Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Umbile la Kiyahudi Halitanusurika na Mashambulizi ya Makombora ya Khilafah Rashida

(Imetafsiriwa)

Habari:

“Picha za satelaiti za shabaha mnamo siku ya Jumanne – kambi ya anga ya Nevatim kusini mwa ‘Israel’, nyumbani kwa ndege zake za kivita aina ya F-35-zinaonyesha kwamba zaidi ya makombora 32 ya Iran yaliweza kutua ndani ya eneo la kambi hiyo, kulingana na uchambuzi wa Profesa Jeffrey Lewis, katika Taasisi ya Middlebury ya Mafunzo ya Kimataifa huko Monterey, California.” [Wall Street Journal]

Maoni:

Mwenyezi Mungu (swt) amewafahamisha Waumini kwamba Mayahudi watapigana tu wanapokuwa ndani ya ngome zao madhubuti. Amesema Mwenyezi Mungu (swt):

[لَا یُقَاتِلُوْنَكُمْ جَمِیْعًا اِلَّا فِیْ قُرًی مُّحَصَّنَةٍ اَوْ مِنْ وَّرَآءِ جُدُرٍ ؕ بَاْسُهُمْ بَیْنَهُمْ شَدِیْدٌ ؕ تَحْسَبُهُمْ جَمِیْعًا وَّقُلُوْبُهُمْ شَتّٰی ؕ ذٰلِكَ بِاَنَّهُمْ قَوْمٌ لَّا یَعْقِلُوْنَ]

“Hawatapigana nanyi kwa mkusanyiko isipo kuwa katika vijiji vilivyo zatitiwa kwa ngome, au nyuma ya kuta. Wao kwa wao vita vyao ni vikali. Utawadhania kuwa wako pamoja, kumbe nyoyo zao ni mbali mbali. Hayo ni kwa kuwa wao ni watu wasio na akili.” [Surah Al-Hashr 59:14].

“Iron Dome”, “Sling's David” “Arrow 2”, “Arrow 3” zilikuwa kuta imara za ngome ambazo Mayahudi walifikiri zingewalinda. Ukweli ni kwamba jeshi la Iran lilionyesha uwezo wa kuvunja ngome hii yenye kuta nyingi. Iran ilitumia makombora ya balistiki katika shambulizi hilo. Baadhi waliripoti matumizi ya makombora balistiki ya kawaida ya Shahab-3, ambayo yana usahihi duni wa kugonga shabaha ndani ya eneo la 2500m CEP (dosari mviringo inayowezekana). Wengine wanaripoti matumizi ya vibadala vya kisasa aina ya Khybershikan, Fattah na Emad ambavyo vina makadirio ya usahihi wa shabaha ya 10m. Kibadala cha Emad cha makombora ya aina ya Shahab-3 linaweza kubeba uzani wa hadi 750kg, ilhali uzani wa Fattah na Khybershikan ni hadi 500kg. Makombora ya Fattah na Khybershikan hutengana na gari la kusafirishia, na yana uwezo wa kuingia kwa urahisi, hivyo kufanya udukuzi wake kuwa mgumu zaidi.

Kuhusu matokeo ya mashambulizi hayo, licha ya hayo, watawala wa Iran hawakutumia makombora hayo kwa uwezo wao wote. Makombora hayo yalilenga kambi mbili za jeshi la anga ambazo ni Nevatim na Tal Nof, pamoja na makao makuu ya Mossad. Hata hivyo, picha za setilaiti zinazopatikana zinaonyesha uharibifu mdogo kwa barabara ya kurukia ndege, na majengo machache, kwenye kambi ya anga ya Nevatim katika Jangwa la Negev, ambayo inahifadhi ndege za kivita aina ya F-35. Makombora yaliyolenga Mossad yalianguka umbali wa mita 700 kutoka kwa shabaha, na kuchimba shimo lenye upana wa futi 20 katikati ya barabara. Saizi ndogo ya simo lililoachwa nyuma na makombora ya Iran, na mengi yakianguka chini ya shabaha yao, inazua swali la halali ikiwa tangu mwanzo kulikuwa na nia kubwa ya kusababisha uharibifu mkubwa.

Mashambulizi ya Pamoja ya Silaha za Angani ya Kilo 900 (JDAM) yaliunda shimo lenye upana wa futi 50, lenye eneo la mlipuko la futi 200. Kwa hivyo, kwa nini mifumo ya juu ya silaha za nishati ya kinetiki, zinazosonga kwa kasi kubwa zenye athari, na zenye uwezo sawa wa kulipuka, zizalishe mashimo madogo zaidi? Ni wazi, uongozi wa Iran ulipunguza kwa makusudi uwezo wa uharibifu wa mifumo hii ya silaha. Mithili ya watawala wengine wa Waislamu, watawala wa Iran wanadhibiti matumizi ya uwezo wa kijeshi wa Ummah kufikia maslahi ya kitaifa. Mistari mekundu kwa watawala wa Waislamu imewekwa na Amerika na mpangilio wake wa kikanda.

Mwenyezi Mungu (swt) amewaamrisha Waislamu kuandaa silaha zinazotia hofu katika nyoyo za maadui. Amesema Mwenyezi Mungu (swt):

[وَأَعِدُّوا۟ لَهُم مَّا ٱسْتَطَعْتُم مِّن قُوَّةٍۢ وَمِن رِّبَاطِ ٱلْخَيْلِ تُرْهِبُونَ بِهِۦ عَدُوَّ ٱللَّهِ وَعَدُوَّكُمْ وَءَاخَرِينَ مِن دُونِهِمْ لَا تَعْلَمُونَهُمُ ٱللَّهُ يَعْلَمُهُمْ ۚ وَمَا تُنفِقُوا۟ مِن شَىْءٍۢ فِى سَبِيلِ ٱللَّهِ يُوَفَّ إِلَيْكُمْ وَأَنتُمْ لَا تُظْلَمُونَ]

“Basi waandalieni nguvu kama muwezavyo, na kwa farasi walio fungwa tayari-tayari, ili kuwatishia maadui wa Mwenyezi Mungu na maadui zenu, na wengineo ambao hamwajui, lakini Mwenyezi Mungu anawajua. Na mkitoa chochote katika Njia ya Mwenyezi Mungu mtarudishiwa, na wala nyinyi hamtadhulumiwa.” [Surah Al-Anfal 8:60].

Kwa Rehema za Mwenyezi Mungu (swt), Umma unamiliki makombora yenye uwezo wa kuharibu miundombinu ya kimkakati na uwezo wa kijeshi wa umbile la Kiyahudi. Ina wana na mabinti mahiri kote ulimwenguni ambao wanaweza kufanya maendeleo makubwa katika teknolojia ya makombora. Hata hivyo, Ummah hauna uongozi wa dhati ambao utatumia makombora kwa uwezo wake wote. Watawala wa sasa wa Waislamu wameugawanya na kuudhoofisha Ummah kupitia utaifa. Wanahakikisha utawala wa mfumo wa kimataifa wa Marekani. Wanazidisha nguvu za kijeshi za Ummah kwa sifuri. Umma kamwe hautawahi kuona ushindi chini ya watawala wa sasa na dola zao za kitaifa.

Ni wazi sasa kwetu sote kwamba Umma lazima uyatake majeshi yake yawang'oe watawala wa Waislamu. Ummah lazima uyatake majeshi yatoe Nusrah yao kwa Hizb ut Tahrir kwa ajili ya kusimamisha Khilafah Rashida kwa Njia ya Utume. Ni Khilafah Rashida ndiyo itakayokusanya majeshi kuikomboa ardhi inayokaliwa kwa mabavu, na kuweka mfumo wa dunia kwa misingi ya utawala wa Dini.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Muhannad Mujtaba – Wilayah Pakistan

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu