Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Mafunzo Baada ya Mwaka Mmoja wa Mauaji ya Halaiki mjini Gaza

(Imetafsiriwa)

Habari:

Mwaka mzima umepita tangu tarehe 7 Oktoba 2023. Mwaka wenye mauaji ya halaiki na jinai zisizoelezeka dhidi ya Waislamu wa Palestina zinazoshuhudiwa na wote wenye macho ya kuona. Ni mafunzo gani tunaweza kupata tukitazama nyuma mwaka huu wa umwagaji damu na kutazamia mustakabali mwema kwa Palestina na Umma wa Kiislamu?

Maoni:

Mafunzo ya Ujasiri na Ustahamilivu kutoka kwa Waislamu wa Gaza

Waislamu wa Gaza wameonyesha nguvu na ustahamilivu mkubwa mbele ya ukandamizaji na ukatili usiokoma. Ujasiri wao ni ukumbusho kwetu sote maana ya kusimama kidete katika Imani na kumtegemea Mwenyezi Mungu, hata dhidi ya matatizo makubwa. Mapambano yao ya kila siku dhidi ya uvamizi wa Kizayuni, bila ya majeshi au usaidizi, yanaonyesha nia isiyoweza kuvunjika ya kupinga dhulma. Gaza imekuwa ishara ya nafsi ya Umma wa Kiislamu, ambayo haiwezi kupondwa kamwe, na itaendelea kuwa tayari kujitolea, mpaka ushindi ulioahidiwa wa Mwenyezi Mungu utakapopatikana. Zaidi ya hayo, Waislamu shupavu wa Gaza wamefichua kwa mara moja udhaifu wa uvamizi wa Kizayuni, ambao – licha ya ukatili wake wa kupindukia – unaendelea kutikiswa hadi msingi wake na upinzani kwa njia rahisi, na kamwe hautaweza kusimama kwa makabiliano na jeshi la kawaida la Waislamu.

Mafunzo ya Usaliti kutoka kwa Tawala katika Nchi za Waislamu

Tawala za nchi za Waislamu, bila ubaguzi, zimeiangusha Gaza na Palestina. Licha ya dhulma ya wazi, watawala katika ulimwengu wa Kiislamu wanaendelea na ushirikiano wao wa khiyana na ukaliaji kimabavu wa Kizayuni na utumwa wa Magharibi. Wametanguliza viti vyao vibovu vya utawala, utajiri wa duniani, na utumwa wa hila kwa mabwana zao wa kikoloni wa Magharibi kuliko kuwatetea wanyonge na wanaokandamizwa. Huku Al-Aqsa ikiendelea kukaliwa kimabavu, na Gaza inapigwa mabomu na njaa, wanaendelea kufunga mipaka na kutoa kauli tupu badala ya kutuma majeshi. Badala yake, baadhi yao walifungua mipaka ili kuruhusu tu vifaa kwa Wazayuni wauwaji wa halaiki, huku wengine wakionyesha uadui wa kisanii kwa Wazayuni, bila hatua zozote za kukomesha uvamizi huo au kuudhuru kwa njia yoyote thabiti; hivyo kuupa tu ujasiri kupanua jinai zake. Kufeli huku kunatokana tu na kutokuwa na nia, bali ni usaliti mwingine wa tena wa moja kwa moja wa Ummah, unaodhihirisha utiifu wa tawala hizi kwa maadui wa Uislamu.

Mafunzo Kuhusu Ulimwengu na Jumuiya ya Kimataifa

Jumuiya ya kimataifa kwa mara nyingine tena imejidhihirisha kuwa ganda tupu, linaloendeshwa na unafiki na undumakuwili. Huku wakidai kutetea haki za binadamu na uadilifu, mjini Gaza tunaona kwamba sheria zao zinatumika tu kulingana na matakwa ya kisiasa ya wenye nguvu, na msaada wao unaenea tu kwa wale wanaotumikia maslahi yao. Umoja wa Mataifa na taasisi nyingine za kimataifa zimekuwa zikishughulika vyema na kukaa kimya na kushiriki vibaya mno wakati mauaji ya halaiki yakiendelea na kupanuka. Hii inatufundisha kwamba ukombozi wa Palestina hautakuja kamwe kupitia diplomasia au maazimio ya kimataifa. Taasisi na maazimio haya sio kwamba hayafanyi kazi, badala yake, yalianzishwa kwa lengo hasa la kuhifadhi utawala wa wakoloni wa Magharibi, ambao kwao ukaliaji wa kimabavu wa Kizayuni ni mkono wake mwengine.

Uvamizi wa Kijeshi Utaisha kupitia Ukombozi wa Kijeshi

Historia na uhalisia wa sasa zinatufundisha kwamba uvamizi wa kijeshi wa Wazayuni unaweza tu kuondolewa kwa ukombozi wa kijeshi. Muhimu zaidi, hii ni amri ya Mwenyezi Mungu swt. Hakuna suluhisho jengine ambalo linakubalika Kiislamu au kimantiki. Gaza si janga la kibinadamu lisiloelezeka; ni sehemu ya vita dhidi ya Ummah. Uongozi wa Kiislamu pekee, Khilafah Rashida, ndio utakaovunja minyororo ya ukandamizaji na mgawanyiko wa kitaifa na kutuma majeshi kuikomboa Palestina yote. Jaribio lolote la kutafuta suluhu kwa njia ya mazungumzo na vikosi vinavyokalia kimabavu vitahusisha kusalimisha Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina, na kufanya usaliti dhidi ya Mwenyezi Mungu, Mtume Wake (saw) na Umma wa Kiislamu.

Mafunzo Kuhusu Sisi Wenyewe: Je, Tunasimama Wapi?

Ni lazima pia tujiangalie ndani na kujiuliza: Je, sisi kama Umma tunasimama wapi? Tunabeba jukumu la pamoja la kufanya kazi kwa ajili ya ukombozi wa Ummah na kusimamishwa kwa Uislamu kama mfumo kamili wa maisha. Gaza imefichua sio tu uzembe na kutoweza kwetu chini ya tawala za kisaliti za sasa, lakini pia uwezo wetu. Tunasimama kwenye njia panda ambapo ima tunaweza kuendelea kukubali kutawaliwa kwetu na utaratibu wa sasa wa kisiasa au tunaweza kufanya kazi ya kusimamisha tena Khilafah ambayo itawakomboa na kuwaunganisha Waislamu, na kuregesha haki, usalama na utu.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Elias Lamrabet

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu