Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Mbweha ni Mbwa Mwitu Anayetuma Maua… Mbweha Ana Hila Nyingi…

(Imetafsiriwa)

Habari:

Aliyekuwa balozi wa Marekani katika umbile la Kiyahudi, Martin Indyk, mnamo Alhamisi tarehe 20 Juni aliamua kuondoa mwaliko kwa Waziri Mkuu wa Kiyahudi Benjamin Netanyahu kutoa hotuba mbele ya Bunge la Congress. Hii ni ili aombe radhi kwa kuutuhumu utawala wa Rais Joe Biden kwa kuinyima silaha “Israel,” huku vyombo vya habari vya Kiyahudi vikisema kuwa Netanyahu anapendelea makabiliano ya hadharani na Washington. Netanyahu amepangwa kutoa hotuba mbele ya mabunge yote mawili ya Congress mnamo Julai 24, kwa kisingizio kwamba hii inaashiria uhusiano wa kudumu kati ya Marekani na umbile la Kiyahudi. Kauli za Indyk zinajiri baada ya mkutano wa Netanyahu Jumanne iliyopita, 18 Juni, ambapo aliishambulia Marekani, akisema, “Ni jambo la kushangaza kwamba katika miezi michache iliyopita, utawala umekuwa ukizuia silaha na zana kwa “Israel.”... “Israel” mshirika wa karibu wa Marekani, inayopigania maisha yake, ikipigana dhidi ya Iran na maadui wetu wengine wa kawaida.” Pia alisema kuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Anthony Blinken alimhakikishia kwamba utawala wa Biden unafanya kazi ya kukomesha vikwazo vilivyowekwa kwa usafirishaji wa silaha kwenda “Israel,” ambapo Blinken alikataa kuthibitisha. Mei mwaka jana, utawala wa Biden ulisitisha shehena ya mabomu yenye uzito wa pauni 2,000 na pauni 500, kutokana na wasiwasi kuhusu athari yanayoweza kuwa nayo katika maeneo yenye watu wengi. Lakini dola ya Kiyahudi bado imepangiwa kupata silaha za Marekani zenye thamani ya mabilioni ya dolari (Imetafsiriwa kutoka Al Jazeera Kiarabu).

Maoni:

Tangu shambulizi la kikatili lilipoanzishwa dhidi ya Gaza baada ya tarehe 7 Oktoba 2023, ambapo dola ya Kiyahudi ilikuwa ndio kiongozi mkuu, vyombo vya habari vimekuwa vikisambaza habari za mizozo kati ya wahalifu wabaya zaidi, kutoka miongoni mwa viongozi wa Magharibi na dola ya Kiyahudi. Habari hizo zinataja hasira, shutuma, chuki na mfadhaiko, kutoka kwa dola mbalimbali za kimataifa, zikiongozwa na utawala wa Biden, kuelekea kwa Netanyahu na serikali ya kihalifu anayoiongoza.

Kibaya zaidi ni kwamba wafuatiliaji, wanaharakati na wataalamu wengi wa vyombo vya habari, kutoka sehemu mbalimbali za dunia, wanapotoshwa na kimbunga hiki cha tuhuma.

Wamepotoshwa hadi kufikia hatua ya kutegemea “sintofahamu” hizi za kimaneno au "upinzani" rasmi ili kukomesha mauaji ya halaiki huko Gaza. Ni kana kwamba maandamano yanayoandaliwa katika barabara za Tel Aviv yatawapa ushindi watu wa Gaza, au kukomesha uhalifu wa Kiyahudi.

Hakuna shaka katika vita hivi vya kikatili kwamba Magharibi ndiyo kamba yenye nguvu ambayo dola ya Kiyahudi inaning'inia.

Ndio kitovu kinachochochea maovu yake. umbile hili la kuchukiza lisingesimama dhidi ya Ummah huu, wala lisingeweza kustahamili hata kundi dogo la Waislamu, lau si kamba hii. Hakuna shaka pia kwamba mizozo inayodaiwa kati ya washirika wa Mkruseda, na wakala wao, dola kibaraka na kambi ya kijeshi katika eneo, umbile la Kiyahudi, haikuathiri ushirikiano wao, katika kuunga mkono umbile hilo la Kiyahudi kwa pesa, silaha, na wanajeshi... Migogoro inayodaiwa haikuzuia mauaji ya umbile la Kiyahudi, wala hata kupunguza kasi ya uhalifu wake. Kwa hivyo vyombo vya habari vinaongeza sauti na vilio kwa migogoro gani?!

Uchambuzi wowote wa kisiasa lazima ujikite katika fahamu thabiti za kisiasa, ambazo ni maregeleo ambayo uhalsia wa kisiasa unachambuliwa.

Uchambuzi hauwezi kuwa kinyume na fahamu za kisiasa ambazo mchambuzi au mwangalizi wa kisiasa anaziamini. Kwa hiyo, kuelewa fahamu kwamba serikali kibaraka wakala, ambayo inategemea dola kuu, haiwezi kuasi dhidi ya mabwana zake, ni muhimu. Hatima yake iko mikononi mwa dola hiyo kuu. Hakuna upole au uvumilivu katika siasa katika mambo kama haya, hata ikibidi kugeukia mauaji ya kisiasa, kama ilivyotokea kwa Kennedy, Rabin, na wengineo. Ufahamu kama huo unatilia shaka “sintofahamu” katika taarifa zinazosambazwa na vyombo vya habari. Ufahamu kama huo unakanusha kuwepo kwa uasi halisi wa dola ya Kiyahudi, dhidi ya utawala wa Marekani na nchi nyingine za muungano wa Mkruseda.

Mizozo rasmi inayotangazwa hapa na pale, na machozi ya mamba ambayo yanatolewa na pande zote, ikiwa ni pamoja na mashirika ya kimataifa, kama vile “mahakama ya kimataifa ya dhuluma” na “mahakama ya kimataifa ya uhalifu,” yote ni kupoza rai jumla na kuweka matumaini juu ya utaratibu uliopo. Zinapaswa kuupa muungano wa Makruseda, na pamoja nao Mayahudi, muda wa kutosha wa kuua zaidi, na kuwaangamiza adui zao. Zinapaswa pia kuandaa rai jumla ya ulimwengu, pamoja na ulimwengu wa Kiislamu, kukubali njama za “suluhisho la dola mbili.”

Iwapo Ummah na majeshi yake yaliyowekwa katika kambi zao, hawatasonga kuwapindua watawala vibaraka katika ulimwengu wa Kiislamu, na kusimamisha Khilafah kwa Njia ya Utume kwenye magofu yao, basi muungano wa Makrusada utaweza

kutekeleza mpango wake muovu. Utakuwa na nguvu zaidi katika ardhi zetu. Si jambo la mbali kufikiria kwamba dola ya Kiyahudi itawekwa kama mfalme juu ya dola za madhara ziliyopo katika Ulimwengu wa Kiislamu. Hii itakuwa ndani ya mpango unaojulikana kama mpango wa kufuata “dini ya Ibrahim.” Kisha Ummah utahitajika kufanya juhudi zaidi, damu, na mateso ili kukombolewa kutokana na adui huyu muovu. Hebu watu wenye utambuzi katika Ummah nawajihadhari na hili na warekebishe hali zao kabla hawajachelewa.

[وَإِنْ تَتَوَلَّوْا يَسْتَبْدِلْ قَوْمًا غَيْرَكُمْ ثُمَّ لَا يَكُونُوا أَمْثَالَكُمْ]

“Na mkigeuka atawaleta watu wengine badala yenu, nao hawatakuwa kama nyinyi.” [Surah Muhammad 47:38]

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Bilal al-Muhajir – Wilayah Pakistan

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu