Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Kupanua Faida ya Kimkakati Kulinda Damu ya Waislamu huko Gaza

(Imetafsiriwa)

Habari:

Wizara ya Ulinzi ya Marekani ilitoa taarifa ifuatayo mnamo 18 Disemba 2023, "Taarifa kutoka kwa Waziri wa Ulinzi Lloyd J. Austin III juu ya Kuhakikisha Uhuru wa Urambazaji katika Bahari Nyekundu. Kuongezeka kwa hivi karibuni katika mashambulizi ya ovyo ovyo ya Houthi kutoka Yemen kunatishia mtiririko huru wa biashara, kuhatarisha mabaharia wasio na hatia, na kukiuka sheria za kimataifa. Bahari Nyekundu ni njia muhimu ya maji ambayo imekuwa muhimu kwa uhuru wa urambazaji na barabara kuu ya kibiashara inayowepesisha biashara ya kimataifa ... Operesheni Ulinzi wa Ustawi inaleta pamoja nchi nyingi ikijumuisha Uingereza, Bahrain, Canada, Ufaransa, Italia, Uholanzi , Norway, Ushelisheli na Uhispania, kushughulikia kwa pamoja changamoto za usalama katika Bahari Nyekundu ya Kusini na Ghuba la Aden, kwa lengo la kuhakikisha uhuru wa urambazaji kwa nchi zote na kuongeza usalama wa kikanda na ustawi."

Maoni:

Huku Ummah wa Kiislamu ukisubiri kwa uvumilivu majibu yanayostahiki kwa mauaji ya Gaza kutoka kwa wanamgambo wenye nguvu wa Misri, Uturuki, Jordan, Saudia, Iran na Pakistan, wanamgambo wa Houthi wenye vifaa hafifu wamesababisha mgogoro, ambao wanyoofu katika vikosi vya majeshi lazima lazima wazingatie.

Mahouthi walitumia udhaifu wa kimkakati wa Mlango wa Bahari wa Bab el-Mandeb katika Bahari Nyekundu kunyonga njia ya baharini kwa meli za biashara. Kimsingi inasitisha shughuli za kampuni zote kuu za usafiri wa meli. Marekani kisha ikatangaza kikosi kipya cha ulinzi wa baharini ili kuhakikisha uhuru wa urambazaji katika Bahari Nyekundu.

Bila kujali uchanganuzi juu ya kwa nini na kwa sababu gani, hatua za Mahouthi zinaonyesha kuwa kwa rasilimali kidogo, hatua za kimkakati zinaweza kuchukuliwa ili kupambana na mfumo wa kikoloni wa kilimwengu wa Marekani, na washirika wake wa Kimagharibi, ili kuzuia uhalifu wao katika nchi za Waislamu. Hii ni huku ikijulikana kuwa ni msaada kwa umbile la Kiyahudi na Dola ya Kibaniani.

Mwenyezi Mungu (swt) ametoa faida nyingi za kimkakati kwa Waislamu kote ulimwenguni. Hizi zinaweza kutumiwa kwa ufanisi na kuongezwa kwa niaba ya Waislamu, kulinda damu na heshima ya Waislamu. Walakini, hii inahitaji utashi mkali na ikhlasi ambayo ni uongozi wa Kiislamu pekee ndio unaoweza kutoa.

Hivi sasa, kile kinachowazuia Waislamu kufanya hivyo ni watawala vibaraka wa Waislamu. Wanalinda tu maslahi ya Marekani na Magharibi. Maafisa katika majeshi ya Waislamu lazima watambue kuwa ni watawala wao wasaliti ndio wanaowazuia kuwasaidia Waislamu huko Gaza, na kuikomboa Palestina.

Kwa kuwaondoa watawala hawa wasaliti na kusimamisha tena Khilafah kwa Njia ya Utume, maafisa wa jeshi hatimaye wataongozwa na uongozi wa Kiislamu. Khalifa anaweza kutumia kwa urahisi na kwa ufanisi faida za kimkakati zinazozunguka ulimwengu wa Kiislamu kuupiga vita utawala wa Marekani na Magharibi.

Abu Hurairah amesimulia kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu (swt) amesema,

«إِنَّمَا الإِمَامُ جُنَّةٌ يُقَاتَلُ مِنْ وَرَائِهِ وَيُتَّقَى بِهِ فَإِنْ أَمَرَ بِتَقْوَى اللَّهِ وَعَدَلَ فَإِنَّ لَهُ بِذَلِكَ أَجْرًا وَإِنْ أَمَرَ بِغَيْرِهِ فَإِنَّ عَلَيْهِ وِزْرًا»

“Hakika Imam ni ngao watu hupigana nyuma yake na hujihami kwake. Akiamrisha uchaMungu na akafanya uadilifu basi hakika kwa hilo atapata ujira, na akiamrisha kinyume yake basi hakika ni mzigo (wa dhambi) juu yake.” [An-Nisaa’i]

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Ali Tariq – Wilayah Pakistan

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu