Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Vichwa vya Habari: 13/08/2022

Vichwa vya Habari:

• Onyo la Amerika: Nchi za Afrika Kuadhibiwa endapo Zitafanya na Biashara Bidhaa Zilizowekewa Vikwazo

• Mwaka Mmoja tangu Kuondoka kwa Amerika nchini Afghanistan, Baadhi Wamefadhaishwa na Kutosomwa Mafunzo

• PTI Yaajiri Makampuni Kuboresha Sura Yake nchini Amerika

Maelezo:

Onyo la Amerika: Nchi za Afrika Kuadhibiwa endapo Zitafanya Biashara na Bidhaa Zilizowekewa Vikwazo

Mataifa ya Kiafrika yapo huru kununua nafaka kutoka Urusi lakini yatakumbana na matokeo endapo yatafanya biashara kwa bidhaa zilizowekewa vikwazo mfano mafuta ya Urusi, Balozi wa Amerika katika Umoja wa Mataifa alionya. “Nchi zinaweza kununua bidhaa za kilimo za Urusi, ikiwemo mbolea na ngano,” Linda Thomas-Greenfield alisema alipo zuru mji mkuu wa Uganda Kampala, baada ya kukutana na Rais wa nchi hiyo Yoweri Museveni. Museveni ni mshirika wa Amerika, ambaye, hata hivyo, hajapinga uvamizi wa Urusi nchi Ukraine na ameonyesha huruma kwa Moscow. Aliongeza kwamba endapo nchi itaamua kuamiliana na Urusi na mahali palipo na vikwazo, basi hiyo nchi, “itakuwa imejiweka kwenye hatari ya kuchukuliwa hatua dhidi yake.” Safari yake hiyo imekuja wiki moja baada ya safari ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Sergey Lavrov kuitembelea Afrika ambaye alipinga vikali shutuma kwamba uvamizi wa nchi yake wa Ukraine ndio unaohusika pekee kwa mgogoro hatari wa chakula unaoanzia Sudan Kusini hadi Somalia. Amelaumu “muitikio usiostahili wa Magharibi, iliyo tangaza vikwazo” kwa uhaba wa chakula katika masoko kufuatia mzozo wa kivita na Ukraine. Ukraine na Urusi ndio wasambazaji wakubwa wa ngano, mawele, mafuta ya uto na alizeti, na aina nyingine za nafaka duniani, kutokana na mapambano yanayoendelea katika Ukanda wa Bahari Nyeusi, unaofahamika kama “kapu la chakula duniani,” ikapelekea kupanda kwa bei, ikitishia ustawi wa kisiasa katika mataifa yanayoendelea na kupelekea nchi kupiga marufuku uagizaji wa baadhi ya vyakula. Nchi nyingi za Afrika — zikiwemo baadhi zilizo kwenye ukingo wa baa la njaa — zinategemea zaidi uagizaji wa nafaka kutoka Urusi na Ukraine. [chanzo: North African Post]

Mpango mkakati wa Amerika kwa nchi za Afrika ni kuadhibu nchi za Afrika kutokana na kununua chakula kutoka Urusi. Mchuano mpya wa Amrika kugombea Afrika unalenga zaidi kuipiga marufuku Urusi na China kuzinyonya rasilimali za nchi za Afrika. Badala yake, Amerika inataka kufanya ukoloni mambo leo peke yake kwa kuitoa Urusi na China nje ya mchuano.

Mwaka mmoja baada ya Amerika kuondoka Afghanistan, Baadhi Wamefadhishwa na Kutosomwa Mafunzo

Tarehe 21 mwezi wa saba, mamia ya wanadiplomasia na maafisa mbali mbali wa usalama wa Amerika kutoka Wizara ya Kigeni ya Amerika, walituzwa zawadi tofatuti tofauti za ushujaa za kifahari za wizara hiyo kwa kusaidia kuwahamisha watu 124,000 kutoka Kabul mnamo Agosti 2021, ikiwa ni pamoja na Raia wa Amerika, wakaazi halali wa kudumu na makumi ya maelfu ya washirika wa Afghan. “Walifanya kazi kwa karibu na Wizara ya Ulinzi, na taasisi nyengine muhimu, na wakatoa muundo wa uongozi katika kusaidia na kuwepesisha operesheni za wizara hiyo katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Hamid Karzai kati ya tarehe 15 hadi 30 Agosti,” Msemaji mmoja wa Wizara ya Kigeni aliiambia VOA. Mmoja wa wanufaikaji aliyehojiwa na VOA, kwa sharti la kutotambushwa, kuhusu hali ilivyokuwa, aliimithilisha sherehe ya tuzo hiyo na  “tiba ya kundi” iliyosaidia kuweka muktadha hisia yake ya unyonge wakati wiki mbili za uchovu na hatari za kuwasafirisha kwa ndege Waamerika na Waafghan huku Kabul haraka ikianguka kwa Taliban. “Hakika tulimenyeka kweli kweli”, alisema. “Tulitazama bila ya uwezo yale ambayo hatukuweza huyafanya, maisha tuliyoshindwa kuyaokoa.” Baada ya operesheni kuisha, asema alipata matibabu ya afya ya akili na alitumia muda mwingi mwaka uliopita kufikiria yaliotokea kwa miaka 20 ya vita na tukio la machufuko lililotokea wakati wa vikosi kuondoka — shambulizi la kuijitoa mhanga lililoua watu 180 ikiwa ni pamoja na wanajeshi 13 — na kuwaacha nyuma makumi ya maelfu ya washirika wa Kiafghan. Yeye na wengine waliohusika na usafirishaji halaiki kwa ndege walionyesha kufadhaika kwa kile wanachokiona kama ukosefu wa uwazi kwa utawala juu ya mafunzo yaliyopatikana kutokana na kujiondoa kwa jeshi la Amerika baada ya nchini kuanguka kwa  haraka mikononi mwa Taliban. “Nina hasira sana kwamba tulifanya hivyo. Tuliweka hatarini maisha ya watu wengi,” alisema. “Hilo lilitokeaje? Kuna vitu vingi vilifeli vilisababisha kutokea kwa hilo.” Uchaguzi mdogo ukiwa njiani unakuja mnamo Novemba, utawala wa Biden unaonekana kuficha makosa yaliosababisha hali kuwa vile katika hatua ya mwisho ya vita vya muda mrefu katika historia ya Amerika. Utawala huo umekuwa ukitakiwa kuweka uwazi, ikiwa ni pamoja na kutoka kwa wabunge wa Republican wa bunge la Congress ambao wanataka  kuundwa kwa tume na usikizwaji kuwa wazi kwa umma.

Kwa upana zaidi, kwa ujumla kuna hali ya kuvunjika moyo na kusikia vibaya kwa baadhi ya viongozi wa ngazi tofauti tofauti katika jeshi kwamba  “rasilimali na juhudi zaidi hazijafanyika” kujifunza kutokana na vita vya Afghan, alisema Jonathan Schroden, mkurugenzi wa Mpango wa Kupambana na Vitisho na Changamoto katika Kituo cha Uchambuzi cha Jeshi la Wanamaji, kundi la utafiti wa kijeshi la kujitolea. “Ni muhimu sana kujifunza na kupata kuelimika. Kurudia kutazama kwa makini hali ilivyotokea, namna ya kufanya uokoaji, ni muhimu sana,” aliiambia VOA. “Hivi sasa, mbali na SIGAR inavyofanya, hakuna juhudi yoyote katika serikali ya Amerika ya kufanya hivyo.” Vita vya Afghanistan vimeua zaidi ya wanajeshi  2,400  wa Amerika na kugharimu dolari milioni 300 kila siku kwa muda miaka 20. Utafiti jumuishi wa kuaminika wenye kutambua utendakazi bora na changamoto katika asasi tofauti tofauti za serikali ya Amerika ikiwa ni pamoja na operesheni nzima mzima ni muhimu mno, alisema Mark Jacobson, aliye saidia upangiliaji wa uokoaji wakati kujiondoa na akatumikia cheo cha mwakilishi wa NATO nchini Afghanistan. [Chanzo : Voice of America (VoA)]

Ni wazi kwamba hii ni vita ya muda mrefu zaidi ya Amerika, ambayo iliishia  kwa Amerika kupata aibu. Baada ya kutumia utajiri wote na damu, amerika imeishia kushindwa nchini Afghanistan. Hii pia inaibua swali jingine ni kwanini Taliban ilifanya haraka kukamilisha mkataba na Amerika, wakati ambapo kundi hilo lilikua tayari limepata ushindi. Uharaka wa kutaka mamlaka umelifanya kundi Talibani kupata tabu hadi muda huu katika uchumi na kutengwa na mataifa.

PTI Yaajiri Makampuni Kuboresha Sura Yake nchini Amerika

Chama cha Pakistan cha Tehreek-i-Insaf’s (PTI) kimeajiri kampuni ya  uhusiano wa umma ili kuboresha sura yake nchini Amerika, sehemu ambayo ilikuwa ikichukuliwa kama chama cha kupinga Amerika tangu mwezi April, kipindi ambacho mwenyekiti wake na waziri mkuu wa zamani Imran Khan alipoishutumu  Washington  kwa kuwaunga mkono wanaotaka kupindua serikali yake kupitia kura ya kutokuwa na imani. Bw. Khan na chama chake wamekuwa wakiendesha kampeni wakidai kwamba Amerika inawaunga mkono “wanasiasa wa ndani” ili kuipindua serikali yake kupitia njama, na kuweka serikali inayoitaka. Pamoja na hayo, hali hii ya sasa inaonyesha kwamba chama kinarekebisha makosa yake kufuatia kampeni inayofanywa na kiongozi wake, kuthibitisha Amerika kupata ushindi wa umma nchini  Pakistan. “Makubaliano haya ni kati ya kampuni mmoja ya uhusiano wa umma, sio mshawishi, na kundi la raia wa Amerika,” Sajjad Burki, mwenyekiti wa PTI alisema. “Hatushawishi kwa ajili PTI ya Pakistan, na bila shaka hatufanyi hivyo kupitia utawala wa Amerika.” Makubaliano yaliosainiwa 1 Agosti kati ya David Fenton of Fenton/Arlook na mwanasheria wa PTI USA Salman Ravala yalianza utekelezwaji mnamo 9 Agosti. Imetaja kwamba PTI USA “haiongozwi, haimilikiwi, wala haisimamiwi na chama chochote cha kisiasa cha kigeni, lakini katika baadhi ya dhurufu kitaelekeza na chama cha kigeni cha kisiasa nchini Pakistan”. PTI USA kitailipa kampuni hiyo dolari 25,000 kwa mwezi, “ zilizo kusanywa kutoka kwa wafuasi wa PTI ambao ni wakaazi halali wa Amerika”, Atif Khan, afisa mwingine wa PTI, kutoka Dallas, Texas, alisema. Nyaraka zilizokusanywa mnamo 9 Agosti zilionyesha chama hicho kimeihusisha Fenton/Arlock LLC katika kusaidia PTI kufikia “malengo kupitia uhusiano na Amerika pamoja na watu wa Pakistan wanaoishi Amerika”. Nyaraka hizo zimeonyesha namna ambavyo chama kilivyojaribu kuimarisha uhusiano na utawala wa Biden baada ya tuhuma za uongo za kuhusika kuwaunga mkono wapinzani kupindua serikali ya PTI kupitia “njia zisizo halali”, ikiwa ni pamoja na kukiunga mkono chama cha Pakistan Democratic Movement ambacho kiko mamlakani jijini Islamabad. Chini ya makubaliano hayo, chama chenye mafungamano na New York PTI USA ni mteja wa shirika la uhusiano wa umma, ambalo limeajiriwa kwa miezi sita sasa kwa ajili ya kusimamia mahusiano ya ummah na vyombo vya habari katika chama hicho. Shirika kama hilo mwanzoni pia lilitambulishwa katika ubalozi wa Pakistani nchini Amerika wakati PTI ilipokuwa mamlakani. Waziri mkuu wa zamani Imran Khan pia alikula chajio katika eneo hilo la Fenton mwaka 2019 alipozuru New York kuhudhuria kikao cha kongamano kuu la Umoja wa Mataifa. [chanzo: Dawn]

Baada ya kudumu kuilaumu Amerika kutaka kumng’oa mamlakani, Khan hivi sasa anataka kurekebisha mafungamano na utawala wa Biden. Kurudi nyuma kwa msimamo wa IK kunajulisha kwamba PTI pamoja na vyama vyengine vya kisiasa vinaitegemea Amerika katika mustakbali wa vyama hivyo. Khan amekuwa akilalamikia utumwa wa kiakili unaofanywa Magharibi na sasa kurudi kwake nyuma kuwa yeye pia ni mtumwa wa  Amerika.

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu