wa maana ya Dalalat Iqtidha ilhali ni sababu. Na ukauliza ni kwa nini sababu haikutajwa katika ufafanuzi wa Iqtidha huku sharti likitajwa. Jibu ni kuwa kuna tofauti, na hili liko wazi kutokana na uhalisia wa Dalalat Iqtidha (maana inayo hitajika inayo ashiriwa kupitia dalili) na (chochote kinacho pelekea wajib nacho pia ni wajib). Uhalisia huu ni tofauti: Dalalat Iqtidha inatokana na utafiti wa kilugha unao husiana na matamshi ya maneno (Mantouq) na ufahamu wa maneno (Mafhoum) nk., lakini (chochote kinacho pelekea wajib nacho pia ni wajib) ni misingi ya kifiqhi yaani, hukmu kamili; haipaswi kuchanganyikiwa nazo pamoja kwa sababu Dalalat Al-Iqtidha inafahamika kwa misingi ya lugha, lakini misingi ya kifiqhi inafahamika kwa mujibu wa dalili za kisheria ambazo kwazo misingi hiyo imevuliwa yaani, zote zina msingi ambao kwao kila moja imejengwa juu yake kama ilivyo wazi kutokana na fafanuzi zao:

Kwanza: Dalalat Al-Iqtidha (maana inayo hitajika inayo ashiriwa kupitia dalili): wanavyuoni wa fiqhi wametoa fafanuzi tatu muhimu kuhusu Dalalat Al-Iqtidha:

- Kwanza: hakutaja sharti au sababu, bali anataja ishara ya ulazima inayo hitajika na matamshi ya maneno (Mantouq) ya ukweli (Sidq) wa mzungumzaji au uwepo wa lafdh sahihi, na fafanuzi hizi ziko:

* Katika “Al-Ihkam Fi Usul Al-Ahkam” cha Abu Al-Hassan Sayyid ud-Din Al-Aamadi [aliye kufa: 631 H]

[Ufafanuzi wa kwanza Dalalat Al-Iqtidha: ni kile kinacho ashiriwa lakini si kwa njia ya moja kwa moja kupitia muundo wake au hali yake na ambacho hakiko huru; na ima kiwe kimedhamiriwa waziwazi na mzungumzaji au usahihi wa maneno yanayo tamkwa kukihusu uwe umesitishwa au haujasitishwa; ikiwa umesitishwa maana ya lafdh huitwa Dalalat Al-Iqtidha…] Na hivi ndivyo inavyo tajwa katika kitabu changu, Tayseer Al-Wusool Ila Al-Usul.

- Wa pili umedumisha ufafanuzi huo huo, lakini ukaupatia malezo zaidi, na hali yake inazungumzia sharti pekee kwa sababu iliona kuwa sharti ndio kitu cha kwanza kinacho kuja akilini katika ishara ya ulazima kwa matamshi ya maneno, na mengine yanafuata kupitia dalili. Hivyo basi, walipotoa mfano wa kumwacha huru mtumwa, walijadili sharti la kumwacha huru mtumwa huyo ambalo ni umilikaji, na hawakugusia juu ya sababu ya umilikaji, ambayo ndio muundo wake kwa sababu hii haifikiwi kwa Dalalat Al-Iqtidha, bali kwa dalili. Mfano uliowekwa ni "Mwache huru mtumwa wako kutoka kwangu" ambao unafahamika kupitia Iqtidha kama ithbati ya umilikaji kwanza ili kusahihisha uachaji huru mtumwa, na sababu ya kushikilia umilikaji kwa muundo fulani, hii inafahakima kutoka katika dalili za Shariah, na kutoka na fafanuzi hizi ni:

* Katika Al-Mustasfa fi ‘Ilm Al-Usul cha Abu Hamed Muhammad bin Muhammad Al-Ghazali At-Tusi (aliye kufa: 505 H) kinaeleza:

(Sanaa ya pili: ambayo inachukuliwa kutokana na lafdh na sio kutokana na muundo wake bali hata kutokana na yaliyomo ndani yake na maregeleo yake, nazo ni sehemu tano; ya kwanza: ile inayo itwa Iqtidha (maana inayo hitajika), ambayo inaashiriwa na lafdh, na sio matamshi (mantouq), lakini inahitajika na lafdh ima kwa mujibu wa mzungumzaji kutoweza kuwa mkweli isipokuwa kwayo, au maneno ya kisheria hayawezi kuwepo ila kwayo, au haiwezi kuthibitishwa kiakili isipokuwa kwayo. Mfano wa lile linalo thibitishwa kuwa Iqtida' (maana hitajika) kwa maana ya matamshi ya maneno (mantouq) kupitia Shariah ni msemo: "Mwache huru mtumwa wako kwangu"; inajumuisha umilikaji, na inauhitaji japo haujatamkwa, lakini maneno yaliyo tamkwa ya kumwacha huru mtumwa ni sharti la kisheria: umilikaji umetangulia ambalo ni sharti la lafdhi))

Na haya haya ndiyo yaliyotajwa katika “Al-Bahar Al-Muheet Fi Usul AL-Fiqh” na Zarkashi (aliye kufa 794 H).

- Ya tatu ilidumisha maana mbili zilizo tangulia, lakini ikalipa sharti maelezo zaidi; amesema kuwa sharti la maana ni lile linaloiashiria, kupitia uwiano kamili na sio nusu. Miongoni mwa maana hizi:  

* Kwa mujibu wa “Al-Mahsoul fi ‘ilm Al-Usul” na Muhammad bin Omar bin Al- Hussein Al-Razi (606 H):

(Ama kigawanyo cha Dalalat Al-Iltizam, (ishara ya kujifunga), tunasema maana ya kuashiria uwajibu, ima ichukuliwe kutoka katika maana za maneno binafsi au kutoka katika mpangilio wake. Na ya kwanza imegawanyika sehemu mbili kwa sababu maana iliyo kusudiwa kupitia uwajibu huo ni ima sharti la maana iliyo kusudiwa kupitia uwiano au tagaa lake. Ikiwa ni ya kwanza, huitwa Dalalat Al-Iqtida; ile yenye sharti huenda ikawa ni ya kiakili, kama msemo wa Mtume (saw):

«رفع عن أمتي الخطأ والنسيان»

“Ummah wangu umesamehewa kukosea na kusahau”, akili imeashiria kuwa maana hii si halali isipokuwa tujumuishe ndani yake hukmu ya sheria. Yaweza kuwa ya kisheria kama maneno yake: 'Naapa kwa Mwenyezi Mungu nitamwacha huru mtumwa huyu'. Anahitaji kuwa na umiliki; vinginevyo, hawezi kutimiza maneno yake ya Kisheria ila baada yake (umiliki).  

Kama tulivyo sema, fafanuzi hizi tatu kiujumla hazitofautiani ila katika kimaelezo kuhusiana na sharti.

Katika Shakhsiya ya Kiislamu Juzuu 3, tuliona kuwa ufafanuzi kwa mujibu wa utafiti wa lugha ni katika maudhui ya sharti na uwiano (Mutabaqa), hivyo tumesema:   

* (Dalalat Al-Iqtidha ni lazima itoe maana inayo hitajika ya maneno, kupitia kuwa sharti la maana iliyo kusudiwa kupitia uwiano, na kwamba akili ndiyo inayoihitaji, na sheria huenda ukaihitaji, ima kwa ajili ya ukweli wa mzungumzaji au usahihi wa tukio linalo zungumzwa; kwa mfano maneno ya Mwenyezi Mungu (swt)

 (قَاتِلُوا الَّذِينَ يَلُونَكُم

“Piganeni na wale makafiri walio karibu yenu” [At-Tawba: 123]. Maneno yake: (قَاتِلُوا) “Piganeni” inahitaji mkusanyiko wa vifaa, silaha, zana, mafunzo ya kivita, nk. Hili ndilo linalo hitajika na akili; ni sharti la usahihi wa tukio linalo zungumzwa: (قَاتِلُوا) “Piganeni”.

Na kama unapo mwambia mwengine 'Mwache huru mtumwa wako kwa ajili yangu kwa thamani ya dirham elfu moja', maana inayo kusudiwa katika maneno: 'mwache huru mtumwa kwa mauzo au zawadi', na kwamba fahamu hutegemea juu ya utambuzi wa maana hii ya kisheria, kwa kuwa hakuna uachaji huru mtumwa isipokuwa kupitia yule anaye milikiwa na mwanadamu. Kana kwamba imesemwa: 'muuze au nipe (kama zawadi) mtumwa huyu', kisha uwe mwakilishi wangu katika kumwacha huru. Hili ndilo linalo hitajika na sheria, ambalo ni sharti la usahihi wa tukio hilo wa lile lililo tamkwa «أعتق» “mwache huru” na mithili ya maneno yake (saw):

«إِنَّ اللَّهَ وَضَعَ عَنْ أُمَّتِي الْخَطَأَ، وَالنِّسْيَانَ، وَمَا اسْتُكْرِهُوا عَلَيْهِ»

“Mwenyezi Mungu amewasamehe Ummah wangu kukosea, na kusahau, na kutenzwa nguvu” [Ibn Majah], yaani ameondoa hukmu ya kukosea, kusahau, na kutenzwa nguvu. Haiaminiwi kuwa ameviweka vitu hivi hivi ikizingatiwa kuwa pasi na shaka vitatokea; hili ndilo linalo hitajika na sheria, kwa ajili ya kuhitajika ukweli wa mzungumzaji). Kama unavyoona, ni ufafanuzi kamilifu wa Dalalat Al-Iqtidha katika nyanja zake zote na Mwenyezi Mungu ndiye Msaidizi.

Pili: hukmu kamili (kila linalo pelekea katika wajib hilo pia ni wajib); ufafanuzi wake haukomei katika utafiti wa kilugha, bali unakwenda zaidi ya dalili za kisheria. Walikichunguza kitu kinacho hitaji kufanyika ili wajib utekelezwe, ima kiwe ni sehemu yake au kando yako, kama vile sababu, au sharti au kizuizi (Mani') na hawakujifunga kwa hili kupitia Dalalat Al-Iqtidha. Badala yake waliangazia juu ya dalili. Kwa mfano, walipotoa mfano katika mlango wa (kila linalo pelekea katika wajib hilo pia ni wajib), walisema (ima sababu iwe ni halali (kisheria), kama vile uachaji huru mtumwa wa lazima). Ambao ni katika hali ambapo mtumwa huyo ni milki yako, na unataka kumwacha huru, masharti ya umiliki yangalipo, na unataka kufahamu muundo wake; hili ufahamu wake hauko katika Al-Iqtidha bali ni muhimu lijengwe juu ya msingi wa dalili … na tofauti iko wazi kati ya mfano huu wa kuwa ni milki yako na kati ya mfano wa nyuma katika taarifa yako (mwache huru mtumwa wako kwa ajili yangu), hii hufahamika kupitia Iqtidha yaani, ni lazima kwanza umiliki mtumwa  vinginevyo huwezi kumwacha huru ikiwa anamilikiwa na mwengine? Umilikaji ni sharti la kutokea kwa taarifa hiyo (mantouq). 

Na kwa sababu ya dalili hii imetabanniwa hapa, na ijtihad kufanyika, hii ndio sababu kwa nini walihitilafiana juu ya kitu ambacho bila hicho wajib hauwezi kutimizwa; ilisemwa kuwa kitu hiki ni lazima kiwe wajib endapo kitakuwa ni sababu au sharti, ikiwa kitakuwa ni sababu na sio sharti, kikiwa kitakuwa ni sharti na sio sababu au sio hivi wala vile, bali kupitia kukomea kwake (Tawaquf). Ufafanuzi wa hili uko katika “Al-Bahr Al-Muheet” "1/254" cha Zarkashi (aliye kufa 794 H), pia katika “Sharh Al-Kawkab Al-Muneer” 1/182 cha mwandishi "Taqi ud-Din Abu Al-Baqa’ Muhammad al-Futuhi aliye julikana kama Ibn An-Najjar (aliye kufa: 972 H) na kwa wale ambao wanataka kujua zaidi, wanaweza kuvirudia.  

Ufahamu aghalabu kwetu umetajwa katika Shakhsiya ya Kiislamu Juzuu 3, kwa kutegemeza dalili ambayo kwayo misingi hiyo huvuliwa, nao ni kuwa kila kitu kinacho hitajika kwa ajili ya wajib kufanyika hicho pia ni wajib, chochote kile: sababu au sharti, na aina yake yoyote ile. Hivyo basi, baada ya sisi kusema katika ufafanuzi "Chochote kinacho hitajiwa kwa ajili ya kutekelezwa wajib ni katika sehemu mbili: ya kwanza ni kuwa wajib ni sharti juu ya kitu hicho, na ya pili ni kuwa wajib sio sharti kwake, yaani kwa kitu hicho. Ikiwa wajib ni sharti juu yake, hakuna ikhtilafu kuwa kupata sharti hilo sio wajib, bali wajib huo uwajib wake umeletwa na dalili, kama wajib wa swala fulani; twahara ni sharti kwake. Twahara sio wajib kutoka katika hotuba ya swala, bali ni sharti la kutekeleza wajib. Wajib katika hotuba ya swala ni swala yenyewe endapo sharti litapatikana." Baada ya sisi kufafanua uhalisia wa sharti, tulitamatisha utafiti kwa kusema:    

(Kitu ambacho bila yake wajib hautekelezeki pia ni wajib, ima kupitia hotuba ya uwajibu wenyewe, au kupitia hotuba nyIngineyo, ima kitu hiki kiwe ni sababu, ambayo uwepo wake unahitaji kuwepo kwake na kukosekana kwake, kutokuwepo kwake, au sharti, ambalo kukosekana kwake kunahitaji kutokuwepo kwake na kuwepo kwake hakuhitajii kuwepo au kutokuwepo kwake. Ima iwe sababu ni ya kisheria, kama vile muundo wa namna ya kuacha huru mtumwa kwa lazima, ya kiakili, kama vile mtazamo uliopatikana wa ilimu ya wajib, au ya kawaida kama ukataji shingo katika mauwaji ya wajib, na ima sharti pia liwe la kisheria, kama udhu, au la kiakili, ambalo ni muhimu kwa yule aliyeamrishwa kwalo kiakili. Kama kuacha lile lililo kinyume na lililoamrishwa, au la kawaida ambalo kawaida halitenganishiki kwalo, kama kuosha sehemu ya kichwa katika udhu. Wajib wa kitu hicho huwajibisha lile ambalo bila yake wajib hautekelezeki. Yaani, utekelezaji wa kitu hicho huhitajia utekelezaji wa kile ambacho hakiwezi kufanyika bila hicho, na hivyo basi hukmu ya "chochote kinacho pelekea wajib hicho pia ni wajib".) Mwisho

Hivyo basi, jibu la swali la kwanza la ni kwa nini sharti limetajwa katika ufafanuzi wa Dalalat al-Iqtidha na sio sababu liko wazi, kama ilivyo tajwa juu na nalirudia hapa:

(Kwa sababu sharti ndio kitu cha kwanza kinachokuja akilini katika ishara ya ulazima kwa matamshi ya maneno (mantouq) na mengineyo yatakuwa sehemu yake kupitia dalili, hivyo pindi yanapopiga mfano wa kumwacha huru mtumwa, yaligusia juu ya sharti la kumwacha huru mtumwa, ambalo ni umilikaji na hayakugusia sababu ya umilikaji ambayo ndio muundo kwa sababu hili halikufikiwa kupitia Dalalat Al-Iqtidha bali kupitia dalili. Hivyo mfano yaliyotoa "Mwache huru mtumwa wako" hufahamika kupitia Iqtidha na huhakikisha umilikaji kwanza ili kuhalalisha uachaji huru wa mtumwa huyo, na sababu ya mkataba wa umilikaji kwa muundo maalumu hufahamika kutokana na dalili).   

Kama ninavyo jua, wanavyuoni wa kifiqhi hawakuingiza sababu katika kufafanua Dalalat Al-Iqtidha. Hili ndilo jibu la swali la kwanza kama nijuavyo mimi na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi zaidi na Mwingi wa hekima.

Swali la pili: Ni kwa nini ufafanuzi huu unajumuisha:

(Dalalat Al-Iqtidha ndio inayohitajika katika maana za maneno, na lazima iwe ni sharti la maana ya kitu kinacho kusudiwa kupitia uwiano). Kutaja uwiano kamili (mutabaqa) na wala sio sehemu tu (tadhamun) ni kwa sababu ishara ya kukusudia na ishara ya ulazima ni natija ya ishara ya uwiano, yaani sio asili yake na huu hapa ufafanuzi: 

1- Asili ya ishara ni uwiano (Mutabaqa), yaani, ishara ya maana ya neno kwa maana yake kamili, na neno hilo haliongezi sehemu ya maana "yaani (tadhamun)" pekee kupitia upeanaji au ufungaji, kwa maana nyingine, kutokana na sababu yenye kushinikiza pekee kwa mujibu wa utafiti wa kilugha katika sehemu hii.

2- Ishara ya ulazima (iltizam) ni maana ya kiakili ya maana ya tamshi la neno yaani sehemu yake, na kwa kuwa asili katika ishara ya neno ni uwiano, yaani maana halisi, hii ndio jinsi ya umuhimu wa kuwa sehemu yake, yaani, kupitia maana kamili ya "uwiano". Na kwa sababu hii ni muhimu kama ilivyo onyeshwa katika jibu la swali la kwanza kuwa ni sharti katika kupandikiza maana ya tamshi la neno (Mantouq): hivyo basi, ufafanuzi wa Dalalat Al-Iqtidha kama ilivyo elezwa katika Shakhsiya ya Kiislamu Juzuu 3: (Dalalat Al-Iqtidha ni lile linalo hitajika ili kupata maana za maneno, kupitia kuwa sharti la maana inayo kusudiwa kupitia uwiano) 

Kwa kiasi fulani hili liko wazi katika Al-Iqtidha. Kitu kinacho hitajika kupitia dalili, yaani, maana ya kiakili ya dalili, waweza kuwa tu katika uwiano kwa maana kamili na hakuna kinacho tolewa kutokana nayo isipokuwa kupitia dalili, kwa mfano:

- "Pigana" … maana ya kiakili yaani Dalalat Al-Iqtidha ni vifaa vya kupigana katika vita kwa ujumla wa silaha zote ziwezekanazo na haisemwi tu kupitia upanga, na nyinginezo haziingii katika ishara ya ulazima, au kanuni na nyinginezo, na haiingii katika ulazima, na kadhalika, bali kupitia maana kamili ya "uwiano". Kila silaha inayowezekana ambayo yaweza kutumiwa katika vita hujumuishwa katika wajib huu. 

- “Na kiulize kijiji” ... maana ya kiakili yaani Dalalat Al-Iqtidha ni watu wa kijiji. Kaka zake Yusuf (as), walimwambia baba yao kuthibitisha ukweli wa maneno yao kupitia kuwauliza wanakijiji na iko katika maana kamili, yaani muulize kila ambaye ni katika wanakijiji ili uone uhalali wa maneno yetu. Haingii akilini kuwa kaka zake Yusuf walitaka baba yao awaulize baadhi ya wanakijiji na ni marufuku kuwauliza baadhi ya wengine kwa sababu itakuwa ni hoja dhidi yao na upande wao, ambapo walitaka baba yao awaulize watu maalumu wanaokubaliana nao!

Hivyo basi maana hubadilika. Kwa hivyo, Dalalat Al-Iqtidha "الأهل" “watu" ni maana kamili kupitia "uwiano"

- 'Mwache huru mtumwa wako kwa ajili yangu': maana ya kiakili ni kuwa unammiliki basi mwache huru, na umilikaji hapa ni kuwa una umilikaji kamilifu ili uruhusiwe kumwacha huru, yaani kupitia uwiano, "maana kamili" na kadhalika. Hivyo basi, maana ya "maana ya kiakili" ya tamko la neno (Mantouq)" lazima iwe kupitia uwiano, yaani, katika maana yake kamili na hakuna kinachoiondoa kutokana nayo isipokuwa kupitia dalili na sio sehemu ya maana hiyo, yaani Tadhamun.

Nataraji kuwa jibu hili linatosheleza na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi zaidi na ni Mwingi wa hekima.

Ndugu yenu,

Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah

03 Safar 1441 H

Jumatano, 02/10/2019 M

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoAlhamisi, 02 Aprili 2020 20:32

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu