Jumanne, 24 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/26
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Dada zetu Waislamu Wameachwa Kufa Peke Yao bila ya Ulinzi na Utukufu wa Khilafah

(Imetafsiriwa)

Habari:

Raia wa Uingereza na mwanamume Muislamu, mwenye umri wa miaka 85, alipigwa risasi na kulazimika kuondoka Sudan huku mkewe, Muislamu mwenye ulemavu, akifa kwa njaa, baada ya kuachwa nchini Sudan huku ubalozi mdogo wa Uingereza ukikataa msaada wa kumsaidia. (BBC, 26 Mei 2023)

Maoni:

Tukio hili la kushangaza lilitokea huku wanandoa hao wakiishi karibu na ubalozi wa Uingereza. Ilifahamika kwamba dada huyo alikuwa umbali wa hatua kadhaa tu kutoka katika afisi ya nchi hiyo ambayo ilikuwa na majukumu ya ukaazi wake kama mmiliki pasi ya kusafiria ya Uingereza.

Abdalla Sholgami, mwenye umri wa miaka 85 mmiliki wa hoteli jijini London, aliishi na mkewe mwenye umri wa miaka 80, Alaweya Rishwan, ambaye ni mlemavu, karibu na kambi ya kidiplomasia ya Uingereza jijini Khartoum, BBC ilisema.

Kulingana na ripoti hiyo, Sholgami hakupewa msaada wa kuondoka Sudan na badala yake aliambiwa aende kwenye uwanja wa ndege maili 25 nje ya Khartoum. Alitarajiwa kuvuka eneo la vita akiwa peke yake ili kupanda ndege ya uokoaji.

Akiwa amekabiliwa na njaa na bila ya maji, Sholgami alilazimika kumwacha mke wake ili kutafuta msaada. Akiwa mbali alipigwa risasi tatu - mkononi, kifuani na sehemu ya chini ya mgongo na wadunguaji katika eneo hilo. Alinusurika baada ya kupelekwa kwa mwanafamilia mmoja katika sehemu nyingine ya Khartoum.

Familia hiyo ilisema kuwa mke wa Sholgami aliachwa ajitegemee na haikuwezekana wao kumfikia katika eneo lililozingirwa na wadunguaji. Matokeo yake, alikufa kwa njaa peke yake.

Mwanafamilia mmoja alisema, "Kilichotokea kwa babu na nyanya yangu kilikuwa uhalifu dhidi ya binadamu, sio tu wa Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF), sio tu wa jeshi la Sudan, lakini wa ubalozi wa Uingereza, kwa sababu ndio pekee ungeweza kuzuia hili lisitokee kwa babu na nyanya yangu.”

Sholgami alifanikiwa kutorokea Misri, ambako anapokea matibabu baada ya kufanyiwa upasuaji bila ganzi jijini Khartoum na mwanawe ambaye ni daktari.

Matukio hayo ya kutisha ya kuwaacha wanawake wasio na ulinzi peke yao ni ushahidi wa mifumo ya kishenzi na ya kioga ambayo iko katika ulimwengu wote wa Kiislamu. Ni jambo lisilofikirika kwamba viongozi watukufu wa Khilafah wangekubali kwamba jambo hili litokee. Wakati Sayyidna Umar Farooq alipoteuliwa kuwa khalifa wa pili, alinukuliwa akiwaambia watu wake: “Enyi watu, jueni kwamba mimi nimeteuliwa kusimamia mambo yenu, basi tambueni kwamba ukali wangu sasa umedhoofika, lakini nitaendelea kuwa imara na mkali juu ya madhalimu na maovu na nitayatia mashavu yao kwenye uchafu, fahamuni pia kwamba nitalitia shavu langu mwenyewe kwenye uchafu ili kuwalinda wachamungu.”

InshaAllah tutaregea kwenye ruwaza hii bora zaidi kwa wanadamu kwa idhini ya Mwenyezi Mungu (swt) na kupitia bidii yetu ya kutimiza faradhi hii.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Imrana Mohammad
Mwanachama wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu