Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Mufti wa Tajikistan Aunga Mkono Kupigwa Marufuku Hijab

(Imetafsiriwa)

Habari:

Saidmukarram Abdukodirzoda, Mwenyekiti wa Baraza la Maulamaa wa Tajikistan, aliunga mkono rasimu ya sheria inayopiga marufuku "mavazi ngeni" na kusema kwamba mavazi ya kitaifa yanapaswa kuzingatia kanuni za Kiislamu. Alielezea kanuni za Kiislamu za suala hili hewani kwenye TV "Tajikistan" baada ya majadiliano juu ya kupigwa marufuku uagizaji, uuzaji na uvaaji "nguo zilizo ngeni na utamaduni wa kitaifa". Alisema kuwa Sharia inafafanua kanuni za mavazi kwa wanaume na wanawake, na kwa mujibu wake tunaweza kuvaa mavazi ya kitaifa.

"Watu wa Tajik wana nguo zao maalum. Waarabu pia wana nguo zao maalum. Kila taifa lina nguo zake maalum, na wakati huo huo, kanuni za Sharia zinazingatiwa. Hili ndilo muhimu, mengine si muhimu. Sio lazima kufuata na kuiga kwa upofu mavazu ya mtu mwingine", - alisema mwenyekiti wa Baraza la Ulamaa.

Maoni:

Leo, watu wa Tajikistan wanakabiliwa na jambo lile lile ambalo babu zetu walilipitia miaka 100 iliyopita, wakati viongozi wa Soviet katika miaka ya 20-30 ya karne iliyopita, kama sehemu ya kampeni ya "Khuchum", walianza kuwavua nguo kwa nguvu wanawake wa Kiislamu. Utawala wa Rahmon, ambao umekuwa ukipigania mwamko wa kidini kwa miongo miwili na kuwaingiza usekula kwa lazima watu wa Tajik, ulipiga marufuku uvaaji wa mavazi ya Kiislamu kwa wanawake kwa kisingizio cha kutofuata mila za kitaifa za watu wetu. Mara tu baada ya kupitishwa kwa toleo jipya la sheria "Juu ya udhibiti wa mila na matambiko", bila hata kusubiri marekebisho kuanza kutumika, walianza misako mikubwa ya kuwatambua wanawake wenye hijab.

Hii si mara ya kwanza kwa Saidmukarram Abdukodirzoda kuhalalisha uamuzi wowote dhidi ya Uislamu na mamlaka. Hivyo, hapo awali alihalalisha kupigwa marufuku kwa Hijja kwa watu walio chini ya miaka 40, kupiga marufuku baadhi ya mila zinazohusiana na Idd al-Fitr, kupiga marufuku kufundisha watoto Quran, na kuanzishwa kwa sherehe za Mwaka Mpya.

Tukumbuke kwamba hii si mara ya kwanza kwa utawala wa Tajik kujaribu kupitisha sheria ya kupiga marufuku mavazi ya Kiislamu kabisa. Mnamo mwaka wa 2018, serikali tayari ilijaribu kupitisha sheria kama hiyo, wakati kikundi cha wafanyikazi cha kati ya idara kiliundwa kwa mujibu wa agizo la utawala wa rais kulingana na pendekezo la Kamati ya Masuala ya Wanawake ya kupiga marufuku wanawake na wasichana wenye satr na hijab kuingia katika taasisi, mashirika na biashara zote, bila kujali umiliki. Kisha, chini ya shinikizo la umma, serikali ililazimika kuachana wazo lake. Wakati huu, inaonekana, serikali ya Rahmon imedhamiria kwa dhati kuona mambo yamepita, ikimjumuisha, kama kawaida, mufti wake wa mfukoni.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Muhammad Mansour

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu