Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Uhakiki wa Habari: 21/06/2023

Kambi ya Siri ya China nchini Cuba

Maafisa wakuu wa Marekani wanaamini kuwa Beijing iko kwenye mazungumzo na Cuba ili kuanzisha kambi iliyo umbali wa maili 100 kutoka pwani ya Florida, ili kukusanya taarifa za kijasusi kusini mashariki mwa Marekani. Haitakuwa mara ya kwanza kwa China kujaribu kupeleleza mawasiliano ya kielektroniki ya Marekani, inayojulikana kama ujasusi wa ishara. Puto la kijasusi linaloshukiwa kuwa la China lililopitia Marekani mwezi Februari lilikuwa na uwezo wa kukusanya taarifa za kijasusi na inaaminika kuwa zilirushwa hadi Beijing katika muda wa karibu, vyanzo viliiambia CNN wakati huo. Ufichuzi huo kuhusu uwezekano wa kambi ya kijeshi ya China nchini Cuba unakuja wakati mahusiano kati ya Marekani na China yamefikia kiwango cha chini, kufuatia tukio la puto hilo la kijasusi na mienendo kadhaa ya kichokozi ya ndege na meli za China dhidi ya mali za Marekani katika Bahari ya Kusini ya China.

Cuba daima imekuwa muhimu kwa Marekani kwa sababu inasimamia ufikiaji mpana wa Marekani kwa ulimwengu na vile vile njia za Florida. Kwa kuwa chini ya maili 100 kutoka Florida, kudhibiti Kisiwa kikubwa zaidi cha Caribbean ni muhimu mno kijiografia kwa Marekani. Endapo dola nyengine itakuwa na udhibiti juu ya Cuba, watakuwa na uwezo wa kuzuia meli za Marekani na miradi ya ulinzi kuelekea kusini mashariki mwa Marekani.

China Yaimarisha Diplomasia Mashariki ya Kati

China imejitolea kuwa mpatanishi kati ya makundi hasimu ya Palestina na kuwezesha mazungumzo ya amani na 'Israel', katika ishara ya hivi karibuni ya dhamira ya Beijing ya kupanua dori yake ya kidiplomasia katika Mashariki ya Kati. Katika mkutano kati ya rais Xi Jinping wa China na mkuu wa Mamlaka ya Palestina (PA), Mahmoud Abbas, jijini Beijing mnamo tarehe 14 Juni, viongozi hao wawili pia walisema kwamba wametia saini ushirikiano wa kimkakati. Katika hotuba yake mwanzoni mwa mkutano wake na Abbas, Xi alisema Beijing inaunga mkono "sababu ya haki ya watu wa Palestina kuregesha haki zao halali za kitaifa" na kwamba "iko tayari kucheza dori kubwa katika kuisaidia Palestina kufikia maridhiano ya ndani na kukuuza mazungumzo ya amani”.

Xi alisisitiza uungaji mkono wa hapo awali wa China kwa suluhisho la dola mbili kwa mzozo wa 'Israel' na Palestina, kwa msingi wa mipaka ya kabla ya 1967 na Jerusalem Mashariki kama mji mkuu wa taifa huru la Palestina, na pia alitetea kuwepo msaada wa maendeleo ya kimataifa kwa Wapalestina. Pamoja na mshirika wake mkuu, Urusi kushuka nchini Ukraine China imejaribu kujionyesha kama mpatanishi wa kimataifa. Lakini wakati nchini Ukraine mapendekezo yake hayakuchukuliwa kwa uzito, nchini Palestina, Beijing inatoa wito wa mpango wa Marekani kwa eneo hilo, ambao kwa muda mrefu umekuwa ni suluhisho la dola mbili.

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu