Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Wataalamu wa Haki Waonya dhidi ya Kutenganishwa kwa Nguvu kwa Watoto wa Uyghur nchini China

(Imetafsiriwa)

Habari:

Mnamo tarehe 26 Septemba 2023, wataalamu watatu huru wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa waliripoti kwamba kuna utenganishwaji wa lazima na sera za lugha kwa Uyghur na watoto wengine wa Kiislamu walio wachache katika shule za bweni zinazomilikiwa na serikali katika mkoa wa Xinjiang nchini China, ambapo ni sawa na kuoanishwa kwa lazima ndani ya thaqafa ya Kichina. Wataalamu hao watatu walisema wamepokea taarifa kuhusu kuondolewa kwa kiasi kikubwa cha vijana kutoka kwa familia zao, wakiwemo watoto wadogo sana ambao wazazi wao wako uhamishoni au "wamewekwa ndani"/wamezuiliwa. Watoto hao wanatendewa kama “mayatima” na mamlaka za Serikali na kuwekwa katika shule kamili za bweni, shule za chekechea, au makao ya yatima ambako Mandarin inatumiwa pekee, sio lugha ya asili waliyolelewa nayo. Ripoti hiyo imenukuliwa hapo chini;

“Watoto wa Uyghur na wengine walio wchache katika taasisi za mabweni zinazodhibitiwa huenda wakawa na maingiliano machache na wazazi wao, familia kubwa au jamii kwa sehemu kubwa ya ujana wao. Hii itasababisha kupotea kwa uhusiano na familia na jamii zao na kuhujumu mafungamano yao na kitambulisho chao cha kitamaduni, kidini na lugha.”

Maoni:

Umma wa Muhammad (saw) umeshuhudia mateso makali ya ndugu na dada zao nchini China kwa muda wa miaka 6 iliyopita. Kambi za kwanza za uzuizi kwa Waislamu zilianzishwa mwaka 2017 na utawala wa katibu mkuu wa CCP Xi Jinping. Kati ya 2017 na 2021, shughuli ziliongozwa na Chen Quanguo, ambaye zamani alikuwa mwanachama wa CCP Politburo na katibu wa kamati ambaye aliongoza kamati ya chama na serikali ya kanda hiyo. Katika mahojiano ya habari ya Guardian ya mwanamke mmoja wa zamani wa Kiislamu katika mojawapo ya ‘kambi za kuelimisha upya, alikuwa na yafuatayo ya kusema kuhusu maisha yake aliyoyapitia kwa muda wa miaka miwili;

“Jinsi ya kuwaambia wapendwa wangu kwamba niliishi chini ya unyanyasaji wa polisi….walitamani kwetu, miili na roho zetu… Ya wanaume na wanawake ambao waligeuza fikra zao vilivyo – maroboti yaliyonyang’anywa ubinadamu, yakitekeleza maagizo kwa bidii… wakikinaika kuwa tulikuwa maadui tuliostahiki kupigwa - wasaliti na magaidi - walitunyang'anya uhuru wetu. Siku moja, mmoja wa wanafunzi wenzangu, mwanamke mwenye umri wa miaka 60, alifunga macho yake, kwa hakika kutokana na uchovu au hofu. Mwalimu alimpiga kofi la kikatili. “Wadhani sijakuoni ukiswali? Utaadhibiwa!” Walinzi walimkokota kwa nguvu kutoka chumbani. Saa moja baadaye, alirudi na kitu alichoandika: kujikosoa kibinafsi. Mwalimu alimfanya atusomee kwa sauti. Alitii, uso ulioparara, kisha akaketi tena. Alichokifanya ni kufunga macho yake. Walitufungia kama wanyama mahali fulani mbali na ulimwengu mwingine, nje ya wakati: katika kambi…..mkono ulisukuma vibamba kwenye fuvu langu la kichwa, na mkono mwingine ukanyakua vipande vya nywele vilivyoanguka kwenye mabega yangu; Nilifunga macho yangu, nikiwa na machozi, nikidhani kuwa mwisho wangu ulikuwa karibu, kwamba nilikuwa nikitayarishwa kwa jukwaa, kiti cha umeme, kuzamishwa majini. Mauti yalitanda kila kona. Wauguzi waliponishika mkono ili “kunichanja,” nilifikiri walikuwa wakinitia sumu. Kiuhalisia, walikuwa wakitusafisha. Hapo ndipo nilipoelewa mbinu ya kambi, mkakati unaotekelezwa: sio kutuua kinyama, lakini kutufanya tupotee polepole. Polepole sana hivi kwamba hakuna mtu angegundua."

Maneno haya ni machache yaliyotokana na hofu walioishi nayo maelfu ya Waislamu katika kanda hiyo. Watu wazima na watoto hawatofautishwi katika jinsi wanavyotendewa kikatili. Kuangamizwa kwa watu huenda kukawa ndio lengo la maadui wa Uislamu, lakini ni lazima tuhuishe utawala ambao utaulinda Ummah wetu unaodhulumiwa, kwani viongozi wa ulimwengu wa Kiislamu wanasaliti uaminifu wao. Uyghur hawapaswi kuishi kwa hofu kwa siku nyengine tena, na ni wajibu wa Ummah huu kupaza sauti na kutenda ili kurudisha Khilafah itakayowaondoa madhalimu milele.

[يُرِيدُونَ أَنْ يُطْفِئُوا نُورَ اللَّهِ بِأَفْوَاهِهِمْ وَيَأْبَى اللَّهُ إِلَّا أَنْ يُتِمَّ نُورَهُ وَلَوْ كَرِهَ الْكَافِرُونَ]

“Wanataka kuizima Nuru ya Mwenyezi Mungu kwa vinywa vyao, na Mwenyezi Mungu anakataa ila aitimize Nuru yake ijapo kuwa makafiri watachukia.” [At-Tawba: 32]

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Imrana Mohammad
Mwanachama wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu