Jumanne, 24 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/26
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Kupandisha Mishahara Hakutakomesha Ukandamizaji wa Mfumo wa Kibepari!

(Imetafsiriwa)

Habari:

Uturuki: Takwimu za mfumko wa bei kwa mwezi Disemba, ambazo zinawahusu mamilioni ya watumishi wa umma wanaofanya kazi na watumishi waliostaafu, zimetangazwa. Kiwango cha ongezeko la mishahara ya watumishi wa umma na watumishi wa umma waliostaafu kimetangazwa. Watumishi wa umma na walio kazini na waliostaafu watapata nyongeza ya asilimia 16,47. Rais Erdogan alijadidisha kiwango cha ongezeko cha mwaka 2023 hadi asilimia 30. (Mashirika Yote ya Habari)

Maoni:

Baada ya kanuni ya hivi punde ya serikali ya Uturuki kuhusu Waliozuiwa Kustaafu Kwa Sababu ya Umri (EYT), macho yalielekezwa kwenye ongezeko litakalofanywa kwa watumishi wa umma na wafanyakazi waliostaafu ambao wameteseka kutokana na mfumko wa bei na gharama ya maisha. Baada ya Taasisi ya Takwimu ya Uturuki (TurkStat) kutangaza data ya mfumko wa bei wa Disemba, viwango vya ongezeko vinavyotarajiwa na mamilioni ya watumishi wa umma, watumishi wa umma waliostaafu na wafanyakazi waliostaafu vilionekana wazi.

TurkStat ilitangaza mfumko wa bei wa kila mwezi kuwa asilimia 1.18 na mfumko wa bei wa mwaka kuwa asilimia 64.27. Kampuni ya Utafiti wa Mfumko wa Bei (ENAG) pia kilitoa data yake yenyewe. ENAG iliripoti kuwa mfumko wa bei wa kila mwezi ulikuwa asilimia 5.18 na mfumko wa bei wa mwaka asilimia 137.55.

Baada ya data iliyotangazwa ya mfumko wa bei, wafanyikazi na wastaafu watapata nyongeza ya asilimia 30 mnamo Januari. Nyongeza hii ya kipuuzi kwa wafanyikazi na wastaafu imesababisha kuvunjika moyo katika duru hizi. Nyongeza kwa wafanyikazi na wastaafu kwa kuonyesha viwango vya mfumko wa bei kuwa chini, lilionekana kuwa la chini pia. Serikali kwa  mara nyengine tena imewaache watumishi na wastaafu wateseke katika hali ya mfumko wa bei. Hata hivyo, Rais Erdogan, katika taarifa yake baada ya kikao cha mwisho cha baraza la mawaziri, alisema kwamba wameazimia kuakisi mapato na utajiri wa Uturuki kwa makundi yote ya taifa, hasa kwa wafanyikazi, na kwamba watashughulikia nyongeza ya mishahara ya watumishi wa umma na wastaafu kwa mwelekeo huu. Hata hivyo, kwa ongezeko hili, kama kawaida, Rais Erdogan amefanya mapato na utajiri wa nchi hii kupatikana kwa makampuni machache tu ya kibepari. Amezifanya benki kuwa tajiri, ambapo zinanyonya watu. Alihamisha utajiri na mapato ya nchi hii kwenye taasisi za fedha na akaonyesha tena kwamba yuko upande wa wamiliki wachache wa mitaji, sio watu. Kwa mfano; Nchini Uturuki, 10% ya matajiri zaidi hupokea 54.5% ya mapato yote, wakati 50% ya maskini zaidi hupokea 12% tu ya mapato yote.

Katika kila jukwaa, Rais Erdogan husema kwamba hawawaachi na kuanzia sasa hatawaacha wafanyikazi na wastaafu kuteseka chini ya mfumko wa bei. Anadai kuwa daima wanalinda haki za wafanyikazi na wastaafu. Hata hivyo, kwa mujibu wa takwimu za mfumko wa bei zilizotangazwa, ni dhahiri kwamba nyongeza inayotolewa kwa wafanyikazi inabakia kutokuwa na uwezo dhidi ya gharama ya maisha. Hata nyongeza ya kima cha chini cha mshahara ilibaki ukingoni mwa njaa.

Mwaka jana pekee, bei za chakula kikuu cha nchi ziliongezeka kwa wastani wa asilimia 300, na bei ya kawi na mafuta iliongezeka kwa wastani wa asilimia 400. Takwimu hizi pekee ni kielelezo cha jinsi nyongeza ya mishahara inayotolewa kwa wafanyikazi na wastaafu ilivyo ya kipuuzi. Kwa njia hiyo hiyo, watu hawa, ambao wameteseka chini ya mfumko wa bei, waliingia mwaka mpya na kuongezeka kwa bei. Kuanzia kwa ushuru wa gari hadi malipo ya bima ya magari, ongezeko kubwa limefanywa kwa bidhaa nyingi kutoka A hadi Z.

Kabla ya kupanda huku kwa bei, serikali iliifariji jamii kisaikolojia kwa kuweka kanuni mpya kwa wanaopata mishahara ya chini na EYT. Lakini, misaada hii haikuchukua muda mrefu. Serikali ikarudisha na kikombe kile ilichotoa kwa kijiko cha chai. Itaendelea kuchukua na mwiko baada ya uchaguzi. Kwa kweli, iwe ni nyongeza ya kima cha chini cha mishahara ya serikali, EYT, ongezeko la hivi punde zaidi la mishahara ya watumishi wa umma na wastaafu, ndiyo, hatua hizi zote ni uwekezaji wa uchaguzi wa 2023. Ni hongo ya uchaguzi. Lau kama si kwa uchaguzi wa 2023, je, serikali ingechukua hatua hizi kuhusu masuala haya? Ikiwa maamuzi kama haya yangeweza kuchukuliwa katika kipindi hiki ambapo nchi iko katika shida za kifedha, yatachukuliwa kwa hali zote inapokosekana mgogoro wa kiuchumi. Kwa hivyo, kwa nini hayakuchukuliwa? Haki ya watu, raia, mfanyikazi, mstaafu alipewa nani? Katika hotuba aliyotoa kuhusu EYT mnamo 2019, Erdogan alisema, "Hata kama tutashindwa kwenye uchaguzi, niko nje yake. Je, hakusema kuwa hesabu hii ni hesabu isiyo sahihi? Kwa hivyo ni nini kimebadilika leo? Hii inamaanisha kuwa serikali inaweza kuchukua hatua kama hizo wakati wowote, hata ikiwa ni kushinda uchaguzi wa 2023. Ilimradi inataka kuchukua [hatua kama hizo].

Kwa upande mwingine, tunapoitazama historia ya miaka 1300 ya Uislamu, haijawahi kutokea mateso ya kiuchumi kama haya. Hakukuwa na kipindi ambacho upandishaji wa bei ulifanywa mmoja baada ya mwingine, uwezo wa ununuzi wa watu kupungua, taabu na umaskini kuenea sana, na jasho la uso wa mfanyikazi na mtumishi wa serikali kunyonywa sana. Kwa sababu Dola ya Kiislamu inakidhi mahitaji ya kimsingi ya watu. Haifanyi umeme, maji, gesi asilia na mali nyengine zinazomilikiwa na umma kupatikana kwa makampuni machache ya kibepari. Inazitumia kwa manufaa ya watu. Vivyo hivyo, hakuna ushuru wa kudumu unaopinda migongo ya watu na kuwaletea mzigo mkubwa. Kuna maendeleo, ustawi, amani na furaha pekee. Namuomba Mola wangu Mlezi aturuzuku dola kama hiyo siku za hivi karibuni, Inshallah...

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Yilmaz CELIK

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu