Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Ndugu Mkongwe zaidi Kuachiliwa Huru kutoka Guantanamo

(Imetafsiriwa)

Habari:

Shirika la habari la NPR liliripoti kwamba mfungwa mzee zaidi katika Guantanamo Bay aliachiliwa huru akiwa na umri wa miaka 75 na hivyo kupunguza idadi ya watu hadi 35. Saifullah Paracha alirudishwa nyumbani katika nchi yake ya asili ya Pakistan katika wiki ya mwisho ya Oktoba 2022. Kuachiliwa huru huku kuliidhinishwa kwa msingi wa ukweli kwamba hakukuwa na ushahidi wowote wa kuzuiliwa kwake na kwamba hakuwezi kuwa na uhalali zaidi wa kumweka gerezani. Mwandishi wa NPR Sacha Pfeiffer alikuwa kwenye gerezani humo wakati wa kuachiliwa huru na aliweza kupata taarifa za moja kwa moja juu ya hali ya wafungwa katika gereza hilo maarufu.

Maoni:

Hadithi ya ndugu huyo mkongwe ya ukandamizaji ilianza mwaka wa 2002 na kukamatwa kwake na majeshi ya Marekani chini ya tuhma ya kuwa na uhusiano na wapiganaji wa Al Qaeda nchini Pakistan. Alipelekwa Afghanistan na kuteswa kabla ya kuzuiliwa Guantanamo Bay pamoja na wafungwa wengine zaidi ya 700. Alipewa jina la utani la "mfungwa wa milele" hili ni neno linalopeanwa kwa wale waliopewa kifungo kisichojulikana bila ya uwezekano wa kuachiliwa huru. Aliachiliwa kwa matakwa ya Mwenyezi Mungu (swt) ambayo yanatumika kama ukumbusho kwamba Muumba Mtukufu ndiye anayesimamia mambo ya waumini na ni lazima tuwe imara katika Imani bila ya kujali adhabu za Dunia hii.

(قُلْ مَنْ بِيَدِهِ مَلَكُوتُ كُلِّ شَيْءٍ وَهُوَ يُجِيرُ وَلَا يُجَارُ عَلَيْهِ إِنْ كُنْتُمْ تَعْلَمُونَ)

“Sema: Ni nani mkononi mwake umo Ufalme wa kila kitu, naye ndiye anaye linda, wala hakilindwi asicho taka, kama mnajua?” [Quran 23: 88]

Bodi ya parole huko Guantanamo ilitathmini kwamba hakuwa tena ni tishio kwa serikali ya Marekani na ilikuwa ni hitimisho hili baada ya miaka 20 ya kizuiliwa kwa dhulma ambapo ilisababisha kuachiliwa huru kwake. SubhanAllah, ni fidia ya Jannat pekee ndiyo inaweza kuwapa haki Waislamu wengi ambao wameteswa na kuzuiliwa kinyume na matakwa yao. Bado hatujui ni nini kilimpata dada yetu mpendwa Dkt. Afia Siddique, ambaye alilazimika kuwatelekeza watoto wake miaka hii yote kwani pia aliwekwa kizuizini kwa mashtaka ya uwongo ya 9/11.

Maisha ya Waumini hayapotei kwa ajili ya huduma ya Dini, kamwe tusiruhusu mifano hii itoe hofu katika nyoyo zetu tunapofanya kazi ya kuregesha Khilafah. Waislamu hawa wanatumika kama mifano ya kutuzuia kufanya kazi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu (swt). Tunaomba kwamba Waislamu kote duniani waregeshwe kwa watoto na familia zao na kwamba Khalifa Mtukufu ateuliwe ili kuhakikisha kwamba vitendo hivi vya dhulma mikononi mwa maadui wa Mwenyezi Mungu (swt) vinakomeshwa mara moja!

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Imrana Mohammad
Mwanachama wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu