Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 

Vichwa vya Habari 6/12/2022

Vichwa vya Habari:

  • Nchi za NATO Zaishiwa na Silaha huku Ujerumani Ikisalia na Akiba ya 'siku 2'
  • Kwa nini Ulaya lazima Iachane na Marekani kuhusu Sera ya China ili Kuepusha Maafa ya Kiuchumi Duniani
  • COAS sio Waziri Mkuu ndiyo huamua Mafungamano ya Marekani na Pakistan

 

Maelezo:

Nchi za NATO Zaishiwa na Silaha huku Ujerumani Ikisalia na Akiba ya 'siku 2'

Vita nchini Ukraine vimefichua udanganyifu mkubwa katika udhibiti mpya wa hifadhi za silaha baada ya Vita Baridi, na kuacha baadhi ya nchi zikijitahidi kukabiliana na mahitaji ya ulinzi. Ujerumani imekuwa ikikabiliwa na shinikizo la kudumisha dhamira yake ya ulinzi kwa NATO huku ikiipa Ukraine silaha zinazohitajika ili kukabiliana na Urusi. Kulingana na ripoti za ndani, Jeshi la Ujerumani limebakiwa na silaha za "siku mbili" pekee ili kuendeleza mapambano changamfu inapohitajika. Mtaalamu wa masuala ya Ujerumani Oliver Moody alibainisha kuwa Berlin sio nchi pekee ya NATO iliyoachwa ikikabiliwa na masuala ya akiba huku akibainisha mwisho wa Vita Baridi karibu miaka 30 iliyopita ulileta mabadiliko kuelekea aina zaidi za kiteknolojia za vita, na kuacha akiba ya silaha kuwa chache. Mwandishi wa Berlin aliiambia Times Radio: "Ni muhimu kusema hili si tatizo la Ujerumani pekee. Ni tatizo sehemu kubwa ya Ulaya. Kimsingi, matumizi kwa ajili ya ulinzi yalipunguzwa katika dola nyingi za Ulaya baada ya kumalizika kwa Vita Baridi na kisha, haswa katika miongo miwili iliyopita tangu 9/11, kumekuwa na aina ya usanidi kuelekea silaha mahiri kwa vitu kama vile kupambana na uasi, teknolojia ya hali ya juu, mizozo isolingana kiuwezo. "Na kisha kwa ujio wa vita nchini Ukraine, ni wazi kiasi kikubwa sana cha silaha, hasa, makombora haya ya millmitre 155 yamehamishiwa hadi Kikosi cha Wanajeshi wa Ukraine." Bw Moody aliendelea: "Kinachotofautisha kuhusu Ujerumani ni kwamba tatizo hili limejulikana kwa muda mrefu sana, kwa kiasi fulani ukubwa wake kwa kuwa inaonekana watahitaji kutumia angalau euro bilioni 20 kujaza upya akiba ili kukidhi mahitaji ya chini ya NATO. "Na hatimaye, kwamba majibu yamekuwa ya polepole sana kwamba bado hawajaweka maagizo yoyote ya maana. Wamepata tu bilioni 1.1 zilizotengwa kwa ajili ya silaha katika mwaka ujao licha ya kuwa na hazina ya uwekezaji ya bilioni 100 kwa ajili ya vikosi vyao vya kijeshi." Ujerumani imepitia mabadiliko ya kihistoria kufuatia uvamizi wa Ukraine, ikitangaza mipango ya kutuma silaha kusaidia Serikali ya Kyiv katika msukumo wake dhidi ya Urusi muda mfupi baada ya uvamizi huo kuanza Februari. Lakini uamuzi wa Olaf Scholz ulizusha mzozo wa ndani ambao hadi leo umeacha msimamo wa Ujerumani kuhusu vita vya Ukraine kugawanyika. [Chanzo: Daily Express]

Vita vya Iraq, Afghanistan na Ukraine vimefichua uhalisia wa dola kubwa wa kutoweza kushinda vita visivyolingana kiuwezo. Na sasa uhaba wa silaha sisitiza tu kwamba msimamo mmoja wa Waislamu chini ya Khilafah haungeweza tu kuukomboa ulimwengu wa Kiislamu bali pia kuzinyenyekesha dola za kigeni kote ulimwenguni.

Kwa nini Ulaya lazima Iachane na Marekani kuhusu Sera ya China ili Kuepusha Maafa ya Kiuchumi Duniani

Mtazamo kwamba uchumi wa dunia unatarajia kugawanyika katika kambi mbili hasimu - moja ikiongozwa na Marekani na nyingine na China, huku wengine wakiwa "wafuasi wa kambi" - kwa bahati mbaya unazidi kuimarika. Lakini uhalisia huu itatimia ikiwa tu utakubaliwa na sio kupingwa vikali. Mgawanyiko mkubwa hautatokea mara moja, lakini uko njiani. Bado kungali na wakati wa kubuni hatua za kupambana na kuunda nguzo za kupambana na usawazishaji wa ushawishi, lakini hii itahitaji hatua kali za kisera kwenda nje ya uwanja wa Marekani-China. Kichocheo kinachowezekana cha mabadiliko kinaonekana, ingawa yatakuja tu kwa gharama ya mdororo mkubwa wa kiuchumi. Ni kwamba matarajio ya kuongezeka kwa matatizo ya kiuchumi barani Ulaya na Marekani yatawalazimisha wanasiasa kutabanni mitazamo isiyopinda ya kimfumo. Gharama ya kutochukua hatua inaweza kuwa mbaya sana. Kwa upande wa kiuchumi, mfumko wa bei unaweza kukita mizizi kwa sababu uzalishaji wa bidhaa utakuwa chini ya ufanisi na wenye gharama kubwa zaidi katika mfumo wa uliosambaratika wa kiulimwengu. Kadiri bei zinavyopanda, ndivyo pia mahitaji ya mishahara yanavyo panda, na kadhalika. Biashara na uwekezaji kati ya uchumi wa dola hizo mbili zenye nguvu zitaathirika kadiri vikwazo na hatua za kupambana na vikwazo zitakavyoongezeka, na hatima ya kiuchumi ya dola zengine ambazo yamepunguzwa hadi kuwa satelaiti za dola hizi mbili zitateseka kama matokeo yake. Makabiliano ya kinguvu yatakuwa uwezekano halisi.

Hakuna dola nyengine yoyote kipeke yake inayoweza kushindana, katika suala la nguvu ya kiuchumi na kidiplomasia, na dola yenye uchumi mkubwa zaidi na yenye uchumi wa pili kwa ukubwa zaidi duniani, na miungano mipya kati ya mataifa mengi madogo hautakuwa magumu sana. Ni jumuiya pana pekee ya Ulaya ndio inayoweza kutoa nafasi ya tatu inayohitajika. Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na Waziri Mkuu wa Uholanzi Mark Rutte wameonyesha nia ya kutofautisha msimamo wao kuhusu China na ule wa Marekani. Chansela wa Ujerumani Olaf Scholz hivi karibuni aliongoza ujumbe wa biashara na nia njema nchini China. Hilo linaweza kuwa pendekezo la umoja wa Ulaya. Msimamo wa Uingereza kuhusu China pia utahitaji kubadilika. Dori ya Uingereza inaweza kuwa muhimu sana, ingawa ya kufifisha hadhi ya Uingereza machoni mwa ulimwengu kwa sasa kama matokeo ya kuchanganyikiwa ambayo nchi hiyo imetoa ya kusimamia mambo yake ya kisiasa chini ya Chama tawala cha Conservative. Inavutia kuona ushindani wa Marekani na China kama vita kati ya wema na uovu, kati ya demokrasia na udikteta. Kuna ukweli fulani katika madai haya, lakini tatizo hakika ni kuhusu ushindani wa kiuchumi, ambao unajivisha guo la kuwa wasiwasi juu ya haki za binadamu na masuala ya usalama. Ulimwengu unahitaji kufikiria jinsi ya kukwepa msisimko wa mitazamo finyu kama hii ambayo inaweza tu kusababisha mwisho mbaya. Ili hilo litokee, tunahitaji kipengele kipya cha kusawazisha katika mlingano wa nguvu za kiulimwengu, na mwamko zaidi wa Ulaya unaonekana kuwa ndio chaguo pekee linalowezekana kwa sasa. [Chanzo: South China Morning Post]

Ni dhahiri kabisa Marekani imetumia vita vya Ukraine kudhoofisha Urusi pamoja na Ulaya. Lengo jengine la Amerika ni China, na hadi sasa Beijing haijaingia kwenye mtego wa Taiwan uliowekwa na Amerika. Hata hivyo, Wachina hawana nafasi ya kuishawishi Ulaya kujitenga na Amerika. Kuna uwezekano zaidi kwamba Amerika itaisukuma Ulaya mbali na China na hivyo kuutenga uchumi wa China.

COAS sio Waziri Mkuu ndiyo huamua Mafungamano ya Marekani na Pakistan

Kuregea kwa waziri mkuu wa zamani Imran Khan madarakani - au la - hakutakuwa na athari kubwa kwa mustakabali wa mahusiano ya Marekani na Pakistan kwani maamuzi kama hayo jijini Islamabad yanachukuliwa na mkuu wa jeshi, sio waziri mkuu. Mtazamo huu ulitolewa katika semina ya Jumatatu jioni katika mji mkuu wa Marekani. "Sidhani kwamba mustakbali wa mahusiano kati ya Marekani na Pakistan unategemea nani atakuwa Waziri Mkuu nchini Pakistan ... muhimu zaidi ni nani atakuwa mkuu wa majeshi," alisema Lisa Curtis, ambaye alisimamia masuala ya Asia ya Kusini na Kati katika ikulu ya White House wakati wa Trump, akiongeza kuwa jeshi ndilo linalodhibiti ufanyaji maamuzi kuhusu masuala muhimu kwa Marekani, kama vile mpango wa nyuklia, mahusiano ya Pakistan na India, na kupambana na ugaidi. Lakini Bi Curtis pia alisema aina hii ya demokrasia mseto haitakuwa nzuri kwa Pakistan kwani ni "aina ya serikali isiyo na utulivu". Alipoulizwa jinsi kuregea kwa Bw Khan kunaweza kuathiri mahusiano ya Marekani na Pakistan, alisema: "Ingawa Imran Khan aliitumia Marekani kama mbuzi wa kafara alipopoteza mamlaka, kama angechaguliwa tena, kutakuwa na kiasi fulani cha uhalisia ambao unaweza kuwa sehemu ya mlingano." Anaamini kungekuwa na "juhudi ya kufanya marekebisho uhusiano na Washington". Douglas London, mfanyikazi wa zamani wa CIA na mchambuzi; Javid Ahmad, balozi wa zamani wa Afghanistan katika Imarati; na Hussain Haqqani, balozi wa zamani wa Pakistan jijini Washington pia walishiriki katika mjadala huo. Marvin Weinbaum, mkurugenzi wa Mafunzo ya Pakistan/Afghanistan katika Taasisi ya Mashariki ya Kati (MEI), Washington, alisimamia kikao kilichoandaliwa na taasisi yake. Bi Curtis na Bw Haqqani wanaamini kuwa Pakistan na Marekani hazikuwa karibu kama wakati Marekani ilipokuwa bado Afghanistan. Bi Curtis alisema Marekani ilitaka kuhakikisha Pakistan haisongei karibu na China na kwamba maoni hasi ya Islamabad kuhusu Afghanistan bado yanatawala. Marekani, aliongeza, "inataka Pakistan kuiunga mkono nchini Ukraine". Bw London alibainisha kuwa mvutano kati ya nchi hizo mbili umepungua tangu Marekani ijiondoe kutoka Afghanistan, na Washington haikutaka kuipoteza Islamabad kabisa kwani ni dola ya nyuklia. Sasa, alisema, kulikuwa na "uwazi zaidi" kati ya huduma za ujasusi na kijeshi za nchi hizo mbili, lakini "nyenzo kidogo". [Chanzo: Alfajiri]

Maadamu uongozi wa sasa wa kiraia na jeshi unaendelea kutawala, Raj wa Marekani nchini Pakistan atashinda bila kuzuiwa. Khan na wengine kama yeye hawataweza kamwe kuwakomboa Wapakistan kutoka kwa Pax Americana. Ni Khilafah pekee kwa njia ya Utume ndiyo itaweza kukomboa Pakistan na Waislamu kote ulimwenguni kutoka kwa dola za kigeni.

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu