Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Vichwa vya Habari 16/11/22

Vichwa vya Habari:

Makombora ya Urusi Yapotea Njia na Kuanguka Poland

Taliban Yatoa Maagizo ya Utabikishwaji Kikamilifu wa Adhabu za Kisharia

Maelezo:

Makombora ya Urusi Yapotea Njia na Kuanguka Poland

Urusi ilianzisha mashambulizi ya anga dhidi ya Ukraine, siku chache tu baada ya kujiondoa kidhalilifu kutoka kwa mji wa Kherson. Kombora moja lilitua katika mpaka wa Ukraine nchini Poland na kuua watu wawili. Kombora hilo lilitua karibu na Przewodow, chini ya maili tano kutoka mpaka wa Ukraine na takriban maili 40 kaskazini mwa Lviv, Ukraine. Waziri Mkuu wa Poland aliitisha mkutano wa dharura wa usalama katika Umoja wa Mataifa na kuna mazungumzo ya Poland kutumia Kifungu cha 5 cha Mkataba wa NATO, kulazimisha kila mwanachama mwingine kuitetea Poland. Urusi haijatangaza rasmi vita dhidi ya Poland au NATO, lakini ongezeko hili litaijaribu azma ya NATO.

Taliban Yatoa Maagizo ya Utabikishwaji Kikamilifu wa Adhabu za Kisharia

Kiongozi Mkuu wa Taliban wa Afghanistan Mullah Haibatullah Akhundzada aliamuru utabikishwaji na utekelezwaji kamili wa sheria ya Kiislamu, kulingana na tweet kutoka kwa msemaji wa Taliban Zabihullah Mujahid. Mujahid alimnukuu Akhundzada akisema kwamba kesi za jinai "ambapo masharti yote ya Sharia ya Hudud na Qisas yametimizwa, ninyi mnawajibika kutabikisha. Hii ni hukmu ya Sharia, na amri yangu, ambayo ni wajibu." Tangazo hilo huenda likawa ni jibu la shinikizo kutoka kwa maafisa wa Taliban ambao wanaona harakati hiyo na serikali ya Kabul zinalegeza msimamo ujumbe wa harakati ili kupata uhalali wa kimataifa. Tangu kuchukua mamlaka ya Afghanistan Taliban wamekuwa wakijaribu kuleta utulivu katika taifa hilo la milimani, lakini kufungiwa kwa mali za kimataifa na misaada ya kiuchumi kumezuia mipango hiyo. Kwa upande wa sera ya kigeni Taliban wameweka uhusiano wazi na mataifa yote ya kikanda kwa matumaini ya kupata manufaa ya kibiashara.

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu