Jumanne, 24 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/26
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Marekani Yaimiminia Fadhila Iran ili Kuharakisha Ufufuaji wa JCPOA

(Imetafsiriwa)

Habari:

• Iraq imepewa msamaha wa vikwazo na Marekani, na kuiruhusu kutoa dolari bilioni 2.76 za fedha za Iran kutokana na malipo ya mauzo ya nje ya gesi, kulingana na Yahya Al-e Eshaq, Mwenyekiti wa Muungano wa Chama cha Biashara cha Iran-Iraq.

• Fedha hizi zinatarajiwa kukidhi matakwa ya Benki Kuu ya Iran na kuhakikisha ununuzi wa bidhaa muhimu, ambao huenda ukasaidia kuleta ustawi wa soko la ubadilishanaji wa fedha za kigeni.

Maoni:

Habari hizi zina umuhimu katika muktadha wa hatua za Marekani-Iran kwenye faili ya nyuklia ya Iran. Utawala wa Biden umefanya lengo kuu la sera ya kigeni kuwa ni kufufua makubaliano ya nyuklia ya 2015 yanayojulikana kama Mpango Mpana wa Hatua za Pamoja (JCPOA), ambao serikali ya Trump ilijiondoa kutokana nao. Hatua hiyo ya mwisho ilifanywa ili kuutia adabu utawala wa Iran hususan Kikosi cha Quds kinachoongozwa na IRGC ambacho kilijitanua katika nchi mbalimbali za ulimwengu wa Kiarabu baada ya utawala wa Obama kutia saini mapatano ya JCPOA. Utawala wa Trump uliidhinisha shambulizi la droni ambazo zilimuua Kamanda wa Kikosi cha Quds, Qassim Soleimani wakati akiondoka kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Baghdad mnamo 2020. Mauaji haya yaliidhoofisha sana Kikosi cha Quds katika eneo hilo, na mkuu wake mpya Esmail Qaani kukosa haiba na ushawishi wa kudumisha wanamgambo wanaoungwa mkono na Iran kwenye safu ya Iran. Utiaji saini wa Marekani katika mapatano ya JCPOA wakati huo uliendana na maslahi ya Marekani ya kuuruhusu utawala wa Iran kutembea kwa uhuru katika eneo hilo hususan kuusaidia utawala wa Syria uliokuwa ukingoni mwa kuporomoka. Hili lingekuwa tetemeko la ardhi la kisiasa kwa Marekani, na wale wanaotaka kutabikisha mfumo wa Kiislamu kuchukua nafasi, ambapo ingetupa masuala yote ya kimkakati ya Marekani katika kizungumkuti.

Kwa kuzingatia sera mpya za kigeni za utawala wa Biden, unafanya kazi kufufua JCPOA au hata kutoa makubaliano ya muda ambayo yanaridhisha pande zote mbili. Kuna ushahidi kadhaa kuashiria juhudi za Marekani za kuanzisha mazungumzo ya nyuklia baada ya kukwama jijini Vienna. IAEA ikimaliza uchunguzi wake kuhusu kurutubishwa kwa madini ya uranium iliyopatikana katika maeneo ambayo hayajatangazwa nchini Iran, Bodi ya Magavana wake hivi karibuni haikutoa azimio la kuikosoa Iran licha ya kuendelea kurutubisha madini ya uranium juu ya kiwango cha usafi wa asilimia 60, Iraq ikitoa deni kwa Iran, uwezekano wa Korea Kusini pia kuachilia mali za Iran zilizozuiwa, ziara ya chini chini ya Mshauri Mkuu wa Usalama wa Kitaifa wa Biden Brett McGurk nchini Oman kujadili faili ya nyuklia ya Iran, ziara ya sultan wa Oman jijini Tehran (mkutano ulijumuisha mpatanishi mkuu wa nyuklia wa Iran Ali-Bagheri Kani), kubadilishana wafungwa kati ya Ubelgiji na Iran, ukiukaji wa Tehran wa ahadi zake za Machi kwa IAEA, na mazungumzo ya kubadilishanaji upya wa wafungwa kati ya Marekani na Iran, zote ni ushahidi wa wazi wa njia ya Marekani kuingia katika makubaliano, yawe ya zamani au mapya na utawala wa Iran. Hatua hizi zimetokea kwa muda mfupi, ikionyesha hamu ya utawala wa Biden kupata makubaliano hayo. Kwa nini hali iko hivi? Mazingatio kadhaa yanafanywa.

1. Marekani inataka kusuluhisha uhasama katika Mashariki ya Kati ili iweze kuzingatia kuhama ili kukabiliana na tishio linaloletwa na China. Matokeo yake, tumeona suluhu na maridhiano yasiyo na kifani yakifanyika, hata kuna harakati kwenye njia ya Misri na Iran kuvunja husuma baada ya miongo kadhaa ya uhasimu kati ya nchi hizo mbili.

2. Utawala wa Iran unafanya kazi kwa karibu katika masuala ya sera za kigeni na Marekani; hili ni dhahiri nchini Afghanistan, Iraq, na Syria. Kwa hivyo, si kwa manufaa ya Marekani kwa utawala wa Iran kuanguka bali inaonekana kuupatia afueni na ikiwezekana kurekebisha tabia yake linapokuja suala la faili fulani za kikanda kama vile Syria na Yemen. Aidha tishio hilo la Iran, lilizidi kuchanganua karata za Ghuba na za Kizayuni mikononi mwa Marekani, huku wahusika wote hao wakiitazamia Marekani kupata mwavuli na dhamana ya usalama, na hivyo kuhakikisha ushawishi na uongozi wake katika eneo hili.

3. Uchaguzi wa urais wa Marekani umepangwa kufanyika 2024, huku mchujo ukiendelea. Inaonekana kana kwamba utawala wa Biden unataka kutatua faili ya nyuklia ya Iran kabla ya mchuano wa urais kuanza; la sivyo, itakabiliwa na mashambulizi kutoka kwa wafuasi wa chama cha Republican na Wazayuni ambao watapatiliza kutumia uzi huu mwembamba kumhujumu mgombea wa Democrat. Ikiwa Biden atapata kutiwa saini mkataba huo, Wanademokrasia wataweza kuonyesha ahadi ambayo walikuwa wametoa katika mchuano uliopita; kutatua faili ya nyuklia ya Iran kwa kutumia diplomasia laini.

Hata hivyo, Wairani ni kikwazo, na Kiongozi Mkuu Ali Khamenei anahitaji kuwafurahisha wenye msimamo mkali. Hata hivyo, hotuba yake ya hivi majuzi kwa mabalozi na wanadiplomasia wa Iran ilionyesha kubadilika kwa upande wake na alitoa wito kwa wengine kuonyesha kubadilika katika sera za kigeni, na maelewano yasiyoonyesha kushindwa au hasara. Inaonekana alikuwa akiweka msingi wa kutia saini mkataba na Marekani. Hata hivyo, hana budi kukanyaga ardhi kwa uangalifu, kwani anatarajia kutengeneza mazingira ya mwanawe kumrithi; hili linaweza tu kutokea ikiwa IRGC yenye nguvu na watu wenye msimamo mkali watamuunga mkono.

Marekani-Iran zitaendelea kucheza na mikono yao iliyojificha licha ya kutopenda kwa wazi baina kuficha ukweli kwa watu. Ili kukomesha michezo hii, na kuhakikisha matumaini ya kweli kwa eneo hili, kuna haja ya kusimamisha tena Khilafah ambayo itaufurusha uingiliaji wa Marekani katika eneo hili na kutokubali mikataba ambayo inahatarisha usalama wake kwa ajili ya maslahi na ajenda za wakoloni.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Mohammed Abu Dawud

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu