Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Uhakiki wa Habari 05/12/2020

Biden Ajihakikishia Ahadi ya Kutosha ya Kura za Chuo cha Uchaguzi ili kuwa Rais

Rais wa Amerika hachaguliwi na watu bali na chuo kidogo cha uchaguzi ambacho kinajumuisha wapiga kura kutoka kila jimbo ambapo Rais anapaswa kushinda angalau 270. Chuo cha uchaguzi hakitapiga kura hadi tarehe 14 Desemba 2020 na matokeo yatapokelewa tu na Bunge la Congress mnamo 6 Januari 2021.

Demokrasia kama inavyofafanuliwa kifalsafa haipo popote ulimwenguni. Magharibi ilitabanni wazo la demokrasia kwa kuchelewa baada ya shinikizo la umma ambalo lilikuwa likiendeshwa na kipote kidogo cha wapenda mada, ambao walificha jambo lisilo la kidini la demokrasia kutoka kwa Wakristo wa Magharibi. Badala ya kupinga mawazo ya kupenda mada, kipote kidogo cha warasilimali wa Magharibi waliridhiana nayo, wakitabanni maoni ya kimada kama uhuru na demokrasia na kuyaunda kwa misingi ya kisekula. Magharibi haitekelezi demokrasia bali kile wanachokiita demokrasia ya uwakilishi. Watu huchagua wawakilishi, na kisha wawakilishi wanatawala kwa kadri wanavyoona inafaa, ikiwa hii ni kwa mujibu wa matakwa ya watu. Taasisi ya Amerika ya chuo cha uchaguzi ni ukumbusho mmoja tu wa jinsi watu sio wanaotawala, ingawa ndivyo wanavyosadikishwa kuamini. Demokrasia ya Magharibi ni kifuniko tu cha utawala na kipote kidogo cha warasilimali wanaotawala ambao ni waaminifu kwa maslahi yake tu. Uislamu pekee ndio uliofanikiwa katika kuasisi sheria ambayo iliwahudumia watu kikweli, kwa kukatiza utawala kutoka kwa maslahi yenye nguvu na kuifanya itumike tu kwa Sharia ya Kiislamu isiyoweza kubadilika.

Somalia, Qatar, India

Sasa katika wiki zake chache za mwisho, Rais wa Amerika Donald Trump anaendelea kujionyesha kuwa mwaminifu kwa wale waliompigia kura, ingawa maamuzi yake ya sera yanaendelea kutumikia maslahi ya serikali. Amerika ndio nguvu kuu ya ulimwengu, na imeuzunguka ulimwengu na karibu kambi elfu moja za kijeshi na vikosi vilivyopelekwa katika nchi zaidi ya 150 ulimwenguni. Amerika haina nia ya kupunguza ujeshi huu uliokithiri. Lakini, umma wa Amerika una tabia ya kimsingi ya kujitenga, wakiutazama "Ulimwengu Mpya" wao kama ulio huru kutokana na shida za "Ulimwengu wa Zamani" ambao wanafikiri wameuacha nyuma, tabia ambayo Trump aliweza kucheza nayo katika kukwea kwake madaraka. Kwa hivyo Trump anawasilisha kila nafasi ndogo ya kuvibadilisha vikosi vya jeshi la Amerika kama uondoaji mkubwa. Kulingana na taarifa ya Pentagon, kama ilivyoripotiwa na gazeti la Guardian, "Amerika haiondoki au kujitenga na Afrika. Tunabaki kujitolea kwa washirika wetu wa Kiafrika na kuhimili msaada kupitia njia kamili ya serikali." Taarifa hiyo ilifafanua zaidi, "Huku kukiwa na mabadiliko ya msimamo wa nguvu, hatua hii sio mabadiliko katika sera ya Amerika. Tutaendelea kudhalilisha mashirika yenye msimamo mkali ambayo yanaweza kutishia nchi yetu huku tukihakikisha tunadumisha manufaa yetu ya kimkakati katika ushindani mkubwa ya mamlaka."

Kulingana na ripoti za vyombo vya habari, Jared Kushner, mkwe wa Trump na muwasilianaji mkuu na Mohammad bin Salman, anafanya kazi kikamilifu kuregesha uhusiano kati ya Saudi Arabia na Qatar. Kuna sababu nyingi za kutaka kufanya hivyo. Qatar, inaendelea kushikamana na maslahi ya Uingereza na kwa hivyo inaweza kuwa shida zaidi kwa Amerika kutawala. Ususiaji wa kikanda Qatar ulikusudiwa kama aina ya nidhamu kwa upande wa Amerika, ambapo Amerika sasa inamalizika, labda kwa badali ya malipo ya makubaliano fulani kutoka Qatar. Maadamu ulimwengu wa Kiislamu utabaki umegawanyika katika nchi kadhaa tofauti tofauti, Magharibi beberu itaendelea kutafuta njia za kuzitumia baadhi serikali zetu dhidi ya zingine. Suluhisho pekee la hili ni kufuata matakwa ya Kiisilamu ya kuwa na uongozi mmoja pekee kwa Waislamu wote, ili ulimwengu wote wa Kiislamu uletwe chini ya serikali moja, inayoongozwa na Khalifa muongofu.

Makumi ya maelfu ya wakulima kutoka majimbo ya Punjab na Haryana wanapambana na serikali ya Waziri Mkuu wa India Narendra Modi, wakikabiliwa na mizinga ya maji na gesi ya kutoa machozi wakiwa wamepiga kambi kwenye baridi kali. Wakulima wadogo nchini India wanakabiliwa na unyanyasaji mkali, na ni kawaida kuona ripoti za kila mwaka za idadi kubwa ya wakulima wa India wanaojiua. Ardhi ya India, inayonyweshwa maji na mito ya Himalaya na kufurahiya hali nzuri ya hewa kwa kilimo, labda ndio yenye rutuba zaidi ulimwenguni. Chini ya utawala wa Waislamu, ustawi wa India ulikuwa kiasi kwamba ikawa ndio eneo lililokuwa na maendeleo zaidi kiuchumi duniani kwa sababu ya utekelezaji wa nidhamu ya uchumi ya Kiislamu, ambayo ina sera bora na pana ya kilimo. Lakini Waingereza waliiondoa nidhamu hii na kuibadilisha na nidhamu ya unyonyaji, na kusababisha njaa mbaya ya kihistoria iliyoua mamilioni. Baada ya ukoloni kumalizika, badala ya kurudi kwenye mafunzo ya utawala wa Kiisilamu, serikali ya kisekula ya India iliendeleza sera za kiuchumi za Kimagharibi zilizofeli ambazo zinaendelea kuwanyonya wanyonge kwa faida ya wenye nguvu. Kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, Ummah wa Kiislamu hivi karibuni utasimamisha tena Dola ya Kiislamu ya Khilafa kwa njia ya Mtume (saw), na India itarudi kwa mara nyengine tena kwa utawala wa Uislamu.

Uingereza Yaendelea Kuunda Shinikizo kwa Sera za Mabadiliko ya Anga

Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson wiki hii alitangaza hatua kali za kupunguza uzalishaji wa gesi ya carbon dioxide ifikapo mwaka 2030. Uingereza, kwa muda mrefu nguvu iliyofichwa nyuma ya harakati za mabadiliko ya hali ya hewa, inazidi kujitokeza wazi juu ya msaada wake kwa sera za mazingira. Ni kweli kwamba Magharibi imeharibu mazingira, Uingereza zaidi kuliko wengine kwa sababu ya urithi wake kama mwanzilishi wa Mapinduzi ya Viwanda ya Magharibi, na unyonyaji wake mkubwa wa makaa ya mawe kama chanzo cha nishati kwa umeme, utengenezaji na usafirishaji. Lakini juhudi za sasa za Uingereza zimezaliwa sio kutokana na kujali kwake mazingira bali kumharibu mpinzani wake na koloni lake la zamani, Amerika, ambayo bado inategemea sana mafuta ya visukuku.

Uislamu uliunda njia ya maisha kwa utulivu zaidi na maumbile na kwa hivyo haihitaji sana viwango vya juu vya uzalishaji wa nishati. Kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, Dola ya Kiislamu ya Khilafah Rashida kwa njia ya Mtume (saw) itafufua njia ya maisha ya Kiislamu na kutumia teknolojia bora zaidi sio tu kuongezea faida ya juu bali kuunda miondoko ya maisha ya hali ya juu ambayo inadhamini ustawi kwa wote huku ikihifadhi na kusimamia yote yaliyo ndani ya Ardhi kwa njia bora zaidi. Kulingana na Hadith moja iliyopokewa na Imam Bukhari (ra), iliyosimuliwa na Anas ibn Malik (ra): Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema,

«مَا مِنْ مُسْلِمٍ يَغْرِسُ غَرْسًا أَوْ يَزْرَعُ زَرْعًا فَيَأْكُلُ مِنْهُ طَيْرٌ أَوْ إِنْسَانٌ أَوْ بَهِيمَةٌ إِلَّا كَانَ لَهُ بِهِ صَدَقَةٌ»

“Hakuna Muislamu yeyote anaye panda mti au mbegu, kisha ndege, au mtu, au mnyama akala kutokana nazo, isipokuwa inakuwa ni sadaka kwake.” [Bukhari 41:1]

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu