Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

‘Hatua ya Dubai’ Inafichua Uchafu wa Demokrasia - Ni kwa Mfumo wa Kiislamu pekee ndipo Utulivu wa Kweli unaweza Kufikiwa

(Imetafsiriwa)

Habari:

Malaysia: Tangu kuibuka uvumi kwamba kutakuwa na mabadiliko ya serikali kupitia kile kinachoitwa ‘Hatua ya Dubai’, tayari kumekuwa na mamia ya ripoti za polisi kuhusu suala hilo kutoka pande mbalimbali nchini kote. Kulingana na polisi, shughuli zote zinazohusiana na ‘Hatua ya Dubai’ zinaweza kuhitimishwa kama shughuli zinazoweza kuvuruga utulivu wa umma na kusababisha wasiwasi. 'Dubai Step' ni nini hasa? Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Mawasiliano ya Jamii (J-KOM), Datuk Ismail Yusop katika taarifa yake alidai kuwapo kwa vuguvugu linalojulikana kwa jina la 'Dubai Step' linalofanywa na wapinzani wenye lengo la kuiangusha Serikali ya Umoja. Ismail alidai kuwa mkutano uliohusisha viongozi wa chama cha upinzani cha Perikatan Nasional (PN) na vyama kadhaa vya serikali ulifanyika Dubai kujadili idadi ya Wabunge ambao wanaweza kuelekeza uungaji mkono wao kwa upinzani.

Maoni:

Datuk Ismail Yusop anaichukulia juhudi za kuiangusha Serikali ya Umoja kupitia madai ya 'Hatua ya Dubai' kuwa ni harakati ya uhaini ingawa watendaji kadhaa wa sheria wanaojulikana wana maoni kinyume wakitaja kwamba kitendo hiki kinaruhusiwa na Kifungu cha 43 cha Katiba ya Shirikisho. Iwapo mtu atazingatia hali ya hivi karibuni ambapo pendekezo la kuunda sheria mpya ya kuzuia mabadiliko ya Waziri Mkuu hadi uchaguzi ujao ufanyike (Sheria ya Bunge la Muda maalum) kuna uwezekano mkubwa kwamba hii inayodaiwa 'Hatua ya Dubai' imeundwa kucheza na hisia za watu. Hatua kama ya Dubai inaweza kusababisha kukosekana kwa utulivu na machafuko katika utawala wa nchi na inaweza kudhoofisha mipango yote ambayo Serikali inafanyia kazi hivi sasa. Kwa hiyo, ni muhimu sana kwa wabunge na wananchi kuunga mkono mapendekezo ya sheria mpya! Inawezekana kwamba uvumi huu wa 'Hatua ya Dubai' ni ujanja wa kisiasa tu! Hiyo ndiyo demokrasia kwako!

Kinyume chake, mfumo wa utawala wa Kiislamu (Khilafah) ni tofauti kabisa na mfumo uliobuniwa na mwanadamu kama unaotekelezwa nchini Malaysia, ambao unatekeleza demokrasia ya mtindo wa Westminster. Katika Uislamu, hakuna kikomo kwa idadi ya vyama vya kisiasa vinavyoweza kuwepo. Hata hivyo, vyama hivi vya kisiasa lazima viegemee kwenye itikadi ya Kiislamu. Vyama vya kisiasa ndani ya Khilafah vipo kwa madhumuni ya da’wah na kumhesabu Khalifa. Hakuna mtu yeyote anayeruhusiwa kuanzisha chama cha kisiasa kinachokwenda kinyume na Aqidah ya Kiislamu. Kuanzia hapo, ikiwa Khalifa ameteuliwa, hawakilishi chama chochote kwa sababu itikadi ya vyama vyote vya kisiasa ni sawa na itikadi aliyonayo Khalifa ambaye ni Uislamu. Anachoamua Khalifa lazima kiwe na msingi wa Uislamu tu. Khalifa anawajibika kutekeleza Sharia kwa uadilifu kwa Waislamu wote na wasiokuwa Waislamu. Wasiokuwa Waislamu watapata haki zao katika nyanja zote za maisha zilizowekwa na Uislamu mradi tu watii utekelezaji wa mfumo wa Kiislamu juu yao. Kwa hiyo, maadamu Khalifa anautekeleza Uislamu, basi kila mtu, pamoja na vyama vyote vya kisiasa lazima wamtii. Hii ina maana kwamba maadamu Khalifa anatekeleza Sharia, hawezi kung'olewa madarakani kwa sababu tu ya kutokubaliana au kosa, maadamu Uislamu bado unatekelezwa. Hata hivyo, Khalifa bado anaweza kufunguliwa mashtaka katika Mahakama ya Madhalim iwapo atafanya dhulma dhidi ya watu. Hili ndilo linaloifanya Khilafah iendelee kuwa thabiti, imara na isiopingwa maadamu Khalifa ataendelea kuwa imara katika kutekeleza Sharia ya Kiislamu kwa ukamilifu.

Leo hii serikali za nchi za Kiislamu zimejaa misukosuko na dhulma kwa sababu ya mfumo wa kurithi kutoka kwa nchi za Magharibi - mfumo uliojaa mianya ambayo imekuwa uwanja wa ghilba za viongozi wa leo ili kunyakua madaraka na mali. Ni kwa kutekeleza kikamilifu mfumo wa Kiislamu ndipo Waislamu wataweza kuona utulivu wa kweli.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Dkt. Mohammad – Malaysia

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu