Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Chini ya Udhamini na Usimamizi wa Marekani: Iran na Umbile la Kiyahudi Zimeungana katika Kuangamiza Ulimwengu wa Kiislamu
(Imetafsiriwa)

Habari:

Gazeti la Uingereza la ‘The Times’ lilifichua kuwa umbile la Kiyahudi liliakhirisha shambulizi lake la kulipiza kisasi dhidi ya Iran wiki iliyopita kutokana na uvujaji wa taarifa nyeti za kijeshi kutoka Marekani. “Kuvuja kwa hati nyeti, inayodhaniwa kuwa tathmini ya mipango ya mashambulizi ya IDF, inalazimisha kufikiri upya katika kukabiliana na shambulizi la makombora la Tehran... kuvuja huko kumefichua kuwa mipango iliyopangwa vizuri mno mapema kujibu msururu (salvo) wa takriban makombora ya balistiki 200 ya Iran yaliyorushwa dhidi yake mapema mwezi huu, ambayo ilikuwa ni kulipiza kisasi kwa Tehran kwa mashambulizi ya ‘Israel’ dhidi ya makundi yake ya wakala ya Mashariki ya Kati... Waraka huo wa siri kuu ulichapishwa kwenye chaneli ya Telegram inayoiunga mkono Iran Ijumaa iliyopita na ilionekana kuwa ni tathmini ya Marekani ya uwezekano wa majibu wa ‘Israel’, kulingana na picha za satelaiti na ujasusi mwengineo. Mwezi Aprili, ‘Israel’ ilijibu mashambulizi ya hapo awali ya makombora ya balistiki ya Iran, makombora na droni kwa kuharibu kituo cha rada nje ya Isfahan katikati mwa Iran... Silaha zilizotajwa katika uvujaji wa Marekani ziliashiria ‘Israel’ huenda ilikuwa inapanga mashambulizi sawa na hayo. “Rocks” ni kombora la masafa marefu kutoka angani hadi ardhini ambalo linaweza kurushwa kutoka kwa ndege za kivita za F-16 au F-35 na limetengenezwa na Rafael, mtengenezaji wa ulinzi wa ‘Israel’. “Golden Horizon” huenda ikakusudia Blue Sparrow, kombora la balestiki linalorushwa hewani ambalo lina umbali wa maili 1,200, kulingana na vyombo vya habari vya ‘Israeli’.” [Times]

Maoni:

Imedhihirika wazi kwamba Marekani, na pamoja nayo umbile la Mayahudi, hawana kikomo kwa mauaji wanayofanya huko Gaza na Lebanon. Wana chuki, na hamu ya kulipiza kisasi, ambayo haikuzimwa na mito ya damu inayotiririka huko Gaza, kwa zaidi ya mwaka mmoja, na kufuatiwa na damu nyingi zaidi nchini Lebanoni. Imefichuliwa kuwa hakuna jibu kwa swali ambalo kwa muda mrefu limekuwa likiulizwa na pande mbalimbali “siku baada ya Gaza.” Imebainika kuwa hakukuwa na mradi wowote wa kisiasa uliopitishwa na utawala wa Marekani, mfadhili wa uhalifu huko Gaza, isipokuwa mauaji yaliyofuata nchini Lebanon. Kwa hivyo, mauaji ya Lebanon yalikuwa jibu la swali la matukio baada ya Gaza. Hii inathibitisha kwamba hakuna mpango uliopitishwa na Amerika na dola ya Kiyahudi iliyoiunga mkono, isipokuwa mauaji zaidi na zaidi, udhalilishaji na unyenyekeshaji. Inaonekana kana kwamba mbinu hii ya usimamizi inalingana na sera ya “machafuko ya ubunifu” iliyopitishwa na kambi ya ‘neoconservative’ ya makauboi wa Marekani. Wanatarajia kwamba mpango utaibuka kutokana na machafuko, ambayo yanawaridhisha, na kutumikia maslahi yao.

Usimamizi na uratibu wa Marekani wa dhana inayoendelea kati ya Iran na umbile la Kiyahudi kuhusu mashambulizi ya kiusanii, ambayo haidhuru pande zote mbili, inakusudiwa kutoa muda zaidi kwa umbile la Kiyahudi kuua vikosi vya upinzani vilivyobaki mjini Gaza na Lebanon. Hii ni pamoja na kuiingiza Iran katika hali ya kisiasa katika Mashariki ya Kati, na kuitumia, pamoja na umbile la Kiyahudi kusimamia eneo hilo kwa njia inayohudumia maslahi ya Amerika pekee. Uhuru ambao Amerika inatoa kwa umbile la Kiyahudi, mwezi mmoja baada ya mauaji yake ya kiongozi wa Hamas nchini Iran, unaangukia katika muktadha huu tu. Ni marudio ya makubaliano yaliyotolewa na Marekani kwa umbile la Mayahudi katika siku za nyuma. Hii yote ni kutokana na ukosefu wa mpango uliotangazwa uliopitishwa na utawala wa Marekani. Marekani na Mayahudi wana chuki na uovu kwa Uislamu na Waislamu, ambazo zimewapofusha. Walipoteza akili zao katika kusimamia hali hiyo kifikra. Sisemi haya kwa hekima yoyote ya duniani, wao ni kama alivyosema Mola wetu Mlezi,

[أُولَئِكَ الَّذِينَ لَعَنَهُمُ اللَّهُ فَأَصَمَّهُمْ وَأَعْمَى أَبْصَارَهُمْ]

“Hao ndio Mwenyezi Mungu alio walaani, na akawatia uziwi, na akawapofoa macho yao.” [Surah Muhammad 47:23]

Hivi basi ni vita vya fahali hawa watatu, Marekani, utawala wa Safavid nchini Iran na umbile la Mayahudi, na hila zao dhidi ya Ummah, ndani ya moyo wa makaazi yake, ash-Sham. Ummah lazima utangaze hali ya hatari dhidi yao kabla haujachelewa. Hawa ni wahalifu wakorofi, kijeshi, kisiasa na kifikra. Ni dola ya Uislamu pekee inayoongozwa na Khalifa aliyeongoka ndio itakayoamiliana na umbile la Mayahudi kwa mujibu wa Sunnah ya Mtume (saw) kwa Bani Quraydah. Ni Khalifa aliyeongoka pekee ndiye atakayeiamiliana na Marekani kwa mujibu wa mfano wa Khilafah Uthmani, ambao uliishinda Amerika, na kuzamisha meli zake baharini, na kuilazimisha kulipa jizya. Ni Khalifa aliyeongoka pekee ndiye atakayeamiliana na utawala wa Iran kwa mujibu wa mfano wa Sultan Selim Yavuz, ambaye aliishinda himaya ya Safavid, na kwa mujibu wa mfano wa Sultan Suleiman Mtukufu, ambaye aliiunganisha na Dola ya Kiislamu.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Bilal al-Muhajir – Wilayah Pakistan

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu