Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Ni yapi Matokeo ya Mgogoro wa Kiuchumi katika Nchi za Asia kufuatia janga hili?

Habari:

"Mifumo ya uhamishaji pesa imeonekana kupungua kutoka nchi hadi nchi mnamo Machi kutokana na mazingira ya janga la virusi vya korona, RBK iliarifiwa na taasisi za uhamishaji pesa za Unistream na Golden Crown. Aghlabu wahamiaji ndio wanaotumia taasisi hizi katika uhamishaji wa pesa. Katika mfumo wa Unistreampayment kiwango cha uhamishaji pesa kutoka Urusi kimepungua hadi asilimia 32 ikilinganishwa na kipindi kama hiki katika mwaka ulio pita – idadi hii imo ndani ya mabadiliko jumla ya soko, mwakilishi wa mfumo wa RBK aliambiwa. Katika taasisi ya Golden Crown mnamo Machi kiwango cha uhamishaji pesa kilipungua hadi asilimia 30 mnamo Aprili kinatabiriwa kuanguka kwa asilimia 50, duru  zilizo  karibu na mfumo huo wa uhamishaji fedha ziliiarifu RBK. Golden Crown ilithibitisha kupungua kwa msongamano.

Wanao ongoza katika viwango vya uhamishaji fedha ni nchi za CIS - takwimu za Benki kuu ya Urusi zinaonyesha kwamba katika mwaka wa 2019 dolari bilioni 6 kutoka dolari bilioni 7.5 zilitumwa huko kutoka Urusi. Takriban nusu ya uhamishaji huo ulikwenda Uzbekistan (dolari bilioni 3), ikifuatiwa na Tajikistan (dolari milioni 699), Armenia (dolari milioni 627.6 ) na Kyrgyzstan (dolari milioni 612 )", ripoti za Asia-Plus zilisema.

Maoni:

Hatua za kimataifa za kukabiliana na kusambaa kwa virusi vya korona vilivyo sababisha mporomoko mkali wa kiuchumi katika nchi nyingi ulimwenguni.  Nchi tajiri kama Amerika inayoweza kumudu kusaidia wananchi wake kwa kuwapatia pesa ili kujiinua kiuchumi na kupatiwa fursa ili watu waweze kujikimu katika kipindi hiki ambacho nyingi katika sekta za uchumi zimefungwa. Leo katika nchi nyingi za Kimagharibi ustawi wa watu kiuchumi upo juu kiasi kwamba kwa akiba ya pesa walizo nazo zinawawezesha kuishi katika karantini na hata baada ya karantini.  Lakini, ni nini kitatokea katika nchi maskini, ambapo inajumuisha takriban nchi zote za Asia ya Kati? Nini katakacho tokea kwa watu kwa kusitishwa mtiririko wa malipo ya pesa kutoka Urusi, ukizingatia, kwa mfano, malipo ya pesa kutoka Tajikistan kuelekea Urusi huchangia nusu ya Utajiri Jumla wa nchi (GDP)? Kulingana na Benki ya Dunia, Tajikistan iko katika nafasi ya kwanza kiulimwengu kwa kiashiria hiki, na Kyrgyzstan ni ya pili ikiwa na asilimia 32 ya Utajiri Jumla wa nchi (GDP).

Ni wazi kwamba matokeo ya mgogoro wa kifedha na kiuchumi wa kidunia wa mwaka 2008 yaliathiri hali za kisiasa katika nchi tofauti tofauti kwa muda mrefu, na kwa mujibu wa wataalamu, imekuwa ndio kichocheo cha kuanza kwa misururu ya mapunduzi katika nchi nyingi ulimwenguni, ukijumuisha ChemiChemi ya Mapinduzi ya Kiarabu, wakati harakati ya kimapinduzi ilipo fagia nchi moja baada ya nyengine za ulimwengu wa Kiarabu. Ilidhihirisha ukweli kwamba nchi za Asia ya Kati ni nchi zinazo tegemea sana kupeleka raia wao nje kwa ajili ya kufanya kazi, ambapo leo kutokana na karantini, ni wazi kuwa ajira hio inatoweka kimaumbile, kutoweka vibaya kwa chanzo cha mapato kwa watu wa nchi za Asia ya Kati kunaogopesha hasa kwa mtikisiko mzito wa kiulimwengu wa kisiasa katika nchi za Asia ya Kati. Hata hivyo, ikiwa hata kabla ya kuanguka kwa uchumi na ufisidifu wa ajabu wa madikteta wa Asia watu walizoea kupuuza uchafu wao na badala yake kuendelea kujitafutia kipande cha mkate kwa kuhamisha nguvu kazi nje, sasa mamilioni ya watu ambao hawawezi tena kurudi Urusi kwa ajili ya kuendelea kufanya kazi  katika kipindi cha kawaida kama hiki kuanzia Januari hadi Aprili wameachwa peke yao na hao wanao itwa kuwa ni "viongozi wa mataifa" katika nchi zao.

Wachunguzi wanahisi kupatikana kwa hatari kubwa katika kipindi cha baadaye dhidi ya kutoridhiwa kwa watawala wa nchi za Asia ya Kati, hasa katika hizo nchi ambazo ni tegemezi zaidi katika kuhamisha nguvu kazi ng'ambo na hazitaweza kuwapatia kazi hao walio kuwa wakifanya kazi nje, ambapo kimsingi Tajikistan ni mojawapo. Na, licha ya ukweli kwamba katika nchi za eneo hilo kwa sasa hakuna hali nzito ya mripuko wa virusi vya Korona, na, Mwenyezi Mungu ajaaliye iwe hivyo hata katika siku zijazo, Asia ya Kati huenda ikaendelea kuhisi matokeo ya kiuchumi ya janga hili kwa miezi mingi na hata miaka

Imeandikiwa kwa Ajili ya Afisi kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Muhammad Mansour

#Covid19    #Korona     كورونا#

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumanne, 28 Aprili 2020 13:58

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu