Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Wale Wanaowaacha Waumini na kutafuta Utukufu, Heshima na Fahari kwa Makafiri!

(Imetafsiriwa)

Habari:

Uturuki: Rais Erdoğan alituma ujumbe wa pongezi kwenye akaunti yake ya mtandao wa kijamii kufuatia kuchaguliwa tena kwa Trump kama rais, na kusema “Ninampongeza rafiki yangu Donald Trump kwa kuchaguliwa tena kuwa Rais wa Marekani baada ya kinyang'anyiro kigumu cha urais.”

Maoni:

Katika ujumbe wake, Rais Erdoğan alisema: “Ninampongeza rafiki yangu Donald Trump kwa kuchaguliwa tena kuwa Rais wa Marekani baada ya kinyang’anyiro kigumu cha urais. Tunatumai kuwa muhula huu mpya wa urais, uliowekwa kwa kura za watu wa Amerika, utaimarisha uhusiano wa Uturuki na Marekani na kukomesha migogoro na vita vya kikanda na kimataifa, haswa kadhia ya Palestina na vita vya Urusi na Ukraine. Ninaamini kuwa kutakuwa na juhudi zaidi kuelekea kuunda ulimwengu wa haki. Ninatumai kuwa uchaguzi huu utaleta matokeo mazuri kwa watu wa Marekani wenye urafiki na washirika na wanadamu wote.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Idara ya Mawasiliano ya Rais, mara baada ya pongezi za Erdoğan, aliwasiliana kwa simu na Rais mteule wa Marekani, Donald Trump. Katika maongezi hayo ya simu Erdoğan alimpongeza Trump kwa kuchaguliwa tena kuwa rais wa Marekani. Rais Erdoğan alieleza nia yake ya kuboresha ushirikiano kati ya Uturuki na Marekani katika muhula huu mpya.

Haikubaliki kamwe kwa Erdoğan kuiita Marekani ambayo imefisadi ardhi, kuua Waislamu, kuiba na kupora rasilimali za chini ya ardhi na juu ya ardhi za Ummah, na kuuingiza ulimwengu wote kwenye machafuko na vita, Myahudi, adui mkuu wa Uislamu na Waislamu na kiongozi wa ukafiri, na mtu ambaye ni rais wake ‘rafiki yangu’. Mazungumzo haya ni, kuyaweka kwa upole, ni kufinikwa kamili kwa akili, ajabu kubwa na udhalilifu mkubwa!

Erdoğan amesahau upesi kiasi gani kuwa Trump alimwandikia barua ya matusi wakati wa urais wake uliopita! Mnamo mwaka wa 2019, wakati wa operesheni za Uturuki nchini Syria, Trump alimwandikia barua Erdoğan akimuonya asiwe “mtu mkali” au “mpumbavu” na kutishia kuwekewa vikwazo vya kiuchumi. Kadhalika, kukamatwa kwa Mchungaji Andrew Brunson nchini Uturuki mnamo 2018 pia kuliathiri uhusiano kati ya viongozi hao wawili. Utawala wa Trump ulitoa matakwa makali ya kuachiliwa kwa Brunson na lira ya Uturuki ilishuka kwa kiwango kikubwa katika mchakato huo. Aidha, Marekani iliiwekea Uturuki vikwazo kadhaa vya kiuchumi na ushuru wa forodha wakati wa utawala wa Trump. Vikwazo hivi vilisababisha mabadiliko makubwa katika uchumi wa Uturuki.

Ununuzi wa Uturuki wa mifumo ya ulinzi wa anga ya S-400 kutoka Urusi wakati huo uliikasirisha Marekani na kusababisha Uturuki kutengwa kutoka mpango wa F-35. Hivyo basi Marekani iliiwekea Uturuki msururu wa vikwazo chini ya Sheria ya Kukabiliana na Wapinzani wa Amerika kupitia Vikwazo (CAATSA) kwa ununuzi wa mifumo ya ulinzi wa anga ya S-400 kutoka Urusi. Ni fedheha iliyoje ambapo Erdoğan bado anamwita Trump kuwa ni rafiki yake wakati inajulikana kuwa Marekani imetuma makumi ya malori ya silaha na risasi kwa PKK/PYD, ambayo serikali imelichukulia kuwa shirika la kigaidi kwa miaka mingi!

Baada ya yote yaliyotokea, inawezaje kuelezwa kuwa Erdoğan angali anatafuta utu, heshima na fahari kwa Amerika na Trump?

Mwenyezi Mungu (swt) anasema:

[الَّذِينَ يَتَّخِذُونَ الْكَافِرِينَ أَوْلِيَاء مِن دُونِ الْمُؤْمِنِينَ أَيَبْتَغُونَ عِندَهُمُ الْعِزَّةَ فَإِنَّ العِزَّةَ لِلّهِ جَمِيعًا]

“Wale ambao huwafanya makafiri kuwa ndio marafiki badala ya Waumini. Je! Wanataka wapate kwao utukufu? Basi hakika utukufu wote ni wa Mwenyezi Mungu.” [An-Nisa 139].

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Yilmaz Çelik

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu