Jumanne, 24 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/26
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Waislamu Wanakataa Maombi ya Kuchukiza ya Msaada ya Abbas kama Udhalilifu

(Imetafsiriwa)

Habari:

"Kiongozi wa Palestina anatoa wito kwa ulimwengu 'kutulinda,' na watu wake wanajibu kwa kicheko cha uchungu" kwa mujibu wa CNN mnamo Julai 14 baada ya Rais wa Palestina Mahmoud Abbas kuzuru Jenin muda mrefu baada ya Vikosi vya Ulinzi vya 'Israel' kumaliza mauaji yao na kuondoka eneo hilo. Watu walikosoa sana ugumba wa Abbas, na hotuba yake ya awali kwa Umoja wa Mataifa mnamo tarehe 15 Mei katika ukumbusho wa kuanzishwa kwa umbile la Kiyahudi huko Palestina ilikabiliwa na kukejeliwa kukubwa na Wapalestina. "Tunapigwa kila siku, tunapiga kelele kila siku. Watu wa dunia, tulindeni! Je, sisi sio wanadamu? Hata wanyama wanapaswa kulindwa. Ikiwa una mnyama, je hutamlinda? Tulindeni...” aliiomba dunia. Watu wa ardhi iliyobarikiwa ya Isra na Miraj hawakufarijiwa na maombi yake.

Maoni:

Ulinganishaji wakati mwingine hufanywa kati ya uvamizi wa Urusi wa Ukraine na ukaliaji kimabavu wa umbile la Kiyahudi wa Palestina, huku mwitikio wa Magharibi ukiwa na mgongano sana. Labda mwandishi wa hotuba ya Abbas alifikiri kwamba ombi moja zaidi la msaada lingeweza kuleta wokovu. Waislamu wachache wangeweza kutapatapa kiasi cha kupata faraja kutokana na wito wa kiongozi wa Kiarabu kwa nchi za Magharibi kuwalinda chini ya kivuli cha - angalau kutupa haki sawa na wanyama. Viongozi wetu daima wanaweza kujidhalilisha zaidi huku wakizama zaidi ndani ya shimo la uwongo ambalo ni lile liitwalo Mfumo wa Kimataifa wa Kilimwengu, lakini Waislamu wa Palestina waligonga sakafu ya imani potofu muda mrefu uliopita.

Shirika la Ukombozi wa Palestina lilikuwa na ufanisi katika kuhalalisha fahamu kwamba wageni, chini ya pazia la Mfumo wa Kimataifa wa Kilimwengu unaofanya kazi kupitia Umoja wa Mataifa, unapaswa kuwa na dori katika kusuluhisha masuala ya kisiasa ya Waislamu. Eti Umoja wa Mataifa ungekuwa ndio chombo cha kuwasaidia Wapalestina kuregesha ardhi yao kutoka kwa umbile la Kiyahudi. Kwa hiyo, Waarabu walielimishwa kukariri wingi wa maazimio ya Umoja wa Mataifa na kufuata kwa shauku mijadala katika mikutano mtawalia ya Umoja wa Mataifa kuhusu kadhia ya Palestina. Kama sehemu ya kuhalalisha utiifu kwa nchi za Magharibi, uongozi wa PLO na kada walijivunia kutangaza ukiukaji wa haki za binadamu, na majeruhi miongoni mwa Wapalestina wakati wa uasi ulioanza mwishoni mwa miaka ya 1980 kwa lengo la kupata huruma kwa Wapalestina kama wahasiriwa. Kilichotakiwa kwa Wapalestina tu ni kuwa wahanga, huku uongozi ukitoa wito kwa viziwi - 'angalieni yale yanayowapata watu wetu - tuokoeni!'

Kisha, Shirika la Ukombozi wa Palestina baada ya kumakinisha utiifu wa mambo ya Waislamu kwa mfumo wa kimataifa, lilifikia lengo lililowekwa kwa ajili yake la kulihalalisha umbile la Kiyahudi ndani ya ulimwengu wa Kiarabu pindi walipotambua uhalali wa umbile hilo. Hapo ndipo ilipokuja Mamlaka ya Palestina, inayoongozwa sasa na Mahmoud Abbas. Sio dola wala mamlaka, bali ni kibaraka wa umbile la Kiyahudi kusimamia uvamizi wa Palestina kwa bei duni kwa niaba yao. Ombi pekee la Waislamu ni ombi lao kwa vyanzo vyao vya nguvu katika majeshi. Lau kama ule unaojulikana kama Mfumo wa Kimataifa ungejibu, ingekuwa tu kwa ajili ya kuendeleza maangamivu yetu, na sio kuyapunguza. Wakati Marekani na Ulaya zinajibu wito wa Ukraine wa kuomba msaada, ni kwa ajili ya kutajirisha viwanda vyao wenyewe, na kumwaga damu ya watu wa Ukraine hadi tone la mwisho la damu yao ili kuivunja vunja na kuitawala Urusi. Waislamu wasilie ngowa na msaada huo.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Dkt. Abdullah Robin

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu