Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Ajali ya Ndege ya Precision Inadhihirisha Hali ya Kutojali kwa Ubepari

(Imetafsiriwa)

Habari:

Ndege ya Precision aina ya ATR42-500 (twin turboprop) yenye usajili 5H-PWF, na kumbukumbu ya safari PW494 ikiwa na abiria 43 safarini kutoka Dar es Salaam kwenda Bukoba, mkoani Kagera ilianguka ndani ya Ziwa Victoria ndani ya Bukoba siku ya Jumapili 06 Novemba 2022 kiasi cha saa 2.53 asubuhi. Ajali hiyo ilipelekea kufariki dunia watu 19 kama ilivyothibitishwa na shirika la Precision lenyewe, na pia kuthibitishwa na Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania.

Maoni:

Kwa dhati kabisa tunatoa salamu zetu za rambirambi kwa familia zilizoondokewa na watu wao, pia tunawatakia majeruhi wote warejee katika siha zao kwa haraka.

Kuhusiana na ajali hii, inaonekana wazi kwamba kuna hali ya kutojali katika kukabiliana nayo. Ndege ilianguka kufuatia jaribio la kutaka kutua katika hali ya hewa mbaya iliyokuwepo Uwanja wa Ndege wa Bukoba karibu na Ziwa Victoria, katika hali hiyo hapakuwa na hatua za haraka za kutafuta na kuokoa waathirika katika ndege iliyokuwa katika maji yasiokuwa mengi. Inaaminika kwamba ndege ilianguka kiasi cha mita 100 tu kutoka ufukwe wa ziwa hilo. (Gazeti la Mwananchi 10/11/2022).

Pia kama ilivyoripotiwa na Idhaa ya Kiswahili ya Redio ya Marekani tarehe 06/11/2022 na kuthibitishwa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza (Bw. Albert Chalamila) katika mahojiano na  Redio ya  East Africa siku hiyo hiyo ya 06/11/2022, kwamba  mara tu baada ya ajali kuliendelea mawasiliano baina ya marubani na kituo cha kuongozea ndege na maafisa wa serikali. Ikiwa hali ni kama hiyo, kwa nini kikosi cha uokozi hakikuwasili kwa wakati, hali iliyopelekea vifo kuwa vingi hadi kufikia 19, ambapo lau kikosi cha uokozi kingewasili mapema wangeweza kunusuru maisha.

Ajali hii mbaya inathibitisha uchache wa wazamiaji na vifaa vya uokozi, hali iliyopelekea jukumu la uokozi kutendwa na wavuvi na watu binafsi karibu na ufukwe wa ziwa. Abiria walioweza kuokolewa hai ni wale waliodiriki kutoka nje ya ndege baada ya mhudumu wa ndege hiyo kufungua mlango wa nyuma wa ndege hiyo, na wale waliofariki hawakuweza kutolewa nje mpaka ndege ilipohaulishwa na kupelekwa karibu na  fukwe.

Jambo la ajabu ni kuwa ajali ya ndege hii sio ajali ya kwanza kutokea, bali inaonekana hakuna funzo lililopatikana katika masuala ya uokozi. Mwezi wa Novemba 1997 ndege aina ya Piper PA 31-350 ilianguka katika maeneo ya Kibo, sehemu ya Mlima Kilimanjaro ikiwa futi 15,400 kutokana hali mbaya ya hewa. Mwezi Disemba 2018 ndege ya Precision Air ATR-72 nayo ilizingirwa na makundi ya ndege kupelekea kutua kwa dharura katika Uwanja wa Ndege wa Mwanza, na mwezi wa Februari 2022 ndege inayomilikiwa na kampuni ya Fly Zanzibar Limited ikiwa na watu 14 ilianguka baharini karibu na mwambao wa visiwa vya Ngazija. Hii ni mifano michache, lakini bado hakuna kilichotendwa kuboresha huduma za kukabiliana na dharura.

Hali hii inaonesha waziwazi maumbile ya ndani ya mfumo wa kibepari ambao haujali maisha wala ustawi wa binadamu. Lakini pia ni kielelezo cha wazi cha mfumo huo kutokuwa na ghera wala utashi wa kukabiliana ipasavyo na masuala nyeti hata yale ya kufa na kupona.

Nchi zinazoendelea na ulimwengu kwa ujumla unahitaji mfumo wa uadilifu na insafu ambao ni Uislamu. Kwa kupitia utawala wake wa Khilafah utajali utu, hadhi yao na maisha yao, kwa kuwa mfumo huo (Uislamu) una nguvu ya kweli ya kiroho ya kufungamanisha kila kitendo kwamba kitahesabiwa katika maisha yajayo ya akhera.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Said Bitomwa

Mwanachama wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Tanzania

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu