Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Tajikistan Itaunganishwa kwenye Mtandao wa Intaneti ya China

(Imetafsiriwa)

Habari:

Katika siku za usoni, muunganisho wa moja kwa moja wa mitandao ya mawasiliano ya Jamhuri ya Tajikistan na mitandao ya mawasiliano ya Jamhuri ya Watu wa China itatekelezwa, Khovar anaripoti hili kwa kuzingatia Huduma ya Mawasiliano chini ya Serikali ya Jamhuri ya Tajikistan.

"Ili utekelezaji wa haraka muunganisho wa moja kwa moja kati ya mitandao ya mawasiliano ya Jamhuri ya Tajikistan na mitandao ya mawasiliano ya Jamhuri ya Watu wa China, kazi ya kivitendo kwa sasa inafanywa kwa kasi ya haraka. Ni muhimu kuzingatia kuwa hatua hizi zinachangia katika uundaji wa laini za mawasiliano ya kasi hali ya juu ya kimataifa ya fiber-optic ili kuunganishwa na mitandao ya intaneti ya kiulimwengu. Hii pia itaongeza umuhimu na usafirishaji wa mitandao ya mawasiliano ya nchi hii na kuondoa kutengwa kimawasiliano kwa Jamhuri", - shirika la habari la serikali linaarifu.

Maoni:

Ikumbukwe kwamba leo Tajikistan ina mojawapo ya huduma za intaneti za kasi ya polepole zaidi ulimwenguni; Trafiki yote hupitia mkiritimba mkuu wa sekta hiyo, Huduma ya Mawasiliano, inayoongozwa na mshirika wa Rais wa Tajikistan, Beg Sabur. Waandishi wa habari bila mipaka waliripoti kwamba tovuti kuu za habari na majukwaa ya mitandao ya kijamii ilizuiliwa karibu kila wakati.

Hata hivyo, ni kipi kinachowasubiri watumiaji wa Tajik baada ya kuunganishwa na mtandao wa Intaneti ya China? Inajulikana vyema kuwa China ina aina ya udhibiti mkali zaidi ulimwengu katika uwanja wa mawasiliano ya simu na Intaneti, rasilimali zote za mtandao wa kimataifa na Intaneti na mitandao ya kijamii zimezuiliwa, matumizi ya huduma za VPN ni marufuku, na huduma za ujumbe wa hapo kwa hapo za kigeni zote zimezuiliwa. Pia kuna faini kubwa na adhabu za jinai kwa kukiuka vidhibiti vya serikali.

Ni dhahiri kwamba uunganishwaji wa mitandao ya Tajikistan na mawasiliano ya China unawaahidi wakaazi wa nchi yetu kupunguzwa mno kwa upatikanaji wa habari za ukweli juu ya yale yanayotokea, ambapo itasababisha kutengwa zaidi kwa idadi ya watu kutoka kwa ulimwengu wa nje.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Muhammad Mansour

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu