Jumanne, 24 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/26
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Mfumo wa Kibepari Unawaruhusu Watawala Kuusaliti Uislamu

(Imetafsiriwa)

Habari:

Dkt. Aafia Siddiqui alikamatwa mwaka 2008 nchini Afghanistan. Mnamo 2010, Dkt. Siddiqui alitiwa hatiani na mahakama ya Marekani na kuhukumiwa kifungo cha miaka 86 jela. Dada mkubwa wa Dkt. Aafia alikutana naye baada ya miaka 20 katika Ngome ya Fort Worth ya Marekani ambako anazuiliwa kwa sasa. Wakati akikutana na dada yake, Dkt Fauzia hakuruhusiwa kumgusa dada yake wala hakuruhusiwa kumuonyesha picha za watoto wa Dkt. Aafia. Dada hao wote wawili walikutana katika chumba kilichotenganishwa na ukuta mnene wa kioo.  (Dunyanews)

Maoni:

Dkt. Fauzia aliongeza kusema kuwa Dkt. Aafia hakuwa katika hali nzuri na ilimchukua takriban saa moja kwa Dkt. Aafia kueleza yale anayopitia kila siku. Alikuwa akingoja kukutana na mama yake na watoto na hata hakujua kuwa mama yetu alikufa karibu mwaka mmoja uliopita. Dkt. Fauzia alisema Aafia alipoteza meno yake ya mbele katika jaribio la kutaka kumuua ndani ya jela na alikuwa na kovu kichwani. Inasemekana kuwa, Dkt. Aafia amekuwa akishinikizwa kupitia mbinu tofauti za mateso ili kuongea mambo ambayo hata hayajui. Ingawa Dkt. Fauzia alieleza kile ambacho amekifahamu katika mkutano wa hivi karibuni lakini bado siri nyingi hazijafichuka. Lakini tunaweza kutarajia kile ambacho makafiri hawa wanaweza kuwafanyia Waislamu. Tumeshuhudia maadui wa Mwenyezi Mungu (swt) wakienda kwa urefu wowote wawezao kuufikia.

Hili halikujulikana kwa uongozi wa Pakistan wakati wa Jenerali Musharraf na baraza lake la mawaziri walipomkabidhi dada wa Kiislamu kwa makafiri, ni mfumo unaomwezesha Musharraf na wenzake kuusaliti Uislamu na maadili ya Kiislamu kwa manufaa ya kidunia. Kinyume chake chini ya mfumo wa Khilafah Sindh yote ilitekwa ili kulinda maslahi ya Waislamu. Kulikuwa na ripoti za mashambulizi dhidi ya meli za biashara za Waislamu wa Kiarabu na unyanyasaji wa wafanyibiashara Waislamu huko Sindh. Hajjaj bin Yusuf aliona umuhimu wa kulinda maslahi ya Waislamu na kuhakikisha usalama wa njia zao za biashara. Kwa hiyo Hajjaj bin Yusuf, gavana wa Khilafah ya Bani Umayya huko Iraq, alimtuma Muhammad bin Qasim kwenda Sindh (eneo katika Pakistan ya leo) kwa sababu kadhaa. Muhammad bin Qasim alifanikiwa kuongoza vikosi vya Bani Umayya na akaiteka Sindh mwaka 711 M, na kuanzisha utawala wa Kiislamu katika eneo hilo.

Dkt. Aafia Siddiqui ni mfano mmoja tu wa wale wanaoitwa watawala wetu bado wanashughuli nyingi katika kuusaliti Uislamu na Waislamu na wako tayari kufanya lolote lile ili kuwafurahisha mabwana zao wa Magharibi ili mabwana zao wawape mwiba. Hili litaendelea na ni dhahiri kwetu sote kwamba chini ya mfumo huu wa kirasilimali wa kimagharibi, maslahi ya Waislamu daima yatahatarishwa kama tulivyoshuhudia huko Kashmir, Afghanistan na kuanzisha vita dhidi ya damu yetu wenyewe kwa jina la vita dhidi ya ugaidi. Sasa ni juu yetu kuuondoa mfumo huu uliotengenezwa na binadamu na kuubadilisha kwa Khilafah kwa njia ya Utume.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Mohammad Adil

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu