Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Wanawake Waislamu Hawahitaji Sherehe za Kila Mwaka za Kufeli Kiulimwengu katika Kusuluhisha Matatizo ya Wanawake. Tunahitaji Khilafah itakayokuwa Mlinzi na Ngao Yetu

Habari:

Siku ya Kiulimwengu ya Wanawake (IWD) mnamo 8 Machi iliadhimishwa kwa sherehe sawia na za kila mwaka, maandamano na mikutano katika nchi duniani kote, ikijumuisha ardhi za Waislamu ili kutambua mafanikio yaliyofikiwa na wanawake duniani pamoja na ulinganizi wa utendaji ili kuzidi kuchangamkia suala la usawa wa kijinsia ndani ya mujtama na kuwalinda wanawake na kuboresha haki zao na viwango vya maisha yao. Kauli mbiu ya mwaka 2020 ilikuwa ‘Usawa kwa Kila Mmoja’ ambayo ililingania kwa utendaji wa pamoja ili kufikia usawa wa kijinsia ndani ya serikali, sehemu za kazi, michezo na kuangaziwa na vyombo vya habari pamoja na sekta nyingine ndani ya dola. Kauli mbiu ya UN ya maadhimisho ya IWD mwaka huu ilikuwa, “Mimi ni Kizazi cha Usawa: Kufikia Haki za Wanawake”, ambayo ni sehemu ya kampeni ya kiulimwengu iliyozinduliwa na wanawake wa UN mnamo 2020 inayolenga kukishajiisha kizazi kipya cha wanawake ndani ya nchi tofauti duniani, ikijumuisha ardhi za Waislamu, ili kupigia debe ulinganizi wa usawa wa kijinsia ndani ya mataifa yao.

Maoni:

Fahamu ya ‘Usawa wa kijinsia’ inayolingania usawa katika haki, dori na majukumu ya wanaume na wanawake ndani ya maisha ya familia na mujtama, inawasilishwa kama aina fulani ya dawa ya kimaajabu ambayo kwamba dola na watutu binafsi lazima wainywe ili kuwaboreshea wanawake hali zao, viwango vya maisha yao, ulinzi na haki zao. Hata hivyo, usawa wa kijinsia na sera za ukombozi wa wanawake hazikufaulu katika kupunguza viwango vya vurugu wanazokumbana nazo wanawake ndani ya mujtama zao au katika kuwanyanyua kutokamana na hali ngumu ya kiuchumi au hali ya ukandamizaji. Ndani ya nchi kama Tunisia na Uturuki kwa mfano, ambazo zinajulikana kama viongozi katika sheria za usawa wa kijinsia ndani ya ulimwengu wa Waislamu, kiwango cha vurugu zinazolenga wanawake ni viwango vya kushtusha mno. Kwa mujibu wa takwimu za 2016 kutoka Wizara ya Wanawake, Familia na Watoto nchini Tunisia, asilimia 60 ya wanawake nchini wanapitia vurugu za kinyumbani, ilhali Uturuki, kwa mujibu wa Wizara ya Haki kutoka mnamo 2003 – 2014, kulikuwa na ongezeko la asilimia 1,400 katika idadi ya mauaji ya wanawake. Kwa kuongezea, ni kipi kilichofanywa na sheria na makubaliano ya usawa wa kijinsia kama vile BPfA na CEDAW ili kulinda maelfu ya wanawake nchini Syria ambao wanachinjwa na wachinjaji Assad na Putin; au kutoa hifadhi yenye hadhi kwa mamilioni ya wakimbizi kutoka katika vita ambao wanaishi katika kambi zisizostahiki wanadamu; au kulinda maelfu ya wanawake na wasichana Waislamu wa Rohingya na Wauyghur wanaoteswa pamoja na wale wa Palestina, Kashmir, Afrika ya Kati na kwingineko ambao wametaabika, wameadhibiwa, wamevunjiwa heshima na kuuawa na wakandamizaji na wavamizi wao? Na ni kwa namna gani sera hizi za usawa zimewaondolea umasikini unaowakumba mamilioni ya wanawake ndani ya dola kuanzia mashariki – magharibi? Kwa mujibu wa Benki ya Dunia, takribani nusu ya watu duniani – bilioni 3.4 ya watu – wanapata shida katika kukidhi mahitaji yao msingi, ilhali nchini Uingereza, ni moja ya nchi ambazo ulinganizi wa usawa wa kijinsia ulikoanzia karne mbili zilizopita, asilimia 45 ya wazazi binafsi – asilimia 90 yake ni wanawake – wanaoishi katika umasikini (kwa mujibu wa Kitengo cha Kazi na Pensheni cha serikali ya UK). Na ni kipi haswa ambacho ajenda za ukombozi wa wanawake na usawa wa kijinsia zinazotekelezwa na mashirika ya kimataifa, ya wanawake na serikali za Pakistan na Afghanistan ili kuboresha fursa za kielimu kwa makundi ya wanawake na wasichana nchini humo? Nchini Afghanistan leo, asilimia 40 ya shule zote nchini hazina majengo, na takribani thuluthi mbili za wasichana Waafghan hawaendi shule (Human Rights Watch, 2017) na asilimia 84 ya wanawake nchini hawajui kusoma na kuandika (Afghanistan Central Statistics Organization, 2017).

Kiukweli, usawa wa kijinsia sio chochote bali ni dawa ya kuzigandisha hisia na kuziweka mbali na utambuzi kwamba ni nidhamu ya kirasilimali pamoja na fikra na misingi yake ya kisekula na kihuria, pamoja na mifumo iliyotungwa na wanadamu na nidhamu zinazotekelezwa katika ardhi, ambazo kwamba ndizo zinazobeba jukumu la ukosefu wa haki, vurugu na uhalifu mwingine dhidi ya wanawake kimataifa. Hii inajumuisha kukuza vita vya kutafuta faida kwa dola za kisekula na kutoa msaada kwa madikteta wanaowafanyiakazi pasi na kuzingatia ukandamizaji wa wanaume na wanawake wanaowatawala. Hivyo basi, harakati za ukombozi wa wanawake zimeshughulisha juhudi na muda mwingi wa wanawake katika vita visivyoshindika ambavyo vimefeli hata kupunguza kiwango cha matatizo wanayokumbana nayo.

Kiukweli, hakuna mahusiano baina ya kiwango cha sheria na sera za usawa wa kijinsia zinazotekelezwa ndani ya dola na viwango vya maisha vya wanawake wao. Hata hivyo, kunayo mahusiano baina ya miaka iliyopita tangu kupotezwa kwa dola ya Khilafah na kiwango cha maangamivu, tabu na idhilali inayoathiri wanawake ndani ya ardhi za Waislamu na hususan wanawake Waislamu ulimwenguni. Hii Rajab ni kumbukumbu ya miaka 99 katika kalenda ya Hijri tangu kuvunjwa kwa dola hii tukufu, Nidhamu ya Mwenyezi Mungu (swt). Ni janga hili ndilo lililokuwa kianzio cha sura ya kiza ya historia ya Ummah huu, ambao wanawake na watoto wake ndio waathirika wakuu, kwani tulipoteza dola ambayo ilisimama kama mlinzi na ngao ya hadhi yetu na pia kwa haki na hali za wanawake. Mtume (saw) alisema,

«الإِمَامُ رَاعٍ وَهُوَ مَسْئُولٌ عَنْ رَعِيَّتِهِ»

“Imamu ni mlinzi na atahesabiwa kuhusiana na anaowatala” Tumepoteza dola ambayo iliasisi ustawi ardhini mwetu na kuhakikisha kuwa daima tunapata na kufurahia viwango vizuri vya maisha, dola iliyoasisi elimu bora na nidhamu ya afya bora ambayo wanawake na wanaume walinufaika nayo pakubwa; na nidhamu ambayo ilikuwa haina nafasi ya kuruhusu aina yoyote ya vurugu au madhara kwa wanawake, na kuyaunganisha majeshi ili kwenda kulinda hadhi yao. Hivyo basi, msisitizo, muda na juhudi zetu kama wanawake Waislamu lazima zielekezwe katika dharura ya kusimamisha tena Khilafah kwa njia ya Utume, kwani ni faradhi kutoka kwa Bwana wetu (swt) na kwa sababu hakuna mabadiliko ya kweli yatakayopatikana katika ardhi zetu, hapa duniani na katika maisha yetu kama wanawake pasi na kurudi kwake.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Dkt. Nazreen Nawaz
Mkurugenzi wa Kitengo cha Wanawake katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

#TurudisheniKhilafah

أقيموا_الخلافة#

#ReturnTheKhilafah

  #YenidenHilafet 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu