Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Kutojali kwa Ulimwenguni: Mapambano ya Warohingya na Wapalestina Yafichua Kutofaa kwa Mfumo wa Kimataifa

(Imetafsiriwa)

Habari:

Wakimbizi wa Rohingya wanaokabiliwa na mateso nchini Myanmar wanastahamili safari hatari za baharini kufika katika jimbo la Aceh nchini Indonesia. Ongezeko la hivi majuzi la waliowasili, linalozidi 1,600 tangu Novemba, linaathiri ukarimu wa kihistoria wa Aceh kwa wakimbizi wa Rohingya. Wanakijiji, ambao kiasili ni wakarimu, wamejaribu kusukuma maboti kuyarudisha baharini, kuashiria kuachana na desturi za zamani. Mmiminiko huo unazizidi rasilimali za ndani, na hivyo kuzua wasiwasi kwamba Indonesia huenda ikafuata nchi jirani kunyima kuingia kwa wakimbizi wa Rohingya. Licha ya hali ngumu, wakimbizi wanatoa shukrani kwa usalama nchini Indonesia ikilinganishwa na Bangladesh. Serikali kuingilia kati inahimizwa kushughulikia mgogoro wa kibinadamu, na wanaharakati wakiangazia majukumu ya Indonesia chini ya Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Sheria ya Bahari. Serikali, kwa kutambua changamoto hizo, inatafuta uwiano kati ya masuala ya kibinadamu na maslahi ya kitaifa huku ikichunguza ulanguzi wa binadamu. Chanzo kikuu kinahusishwa na ghasia zinazoendelea nchini Myanmar, na kusisitiza haja ya ushirikiano wa kimataifa kuregesha amani. (Chanzo: CNA)

Maoni:

Suala linalowakabili wakimbizi wa Myanmar, walioko Indonesia na Bangladesh, kamwe halitatatuliwa hadi tatizo la msingi litatuliwe—mauaji yanayofanywa na utawala wa Myanmar na Mabudha wenye misimamo mikali dhidi ya Waislamu. Jumuiya ya Kimataifa, yakiwemo mataifa ya Kusini-Mashariki mwa Asia, ASEAN, na Umoja wa Mataifa, yanaweza tu kuchukua mtazamo wa kibinadamu kwa vile wanakosa uwezo wa kulazimisha kukomesha mauaji haya.

Tatizo la Warohingya linaakisi hali ya Waislamu katika Palestina ya sasa, wote wakiteseka na masuala ya kisiasa huku ulimwengu ukisalia kimya juu ya mzizi wa tatizo hilo, ukizingatia tu masuala ya kibinadamu. Ni dhahiri kwamba mfumo wa sasa wa kimataifa hauwezi kutegemewa kutatua masuala mbalimbali ya kibinadamu, huku tukisubiri mara kwa mara mataifa makubwa kuchukua hatua. Vyenginevyo, tunakuwa watazamaji tu au waganga wa muda kwa ajili ya ndugu zetu wanaochinjwa na makafiri.

Hili linafaa kuwa funzo kwamba kushindwa kwa mfumo unaotawala katika miongo kadhaa iliyopita hautegemeki. Uislamu na Khilafah pekee ndio unaoweza kutegemewa kikweli kuzuia madhara mbalimbali yanayoletwa na makafiri dhidi ya Waislamu na kulinda Umma wa Kiislamu.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Abdullah Aswar

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu