Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Vichwa vya Habari - 04/03/2020

Vichwa vya Habari:

  • Taliban na Amerika wamekubaliana mpango
  • Uturuki Imedengua Ndege za Kijeshi za Syria, na Kuua Mamia ya Wanajehi wa Syria
  • UK ipo Katika Hatari ya Kufelisha Kizazi

Maelezo:

Taliban na Amerika wamekubaliana mpango

Makubaliano ya amani yalisainiwa kati ya Taliban na Amerika kwa mbwembe na nderemo katika mkutano na waandishi wa habari mjini Doha na Kabul. Amerika. Amerika iliwasilisha mpango huo kama mwanzo wa mwisho wa uvamizi wa Amerika, lau Taliban watajifunga na upande wao wa makubaliano hayo. Nguzo muhimu za makubaliano hayo ni dhamana kwamba Taliban hawatoruhusu kundi lolote kuitumia Afghanistan dhidi ya Amerika, muda ambao vikosi vya Amerika vitakapoondoka, kuanza kwa mazunguzo baina ya serikali ya Afghan na Taliban na makubaliano ya amani ya kudumu na kamilifu.

Katibu wa Mambo ya Nje wa Amerika Mike Pompeo alithibitisha kwamba kiuhakika kuna vipengee viwili vya katika mpango huo ambavyo havijawekwa wazi, na hivyo umma wa marekani hautapewa fursa ya kuvijua vipengee hivyo. Kwa kuwa vipengee hivyo ni vya siri mno basi inashaaria viongozi wa Amerika na Taliban wamekubaliana kuvificha ili umma usivijue.

Uturuki Imedengua Ndege za Kijeshi za Syria, na Kuua Mamia ya Wanajehi wa Syria

Vikosi vya Utururki vimeendelea kulisambaratisha jeshi la Syria kwa mfululizo wa mabomu ya droni na mizinga iliyotokea wikendi, na kumuacha mshirika mkuu wa Syria, Urusi kutathmini ni kwa kiwango gani iingiliekati kusitisha mashambulizi hayo. Uturuki imefanya mashambulizi hayo kuwa ndio kipaumbele chake ikitumia zaidi mashambulizi ya anga kutoka katika droni za kisasa na ndege za F-16s zilizo na teknolojia ya kisasa — na kupelekea kuangushwa ndege mbili za kivita za Syria, helikopta 8, vifaru 135, na magari 77 ya kijeshi na wanajeshi 2,500 wa Syria kufariki, kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa Wizara ya Ulinzi ya Uturuki. Na hivyo kupelekea jeshi la Syria kushindwa kuhudumia vikosi vyake vilivyopo msitari wa mbele vilivyolengwa makomboro kiustadi. Na huku Urusi ikiwa haioni haja ya kwenda vitani moja kwa moja na Uturuki, jeshi la Bashar al-Assad linaweza kuendelea kupata tabu, na kutoa mwanya kwa Uturuki kufikia lengo lake la kuvifurusha vikosi vya utawala nje ya Idlib.

Uturuki imesambaza takribani wanajeshi 7,000 katika maeneo yanayodhibitiwa na waasi katika mji wa Idlib, ambao ulikaribia kuanguka baada ya mashambulizi ya mwezi mzima kutoka kwa jeshi la Syria na huku likitishia kusababisha kufurika kwa wakimbizi milioni moja katika mpaka wa Uturuki. Imechukua miaka tisa Uturuki kulituma jeshi lake na kuvilenga vikosi vya Bashar al asad. Tukio hilo linaonyesha wazi kuwa Uturuki haikuwa na tatizo la nguvu za kijeshi bali ni kisiasa.

UK ipo Katika Hatari ya Kufelisha Kizazi

Kuzidi kwa vurugu, matumizi ya dawa za kulevya na matatizo ya afya ya kiakili miongoni mwa vijana nchini UK inamaanisha mujtama upo katika hatari ya “kufelisha kizazi,” kwa mujibu wa madaktari wa watoto wanavyosema. Mabarobaro Waingereza wanazidi kuwa karibu na kujeruhiwa kutoka na vurugu za vijana na UK iko nyuma ya nchi nyingine ndani ya Ulaya katika kudhibiti vifo vya watoto wachanga kwa mujibu wa utafiti mpana nchini UK kuhusiana na hali ya afya ya mtoto uliofanywa na Chuo cha Kifalme cha Watoto na Afya ya Watoto. Idadi ya watoto wanaoishi katika umasikini, walioko chini ya mipango ya kuwalinda na “kuwatizama” imezidi tangu ripoti ya 2017, na maendeleo kuhusiana na afya ya kiakili miongoni mwa watoto wa miaka mitano hadi 15 yamesita au yamerudi nyuma.

“Sio jambo zuri kulitizama,” alisema rais wa chuo, Prof Russell Viner. “Katika mikakati mingi muhimu tunahatari ya kuwa nyuma ya nchi nyingine za Ulaya. Tuko katika hatari ya kufelisha kizazi lau hatutoibadilisha hali hii. Serikali imetoa matamshi ya kuvutia kuhusiana na uzito wa utotoni na afya za kiakili za watu lakini tunahitaji kutimiza haya na sehemu nyingine.”

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoAlhamisi, 19 Machi 2020 09:23
Yaliyomo ndani ya kifungu hichi: Vichwa vya Habari - 06/03/2020 »

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu