Jumanne, 24 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/26
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Urithi wa Biden - Sheria ya Ulinzi wa Ndoa za Jinsia Moja

(Imetafsiriwa)

Habari:

Joe Biden alitia saini Sheria ya Kuheshimu Ndoa. Mswada wa kulinda haki ya watu wa nchi hiyo kuingia katika ndoa za watu wa jinsia moja na watu wa rangi tofauti uliungwa mkono na wawakilishi wa pande zote mbili katika Bunge la Seneti, kwa mujibu wa makala "Rais wa Marekani Atia Saini Sheria ya Kulinda Ndoa za Jinsia Moja" katika tovuti ya DW. (Chanzo: DW)

Maoni:

Akibadilisha Sheria ya Ulinzi wa Ndoa, ambayo inaasisi ndoa kama muungano kati ya mwanamume na mwanamke, kwa Sheria ya Kuheshimu Ndoa, Rais Biden wa Marekani alitangaza kwamba "Marekani inafanya mambo muhimu kwa ajili ya usawa, uhuru na haki, sio tu kwa baadhi ya watu, lakini kwa wote." Ambapo inaweza kueleweka kuwa usawa, haki na uhuru bado zingali hazijatolewa kwa raia wote wa Amerika. Na hili ni kweli, kwa mfano, ubaguzi unaoendelea dhidi ya wenyeji wa asili wa Amerika.

Ndoa za watu wenye rangi tofauti kati ya weusi na weupe nchini Marekani zimekadiriwa kwa karne nyingi kuwa sio tu zisizokubalika, lakini hata uhalifu. Baada ya mlingano rasmi katika haki, kuanzishwa kwa wale wanaojiita Waamerika wenye asili ya Kiafrika kuwaoa Waamerika wa asili ya Ulaya hakuainishwi tena kama uhalifu. Mpaka leo, hata hivyo, inatazamwa na baadhi ya wahafidhina kutoka kwa Waamerika weupe kama kuvunja kusiko kwa kawaida kwa kwa mila.

Mitazamo kuhusu ushoga nchini Marekani, kama ilivyo katika nchi nyingine za Magharibi, pia imebadilika leo. Mabadiliko ya dhana ya jamii ya Amerika juu yake, kutoka kuwa dhambi, kosa la jinai na dosari ya kiakili, hadi kuwa sheria ya kimaumbile na desturi halali ya maisha, ilianza katikati ya karne ya 20.

Maneno ya Biden kuhusu hatua fulani "kuelekea kuundwa kwa taifa" si chochote zaidi ya ujanja wa kisiasa. Msingi wa kuibuka na kuundwa kwa taifa la Marekani ni Katiba ya Marekani.

Mungu aliyetajwa katika katiba ya Marekani hana uhusiano wowote nayo. Haki na uhuru wote inaoutangaza unatokana na mfumo wa kirasilimali, ambayo msingi wake ni wazo la kutenganisha dini na maisha ya jamii na dola. Fahamu ya "furaha" iliyotajwa katika katiba hii inazingatiwa kuwa sambamba na falsafa ya matumizi wanayoibeba mabepari, na ambayo kwayo thamani ya kiakhlaqi ya kitendo chochote hupimwa na kiwango cha manufaa yanayovuliwa, na furaha ni upokeaji wa starehe ya hali ya juu kabisa.

Wakati huo huo, Katiba ya Marekani inatambua haki ya watu ya kuiondoa serikali yoyote na kuanzisha mpya, "kwa msingi wa kanuni na aina za mpangilio wa mamlaka ambayo, kwa maoni yake, itawapa watu usalama na furaha bora zaidi.” Na kwa kuwa, kwa mujibu wa demokrasia, maoni ya wengi yanachukuliwa kama matakwa ya watu, serikali ya Kidemokrasia, inayoongozwa na Biden, inataka kuomba uungwaji mkono wake ili kudumisha utawala wake. Kwa hivyo, inalegeza msimamo, kusawazisha ndoa za jinsia moja na watu wa rangi tofauti kwa haja ya kutambuliwa kwao na kuheshimiwa kama haki za kimaumbile za raia.

Iwe iwavyo, kwa kweli, ufanyaji usawa huu wa ndoa ya kawaida kabisa, ingawa ya watu wa rangi tofauti na ushoga usio wa kimaumbile, ambao utawala wa Biden unauzingatia kuwa ni hatua ya maendeleo, ni maridhiano ya aibu ambayo wayapaswi kukubaliana nayo. Kwanza, Waamerika watalazimika kutafakari njia ovu ya maisha ya kaumu lut kama haki halali ya kutekeleza uhuru wa kibinafsi, unaotokana na haki za kidemokrasia za binadamu. Pili, haja ya ulinzi wa serikali wa ndoa za watu wa rangi tofauti ni ushahidi wa kuendelea kwa ubaguzi wa rangi na migongano ya kina katika jamii ya Amerika, ambayo sio mipango kama hiyo ya kisheria wala filamu za gharama kubwa za Hollywood hanaweza kuitatua.

Haishangazi kwamba mfumo wa kibepari unaharibu kila inachokigusa. Kwa hivyo, uliharibu mfumo wa kisiasa, na kuugeuza kutoka kujali mambo ya watu hadi kwenye udanganyifu na ufadhili wa uhalifu; mfumo wa kiuchumi, kutoka katika utumuzi adilifu wa mali iliyotolewa na Mwenyezi Mungu Mtukufu – hadi kuwa njia ya uporaji na ukandamizaji. Pia, katika nyanja ya kijamii, badala ya kuhifadhi usafi wa kimaadili na utu wa mwanadamu, mfumo wa ubepari inajiingiza katika maovu na upotovu duni, unaofisidi watu binafsi na jamii nzima.

Ni Uislamu pekee, ulioteremshwa na Muumba kama rehema na mwongozo mwaminifu kwa viumbe Vyake, ndio unaofaa kutatua matatizo yao yoyote, bila kujali tofauti za rangi, zama na eneo la makaazi.

Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

(فَأَقِمْ وَجْهَكَ لِلدِّينِ حَنِيفًا فِطْرَةَ اللَّهِ الَّتِي فَطَرَ النَّاسَ عَلَيْهَا لَا تَبْدِيلَ لِخَلْقِ اللَّهِ ذَلِكَ الدِّينُ الْقَيِّمُ وَلَكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ لَا يَعْلَمُونَ)

“Basi uelekeze uso wako sawasawa kwenye Dini - ndilo umbile la Mwenyezi Mungu alilo waumbia watu. Hapana mabadiliko katika uumbaji wa Mwenyezi Mungu. Hiyo ndiyo Dini iliyo nyooka sawa. Lakini watu wengi hawajui.” [Ar-Rum: 30].

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Mustafa Amin
Mwanachama wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Ukraine

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu