Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Uhakiki wa Habari 13/08/2022

Marekani Yaunga Mkono Tena Ugaidi wa Umbile Haramu la Kiyahudi dhidi ya Waislamu wa Palestina

Mwezi huu umbile haramu la Kiyahudi lilianzisha tena kampeni ya kigaidi dhidi ya Waislamu wa Palestina, na kuua 44 wakiwemo watoto 16. Kulingana na ripoti ya Reuters:

Marekani iliunga mkono kikamilifu haki ya Israel ya kujihami, Wizara ya Mambo ya Nje ilisema mnamo Jumamosi, na ilizitaka pande zote kuepuka uchochezi zaidi huku mashambulizi ya anga ya Israel yakipiga Gaza huku kundi la wanamgambo la Jihad al-Islamiya likirusha makombora kuelekea Israel.

Ripoti ya Reuters pia ilibainisha 'hakuna ripoti za majeruhi makubwa', achilia mbali vifo, kwa upande wa Mayahudi. Katika kipande cha maoni juu ya hili katika Aljazeera:

Katika kujibu umwagaji damu wa mwezi huu mjini Gaza, Rais wa Marekani Joe Biden alithibitisha tena "uungaji mkono wake kwa usalama wa Israeli... ikiwemo haki yake ya kujihami dhidi ya mashambulizi" - ambayo si tamko la kushangaza kutoka kwa mtu ambaye hivi karibuni alijisifia mwenye kwa shauku kama "Mzayuni" wala kuondoka kutoka kwa kauli za kuchosha za mara kwa mara za utawala wa Marekani, ambayo inashikilia kuwa Israel inatekeleza hayo daima na bila shaka kujihami...

mashirika ya vyombo vya habari ya Magharibi pia yamechukua hisa yao kuhakikisha kuenezwa kwa simulizi inayounga mkono Israel badala ya ukweli - na ni mara chache ambapo mauaji ya kijeshi ya Israel dhidi ya raia wa Palestina kimsingi hayatungwi kama makosa ya Wapalestina au matokeo ya "mapigano" kati ya pande hizo mbili. Kwa hakika, CNN na Reuters zilikwenda na "mapigano" katika makala zao juu ya makubaliano ya kusitisha vita ambayo yalianza kutekelezwa usiku wa Agosti 7 - kana kwamba huu ulikuwa ufafanuzi unaofaa kwa hali ambayo watu 44 walikufa kwa upande mmoja na hakuna aliyekufa upande mwingine ...

Gazeti la Washington Post liliiona Operesheni ‘Breaking Dawn’ kama mfano wa "ghasia kali mpakani" - mstari mithili ya huo ulichukuliwa na Associated Press – huku angazo la New York Times likijumuisha ripoti za utata kama vile: "Israel na wanamgambo wafyatuliana huku vifo vikifikia 24".

Mwandishi wa makala ya maoni ya Aljazeera ameeleza mengi zaidi yanayoweza kusemwa katika vyombo vya habari vya kawaida, akiashiria aina ya unafiki kwa upande wa Magharibi juu ya kupuuza ukatili unaofanywa na umbile hilo haramu.

Hata hivyo, vyombo vya habari vya kawaida haviwezi kwenda mbali zaidi kuelezea ukweli wa hali hiyo, ambayo ni kwamba uhalifu wa umbile hilo haramu unafanywa kwa makusudi kwa niaba ya Magharibi yenyewe, sio tu kupuuzwa na Magharibi. Magharibi ndiyo iliyo pandikiza uwepo huu wa kigeni ndani ya moyo wa ardhi ya Waislamu ili kusaidia katika kupanua ubeberu wa Kimagharibi ndani ya Umma wa Kiislamu. Magharibi inajua udhaifu wa Mayahudi; katika zama hizi wao miongoni mwa watu dhaifu zaidi. Kwa hivyo, kama vile mtoto mpotevu aliyedekezwa kupita kiasi, nchi za Magharibi hulishajiisha umbile hilo haramu kuwa na muamala mbaya iwezekanavyo huku ikiwazuia wapinzani wake dhidi ya kulipiza kisasi kwa aina yoyote ile. umbile hilo haramu halingeweza kuwa hai hata siku moja lau serikali za maeneo yanayolizunguka hazingezuia Waislamu kulishambulia.

Vyombo vya habari vya kawaida pia haviwezi kufichua ubatili wa udanganyifu wa dola ya kitaifa ya Westphalia. Maswala ya mwanadamu hayaamuliwi na takriban serikali 200 huru za kitaifa. Kihakika ni dola chache tu kubwa, Marekani ikiwa kiongozi wake, ndizo hufanya maamuzi makubwa zaidi duniani leo. Kubuniwa kwa dola huru za kitaifa kumezuia kuhusishwa kwa lawama kwa dola kubwa ambazo kiuhalisia zinahusika na maovu yaliyopo duniani leo. Ikiwa dola hizi zinataka kuamua maisha ya wengine, basi zinapaswa kufanya hivyo kupitia kupanua maeneo yao ili kujumuisha kwa wazi wazi mengine ndani ya mipaka yao. Lakini kwa kuyaweka katika nchi tofauti, wanaendelea kuyanyonya huku wakikataa uwajibikaji kwa matendo yao.

Suluhisho linalofaa kwa matatizo ya sasa ya mwanadamu halitatoka Magharibi. Kwa idhini ya Mwenyezi Mungu (swt), Umma wa Kiislamu hivi karibuni utasimama na kusimamisha tena Dola ya Kiislamu ya Khilafah kwa njia ya Mtume (saw) ambayo itakomboa maeneo yake yote yanayokaliwa kwa mabavu, kuunganisha ardhi za Waislamu, kutabikisha shariah ya Kiislamu, kuregesha mfumo kamili wa maisha wa Kiislamu, na kubeba nuru ya Uislamu ulimwengu mzima. Dola ya Khilafah, kuanzia kusimamishwa kwake, itajiunga na safu za dola kuu kwa misngi ya idadi kubwa ya watu wake, ukubwa wa eneo lake, rasilimali nyingi, jiografia isiyo na kifani na mfumo wa kipekee wa Kiislamu. Dola ya Khilafah itatengua mfumo wa Westphalia uliopandikizwa na Magharibi na kuirudisha dunia katika amani na ustawi uliokuwepo kabla ya ubeberu wa Kimagharibi, katika kipindi cha miaka elfu moja ambayo Dola ya Khilafah hapo awali ilikuwa dola inayoongoza duniani.

Marekani Yaihonga Yenye Kutapatapa juu ya Makubaliano na Iran

Kwa mujibu wa Politico katika makala yenye kichwa cha habari cha mnamo Ijumaa, 'Muungano wa Ulaya unapendekeza kuondoa shinikizo kwa Walinzi wa Mapinduzi ya Iran ili kufufua makubaliano ya nyuklia':

Ingawa pendekezo la Ulaya, lililosimamiwa na mkuu wa sera za kigeni wa Muungano wa Ulaya Josep Borrell kwa uratibu wa karibu na maafisa wa Marekani, halitaondoa vikwazo vya IRGC kipekee, litapunguza pakubwa ufanisi wake.

Chini ya maandishi yaliyopendekezwa, Wazungu na watu wengine wasio Waamerika wanaweza kufanya biashara na vyombo vya Iran vinavyohusika na "miamala" na IRGC bila hofu ya kuchochea vikwazo vya Marekani, kama ilivyo hali hivi sasa, maadamu mshirika wao mkuu wa kibiashara hatakuwa kwenye sajili ya vikwazo ya Marekani.

“Wasiokuwa Waamerika wanaofanya biashara na watu wa Iran ambao hawako kwenye [orodha ya vikwazo ya Amerika] hawata athiriwa na vikwazo kwa sababu tu ya watu hao wa Iran kushiriki katika miamala tofauti inayohusisha watu wa Iran kwenye [orodha ya vikwazo ya Amerika] (likiwemo Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (IRGC), maafisa wake, au matawi yake au washirika wake)," pendekezo hilo lilisomeka.

Maneno haya yatawaruhusu Wazungu kufanya biashara kwa upana sana kote nchini Iran, ambapo maingiliano ya kibiashara na IRGC yanakaribia kutoepukika, haswa katika suala la biashara. Mwanadiplomasia mmoja aliyefuatilia ripoti hiyo alibaini maneno hayo pia yanapendekeza kwamba vyombo vya IRGC vinaweza kutafuta kukwepa vikwazo vya Amerika kupitia tu kufanya biashara zao kupitia washirika na guo la makampuni inayosababisha kiwango cha utengano, na kuvifanya vizuizi vya Amerika kutokuwa na nguvu kwa kampuni na watu binafsi wasio Waamerika.

Chini ya Rais Joe Biden, Amerika inasonga mbele haraka kujiimarisha upya dhidi ya China, ambayo Amerika inaitarajia kuwa tishio kuu la moja kwa moja kwa eneo la Amerika katika Karne ya 21. Ili kufanya hivyo, Amerika inahitaji kujinasua kutokana na mtego wake wa kina ndani ya Mashariki ya Kati kwa kujenga usanifu thabiti wa kimataifa ambao unaweza kutoa kipimo cha utulivu huku ikiziweka nchi za eneo hilo chini ya udhibiti wa Amerika. Kwa maana nyengine, Amerika iko katika mchakato wa kuimarisha himaya yake ya Mashariki ya Kati, chini ya pazia la uhuru wa dola za kitaifa za Mashariki ya Kati. Iran ni nguzo moja muhimu katika mpango huu. Makubaliano ya nyuklia ya Iran kimsingi hayahusu mpango wa nyuklia wa Iran lakini ni njia ya Amerika kubuni nafasi ya Iran katika mradi wake wa kifalme. Hata hivyo, ili kuhakikisha kwamba ujenzi huu wa himaya unadumu kwa muda mrefu, Amerika inatafuta utiifu wa Ulaya pia. Ulaya inayotegemea nishati bila shaka inateseka sana wakati huu kwa sababu ya masuala ya usambazaji kutokana na vita na Urusi. Kwa hivyo Amerika inajaribu kuitongoza Ulaya kwa mafuta ya Iran.

Hata hivyo, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu (swt) mradi wa kibeberu wa Marekani utafeli. Umma wa Kiislamu utatumia fursa ya kuvurugika kwa fikira za Marekani na kupungua kwa ushiriki wake kupindua tabaka la watawala vibaraka ambao hivi sasa wanasimamia mambo yao kwa niaba ya dola za Kimagharibi, na kuwabadilisha kwa uongozi wa wenye ikhlasi, wenye uwezo, wa asili ambao utakuwa mtiifu kikamilifu kwa Umma wa Kiislamu na Dini yake ya Kiislamu. Mwenyezi Mungu (swt) asema katika Qur’an Tukufu:

(وَعَدَ اللَّهُ الَّذِينَ آمَنُوا مِنكُمْ وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ لَيَسْتَخْلِفَنَّهُم فِي الْأَرْضِ كَمَا اسْتَخْلَفَ الَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ وَلَيُمَكِّنَنَّ لَهُمْ دِينَهُمُ الَّذِي ارْتَضَى لَهُمْ وَلَيُبَدِّلَنَّهُم مِّن بَعْدِ خَوْفِهِمْ أَمْنًا يَعْبُدُونَنِي لَا يُشْرِكُونَ بِي شَيْئًا وَمَن كَفَرَ بَعْدَ ذَلِكَ فَأُوْلَئِكَ هُمُ الْفَاسِقُونَ)

“Mwenyezi Mungu amewaahidi wale walio amini miongoni mwenu na wakatenda mema, ya kwamba atawafanya makhalifa katika ardhi kama alivyo wafanya makhalifa wa kabla yao, na kwa yakini atawasimamishia Dini yao aliyo wapendelea, na atawabadilishia amani baada ya khofu yao. Wawe wananiabudu Mimi, wala wasinishirikishe na chochote. Na watao kufuru baada ya hayo, basi hao ndio wapotovu.” [An-Nur: 55].

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu