Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

  Uhakiki wa Habari 17/09/2022

Putin awa na Kongamano Alilokosa Utulivu huko Asia ya Kati

Kujikwaa kwa Urusi juu ya Ukraine na vinginevyo inapelekea udhaifu wake wa kimataifa unaoongezeka. Katika mkutano wa SCO wiki hii, unaojumuisha China pamoja na dola za Asia ya kati, kukosa utulivu kwa Putin kulionekana.

Kulingana na Financial Times:

Muda mfupi kabla ya shambulizi lake dhidi ya Ukraine, rais wa Urusi alikutana na Xi Jinping wa China jijini Beijing ambaye alitangaza "ushirikiano usio na mipaka" na Urusi. Hata hivyo katika mkutano wa kwanza wa wawili hao tangu uvamizi huo, Putin wiki hii alikubali "maswali na wasiwasi" ya kiongozi wa China kuhusu "mgogoro wa Ukraine". Maoni yake, katika mkutano wa kilele wa Uzbekistan iliyokuwa chini ya Usovieti, yalionekana kuwa makubalino ya kwanza ya hadharani ya tofauti kati yake na Beijing juu ya mzozo huo.

Akiwa njiani kuelekea kwenye mkutano huo, Rais Xi alichukua hatua isiyo ya kawaida ya kutoa usaidizi kwa rais wa Kazakhstan Kassym-Jomart Tokayev katika kutetea ubwana na heshima ya nchi yake iwapo itakabiliwa na "kuingiliwa na majeshi yoyote". Kwa kuwa chanzo kinachowezekana zaidi cha uingiliji ni Moscow - Kazakhstan kaskazini ina idadi kubwa ya Warusi - maneno hayo yalionekana kama onyo la siri kwa Putin.

Siku moja baada ya mabadilishano ya Putin na Xi, Narendra Modi wa India pia alikashifu hadharani uvamizi wa Ukraine kwa mara ya kwanza, akimwambia kiongozi wa Urusi katika mkutano huo huo kwamba sasa "sio enzi ya vita". Modi aliongeza kuwa "alizungumza nawe kwa simu kuhusu hili". Maoni haya ya Waziri Mkuu wa India yaliongeza maana kwamba, baada ya vikwazo vya kijeshi vya Urusi, ushawishi ulikuwa imeshavunjwa.

Uongozi wa Urusi, mwingi wake ukitoka katika huduma za usalama badala ya kutoka kwa vyama vyake vya kisiasa, hauna ujuzi na ufahamu wa kisiasa wa kusimamia uhusiano wa kimataifa wa Urusi. Nguvu ya kijeshi ina thamani kubwa. Lakini dola kubwa haitaweza kutumia vyema nguvu zake bila ya uongozi wa kisiasa wenye uwezo.

Uislamu umetoa kipaumbele kwa uongozi wa kisiasa juu ya uongozi wa kijeshi. Khalifah anawekwa na Ummah wa Kiislamu kupitia bay’ah aliyopewa. Kisha anachukua amri ya moja kwa moja ya jeshi, akihakikisha utiifu wa jeshi kwa uongozi wake. Fauka ya hayo, kumhesabu sio tu haki ya Ummah bali ni wajibu juu yao.

Kwa idhini ya Mwenyezi Mungu (swt), Ummah wa Kiislamu hivi karibuni utalipindua tabaka la watawala vibaraka wanaotawala mambo yao hivi sasa na kuwabadilisha kwa uongozi wa kisiasa wenye ikhlasi, na uwezo utakaofanya kazi ya kuunyanyua Ummah wa Kiislamu kwa mara nyingine tena kwenye nafasi yake stahiki kama taifa linaloongoza duniani, kwa kusimamisha Dola ya Kiislamu ya Khilafah kwa njia ya Mtume (saw) ambayo itaunganisha ardhi zote za Kiislamu, kukomboa maeneo yanayokaliwa kwa mabavu, kutabikisha sharia ya Kiislamu, kuregesha mfumo kamili wa maisha wa Kiislamu na kubeba nuru ya Uislamu kwa ulimwengu mzima. Dola ya Khilafah itajiunga, kuanzia kuasisiwa kwake, na safu za dola kubwa kwa vigezo vya ukubwa wa eneo lake, idadi kubwa ya watu wake, rasilimali nyingi, jiografia isiyo na kifani na mfumo wa kipekee wa Kiislamu. Dola ya Khilafah itakabiliana, kuzidhibiti na kuzituliza dola nyenginezo kubwa za kiulimwengu na kuiregesha dunia kwenye amani na ustawi wa jumla uliokuwepo hapo awali katika kipindi cha miaka elfu moja ambayo hapo awali Uislamu ulishikilia uongozi wa dunia.

Maafa ya Mafuriko ya Pakistan ni Kufeli kwa Mfumo wa Kiulimwengu wa Kirasilimali

Kiwango kibaya cha mafuriko nchini Pakistan kinatarajiwa kuwa na madhara makubwa katika miezi na miaka ijayo.

Kwa Mujibu wa Sera ya Kigeni:

Kulingana na makadirio ya awali, asilimia 65 ya mazao makuu ya chakula nchini Pakistan —ikiwemo asilimia 70 ya mpunga—yamesombwa na mafuriko, na mifugo milioni 3 imekufa. Waziri wa mipango wa Pakistan anasema asilimia 45 ya ardhi ya kilimo sasa imeharibiwa. Eneo kama hilo ni la thamani katika nyakati bora zaidi: Katika eneo lote la ardhi la Pakistan, chini ya asilimia 40 ndiyo inayolimwa, na mmomonyoko wa ardhi unaleta uharibifu mkubwa kwenye ardhi ya kilimo…

Mgogoro wa chakula nchini Pakistan utakuwa na athari za kimataifa. Nchi hiyo ni ya nne kwa mauzo ya mchele duniani, ikiwa na wanunuzi kuanzia China hadi Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara. Kushuka kwa kiasi kikubwa kwa mauzo ya nje kutaongeza tu uhaba wa chakula duniani unaochochewa na kupungua kwa mauzo ya ngano kutoka Ukraine, ingawa hifadhi kubwa ya mchele duniani inaweza kupunguza pigo. Pakistani pia inauza nje mazao mengi yasiyo ya chakula, hasa pamba.

Majanga ya kimaumbile pasina budi huizidi nchi yoyote. Kinyume na dhana ya watu wengi, nchi za Kiislamu zina uwezo mkubwa wa kustahimili majanga kama haya kwa sababu ya mienendo yao ya kijamii yenye nguvu inayokuuza familia na jamii imara. Lakini mifumo ya kigeni inayotabikishwa katika ardhi za Kiislamu inaendelea kuhujumu nguvu zetu.

Pakistan iko katika hatari zaidi ya mgogoro wa tabianchi kwa sababu uchumi wake umeasisiwa juu ya msingi wa kilimo badala ya msingi wa viwanda. Chini ya utawala wa Kiislamu, India ilikuwa ni nguvu ya kiviwanda inayoongoza, viwanda vyake vilijulikana kote duniani. Lakini ukoloni wa Uingereza uliiondoa India katika viwanda na kuinyonya kwa ajili ya kilimo chake, malighafi na vibarua. Ugawanyaji wa Uingereza wa India uliunda Pakistan iliyo na uwezo dhaifu wa kiviwanda. Zaidi ya hayo, Waingereza waliondoka Pakistan sio tu kwa msingi wa kilimo bali pia mauzo ya nje. Kipaumbele kinatolewa kwa yale mazao ambayo yanaweza kusafirishwa nje ya nchi badala ya yale yanayohitajika na wenyeji. Pakistan mara nyingi inahitaji kuagiza mazao ya kilimo pia. Mtindo unaoegemea kusafirisha nje sio mahususi tu kwa Pakistan pekee bali kwa nchi zisizo za Magharibi kwa jumla. Mfumo wa uchumi wa kinyonyaji wa Kirasilimali tayari umesababisha uchumi wa nchi za Magharibi kushindwa pakubwa; wanategemea sana kwa ajili ya kiwango chao cha juu cha maisha, mazao na juhudi za kwengineko duniani.

Hii ni kinyume na utabikishaji wa Uislamu nchini India na ulimwengu wote wa Kiislamu ambao ulitoa mfumo wa haki ambamo kwao misingi sahihi ya kijamii na kiuchumi iliweza kuendelezwa na kuimarika. Uzalishaji mkubwa katika ardhi za Kiislamu ulileta ustawi sio tu kwa Waislamu bali kwa ulimwengu mzima, kupitia sera za biashara za Uislamu zilizo wazi na za ukarimu. Kwa idhini ya Mwenyezi Mungu (swt), Dola ya Khilafah itakayosimamishwa upya itaupindua mfumo wa sasa wa kinyonyaji wa kiulimwengu na kujenga upya mahusiano ya haki ya kijamii na kiuchumi yanayonufaisha Umma wa Kiislamu na wanadamu wote.

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu