Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

  Ufisadi Umekuwa ndio Msingi wa Tabia Yenu

Habari:

Özlem Zengin, Naibu Mwenyekiti wa Kundi la AKP, alisema, "Hili ni eneo letu jekundu" kwa ajili ya marekebisho ya sheria Na. 6284 kuhusu "vita dhidi ya unyanyasaji dhidi ya wanawake", ambayo Yeniden Refah Party (YRP) imeiweka mbele kama sharti la kujiunga na Muungano wa Watu (Cumhur Ittifakı).

Kwa mara nyengine tena, Waziri wa Huduma za Familia na Jamii Derya Yanık alisema, "Kuwepo kwa sheria nambari 6284 ni muhimu sana. Hata ukweli kwamba uwepo wake unajadiliwa haukubaliki kwa maoni yetu." Yanık pia alionyesha kuwa sheria, kama Zengin, "sheria hii ina mistari myekundu". (Mashirika 15.03.2023)

Maoni:

Mwenyezi Mungu (swt) amesema:

(ظَهَرَ الْفَسَادُ فِي الْبَرِّ وَالْبَحْرِ بِمَا كَسَبَتْ اَيْدِي النَّاسِ لِيُذٖيقَهُمْ بَعْضَ الَّذٖي عَمِلُوا لَعَلَّهُمْ يَرْجِعُونَ)

“Ufisadi umedhihiri bara na baharini kwa iliyo yafanya mikono ya watu, ili Mwenyezi Mungu awaonyeshe baadhi ya waliyo yatenda. Huenda wakarejea kwa kutubu.” [Ar-Rum 41].

Watawala, ambao hawajaacha taasisi hata moja ambayo hawajaivunjia heshima kwa Kanuni za Kishirikina walizozitumia kwa miaka mingi kwa Waislamu, wanajaribu njia za kila aina za kuvunja hata familia ambayo tunaweza kuiita msingi madhubuti wa jamii.

Wizara ya Familia na Huduma za Jamii hufanya kazi karibu kama wizara ya huduma ya Kutenganisha familia, jamii, kizazi, kutenganisha wanafamilia, kuwafanya wanandoa kuwa na uadui wao kwa wao. Kutokana na Mkataba wa Istanbul na sheria nambari 6284, ambazo zimeagizwa kutoka nchi za Magharibi kwa miaka mingi, maelfu ya kina baba bado wangali jela kwa kuowa wakiwa na umri mdogo.

Mamia ya maelfu ya wake wamevunja maelfu ya nyumba kwa kuingiza uadui kati ya wanandoa kwa Amri za kutolewa nyumbani, na hivyo kufanya kutowezekana kwao kukusanyika tena. Amri za kutolewa nyumbani zimesababisha uharibifu wa maelfu ya nyumba. Wale wanaonyakua mali za mamia ya maelfu ya watu kwa ukatili wa riziki isiyo na kikomo, ambayo ni haramu, madhalimu wanaojaribu kuwafanya Waislamu wakubali udhalimu wa 'tamko la mwanamke ni muhimu' kama sheria na uadilifu kwa ufahamu ambao hauwezi kuonekana hata katika jamii za malimbukeni ... Ukatili wenu unateketeza jamii, familia! Licha ya uharibifu huu wote, ni uhaini kuiweka kwa ulaini, kwamba bado mungali munanyanyua sheria hii chafu kwa kiwango kitakatifu na kuona mstari mwekundu! Mstari mwekundu kwa Waislamu ni amri na maamrisho ya Mwenyezi Mungu(swt). Vyenginevyo, sheria zilizowekwa na watu ambao wamebadilisha kufilisika kuwa ndio tabia ziko chini ya miguu yetu. Watawala ni wachungaji wa watu wao. Awali ya yote, utaratibu wanaoutawala unapaswa kuwa ni utaratibu unaozingatia imani ambayo jamii inaiamini, kwa mujibu wa imani na maadili yake, inayojumuisha kila mtu kwa uadilifu wake, kutoa usalama kwa raia na kuwajulisha waingiliaji. Familia, kizazi na jamii zitakuwa salama pamoja na watawala watakaobeba hukmu za Mwenyezi Mungu juu ya vichwa vyao, sio nyuma ya migongo yao, na kuzitumia ipasavyo katika kila sehemu ya maisha.

Utaratibu huu wa mateso na sheria zenu zimeichana jamii mbali na imani yake, imeiweka mbali na maadili yake. Muhimu zaidi, umesababisha wito wa pamoja wa shida na misiba. Acheni kubeba mizigo ya madhambi ya watu ambao mumeiangamiza dunia na Akhera yao. Pengine mutachukua ushauri.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Ahmet SAPA

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu