Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Uamuzi wa Mahakama ya Shirikisho kuhusu Utekelezaji Sharia wa Kelantan - Umetumia Sharia ipi?

(Imetafsiriwa

Habari:

Mnamo Agosti 2023, mawakili wawili, Nik Elin Zurina na Tengku Yasmin, waliwasilisha ombi kwa lengo la kubatilisha vifungu18 ndani ya Sharia ya Jinai ya Kelantan. vifungu hivyo, vilivyoainishwa chini ya Sharia ya Kiislamu, viko chini ya mamlaka ya Bunge la Jimbo la Kelantan (DUN). Mnamo Februari 15, 2024, Mahakama ya Shirikisho, katika uamuzi wa walio wengi 8-1, iliamua kwamba vifungu 16 kati ya 18 chini ya Sheria ya Jinai ya Kelantan ni kinyume cha sheria. Mahakama ilisema kuwa Kelantan DUN haina mamlaka ya kutunga sheria kuhusu masuala haya kwa sababu sheria za shirikisho tayari zinashughulikia vifungu  hivyo hivyo. Uamuzi huu unasisitiza ukuu wa katiba ya shirikisho na una athari kwa usimamizi wa sheria za Kiislamu huko Kelantan. Uamuzi huo umeibua majibu mbalimbali kutoka kwa wananchi. Ingawa wengine wanaiona kama maendeleo chanya kwa mfumo wa kisheria wa Malaysia, wengine wanaona kama ukiukaji wa uhuru wa serikali na usumbufu katika utawala wake unaozingatia "kanuni za Kiislamu".

Maoni:

Kiini cha kesi hii ni rahisi - muingiliano wa mamlaka kati ya DUN na Bunge la Kitaifa. Nik Elin aliwasilisha ombi kwa Mahakama ya Shirikisho, ambayo ilibidi irejelee katiba kufanya uamuzi wake. Ilipata mzozo wa kimamlaka, ambapo DUN ilikuwa imetunga sheria zilizoangukia chini ya usimamizi wa shirikisho. Kwa hiyo, vifungu 16 vinavyokinzana vilitangazwa kuwa batili. Uamuzi huo umezua mjadala, huku baadhi ya simulizi zikidokeza kuwa Sharia iko chini ya tishio, mamlaka ya Mahakama za Sharia yanapungua, na Uislamu uko hatarini. Kwa wale wasiopenda kufikiria kwa umakinifu, au wanaochagua kutoingia ndani zaidi, ni rahisi kushawishiwa na simulizi hizi. Tukiweka kando simulizi hizi zenye hisia kali, swali la msingi linazuka: Je, "mahakama ya sasa ya Sharia" na "kanuni za Sharia" ni za Kiislamu kweli? Swali hili linafaa kuchunguzwa kabla ya kushughulikia matishio yanayoonekana kwa Sharia, kwani ni muhimu kutambua ni tafsiri gani ya "Sharia" inayojadiliwa.

Mamlaka ya Mahakama za Sharia katika majimbo yote ya Malaysia yanadhibitiwa na Sheria ya Mahakama ya Sharia (Mamlaka ya Jinai) ya 1965 (Sheria ya 355), ambayo inakataza adhabu za kifungo kisichozidi miaka mitatu, faini isiyozidi RM 5,000, na kuchapwa viboko visivyozidi mara sita. (inajulikana kama adhabu 356). Kwa mfano, mtu akipatikana na hatia ya uzinzi, adhabu ya juu zaidi inaweza kuwa viboko sita, faini ya hadi RM 5,000, au kifungo cha hadi miaka mitatu jela. Kinyume chake, sheria ya Kiislamu inaamuru kuwachapa viboko wazinzi mara mia moja, bila kutambua faini au kifungo kwa makosa hayo. Mwenyezi Mungu (swt) anasema:

[الزَّانِيَةُ وَالزَّانِي فَاجْلِدُوا كُلَّ وَاحِدٍ مِنْهُمَا مِائَةَ جَلْدَةٍ]

“Mzinifu mwanamke na mwanamume, mpigeni kila mmoja wao bakora mia” [An-Nur 24: 2]. Hitilafu hii inatumika pia kwa kesi nyingine nyingi zinazoshughulikiwa na vifungu vilivyobatilishwa, ikionyesha kwamba "maamuzi ya Sharia" yanabanwa na adhabu 356, badala ya kuzingatia Quran au Sunnah.

Kufuatia matokeo ya kesi ya Nik Elin, wito wa kurekebisha katiba umeongezeka. Mwitikio huu ni wa kustaajabisha, kwani unanyanyua katiba kwa njia isiyo dhahiri juu ya Sharia. Wakosoaji wanalalamika kufutwa kwa baadhi ya "hukmu za Sharia" na kuzitetea kwa bidii, lakini wengi wameshikilia katiba kwa muda mrefu. Inazua swali: Je, hawatambui kwamba katiba, zao la utawala wa kikoloni wa Uingereza, imekuwa ndio mfumo wenyewe unaozuia matumizi ya Sharia? Je, si kipingamizi kwa vyama kutetea Sharia huku vikipigania katiba inayoweka ukomo wa kutekelezwa kwake kikamilifu?

Isitoshe, mwitikio wa kesi ya Nik Elin haupaswi kuonekana kama "siku nyeusi" kwa Waislamu, kwani Malaysia haitabikishi kikamilifu Sharia. Kipindi "cheusi" halisi kwa Waislamu kilianza kwa kuvunjwa kwa Khilafah mnamo tarehe 28 Rajab 1342 H (Machi 3, 1924), na kuashiria uingizwaji wa Sharia na mifumo ya kisekula iliyowekwa na dola za kikoloni. Changamoto iliyopo sasa ni kuliongoza taifa kutoka katika hizi "siku nyeusi." Ni lazima kwa pamoja tujitahidi kusimamisha tena Dola ya al-Khilafah ar-Rashidah ala Minhaj Nubuwwah, ambapo mwongozo wa Mwenyezi Mungu (swt) na Sunnah za Mtume Wake unatekelezwa kwa ukamilifu wake, kuchukua nafasi ya sheria na mifumo ya kisekula liyopo.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Dkt. Mohammad – Malaysia

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu