Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Syria ndio Mji Mkuu wa Uzalishaji Mihadarati wa Mashariki ya Kati chini ya Sheria za Kibepari

(Imetafsiriwa)

Habari:

Mnamo tarehe 25 Disemba 2022, serikali ya Jordan ilisitisha usafirishaji wa dawa za kulevya kwenye mpaka wa Syria. Tani moja ya tembe za amphetamine zilisafichwa ndani ya krimu ya tende  kwenye mpaka na Iraq. Jumla ya tembe milioni sita za dawa hiyo inayojulikana kwa jina la Captagon zilipatikana ndani ya malori mawili yaliyokuwa na jokofu. Ilikuwa mojawapo ya usafirisha mkubwa zaidi uliowahi kunaswa na Idara ya Forodha ya Jordan. Captagon inajulikana kama "cocaine ya mtu maskini." Inazalishwa kwa wingi nchini Syria, ambapo vita vya muongo mmoja vimeifanya nchi hiyo kuwa jimbo la mihadarati. Katika kilele cha mzozo huo, makundi ya wapiganaji yalisambaza dawa hiyo kwa wapiganaji - aghlabu ikiwa imejazwa kafeini - ili kuongeza ujasiri wake. Kutokana na umaskini unaoongezeka, Wasyria wengi wa kawaida walianza kujihusisha na biashara hiyo, ambayo ina thamani kubwa zaidi kuliko mahuruji ya halali.

Maoni:

Kuna nukta nyingi za kusikitisha za kuzingatia kutokana na habari hii. Kwanza, mojawapo ya maeneo mazuri zaidi ya Mashariki ya Kati, linalojulikana kwa taasisi zake za kihistoria na elimu, limeharibiwa kabisa. Wazo kwamba kiti cha zamani cha Khilafah sasa ni mji mkuu wa madawa ya kulevya wa eneo la MENA ni janga linalohitaji marekebisho.

Ukweli mwingine mbaya ni kwamba miundombinu ya Syria imeharibiwa sana kiasi kwamba kuna fursa chache za kazi za kuwawezesha idadi ya watu, shughuli za haramu zimekuwa na malipo zaidi ya kifedha kuliko ujuzi muhimu wa kijamii.

Janga la tatu ni jinsi dawa za kulevya zinavyotumika kuwapa ujasiri wa "kirongo" wapiganaji ambao hawajajitolea kwa mbinu na njia ya Mwenyezi Mungu (swt). Iman ni na daima imekuwa rasilimali kuu kwa ujasiri wa waumini na kamwe tusifikirie kitu chochote cha maana zaidi katika nguvu yake ya kutoa ushindi isipokuwa kwa Mwenyezi Mungu (swt).

Vijana wa mataifa wanatiwa sumu kwa kemikali hizi angamivu, na mustakabali wetu unaelekezwa kwenye ukafiri. Tunahitaji Khilafah kwa dharura kuwa na njia madhubuti na za dhati za kupiga marufuku mihadarati ipasavyo. Ripoti ya BBC ilinakili ulaghai wa mamlaka katika vitendo vya magendo, kwani hongo na ufisadi ni vitu vya kawaida huku bidhaa nyingi haramu zikiingia katika eneo kwa kiwango cha faida kubwa.

Tunatoa wito kwa Ummah kufanya kazi kwa ajili ya Khilafah bila kuchelewa na kuitikia wito wa Mwenyezi Mungu (swt);

(يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اسْتَجِيبُوا لِلَّهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُمْ لِمَا يُحْيِيكُمْ)

“Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele.” [Al-Anfaal 8:24].

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Imrana Mohammad
Mwanachama wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu